Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.
Got a question or eager to learn? Discover limitless learning on WhatsApp now - Start Now!

Kilio cha Lugha Ni wimbo najiimbia,nijiliwaze Sina wa kusaidia, nasongwa sina nafasi Kiwa kwetu naumia, kwengine si mahususi Lugha ya mtu mweusi, Kiswahili chalilia Wataalamu ni nani, mulipo mwaninyanyasa Hamna nami...

      

Kilio cha Lugha
Ni wimbo najiimbia,nijiliwaze
Sina wa kusaidia, nasongwa sina nafasi
Kiwa kwetu naumia, kwengine si mahususi
Lugha ya mtu mweusi, Kiswahili chalilia

Wataalamu ni nani, mulipo mwaninyanyasa
Hamna nami imani, wala kupanga siasa
Mwasema sayansini, siku ningalitosa
Mwanambia nikotosa, kuiva sijafika

Ela muelewe sana, Maamuma na Imamu
Mulipokuwa vijana, kwenu nilikuwa timamu
Sasa mumesoma sana, mwaniona ni haramu
Mujue kuwa dawamu, utumwa mwauridhia.

Mzaliwapo mwalia, ‘maa’, maneno ya kwanza
Lugha munayokulia, ya mama zetu ya kwanza
Wa lugha muwedoria, muweze na kuikuza
Sio kujipendekeza, uzungu kuigiza.

Majira ya ukoloni, ukombozi kusambaza
Lugha mulithamini, Kiswahili kufukiza
Hata kule risavuni, kizungu hanikuwaza
Sasa mbona mwanibeza, mbali mwanitupilia?

Sayansi sio asili, msamiatiwe sinao
Sayansi yataka mbali, msamiati ni wa hao
Nitakuwa Kiswahili, kiomba majina yao
Lugha kujikuza kwao, huomba linalofaa.

Enyi viongozi wetu, ipangeni nadharia
Kujenga siasa yetu, tuzidi kuwa huria
Lugha hata ‘mbusha watu, tuche kuriaria
Sifa ni kwa chake mtu, cha mwenzi hutoringia

Utajiri wangu hasa, nikiwatajia wote
Msamiati huwa, ni wa Afrika yote
Na methali za kuasa, nahau na ngeli zote
Na nisemwapo popote, ujumbe hukamilika.

Afrika ndipo petu, pa wabantu halisi
Baba na mama ni Bantu, shina la wangu ukwasi
Warabu na wengi wetu, sio wangu Adinasi
Kwao ‘meomba kiasi, ili kujizidisha

Mfumo mpya hongera, wa elimu humu Kenya
Lugha takuwa imara, ukabila tutafinya
Kiswahili ni ibara, kila mtu kiimanya
Methali imetuonya, mtumwa si mwasilia.

Tamati lugha yalia, yabaguliwa bayana
Kukua imeridhia, msamiati kufana
Wengine wataijulia, kwa marefu na mapana
Lugha yetu ya maana, mwaipuuza yalia.


Maswali
(a) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu
(b) Kwa kutoa hoja nne, eleza kwa nini shairi hililikaitwa kilio cha lugha.
(c) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari.
(d) Eleza toni ya shairi hili.
(e) Tambua uhuru wa kishairi uliotumiwa kwa kurejelea mifano mitatu.
(f) Bainisha nafsineni katika shairi.
(g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kwa mujibu wa shairi.
i. nasongwa
ii. kuriaria
iii. adinasi

  

Answers


Francis
(a) Tarbia- mishororo minne katika kila ubeti

(b)
? Maimamu kuidharau lugha
? Wengi wanaigiza kizungu kuliko Kiswahili
? Kiswahili kutupwa baada ya uhuru
? Kuwa na upungufu wa msamiati
? Msamiati umeombwa ili kuikuza lugha

(c) Yafaa kuelewa Imamu na Maamuma walipokuwa vijana Kiswahili kilikuwa sawa. Baada ya kupata elimu wanakidharau na huo ni kuwa mtumwa.
AU
Kila mmoja aelewe, mlipokuwa vijana mlikitumia Kiswahili. Baada ya kusoma, mmeanza kukidharau, na kwa kufanya hivi, mnafurahia utumwa.

(d) Toni ya huzuni/uchungu- kuhuzunishwa na dharau

(e)
? Inkisari- msamiatiwe
? Utohozi- risavuni
? Mazida- Huria
? Tabdila- maa- mama
? Kilugha/lahaja- kiimanya

(f) Nafsineni ni mwanalugha/mtetezi/mkereketwa wa lugha

(g)
(i) nasongwa- nasumbuliwa/dhulumu/sikitika/nabanwa
(ii) kuriaria- kuzurura/kurandaranda
(iii) adinasi- binadamu/insi/mahuluki
francis1897 answered the question on February 1, 2023 at 09:13


Next: Lau dunia nanena, tuseme si ati ati, Mauti kawa hakuna, katika wote wakati, Vipi tungelisongana, tunaoishi tiati? Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana? Dunia ingetatana, na kizazi katikati, Huku kwazaliwa bwana,...
Previous: Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali T. Arege: Barabara Barabara bado ni ndefu Nami tayari nimechoka tiki Natamani kuketi Ninyooshe misuli Nituliza akili Lakini Azma yanisukuma Mbele ikinihimiza kuendelea Baada ya miinuko na kuruba Sasa naona...

View More Ushairi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions