Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Got a question or eager to learn? Discover limitless learning on WhatsApp now - Start Now!

Kericho District Mock- Kiswahili Paper 3 Question Paper

Kericho District Mock- Kiswahili Paper 3 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2007



102/3
KISWAHILI
KARATASI YA TATU
JULAI / AGOSTI 2007
MUDA: SAA MBILI NA NUSU
JARIBIO LA TATHMINI YA PAMOJA WILAYA YA
KERICHO
HATI YA KUHITIMU KISOMO CHA SEKONDARI 2007
102/3
KISWAHILI
KARATASI YA TATU
JULAI / AGOSTI 2007
MAAGIZO
 Jibu maswali manne pekee.
 Swali la kwanza ni la lazima.
 Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja
 Karatasi hii ina jumla ya alama 80.
 Mtahiniwa ataadhibiwa iwapo hatafuata maagizo.
 Karatasi hii ina kurasa nne zilizopigwa chapa. Hakikisha kwamba kurasa zote zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.
1. USHAIRI
Vita vya ndimi
Huyo! Amshike huyo!
Hakuna bunduki wala kifaru
Bomu na risasi hata hawazijui!
Lakini mno wanashambuliana.
Kwa ndimi zilizonolewa kwa makali
Vipande vya matusi silaha zao.
Yu imara mmoja wao.
Akirusha kombora la neno zito!
Limtingishe adui wake
Na kumgusa hisia kwa pigo kuu.
Pigo linalopenya moyoni kama kichomi
Kuchipuza joto la hasira na kisasi
Katika mapigano yaso na kikomo.
Filimbi ya suluhu inapulizwa kuwaamua!
Ni nani anayekubali suluhu?
Roho zinakataa katakata
Huku ukaidi ukinyemelea na kutawala
kote
Mapandikizi ya watu yakipigana
Vitu shadidi visivyo ukomo
Vita vya ndimi!
Magharibi sasa
Jua linapungia mkono machweo
Nalo giza likinyemelea kwa kiburi na
kasi
Sisikii tena sauti za misonyo
Mate ya watesi yamekauka
Makanwa yao yamelemewa na uchovu
Sasa wameshikana mikono
Nyuso zao zikitabasamu
Ishara ya suluhu!
(a) Hili ni shairi la aina gani? (alama 1)
(b) Eleza sifa za utunzi alizotumia mshairi. (alama 4)
(c) Taja kwa kutolea mifano tamathali za usemi zozote tatu zilizotumiwa katika shairi hili.(alama 3)
(d) Fafanua mishororo hii:
(i) Akirusha kombora la neno zito!
(ii) Makanwa yao yamelemewa na uchovu (alama 4)
(e) Zungumzia mgogoro katika shairi na namna unavyomalizika. (alama 6)
(f) Toa maana ya msamiati huu
(i) Kichomi
(ii) Misonyo (alama2)
KIFO KISIMANI – Kitheka wa Mberia
2. “Ama … mke wako amekuja. Anakuja kukuimbia nyimbo za mapenzi. Msalimie.”
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
(b) Taja mbinu ya lugha iliyotumika hapa (alama 2)
(c) Linganisha sifa za msemaji na msemewa. (alama 4)
(d) Je, ni mambo yapi yaliyosababisha kuanguka kwa utawala wa mtemi Bokono? (alama 10)
RIWAYA
MWISHO WA KOSA na Zainabu Burhani
3
Jibu swali la 3 au la 4.
3. “Majuto ni mjukuu huja baadaye.” Thibitisha methali hii kwa kurejelea riwaya ya ‘Mwisho wa Kosa.’
4. Namwona siku hizi anavaa nguo kama watu wengine, amewacha kuvaa zile sare zao.
Unakumbuka tulivyokuwa tukigombana naye ili avae nguo zake mwenyewe?”
“ Ninakumbuka. Zilikuwa zinavalishwa kabati.”
(a) Fafanua muktadha wa maneno haya. (alama 4)
(b) Nini maana ya: “ Zilikuwa zinavalishwa kabati” (alama 1)
(c) Toa sababu mbili za mabadiliko ya mzungumziwa zinazotolewa na wanenaji hawa. (alama 2)
(d) Mzungumziwa amepitia mabadiliko yapi tangu mwanzo hadi mwisho wa riwaya? (alama 6)
(e) Eleza namna wahusika wa riwaya hii wanavyokirimiana. (alama 7)
MAYAI WAZIRI WA MARADHI NA HADITHI NYINGINE
Msamaria mwema
Jibu swali la 5 au 6
5. …. Maumivu makali yaliichoma mwili wake wote. Alijitahidi kukiinua kichwa chake …….
lakini wimbi kubwa la maumivu lilimzoa na kumkwamiza kwenye kupotewa na fahamu.
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
(b) Eleza shida za mwananchi wa kawaida kulingana na hadithi hii. (alama 10)
(c) Huku ukirejelea hadithi hii, dhibitisha kauli kuwa serikali imeshindwa kutekeleza
majukumu yake. (alama 6)
6. Huku ukirejelea “Mayai waziri wa maradhi na hadithi nyingine,” jadili maswala ibuka
mbalimbali yanayojitokeza. (alama 20)
FASIHI SIMULIZI
7. (a) Tofautisha kati ya mighani na maghani katika Fasihi simulizi. (alama 2)
(b) Eleza sifa zozote nne za mighani. (alama 4)
(c) Kwa kutolea mifano mmoja mmoja taja aina mbili kuu za vitendawili (alama4 )
(d) Fafanua sifa sita za vitendawili (alama 6)
(e) Nyimbo zina dhima gani katika jamii? (alama 4)






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers