Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Got a question or eager to learn? Discover limitless learning on WhatsApp now - Start Now!

Kcse 2011 Kiswhaili Karatasi Ya 3  Question Paper

Kcse 2011 Kiswhaili Karatasi Ya 3  

Course:Kiswahili

Institution: Kcse question papers

Exam Year:2011




SEHEMU A: TAMTHILIA
KITHAKA WA MBERIA: Kifo Kisimani Swali la lazima
1 "Alijiona pwagu. Lakini Butangi ina pwaguzi pia."
Eleza tofauti baina ya wahusika wanaorejelewa. (alama 20)
SEHEMU B: RIWAYA
S.A.MOHAMED: Utengano Jibu swali la 2 au la 3
2 Eleza namna mbinu zifuatazo zilivyotumiwa na mwandishi wa riwaya ya Utengano:
(i) Kwelikinzani
(ii) Sadfa. (alama 20)
3 "Uhuru alioutaka na ulimwengu alioufahamu Maimuna umemdhuru hatimaye."
Thibitisha kauli hii kwa kutoa mifano kumi. (alama 20)
SEHEMU C: USHAIRI
Jibu swali la 4 au la 5
KUJITEGEMEA
1. Nchi ni ile ambayo, imekita ardhini
Siyo ile iombayo, ghaibu na majirani
Taratibu siyo hiyo, wanachi twambizaneni
Daima hukaa chini, maganja ya mpewaji
2. Chumo lote na mitaji, leo limo maganjani
Bepari na wanyonyaji, wasalie maguguni
Shime utekelezaji, vingine havifanani
Daima hukaa chini, maganja ya mpewaji

3. Twaishije tujihoji, wanachi humu nchini
Kila tunachohitaji, kupatakwe ugenini
Hiyo ni tete haviji, tongo tupangusaneni
Daima hukaa chini, maganja ya mpewaji
4. Kuomba wataalamu, ni mwendo haulingani
Tupate wa humu humu, wajuzi wa kila fani
Mbele washike hatamu, kwa mapimo na makini
Daima hukaa chini, maganja ya mpewaji

5. Tuufuate wongozi, pamwe na nyingi imani
Tushiriki kila kazi, na mambo yalomkini
Mikopo ina kinyezi, si kitu cha tumaini
Daima hukaa chini, maganja ya mpewaji

6. Yote hatuyatimizi, alotimiza ni nani
Lakini tuwe maizi, tusizurure mijini
Tukamshabilii kozi, kipanga au kunguni
Daima hukaa chini, maganja ya mpewaji
7. Shujaa itakiwavyo, aonekane vitani
Na sisi vita tunavyo, roho kwa roho ugani 'Kutegemea' vilivyo, kondo tujiamueni Daima hukaa chini, maganja ya mpewaji
Boukhet Amana: Malenga waMrima
Mwinyihatibu Mohammed
Oxford University Press
1977
(a) Mtunzi wa shairi hili ana dhamira gani? (alama 2)
(b) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu moja. (alama 2)
(c) Eleza mambo matatu ambayo mshairi anashauri nchi ifanye ili
kujitegemea. (alama 3)
(d) Taja aina moja ya idhini ya kishairi iliyojitokeza kwa wingi zaidi katika shairi na utoe
mifano mitano ya matumizi yake. (alama 7)
(e) Andika ubeti wa pili kwa lugha ya nathari. (alama 4)
(f) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi:
(i) Ghaibu
(ii) Tukamshabihi.
(alama 2)

HAKI
1. Haki watutisha, tusikuandame, kwa matendo yetu,
Watukorofisha, tusikuandame, kila penye kitu,
Mbona watugwisha, miba ituchonie, kwenye huu mwitu,
Tutokwe nautu!

2. Hatutakufanya, mwana kwa mvyele, aliyemzaa,
Haki watunyima, machumi ya mbele, na nyingi hadaa,
Tuchumayo nyanya, uchungu umbele, hatuna wasaa,
Haki twashangaa!

3. Na kambi nzima, kunaiyenea, hasa hapa petu,
Tunakutazama, kwa kuulizia, kuweza thubutu,
Na kwenye milima, ilotueka, kupandia watu,
Usifanyekatu!

4. Sio hao mabwana, waloteuliwa, kupata mwangaza,
Haki wakubana, lilotarajiwa, kwenye hichi kiza,
Ndevu kuchomana, wengine kuliwa, tukijiingiza,
Kambi yatuviza!

5. Haki huna njia, kizuizi mali, ndio njia panda,
Tukiifatia, hatufiki mbali, wengi tunaganda,
Sio yetu nia, lakini akili, mali ishapenda,
Haki yatuponza!

6. Wala hutasemwa, sababu ni nyoyo, kwisha haribika,
Ya mali kuchumwa, vyovyote iwavyo, itavyopatika,
Wakati mtumwa, ushatumwa ndivyo, na ushatufika,
Kwetu ni mashaka!

7. Haki hufanyiki, papitapo mambo, na vikubwa visa,
Watu hawataki, kutenda kijambo, tunu yao pesa,
Sisi kwetu dhiki, yatunisha tumbo, wao hata hisa,
Nandio yasasa!

8. Haki husimami, kwa viumbe sisi, tuvyojaaliwa,
Na huna ulimi, kuweza tukisi, tukageukiwa,
Zama za uchumi, zishashika kasi, nguvu zishapewa,
Haki wauliwa!

9. Iwe hivi haki, hakuna mmoja, akukumbukae,
Hatuna ashiki, kuvuta la haja, haki ituvae,
Mbona hatutaki, twalia na tija, haki iambae,
Hakitamati!
Suleiman A. Ali: Malenga Wapya

(a) Eleza dhamira ya shairi hili. (alama 2)
(b) Huku ukitoa mfano, eleza aina ya shairi hili. (alama 3)
(c) Taja na ufafanue tamathali ya usemi inayotawala katika shairi hili. (alama 3)
(d) Kwa kutoa mfano mmoja mmoja, onyesha aina tatu za idhini ya kishairi
katika shairi hili. (alama 6)
(e) Andika ubeti wa saba kwa lugha ya nathari. (alama 4)
(f) Mshairi ana maana gani kwa kusema;
(i) Kambi yatuviza
(ii) Kuwezatukisi.
(alama 2)

SEHEMU D: HADITHI FUPI
K.W. WAMITILA: Mayai Waziri Wa Maradhi na Hadithi Nyinginezo
Jibu swali la 6 au la 7
6 "Cheche ndogo hufanya moto mkubwa,"
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
(b) Fafanua maudhui manne yanayohusiana na chanzo cha tukio linalorejelewa
katika dondoo hilo. (alama 8)
(c) Eleza matokeo manne ya tukio linalorejelewa katika dondoo. (alama 8)
7 "Mganga na wateja wake wote walikosa busara." Fafanua ukweli wa kauli hii kwa mifano kumi kutoka hadithi ya 'Siku ya Mganga.'
(alama 20)




SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI
(a) Eleza maana ya malumbano ya utani. (alama 2)
(b) Bainisha sifa nne za malumbano ya utani. (alama 8)
(c) Fafanua majukumu matano ya malumbano ya utani katika jamii. (alama 10)










More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers