Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Got a question or eager to learn? Discover limitless learning on WhatsApp now - Start Now!

Trans-Nzoia District Mock-Kiswahili Paper 3 Question Paper

Trans-Nzoia District Mock-Kiswahili Paper 3 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2007



102 / 3
KISWAHILI
FASIHI
KARATASI YA 3
JULAI 2007
MUDA : MASAA 2 ½
WILAYA YA TRANS- NZOIA BARAZA LA MTIHANI - 2007
Hati Ya Kuhitimu Kisomo Cha Sekondari ( K. C. S.E. )
102 / 3
FASIHI
MUDA : SAA 2 ½
Jibu maswali manne pekee
Swali la kwanza ni la lazima
Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki yaani: Tamthilia,
Riwaya, Hadithi fupi na Fasihi Simulizi.
Usijibu maswali mawili kutoka katika sehemu moja.
Karatasi hii ina kurasa 4 zilizopigwa chapa
Watahiniwa lazima wahakikishe kurasa zote zimepigwa chapa sawa sawa na kuwa maswali yote yamo
1. USHAIRI . Soma shairi kasha ujibu maswali
SIKATE TAMAA
Umeanguka, inuka, simama kama mnazi
Umechunika, inuka, tia dawa kwa ujuzi
Sasa inuka, inuka, kijana ianze kazi
Sikate tamaa
Usife tamaa, nyanyuka, ni muweza wa kutenda
Kuna hadaa, nyanyuka, anza tena kujipinda
Dunia baa, nyanyuka, anza tena kujiunda
Sikate tamaa
Sivunjwe moyo, dunia hivyo itakunyanyasa
Futa kiliyo, dunia, hiyo idhibiti sasa
Ipe kamiyo, dunia, kamwe siache kufusa
Sikate tamaa.
Una nguvu, simama, wewe upambane nao
Una werevu, simama, uzepuke njama zao
Usiche kovu, simama, ujifunze vumilio
Sikate tamaa
Maswali
a) Shairi hili ni la aina gani. ( alama 3)
kimishororo, kimizani na kivina.
b) Eleza lengo la shairi hili. ( alama 2 )
c) Kulingana na mshairi, tungewezaje kuepuka njama tunazofanyiwa. ( alama 2 )
d) Eleza muundo wa ubeti wa kwanza wa shairi hili ( alama 4 )
e) Onyesha kwa kutolea mifano miwili jinsi mwandishi alivyotumia inkisari
( alama 2 )
f) Andika ubeti wa mwisho kwa lugha ya nathari ( alama 4 )
g) Taja mbinu zozote mbili za lugha zilizotumiwa na uzitolee mifano. ( alama 3 )
TAMTHILIA.
KIFO KISIMANI: KITHAKA WA MBERIA
2. Watu! Hawako! Nimewaangalia kwa makini. Hawako!
a) Andika muktadha wa maneno haya. ( alama 4 )
b) Taja sababu ya watu kutokuwepo. ( alama 2 )
c) Fafanua athari zilizotokana na uongozi mbaya katika nchi ya Butangi (alama 14)
3. Huku ukitolea mifano, Eleza mbinu zifuatazo za uandishi zilivyotumika;
i) Jazanda ( alama 8 )
ii) Ndoto ( alama 6 )
iii) Kejeli ( alama 6)
RIWAYA
MWISHO WA KOSA : Z BURHANI
4. Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki. Thibitisha ukweli wa usemi huu ukirejelea riwaya ya mwisho
wa kosa. ( alama 20 )
5. Lakini anafanya kazi, anapata pesa nzuri zaidi yangu mimi.
a) Weka dondoo hili katika muktadha wake. ( alama 5 )
b) Taja maudhui yanayojitokeza katika dondoo hili. ( alama 3 )
c) Jadili sifa na umuhimu wa
i) Mzungumzaji ( alama 6 )
ii) Mzungumziwa. ( alama 6 )
MAYAI WAZIRI WA MARADHI NA HADITHI NYINGINE -FUMBO LA MWANA ;
SINJIRI MUKUBA.
4
6. a) Kwa nini mwandishi akaipa hadithi anwani “ Fumbo la mwana” (alama 3)
b) Eleza maudhui ya Elimu yanavyojitokeza katika hadithi. (alama5)
c) Ni athari gani zinazompata Nanda baada ya kutumia dawa za kulevya. (alama 6)
d) Eleza jinsi kinaya kinavyojitokeza katika hadithi hii. ( alama 6)
FASIHI SIMULIZI.
7. a) Tofautisha kati ya methali na semi. ( alama 2 )
b) Toa mifano miwili miwili ya methali zinazozingatia tamathali zifuatazo;
i) Balagha (alama 2)
ii) Takriri ( alama 2)
iii) Ukinzano (alama 2)
c) (i) Fafanua vijipera vifuatavyo vya mazungumzo.
1) Utani ( alama 2 )
2) Soga ( alama 2 )
3) Ulumbi ( alama 2 )
ii) Taja sifa na umuhimu wa soga. ( alama 6 )






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers