Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Got a question or eager to learn? Discover limitless learning on WhatsApp now - Start Now!

Nandi Central-Kiswahili Paper 3 Question Paper

Nandi Central-Kiswahili Paper 3 

Course:Kiswahili

Institution: Form 4 question papers

Exam Year:2009



102/3
KISWAHILI
KARATASI YA 3
FASIHI
JULAI / AGOSTI 2009
MUDA: SAA 2½

NANDI CENTRAL DISTRICT
JOINT EVALUATION TEST - 2009
Kenya Certificate of Secondary Education (K.C.S.E)




102/3
KISWAHILI
KARATASI YA 3
FASIHI
JULAI / AGOSTI 2009
MUDA: SAA 2½


MAAGIZO:
•Jibu maswali manne pekee
•Swali la kwanza ni la lazima
•Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki yaani Tamthilia, Riwaya, Hadithi Fupi na Ushairi.
•Usijibu maswali mawili kutoka katika sehemu moja.


Karatasi hii ina kurasa 4 zilizopigwa chapa, watahiniwa
lazima wahakikishe kurasa zote zimepigwa chapa
sawa sawa na kuwa maswali yote yamo.
SEHEMU YA A
Fasihi simulizi
1. a) Maghani ni nini?(alama2)
b) Eleza fani zifuatazo za maghani.(alama8)
i) Vivugo
ii) Tondozi
iii) Pembezi
iv) Rara
c) Eleza maana ya neno Ulumbi(alama2)
d) Bainisha sifa za ulumbi.(alama8)

SEHEMU YA B
RIWAYA
UTENGANO – Said A. Mohamed
2. “Nyinyi mliosoma elimu yenu bure. Hamjui mnakotoka wala mnakokwenda…
Usinisemee kizungu miye. Si ndiyo mlivyotuweka tusisome tuwe wajinga….”
a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.(alama4)
b) Itaje mbinu ya lugha iliyotumika hapa.(alama2)
c) Taja sifa za mzungumzaji.(alama4)
d) Kwa kujikita kwa wahusika wafuatao, jadili maudhui ya mabadiliko.(alama10)
i) Mussa
ii) Maksuudi
iii) Maimuna
iv) Farashuu
v) Biti Kocho

3.Dhihirisha uozo wa kijamii kama unavyojitokeza katika riwaya ya Utengano. (alama20)

SEHEMU YA C
TAMTHILIA
KIFO KISIMANI – K. wa Mberia
4.a) “Wewe ndiwe Butangi?”
“La! Lakini mimi ndiye kiongozi wa macho na masikio yake.”
“Na kisu chake cha kuchinjia watu.”
i) Eleza muktadha wa dondoo hili(alama4)
ii) Ni ukinzani upi unaojitokeza katika dondoo hili?(alama6)


.b) Fafanua mbinu zifuatazo za lugha kama zilivyotumiwa na mwandishi wa tamthilia.
i) Uzungumzi nafsia(alama4)
ii) Lugha ya matusi(alama2)
iii) Taswira(alama4)

5.a) Mwandishi anamsawiri mwanamke kama kiumbe aliyedhulumiwa. Jadili(alama10)

.b) Jadili maudhui ya tamaa kama yanavyojitokeza katika tamthilia(alama10)

SEHEMU YA D
HADITHI FUPI
MAYAI WAZIRI WA MARADHI – K. W. Wamitila

6.Eleza kwa kutumia mifano ifaayo vile ambavyo mwandishi wa hadithi ya ‘Uteuzi
wa Moyoni’ amelishughulikia swala la jinsia na utamaduni(alama20)

SEHEMU YA E
USHAIRI
7. Soma shairi lifuatalo kwa makini halafu ujibu maswali yanayofuata.
1 Kijana tuza makini, nikwambie usikile 6. Kileta maji jioni, ndoo jitwike na kata
Chakula mahotelini, si kizuri usikile Kata njema ya majani, laini wezayo kata
Ufikapo mlangoni, kizingiti usikile Kumbuka ya kisimani, huteki ela kwa kata

2. Nenda kaseme nyumbani, kesho asubuhi siji 7. Ninawahi kibandani, nikaliezeke paa
Nitakwenda makondeni, kawashunge shunge siji Nipate lindia nyuni, na wanyama kama paa
Na hata hapo jioni, kama nitakuja siji Kwani kiola angani, naona jua lapaa

3. Na kama wenda mjini, upatapo nyumba panga 8. Kisha takwea mtini, nimeona bivu tunda
Upahame mizimuni, palozingirwa na panga Sina usono moyoni, ela tunda kisha tunda
Hapana tena amani, kutwa mwapigana panga Nimpe wangu mwendeni, jioni nishike tunda

4. Na kesho kija shambani, uonapo mti panda 9. Meanza wao uneni, hapo nami ndipo kamba
Kwea hadi kileleni, ujifiche kwenye panda Leo wenda hawaoni, kama wa bahari kamba
Kaziyo ulinde chini, mimea tuliyopanda Wajijaza kimiani, wakijitatia kamba

5. Kishuka ola shinani, njugu merundika chungu 10. Mtoto wachoma yakini, japo liwe moja kaa
Njugu peleka nyumbani, zisije zikawa chungu Ukikupata takoni, ni shida huwezi kaa
Kaanga sufuriani, au pia kwenye chungu Ela hufaa mekoni, kutoka nswi na kaa




Maswali.
a)Bainisha dhamira ya mtunzi wa shairi hili (alama2)
b)Eleza maana tatu za neno chungu kama lilivyotumika katika shairi (alama3)
c)Andika ubeti wa nane katika lugha nathari (alama3)
d)Eleza muundo wa shairi hili (alama5)
e)Onyesha vile uhuru wa kishairi ulivyotumiwa na malenga (alama4)
f)Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika shairi (alama3)
i) Makondeni
ii) Jitwike
iii) Kiola






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers