Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.
Got a question or eager to learn? Discover limitless learning on WhatsApp now - Start Now!

Lau dunia nanena, tuseme si ati ati, Mauti kawa hakuna, katika wote wakati, Vipi tungelisongana, tunaoishi tiati? Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana? Dunia ingetatana, na kizazi katikati, Huku kwazaliwa bwana,...

      

Lau dunia nanena, tuseme si ati ati,
Mauti kawa hakuna, katika wote wakati,
Vipi tungelisongana, tunaoishi tiati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

Dunia ingetatana, na kizazi katikati,
Huku kwazaliwa bwana, kule kwazawa binti,
Vipi tungelioana, na kuzaa hatuwati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

Lau mauti hakuna, tungesongana sharuti,
Kwa viumbe kukazana, wanadamu na manyati,
Vipi tungelijazana, kwa kusitawi umati?

Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Walakini Subuhana, kapanga sisi na miti,
Ili tusizidi sana, si wengi na si katiti
Maisha ya kupishana, yule ende yule keti,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

Ndipo dunia kufana, ikawa kama yakuti,
Kwa uwezowe Rabana, kaipanga madhubuti,
Maisha kugawiana, kayagawa kwa mauti,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

Njia ingekuwa hapana, pembeni na katikati,
Sote tungeambatana, kama ukosi na shati,
Na njaa ingetutafuna, pa kulima hatupati,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

Peleleza utaona, hayataki utafiti,
Kama tungelikongana, ingekuwa ni bahati,
Vipi tungesukumana, katika hiyo hayati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

Mbele sitokwenda tena, hapa mwisho nasukuti,
Yaoleni waungwana, shauri yake Jabaruti,
Yote tuloelezana, katenda bila senti,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
(Abdalla Said Kizere)


Maswali
a) Pendekeza anwani mwafaka la shairi hili.
b) Je, hili ni shairi la bahari gani? Eleza
c) Eleza vile mwandishi alivyotumia uhuru wa kishairi.
d) Eleza umbo la shairi hili.
e) Fafanua ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa tano.
f) Andika majina mawili ya Mungu kwa mujibu wa shairi.
g) Kwa kutolea mifano, eleza mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika shairi hili

  

Answers


Francis
Najibu
a) Pendekeza anwani mwafaka la shairi hili.
LAU HAKUNA MAUTI

b) Je, hili ni shairi la bahari gani? Eleza
? Mtiririko – vina vya kati vinafanana na vya mwisho pia vinafanana katika shairi lote
Vya kati vya mwisho
na, ti,
na, ti,
na, ti,
ti, na.
? Mathnawi – lina vipande viwili – utao na ukwapi

c) Eleza vile mwandishi alivyotumia uhuru wa kishairi.
(i) Inkisari -kwazawa, ngekuwa, ngetutafuna, nanena, sitokwenda
(ii) Tabdila – Sharuti badala ya sharti
(iii) Kuboronga sarufi – mauti kawa hakuna – ikiwa hakuna mauti,
– katika wote wakati – katika wakati wote
(iv) Lahaja (ya kimvita) – hatuwati (hatuwachi)
– yaoleni (yaoneni)

d) Eleza umbo la shairi hili.
(i) Beti 8
(ii) Mishororo 4 katika kila ubeti
(iii) mizani 16 katika kila mshororo
(iv) vina vya kati vya mwisho
na, ti,
na, ti,
na, ti,
ti, na.
(v) vipande viwili – utao na ukwapi
(vi) Lina kibwagizo “lau hakuna mauti, vipi tungelisongeni?”

e) Fafanua ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa tano.
? Dunia haiwezi kujaa watu kupita kiasi
? Mwenyezi Mungu anajua kupanga
? Baadhi ya watu wafe na baadhi wazaliwe
? Bila kifo tungesongamana/jaa sana

f) Andika majina mawili ya Mungu kwa mujibu wa shairi.
? Subuhana
? Rabana
? Jabaruti

g) Kwa kutolea mifano, eleza mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika shairi hili
? Balagha - k.v Vipi tungelisongana, tunaoishi tiati?
? Tashbihi - ikawa kama ya kuti - Kama ukosi na shati
? Takriri - si ati ati
? - Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
francis1897 answered the question on February 1, 2023 at 09:03


Next: Eleza mambo yanayozingatiwa katika uhuru wa kishairi
Previous: Kilio cha Lugha Ni wimbo najiimbia,nijiliwaze Sina wa kusaidia, nasongwa sina nafasi Kiwa kwetu naumia, kwengine si mahususi Lugha ya mtu mweusi, Kiswahili chalilia Wataalamu ni nani, mulipo mwaninyanyasa Hamna nami...

View More Ushairi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions