Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Got a question or eager to learn? Discover limitless learning on WhatsApp now - Start Now!

Kcse 2010 Kiswahili Karatasi Ya 102/2 Question Paper

Kcse 2010 Kiswahili Karatasi Ya 102/2 

Course:Kiswahili

Institution: Kcse question papers

Exam Year:2010



1 UFAHAMU (alama 15)
Soma kifungu kifnatacho kisha ujibu maswali
Suala la mahusiano ya wanadamu katika jatnii, uainishaji wake na udhihirikaji wake limewashughulisha wataalamu wa elimu jamii kwa dahari ya miaka. Suala hili huwatafakarisha
wataalamu hao kutokana na umuhimu wake katika maisha ya binadamu. Msingi mkuu wa uainishaji wa mahusiano hayo ni kukichuza kipindi cha mahusiano yenyewe. Yapo mahusiano baina ya waja ambayo yanachukua muda mfupi, kwa mfano saa au dakika chache, na mengine ambayo huenda yakachukoa miaka ayami.
Mahusiano ya muda mrefu kabisa ni vale yanayojulikanakama mahusiano ya kudumu. Inamkinika kudai kuwa miundo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi huweza kuyadhibiti mahusiano hayo kwa kiasi kikubwa. Watu wengi huitakidi kuwa uhusiano uliopo baina ya mtu na jamaa yake utachukua muda mrefu, na kwa hiyo ni uhusiano wa kudumu. Hali hii hutokana na uhalisi kuwa tunahusiana na jamaa zetu kwa kipindi kirefu labda tangu ukembe hadi utu uzima wetu. Uhusiano him hautarajiwi kuvunjwa na umbali wa masafa baina yetu; tunaendelea kuwasiliana kwa barua au, katika enzi hii ya utandawazi, kwa kutumia nyenzo za teknohama kama mtandao na simu za mkononi, na kudumisha uhusiano wetu wa kijamaa. Hata hivyo, inawezekana baadhi ya mahusiano ya kijamaa yasiwe ya kudumu. Mathalan, uhusiano uliopo baina ya mke na mume, na ambao unatarajiwa kuwa wa kudumu au wa kipindi kirefu, unawcza kuvunjwa kwa kutokea kwa talaka. Talaka hiyo inavunja ule uwezekano wa uhusiano wa kudumu unaofumbatwa na sitiari ya pingu za maisha.
Katika ngazi ya pili, mahusiano ya kipindi cha wastani, kuna mahusiano yanayohusisha marafiki zetu maishani, shuleni au kwenye taasisi zozote zile, majirani zetu, wenzetu katika mwahali mwa kazi, washiriki kwenye sehemu za ibada au za burudani na wenzetu kwenye vyama tofauti na makundi ya kujitolea. Inawezekana kudahili kuwa baadhi ya mahusiano haya, hususan baina ya marafiki na majirani huweza kuwa ya miongo na daiina. Hali hii huweza kutegemea muundo na mfumo wa jamii. Kwa mfano, kwa wanajamii wanaoishi kwenye janibu fulani mahsusi, na kwa miaka tawili bila ya kuhajiri, uhusiano wao na majirani huweza kuwa wa kudumu. Hali hii inasigana na hali iliyoko kwenye maisha ya mijini. Maisha ya mijini yana sifa ya kubadilikabadilika. Isitoshe, kutokana na mfumo wa maisha ya kibepari yameghoshi ubinafsi mwingi. Mawimbi ya mabadiliko na ubinafsi huweza kuumomonyoa ukuta wa uhusiano wa kudumu.
Mwelekeo wa maisha ya siku hizi ya uhamaji kutoka maeneo au viambo walikoishi watu unasababisha kupombojea kwa mahusiano ya kudumu baina yao na majirani zao. Uhusiano kati ya wenza katika mazingira ya kazi unahusiana kwa kiasi fulani na ule wa majirani. Vimbunga vya ufutw aji kazi, ubadilishaji wa kazi, hali zisizotegemewa na mifumo ya kimataifa pamoja na hata mifumo ya kisiasa huweza kuathiri mshikamano wa wanaohusika kazini.
Kiwango cha mwisho cha mahusiano ni uhusiano wa rripito au wa muda mfupi. Mahusiano ya aina hii hujiri katika muktadha ambapo pana huduma fulani. Huduma hizi zinaweza kuwa za dukani, kwenye sehemu za ibada, kwenye kituo cha mafuta, kwa kinyozi, kwa msusi na kadhalika. Kuna sababu kadha zinazotufanya kuyazungumzia mahusiano ya aina hii kama ya mpito. Kwanza, uwezekano wa mabadiliko ya anayeitoa huduma hiyo ni mkubwa. Si ajabu kuwa unaporudi kwa kinyozi au msusi unatambua aliyekushughulikia hayupo. Hata hivyo, kuna vighairi hususa pale ambapo mtoa huduma anayehusika ni yule yule mmoja.
Mahusiano ya mpito yanatawaliwa na 'uhusiano wa chembe chembe.' Uhusiano wa chembe
chembe, bidhaa ya mfumo wa kibepari, unamaanisha kuwa kinachomshughulisha mtu ni chembe ndogo tu ya mwenzake. Chembe hiyo inaweza kuwa huduma, kwa mfano, gazeti analokuuzia mtu, viatu anavyokushonea, nguo anazokufulia, ususi anaokufanyia n.k. Mahusiano ya aina hii yametovukwa na hisia za utu na ni zao la mirumo ya kisasa ya kiuchumi na kijamii. Mtu anayehusiana na mwezake kwa misingi ya chembe ndogo tu, huenda asijali kama mwenzake amekosa chakula, amefutwa kazi, amefiliwa, ameibiwa na kadhalika.
Suala kuu tunalopaswa kujiuliza ni: je, tunahusiana vipi na jamaa zetu, taasisi zetu, maranki zetu na majirani zetu? Je, uhusiano wetu na raia wenzetu ni wa aina gani? Je, uhusiano wetu na nchi yetu ni wa mpito au ni wa kudumu?

(a) Taja kigezo muhimu cha kuzungumzia mahusiano. (alama 1)
(b) Eleza imani ya watu kuhusu uhusiano baina ya jamaa. (alama 1)
(c) Fafanua athari ya teknolojia kwenye mahusiano ya watu. (alama 2)
(d) Eleza sababu nne kuu za kuharibika kwa mahusiano katika maisha ya leo. (alama 4)
(e) Taja sifa kuu ya mahusiano ya muda mfupi. (alama 2)
(f) Je, kifungu, hiki kina ujumbe gani mkuu? (alama 2)
(g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika kifungu.

(i) inasigana
(ii) yameghoshi
(iii) vighairi






2. MUHTASARI (alama 15)
Jamii ya leo inatawaliwa na kuendeshwa na kanuni ya maarifa. Inawezekana kusema kuwa uchumi wa jamii za leo na zijazo utategemea maarifa zaidi kuliko utakavyotegemea wenzo wowote mwingine. Utambuzi wa uwezo mkubwa wa maarifa katika maisha ya binadamu ndio msingi wa watu kusema 'maarifa ni nguvu.'
Maarifahuelezwakwatamathali hii kutokananauwezo wa: kuyadhibiti, kuyaendesha, kuyatawala na kuyaongoza maisha ya binadamu popote pale walipo. Mtu ambaye ameyakosa maarifa fulani huwa ameikosa nguvu hiyo muhimu na maisha yake huathirika pakubwa. Kwa msingi huu, maarifa yanaweza kuangaliwa kama utajiri mkubwa ambao binadamu anaweza kuutumia kwa faida yake au kwa faida ya wanajamii wenzake. Ukweli huu ndio unaoelezwa na methali ya Kiswahili: 'Elimu ni mali.' Elimu ni chirnbuko la maarifa muhimu maishani.
Msingi wa utajiri na maendeleo ya binadamu popote alipo basi ni maarifa. Je, maarifa kwa upande wake yana sifa gani? Maarifa yenyewe hayana upinzani. Maarifa uliyo nayo huweza kuwa na watu wengine wengi pasiwe na upinzani baina yenu kwa kuwa kila mmoja ana maarifa sawa. Kila mmoja ana uhuru wa kuyatumia maarifa hayo kama chanzo cha kuyazalisha maarifa mengine. Utumiaji wa maarifa yenyewe hauyamalizi maarifa hayo. Maarifa hayawezi kugusika ingawa mtu anaweza kuyanyumbua maarifa yenyewe kwa kuyatumia kwa namna tofauti.
Maarifa huingiliana na maarifa mengine. Maarifa aliyo nayo mtu mmoja huweza kuhusishwa na maarifa aliyo nayo mtu mwingine ili kuvyaza au kuzuka na maarifa tofauti. Maarifa yanaweza kuchukuliwa kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa namna ambavyo mtu hawezi kufanya bidhaa nyingine ile. Kwa mfano, ni muhali mtu kulalamika kuwa hawezi kutembea kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa sababu ana mzigo mzito wa maarifa kichwani.
Sifa nyingine muhimu ya maarifa ni kuwa yanaweza kuwasilishwa kwa njia za ishara au mitindo mingine ya kidhahania. Ikiwa unataka kukihamisha chombo fulani kutoka sehemu moja hadi nyingine, lazima uwazie ukubwa wake, uzito wake na labda hata umbali wa panapohusika. Maarifa huweza kubadilishwa au kugeuzwa na kuwa ishara ambazo huyafanya kuwasilishwa kwa njia nyepesi kuliko kwa mfano ikiwa mtu atayawasilisha katika muundo wa, kwa mfano, kitabu.
Maarifa yana sifa ya uhusianaji. Kipengele fulani cha maarifa huwa na maana kinapowekwa
sambamba au kugotanishwa na kipengele kingine cha maarifa. Huo huwa muktadha mzuri wa kueleweka au kuwa na maana. Kwa mfano, neno 'mwerevu' huweza kuwa na maana kwa kuwekwa katika muktadha wa 'mjinga', 'mjanja', 'hodari' na kadhalika.
Maarifa huweza kuhifadhiwa katika nafasi ndogo sana. Suala hili linaeleweka kwa njia nyepesi tunapoangalia maarifa katika muktadha wa teknolojia. Data zinazowahusu mamilioni ya watu, ambazo zingehitaji maelfu ya maktaba na lukuki ya vitabu, huweza kuhifadhiwa kwenye kifaa kidogo kinachoweza kutiwa mfukoni.
Maarifa hayawezi kudhibitiwa au kuzuiliwa mahali fulani yasisambae. Maarifa huenea haraka sana. Maarifa ni kitu kinachoepuka pingu za watu wanaopenda kuwadhibiti binadamu wenzao. Hata pale ambapo mfumo wa kijamii au wa kisiasa unafanya juu chini kuwadhibiti raia au watu wenyewe, ni muhali kuyadhibiti maarifa yenyewe. Inawezekana kuzidhibiti njia fulani za ueneaji wa maarifa lakini maarifa hayo yatapata upenyu wa kusambaa. Ni kweli kuwa maarifa ni nguvu inayozishinda nguvu zote.

(a) Fupisha aya ya pili na ya tatu. (maneno 55 - 60) (alama 5, 1 ya utiririko)

Matayarisho


Nakala safi

(b) Eleza sifa kuu za maarifa kama zinavyojitokeza kuanzia aya ya nne hadi aya ya nane. (maneno 100 - 110). (alama 10, 2 za utiririko)

Matayarisho


Nakala safi
3. MATUMIZI YA LUGHA (alama 40)
(a) Toa mfano wa neno lenye muundo wa silabi ya irabu pekee (alama 1)
(b) Eleza maana mbili zaneno: Barabara. (alama 2)
(c) Sahihisha sentensi:
Abiria walisafiri na ndege. (alama 1)
(d) Tambua na ueleze aina za vivumishi katika sentensi:
Mwanafunzi mkongwe amepewa tuzo kwa kuwa hodari masomoni. (alama 4)
(e) Andika sentensi ifuatayo katika hali yakinishi.
Usingeacha masomo, usingetaabika vile. (alama 2)
(f) Tunga sentensi ukitumia kielezi cha:
(i) Jumla . (alama 1)
(ii) Namna linganisho . (alama 1)

g) Ainisha shaminsho na chagizo katika sentensi: Vibarua wamefanya kazi haraka ipasavyo.
Vibarua wamefanya kazi haraka ipasavyo. (alama 2)
(h) Eleza maana mbili zinazopatikana katika sentensi: Nenda ukaniletee mbuzi. (alama 2)
(i) Tunga sentensi kudhihirisha matumizi ya ngeli ya U-U. (alama 2)
(J) Andika katika usemi wa taarifa.
"Mito yetu imechafuka sana; itabidi tuungane mikono wakubwa kwa wadogo, wanaume kwa wanawake ili tuisafishe." Mwanamazingira alituhimiza. (alama 3)
(k) Changanua sentensi ifuatayo ukitumia mistari au mishale.
Amina na Mustafa huimba taarabu. (alama 4)
(1) Eleza matumizi ya ku katika sentensi:
Sikumwelewa alivyoeleza namna ya kuwatunza mbwa wake. (alama 2)
(m) Tunga sentensi sahihi ukitumia kitenzi la katika kauli ya kutendwa. (alama 2)

(n) Eleza kazi ya kila kitenzi katika sentensi:
Mkulima angetaka kupalilia shamba lake mapema. (alama 4)
(o) Taja na utofautishe vipasuo vya ufizi.
(p) Onyesha jinsi moja moja ya matumizi ya viwakifishi vifuatavyo:- (alama 3)
(i) nusu koloni(;)
(ii) herufi kubwa
(iii) Kishangao(!)

4 ISIMUJAMH (alama 10)
"Benki yenyewe haina kitu ... CD4 count yake iko chini ... Ni emergency ... Tutampoteza ikikosekana."
(a) Taja sajili inayorejelewa na manerio haya. (alama 2)
(b) Fafanua sifa nne zinazohusishwa na sajili hiyo. (alama 8)





















More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers