Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Got a question or eager to learn? Discover limitless learning on WhatsApp now - Start Now!

Halmashauri Ya Mitihani Question Paper

Halmashauri Ya Mitihani 

Course:Kiswahili

Institution: Form 3 question papers

Exam Year:2006



1)USHAIRI
Jama, Jama, Jamani
Mbona twabebeshwa mateso hivi
Mizigo mikubwa ya dhiki kama
Kwamba hatuna Hamilton ya kusema
Kukataa ndoa zain lazima
Kukataa ndoa kwa lazima
Kukataa kuozwa wazee
Kukataa kukatishwa masomo
Kukataa tohara ya lazima

Jama,Jama,Jamani
Iweje tuteswe mateso haya
Na Waru wasio Kuwait hata na haya kama
Kwamba hatuna haki ya kulalamika
Kulalamika kutumishwa kama mayaya
Kulalamikia kudhalilishwa kiunyama
Kulalamikia kutolindwa na sheria

Jama, Jama,Jamani
Sasa hii ni awamu nyingine
Na macho tumeyafungua kabisa
Tumekataa kudhalilishwa kabisa
Tumekataa kuteswa kama watumwa
Tumekataa tohara ya lazima
Tumekataa kuozwa.....Tumekataa! Tumekataa
Hii awamu ya"Haki ya Kyoto wa kike "

Maswali

a)Taja mambo matatu yaliyozungimziwa na mshairi kisha ueleze kila moja
b)Eleza muundo wa shairi hili
c)Taja mbinu mbili za lugha alizotumia mshairi kisha ueleze kila moja
d)Kwa nini mshairi huyu anasema hii ni 'awamu' nyingine?
e)Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa na mshairi
i)awamu
ii)kudhalilishwa
iii)dhiki

TAMTHILI
KIFO KISIMANI
2."Nakubaliana nawe! Unazijua vizuri sana kanuni za ardhi. Na hapo ndipo pana tatizo,unazijua vyema lakini wakati huo huo uunazipuuza kama kwamba hazipo"
a)Liweke dondoo hili katika muktadha.
b)Eleza hulka za mzungumzaji wa maneno haya
c)Huku ukirejelea mzungumzaji onyesha jinsi maudhui ya ufisadi yanavyojitokeza katika tamthilia ya kifo kisimani
3.Jadili jinsi mwandishi wa Kifo Kisimani alivyofaulu katika matumizi ya mbinu ya Kinaya katika tamthilia take.

RIWAYA
MWISHO WA KOSA:Z.Burhani

4)Mwandishi wa Riwaya ya Mwisho wa Kosa amechora"Mwanamke" kama kielelezo bora change maadili katika kamikaze.Jadili.

5)"Nieleze hasa sababu ya kuumwaga uji wangu namma ile, ndipo nini? Ndipo mchafu kuunywa leo?"
a)Ni akina nani wanaorejelewa katika muktadha wa dondoo hili?
b)Weka dondoo hili katika muktadha wake.
c)Eleza kwa kina tabia za aliyemwaga uji.

HADITHI FUPI
MAYAI WAZIRI WA MARADHI NA HADITHI NYINGINE

6.Ngome ya nafsi -Na Clara Momanyi
a)Eleza kwa kina Masaibu yaliyomkumba Naseko
b)Je masaibu haya yanatokana na nini?fafanua
c)Naseko ni mtu wa arina gani? Eleza

FASIHI SIMULIZI
7.i )Eleza umuhlmu wa nyimbo katika usimulizi.
ii )Taja na kueleza aina za nyimbo.

b)SEMI
Tofautisha semi hizi

i)Nahau na misimu
ii)Eleza maana ya nahau hizi
a)Hawapikiki katika kichungi kimoja
b)Yeye ni jamboree la wageni
c)Amemwaga mtama
d)Amechomekwa mizizi






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers