Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.
Got a question or eager to learn? Discover limitless learning on WhatsApp now - Start Now!

Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata. WASAKATONGE 1. Wasakatonge na juakali Wabeba zege ya maroshani, Ni msukuma mikokoteni, Pia makuli bandarini, Ni wachimbaji wa migodini, Lakini...

      

Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata.
WASAKATONGE
1. Wasakatonge na juakali
Wabeba zege ya maroshani,
Ni msukuma mikokoteni,
Pia makuli bandarini,
Ni wachimbaji wa migodini,
Lakini maisha yao chini
2. Juakali na wasakatonge
Wao ni manamba mashambani,
Ni wachapa kazi viwandani,
Mayaya na madobi wa nyumbani,
Ni matopasi wa majaani,
Lakini bado ni masikini.
3. Wasakatonge na juakali
Wao huweka serikalini,
Wanasiasa madarakani,
Dola ikawa mikononi,
Wachaguliwa na ikuluni,
Lakini wachaguaji duni
4. Juakali na wasakatonge
Wao ni wengi ulimwenguni,
Tabaka lisilo ahueni.
Siku zote wako matesoni,
Ziada ya pato hawaoni,
Lakini watakomboka lini?
(Mohammed Seif Khatib)

(a) “Shairi hili ni la kukatisha tamaa”. Fafanua rai hii kwa kutoa mifano minne.
(b) Taja tamathali ya usemi iliyotawala katika shairi zima na uonyeshe mifano miwili ya jinsi iiivyotumika.
(c) Eleza umbo la shairi hili.
(d) Andika ubeti wa tatu katika lugha ya nathari.
(e) Onyesha mifano miwili ya maadiii yanayojitokeza katika shairi hili.
(f) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi.
(i) Manamba
(ii) Tabaka lisilo ahueni

  

Answers


Francis
Wasakatonge
a)
? Wanajamii wanajishughulisha katika kazi mbalimbali ili kuboresha maisha yao lakini maisha yao ni duni.
? Vibarua (manamba, wachapakazi, mayaya, madobi, matopasi) wanaoajiriwa wanafanya kazi kwa bidii lakini mishahara yao ni duni.
? Viongozi serikalini wamepewa nyadhifa hizo za hadhi lakini hawajibiki kunyanyua hali za waliowachagua
? Tabaka la chini ndio walio wengi katika jamii na ndio tegemeo la jamii lakini wanaishi maisha ya mateso mengi.
? Haijulikani mateso ya walio wengi yatafika kikomo lini

b)
? Kinaya
i) Wasakatonge ndio wengi lakini hawana sauti
ii) Makuli, mayaya, matopasi, wachapakazi nk ni maskini
iii) Wasakatonge wafanyao kazi kwa mateso mishahara yao ni duni
iv) Wapelekao watu serikalini hawashughulikiwi na walowachagua
v) Wazalishao mali hawana chochote bado ni maskini ( manamba, ma- dobi, mayaya, wachapakazi)
? Taswira
i) Wabeba zenge ya marashani
ii) Wasukuma mkokoteni
iii) Makuli bandarini
iv) Wachimbaji migodini
v) Manamba mashambani
vi) Wachapakazi viwandani
vii) Matopasi wa majaani
viii) Wanasiasa madarakani
ix) Mayaya na madobi wa nyumbani (siku zote wako matesoni)
? Takriri
i) wasakatonge
ii) Juakali
iii) Lakini
iv) Wao
v) Ni
? Ulingunuzi/ulinganushi
- wachimbaji migodini lakini maisha-yao ni ya chini
- wachapakazi viwandani lakini maskini

c)
? Kipande kimoja
? Shairi lina kituo/kimalizio
? Mizani hailingani katika kila ubeti
? Beti 4
? Mishororo 6 kila ubeti/ tasdisa / usita au kila uneti una kichwa au kijichwa / anwani na kila ubeti una mishororo mitano
? Mshororo wa kwanza vina vinabadilika (li na – nge)
? Mishororo mitano ina vina vinavyofanana (ni)
? Mishororo wa kwanza katika kila ubeti unapindapinda (pindu)
? Neno lakini limetumiwa mwanzo wa kila kituo- kikwamba

d) Watu wa tabaka la chini/ndio huwapa nyadhifa viongozi/ kutolana na nyandhifa hizo viongozi hupata mali au uwezo wa kiuchumi/ wale waliowachagua maisha yao ni ya kusikitisha.

e)
? Kufanya kazi kwa bidii
? Kuwajibika – kwa umma katika kushiriki kuwachagua viongozi
? Viongozi wanastahili kuadilika kwa kunyanyua hali za umma na kujali hali ya wafanyikazi

f)
? Manamba- vibarua, wafanyikazi
? Tabaka lilisilo ahueni – watu maskini/wasio na hali nzuri kiuchumi/walalahoi
francis1897 answered the question on February 1, 2023 at 12:26


Next: Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata: Kila Mchimba Kisima Musa Mzenga 1. Tenda utendapo tendo, tenda tendo kwa hekima, Lindamane mwenendo, sawa na yakio kalmia, Kalmia yenye upendo, kufurahisha...
Previous: “Huyu ambaye mama alimwona kuwa gae, kumbe sasa ndiye chombo cha kunivisha bahari hii ya dhiki?” (Chozi la Heri)(a) Weka dondoo hili katika muktadha...

View More Ushairi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata: Kila Mchimba Kisima Musa Mzenga 1. Tenda utendapo tendo, tenda tendo kwa hekima, Lindamane mwenendo, sawa na yakio kalmia, Kalmia yenye upendo, kufurahisha...(Solved)

    Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata:
    Kila Mchimba Kisima
    Musa Mzenga
    1. Tenda utendapo tendo, tenda tendo kwa hekima,
    Lindamane mwenendo, sawa na yakio kalmia,
    Kalmia yenye upendo, kufurahisha mtima,
    Kila mchimba kisima, budi hungia mwenyewe.
    2. Utendapo la faraja, tendo ni yako salama,
    Ya kukupa kila tija, na ushindi wa daima,
    Upate njema daraja, duniani na kiyama,
    Kila mchimba kisima, budi hungia mwenyewe.
    3. Utendapo la miuja, tendo ni yako nakama
    Ya kukutia harija, hasara kukuandama,
    Usione afuwaja, mwanza ajue heshima,
    Kila mchimba kisima, budi hungia mwenyewe
    4. Nakwambia uelewe, pulika ninayosema,
    Si ari ya mwenginewe, kumuonya kwa lazima,
    Mtu hufunza mwanawe, Kwanza ajue heshima,
    Kila mchimba kisima, budi hungia mwenyewe.
    5. Nisipokwambia wewe, kukufunza kila jema,
    Kusudi nikuongowe, uepukwe na tujuma,
    Matusi ndimi nipawe, ila na kila lawama,
    Kila mchimba kisima, bundi hungia mwenyewe
    6. Hii si heri ujuwe, matusi kuigandama,
    Hadhi usiniuzuwe, hamithilishwa na nyama,
    Fikiri moyo utuwe, nikupapo taaluma
    Kila mchimba kisima, budi hungia mwenyewe.
    7. shika tena utambuwe, wasia huu ni mwema
    Matendo usipunguwe, mazuri kutenda hima,
    Yatende ubarikiwe, upawe na taadhima
    Kila mchimba kisima, budi hungia mwenyewe.
    8. Yakupasa uchunguwe, kila jambo kulipima
    Upime ufafanuwe, mambo yote kwa alama
    La kuwaka ulijuwe, pia lipi la kuzima,
    Kila mchimba kisima hungia mwenyewe.

    a) Eleza maudhui ya shairi hili.
    b) Ujumbe unaowasilishwa katika shairi hili una hadhira lengwa tatu. Zitaje na utoe mifano.
    c) Eleza umuhimu wa kipokeo kinachotumiwa katika shairi hili

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Soma shairi kisha ujibu maswali yanayofuata: KIBARUWA: Abdilatif Abdalla Kwenye shamba hilo kubwa asilani hakunyi mvuwa! Ni kwa mitilizi ya jasho langu ndiyo hunweshezewa Kwenye shamba hilo kubwa sasa...(Solved)

    Soma shairi kisha ujibu maswali yanayofuata:
    KIBARUWA: Abdilatif Abdalla

    Kwenye shamba hilo kubwa asilani hakunyi mvuwa!
    Ni kwa mitilizi ya jasho langu ndiyo hunweshezewa
    Kwenye shamba hilo kubwa sasa imeshaiva kahawa
    Na bunize ni matone ya damu yangu niliyotowa
    Ndipo mte ukatipuza!

    Buni hiyo itakaangwa buni hiyo itapondwapondwa
    Buni hiyo itasagwa na buni hiyo itafyondwafyondwa
    Bali itabaki nyeusi kama ngozi yangu Kibaruwa

    Waulize ndege kwa nyimbo nyanana watutumbuizao
    Iulize na mito kwa furaha maji itiririkao
    Uulize na upepo mkali kwa ghadhabu uvumao-.

    Viulize: Ni nani araukaye na mapema kuzitema mbuga na kuzilaza?
    Viulize: Ni nani akweaye minazi tangu kuchapo hadi lingiapo giza?
    Viulize: Ni nani abebeshwaye mizigo hadi maungo yakageuka shaza?
    Halfuye hana faida moja apatay wala malipo yanayotoshelezaIsipokuwa kusundugwa na kutupiwa matambara na vyakula viliyooza?
    Viulize: Ni nani huyo ni nani!

    Viulize: Ni nani aliyemaye mashamba na kuyapoliliya?
    Na mimea kochokocho ikajaa kwa uzito ikajinamiya?
    Hatimaye nani atajirikaye mali yakammiminikiya
    Akatoa na kitambi kama mja mzito wa miezi tisiya
    Na akaongeza magari na wanawake kutoka na kuingiya?
    Viulize: Ni nani huyo nani1

    Na hao ndege kwa nyimbo nyanana watutumbuizao
    Nayo hiyo mito kwa furaha maji itirikao
    Na huo upepo mkali wenye ghadhabu uvumao
    Vyote hivyo vitatu vitakujibu kawa umoja wao
    “Ni Kibaruwa Manamba ndiye mtendaji hayo!”

    a) Eleza dhamira ya shairi hili.
    b) Kwa kutoa mifano, eleza aina mbili za idhini ya kishairi alizotumia mshairi
    c) kwa kurejelea ubeti wa tatu taja na ueleze tamathali ya usemi na mbinu ya kimuundo mshairi
    d) Huku ukitoa mifano, eleza kwa kifupi mwelekeo wa mshairi kuhusu vibarua.
    e) Andika ubeti wa tano katika lugha ya nathari
    f) Onyesha utata wa maana katika matumizi ya Kibaruwa Manamba

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata. Dhamiri yangu Dhamiri imenifunga shingoni. Nami kama mbuzi nimefungwa Kwenye mti wa utu. Kamba ni fupi Na nimekwishachora duara. Majani niwezayo kufikia yote nimekula. Ninaona...(Solved)

    Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata.
    Dhamiri yangu
    Dhamiri imenifunga shingoni.
    Nami kama mbuzi nimefungwa
    Kwenye mti wa utu. Kamba ni fupi
    Na nimekwishachora duara.
    Majani niwezayo kufikia yote nimekula.
    Ninaona majani mengi mbele yangu
    Lakini siwezi kuyafikia: kamba, kamba.

    Oh! Nimefungwa kama mbwa.
    Nami kwa mbaya bahati, katika
    Uhuru kupigania, sahani ya mbingu
    Nimeipiga teke na niigusapo kwa mdomo
    Mbali zaidi inakwenda na siwezi tena
    Kuifikia na hapa nilipofungwa
    Nimekwishapachafua na kuhama siwezi.

    Kamba isiyoonekana haikatiki.
    Nami sasa sitaki ikatike, maana,
    Mbuzi wa kamba alipofunguliwa, mashamba
    Aliharibu na mbwa aliuma watu.
    Ninamshukuru aliyenifunga hapa
    Lakini lazima nitamke kwa nguvu
    “Hapa nilipo sina uhuru!”
    (E. Kezilahabi)

    (a) Taja mambo manne ambayo mshairi analalamikia.
    (b) Kwa nini mshairi haoni haja ya yeye kuwa huru?
    (c) Eleza rnaana ya mshororo ufuatao kama ulivyotumiwa katika shairi. “Kamba isiyoonekana haikatiki.”
    (d) Taja na utoe mifano ya aina mbili za tamathali zilizotumika katika shairi hili.
    (e) Kwa kutoa mifano miwili, eleza jinsi matumizi ya mishata yanavyojitokeza katika shairi hili.
    (f) Andika ubeti wa pili kwa lugha nathari.

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • HAKI 1. Haki watutisha, tusikuandame, kwa matendo yetu, Watukorofisha, tusikuandame, kila penye kitu, Mbona watugwisha, miba ituchome kwenye huu mwitu, Tutokwe na utu! 2. Hatutakufanya, mwana kwa...(Solved)

    HAKI
    1. Haki watutisha, tusikuandame, kwa matendo yetu,
    Watukorofisha, tusikuandame, kila penye kitu,
    Mbona watugwisha, miba ituchome kwenye huu mwitu,
    Tutokwe na utu!
    2. Hatutakufanya, mwana kwa mvyele; aliyemzaa,
    Haki watunyima, machumi ya mbele, na nyingi hadaa,
    Tuchumayo nyanya, uchungu umbele, hatuna wasaa,
    Haki twashangaa!
    3. Na kambi nzima, kunaiyenea, hasa hapa petu,
    Tunakutazama, kwa kuulizia, kuweza thubutu,
    Na kwenye milima, ilotueka, kupandia watu,
    Usifanyekatu!
    4. Sio hao mabwana, waloteuliwa, kupata mwangaza,
    Haki wakubana, lilotarajiwa, kwenye hichi kiza,
    Ndevu kuchomana, wengine kuliwa, tukijiingiza,
    Kambi yatuviza!
    5. Haki buna njia, kizuizi mali, ndio njia panda,
    Tukiifatia, hatufiki mbali, wengi tunaganda,
    Sio yetu nia, lakini akili, mali ishapenda,
    Haki yatuponza!
    6. Wala hutasemwa, sababu ni nyoyo, kwisha haribika,
    Ya mali kuchumwa, vyovyote iwavyo, itavyopatika,
    Wakati mtumwa, ushatumwa ndivyo, na ushatufika,
    Kwetu nimashaka!
    7. Haki hufanyiki, papitapo mambo, na vikubwa visa,
    Watu hawataki, kutenda kijambo, tunu yao pesa,
    Sisi kwetu dhiki, yatunisha tumbo, wao hata hisa,
    Nandio ya sasa!
    8. Haki husimami, kwa viumbe sisi, tuvyojaaliwa,
    Na huna ulimi, kuweza tukisi, tukageukiwa,
    Zama za uchumi, zishashika kasi, nguvu zishapewa,
    Haki wauliwa!
    9. Iwe hivi haki, hakuna mmoja, akukumbukae,
    Hatuna ashiki,kuvutalahaja,haki ituvae,
    Mbona hatutaki, twalia na tija, haki iambae,
    Haki tamati!
    (Suleiman A. Ali) Malenga Wapya

    (a) Eleza dhamira ya shairi hili.
    (b) Huku ukitoa mfano, eleza aina ya shairi hili.
    (c) Taja na ufafanue tamathali ya usemi inayotawala katika shairi hili.
    (d) Kwa kutoa mfano mmoja mmoja, onyesha aina tatu za idhini ya kishairi katika shairi hili.
    (e) Andika ubeti wa saba kwa lugha ya nathari.
    (f) Mshairi ana maana gani kwa kusema:
    (i) Kambi yatuviza
    (ii) Kuweza tukisi.

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Capture.JPG (a) Mtunzi wa shairi hili ana dhamira gani? (b) Shairi hili ni la aina gani? Toa...(Solved)

    Capture.JPG


    (a) Mtunzi wa shairi hili ana dhamira gani?
    (b) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu moja.
    (c) Eleza mambo matatu ambayo mshairi anashauri nchi ifanye ili kujitegemea.
    (d) Taja aina moja ya idhini ya kishairi iliyojitokeza kwa wingi zaidi katika shairi na utoe mifano mitano ya matumizi yake.
    (e) Andika ubeti wa pili kwa lugha ya nathari.
    (f) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi:
    (i) Ghaibu
    (ii) Tukamshabihi.

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali 1. Huno wakati mufti, vijana nawausia, Msije juta laity, mkamba sikuwambia, Si hayatti si mamati, vijana hino dunia, Uonapo vyang’aria,...(Solved)

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
    1. Huno wakati mufti, vijana nawausia,
    Msije juta laity, mkamba sikuwambia,
    Si hayatti si mamati, vijana hino dunia,
    Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.

    2. Japo aula kushufu, na machoni vyavutia,
    Dunia wana dhaifu, waugua nisikia,
    Vijana nawasarifu, falau mkisikia,
    Ukiona vyang’aria, tahadhari vitakula.

    3. Jepusheni na zinaa, mlale penye sheria,
    Msije andama baa, makaa kujipalia,
    Jepusheni na zinaa, madhara kukadiria,
    Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.

    4. Ngawa waone wazuri, nadhifu kukuvalia,
    Wajimwaie uturin na mapoda kumichia,
    Si mlango nyumba nzuri, ngia ndani shuhudia,
    Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.

    5. Wawapi leo madume, anasa walopapia?
    Wamepita ja umeme, leo yao sitoria,
    Shime enyi wana shime, bora kumcha Jalia,
    Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.

    6. Nambie faida gani, nambie ipi fidi?
    Upatayo hatimani, waja wakikufukia,
    Ilakufa kama nyani, kasoroyako mkia,
    Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.

    7. Kikiki ikaze kamba, u kijana vumilia,
    Ujifanye kama kwamba, u jiwe huna hisia,
    Wakwambe watalokwamba, kwa lolote vumilia,
    Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.

    8. Vyatiririka tiriri, vina vyanikubalia,
    Alo bora mshairi,pa tamu humalizia,
    Nahitimisha shairi, dua ninawapigia,
    Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.

    9. Ewe Mola mtukuka, si shaka wanisikia,
    Wakinge wanarika, na anasa za dunia,
    Amina wangu Rabuka, dua yangu naishia,
    Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.
    (Mwalaa M.Nyanje)


    (a) Eleza ujumbe wa shairi hili.
    (b) Fafanua kwa kutoa mifano, mbinu nne alizotumia mshairi kutosheleza mahitaji ya kiarudhi katika shairi hili.
    (c) Nafsineni (mzungumzaji) katika shairi hili inasema na pande mbili. Zieleze pande hizo.
    (d) Eleza umuhimu wa maswali ya balagha katika shairi hili.
    (e) Bainisha toni ya shairi hili.

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. Sinongi aushi yangu, hii leo, kwa ukungu wa ujana, Nikaiga rika langu, kwa vileo, na mbio za wsichana, Kiwa ni riziki yangu,...(Solved)

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

    Sinongi aushi yangu, hii leo, kwa ukungu wa ujana,
    Nikaiga rika langu, kwa vileo, na mbio za wsichana,
    Kiwa ni riziki yangu, mapokeo, kuoa na kuona,
    Ni wakati utanena.

    Nashukuru kwa ugumba, wenye ndimi, wanipazao nao,
    Wapitao wakiimba, eti mimi, ningapenda hali zao,
    Haupandiki mgomba, wana nyemi, fisadi wa hadhi zao,
    Eti ni kwa raha zao.

    Ni lipi lenye kukera, kwa Muumbi, marufuku kwenye misa,
    Ni mtu kuwa hawara, wa vitimbi, ama alozawa tasa?
    Ugumba na ukapera, sio dhambi, wala haujawa kosa,
    Waama sina makosa

    Bora tungeni vitabu, magazeti, mutangaze kwa rediyo,
    Muwaite watribu, kina Siti, watuzwa ilimu hiyo,
    Na zaidi muhutubu, kwa umati, muwambe ambayo siyo,
    Kwalo sichafuki moyo

    Hidhuru yote ni bure, sio kitu, kudhiki asodhikika,
    Siwi nikaona ghere, lailatu, nyota njema itafika,
    Kwa shangwe na njerejere, kila mtu, mdomo utafumuka,
    Akiri amejibika.
    (Mwalaa M. Nyanje)


    (a) Eleza jambo ambalo mzungumzaji (nafsineni) katika shairi hili anasingiziwa.
    (b) Fafanua mambo matano ambayo mzungumzaji (nafsineni) anapinga katika shairi hili.
    (c) Eleza umuhimu wa viishio vya beti za shairi hili.
    (d) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari.
    (e) Eleza muundo wa shairi hili.
    (f) Bainisha matumizi mawili ya tafsida katika shairi hili.

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. T. Arege: Watafuta Riziki 1. Watafuta riziki, watatokwa jasho vijijini Wakulima shakiki, wakuza chai na mibuni Vyakula washakiki, visipungue vinyuani. 2. Watafuta riziki, wahaingaikao...(Solved)

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
    T. Arege: Watafuta Riziki
    1. Watafuta riziki, watatokwa jasho vijijini
    Wakulima shakiki, wakuza chai na mibuni
    Vyakula washakiki, visipungue vinyuani.

    2. Watafuta riziki, wahaingaikao mijini
    Kutwa kile na hiki, kama watanga na mipini
    Japo hawasikii, hawakosi kujiamini

    3. Watafuta riziki, wazalendo wa nchi hii
    Kamwe hawajidhiki, tama za moyo kutii
    Bali huafiki, kupingana na ulaghai

    4. Watafuta riziki, pato ambalo la halali
    Ndoto haizimiki, ya kesho kuwa njema hali
    Wiki baada wiki, la haramu jasho hawali


    (a) Fafanua sifa tano za watu wanaozungumziwa katika shairi hili.
    (b) Bainisha umuhimu wa tamathali tatu za usemi zilizotumiwa katika shairi hili.
    (c) Eleza kwa kutoa mifano, mbinu tatu ambazo mshairi ametumia kutosheleza mahitaji ya kiarudhi.
    (d) Ainisha shairi hili kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo:
    (i) idadi ya mishororo katika beti.
    (ii) mpangilio wa vina
    (iii) mpangilio wa maneno

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. Amiri A. S. Andanenga: Sauti ya Kiza 1 Ngakua na mato, ya kuonea Ngalisana kito,cha kuchezea Kilicho kizito, cha kuelea Kikamuenea,...(Solved)

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
    Amiri A. S. Andanenga: Sauti ya Kiza
    1 Ngakua na mato, ya kuonea
    Ngalisana kito,cha kuchezea
    Kilicho kizito, cha kuelea
    Kikamuenea, akivae.

    2 Makusudi yangu,ngaliandaa
    Ngafinyanga chungu, cha mduwaa
    Ngatia vitangu,vinavong’aa
    Ili ziwe taa, kwa apikae.

    3 Mkungu wa tano, wa mduwara
    Ulo bora mno, kisha imara
    Ulo na maono, kuwa ni dira
    Kwenye barabara, itindiae.

    4 Ngaomba Baraka, kwake Rabana
    Punje za nafaka, kila aina
    Chunguni kuweka, kwa kulingana
    Hajaangu suna, yule alae.

    5 Ngafanya bidii, kwenda mwituni
    Sio kutalii, kukata kuni
    Ya miti mitii, huko jikoni
    Isio na kani,ni iwakae.

    6 Kwa yangu mabega, nikathubutu
    Ngabeba mafiga, yalo matatu
    Bila hata woga, kwenye misitu
    Simba tembo chatu, sinitishie.

    7 Miti yenye pindi,na jema umbo
    Ngajenga ulindi, mwema wimbombo
    Fundi aso fundi, penye kiwambo
    Moyo wenye tambo, apekechae.

    8 Singaajiri, ngachimba mimi
    Kisima kizuri, cha chemchemi
    Maji ya fahari, ya uzizimi
    Jua la ukami, siyaishae

    9 Tamati nafunga, kwa kuishia
    Mato ndo malenga, kanikimbia
    Nahofu kutunga, mabeti mia
    Asije chukia, ayasomae.


    (a) Eleza ujumbe wa shairi hili.
    (b) Kwa kurejelea ubeti wa pili, eleza umuhimu wa aina mbili za uhuru wa kishairi aliotumia mshairi.
    (c) Andika ubeti wa saba kwa lugha ya nathari.
    (d) Eleza toni ya shairi hili.
    (e) Fafanua aina tatu za urudiaji zilizotumiwa katika shairi hili.
    (f) Bainisha nafsi neni katika shairi hili.

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. T. Arege: Mwili Leo kitaka nifike, natamani, ila wauma mwili Kwa kazi nihusike, samahani, unahiliki mwili Napenda nihesabike, makundini, ila huwezi mwili. Vitisho kamwe...(Solved)

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
    T. Arege: Mwili

    Leo kitaka nifike, natamani, ila wauma mwili
    Kwa kazi nihusike, samahani, unahiliki mwili
    Napenda nihesabike, makundini, ila huwezi mwili.

    Vitisho kamwe kelele, ninavicha, kwa nafsi na mwili
    Ila ugonjwa utimile, umechacha, na kuudhili mwili
    Msikose simile, magalacha, si gurudumu mwili.

    Vingekuwepo viraka, kuutia, ngeushuruti mwili
    Kifundi kivipachika, kuingia, hata kuridhi mwili
    Upya ukaungilika, kuvutia, roho na wake mwili.

    Lakini kamwe haiwi, kuvipata, vipande vyake mwili
    Sihofu kupata mawi, sitajuta, kupigania mwili
    Hata kufutwa sikawi, nitakita, kidete nao mwili.

    Kazi ninaithamini, ni hakika, akilini na mwili
    Ila kamwe siamini, kusagika, damu, jasho na mwili
    Uwele hususani, kioneka, nguvu hitishi mwili.


    a) Eleza dhamira ya mtunzi wa shairi hili.
    b) Fafanua mbinu nne za lugha zilizotumiwa katika shairi hili.
    c) Eleza toni ya shairi hili.
    d) Ni nani anayezungumziwa na nafsineni katika shairi hili?
    e) Eleza bahari ya shairi hili kwa kurejelea vipande.
    f) Andika ubeti wa mwisho kwa lugha ya nathari.

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. Daima alfajiri na mapema Hunipitia na jembe na kotama Katika njia iendayo kondeni Kama walivyofanya babuze zamani; Nimuonapo huwa anatabasamu Kama mtu aliye na kubwa...(Solved)

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

    Daima alfajiri na mapema
    Hunipitia na jembe na kotama
    Katika njia iendayo kondeni
    Kama walivyofanya babuze zamani;
    Nimuonapo huwa anatabasamu
    Kama mtu aliye na kubwa hamu
    Kushika mpini na kutokwa jasho
    Ili kujikimu kupata malisho.

    Anapotembea anasikiliza
    Videge vya anga vinavyotumbuiza
    Utadhani huwa vimemngojea
    Kwa usiku kucha kuja kumwimbia;
    Pia pepo baridi kumpepea
    Rihi za maua zikimletea
    Nao umande kumbusu miguu;
    Na miti yote hujipinda migongo
    kumpapasa,kumtoa matongo;
    Na yeye kuendelea kwa furaha
    kuliko yeyote ninayemjua
    Akichekelea ha ha ha ha ha ha …

    Na mimi kubaki kujiuliza
    Kuna siri gani inayomliwaza?
    Au ni kujua au kutojua?
    Furaha ya mtu ni furaha gani
    katika dunia inayomhini?
    Ukali wa jua wamnyima zao
    Soko la dunia lamkaba koo;
    Dini za kudhani zamsonga roho
    Ayalimia matumbo ya waroho;
    Kuna jambo gani linamridhisha?
    Kama si kujua ni kutokujua
    Laiti angalijua, laiti angalijua!
    (T. Arege)

    Maswali
    a) Eleza hali ya mzungumziwa katika shairi hili.
    b) Huku ukitoa mifano, onyesha aina mbili za uhuru wa kishairi uliotumiwa katika shairi hili.
    c) Fafanua aina tatu za taswira ukirejelea ubeti wa pili.
    d) Eleza umuhimu wa maswali ya balagha katika shairi hili.
    e) Bainisha vipengele vifuatavyo vya kimtindo katika shairi hili:
    i. tashhisi
    ii. kinaya
    iii. tashbihi
    f) Eleza toni ya shairi hili.
    g) Bainisha nafsineni katika shairi hili.
    h) Changanua muundo wa shairi hili.

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali T. Arege: Barabara Barabara bado ni ndefu Nami tayari nimechoka tiki Natamani kuketi Ninyooshe misuli Nituliza akili Lakini Azma yanisukuma Mbele ikinihimiza kuendelea Baada ya miinuko na kuruba Sasa naona...(Solved)

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
    T. Arege: Barabara
    Barabara bado ni ndefu
    Nami tayari nimechoka tiki
    Natamani kuketi
    Ninyooshe misuli
    Nituliza akili

    Lakini

    Azma yanisukuma
    Mbele ikinihimiza kuendelea
    Baada ya miinuko na kuruba
    Sasa naona unyoofu wake
    Unyoofu ambao unatisha zaidi

    Punde natumbukia katika shimo
    Nahitaji siha zaidi ili kupanda tena
    Ghafla nakumbuka ilivyosema
    Ile sauti zamani kidogo
    “Kuwa tayari kupanda na kushuka.”

    Ingawa nimechoka
    Jambo moja li dhahiri
    Lazima nifuate barabara
    Ingawa machweo yaingia
    Nizame na kuibuka
    Nipande na kushuka

    Jambo moja nakukumbukia: Mungu
    Je, nimwombe tena? Hadi lini?
    Labda amechoshwa na ombaomba zangu
    Nashangaa tena!

    Kitu kimoja nakiamini
    Lazima niendelee kujitahidi kwa kila hatua mpya
    Nijikokote kuiandama hii barabara yenye ukungu
    Nikinaswa na kujinasua
    Yumkini nitafika mwisho wake
    Ingawa wangu mwisho haitauwahi kabla.


    (a) Eleza toni ya shairi hili.
    (b) Tambua nafsineni katika shairi hili.
    (c) Mshairi ana maana gani anaposema “Kuwa tayari kupanda na kushuka” katika ubeti wa tatu?
    (d) Fafanua tamathali tano za usemi zilizotumiwa katika shairi hili ukizitolea mifano mwafaka.
    (e) Eleza ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa tano wa shairi hili.
    (f) Eleza maana ya:
    (i) kuruba
    (ii) barabara yenye ukungu

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Kilio cha Lugha Ni wimbo najiimbia,nijiliwaze Sina wa kusaidia, nasongwa sina nafasi Kiwa kwetu naumia, kwengine si mahususi Lugha ya mtu mweusi, Kiswahili chalilia Wataalamu ni nani, mulipo mwaninyanyasa Hamna nami...(Solved)

    Kilio cha Lugha
    Ni wimbo najiimbia,nijiliwaze
    Sina wa kusaidia, nasongwa sina nafasi
    Kiwa kwetu naumia, kwengine si mahususi
    Lugha ya mtu mweusi, Kiswahili chalilia

    Wataalamu ni nani, mulipo mwaninyanyasa
    Hamna nami imani, wala kupanga siasa
    Mwasema sayansini, siku ningalitosa
    Mwanambia nikotosa, kuiva sijafika

    Ela muelewe sana, Maamuma na Imamu
    Mulipokuwa vijana, kwenu nilikuwa timamu
    Sasa mumesoma sana, mwaniona ni haramu
    Mujue kuwa dawamu, utumwa mwauridhia.

    Mzaliwapo mwalia, ‘maa’, maneno ya kwanza
    Lugha munayokulia, ya mama zetu ya kwanza
    Wa lugha muwedoria, muweze na kuikuza
    Sio kujipendekeza, uzungu kuigiza.

    Majira ya ukoloni, ukombozi kusambaza
    Lugha mulithamini, Kiswahili kufukiza
    Hata kule risavuni, kizungu hanikuwaza
    Sasa mbona mwanibeza, mbali mwanitupilia?

    Sayansi sio asili, msamiatiwe sinao
    Sayansi yataka mbali, msamiati ni wa hao
    Nitakuwa Kiswahili, kiomba majina yao
    Lugha kujikuza kwao, huomba linalofaa.

    Enyi viongozi wetu, ipangeni nadharia
    Kujenga siasa yetu, tuzidi kuwa huria
    Lugha hata ‘mbusha watu, tuche kuriaria
    Sifa ni kwa chake mtu, cha mwenzi hutoringia

    Utajiri wangu hasa, nikiwatajia wote
    Msamiati huwa, ni wa Afrika yote
    Na methali za kuasa, nahau na ngeli zote
    Na nisemwapo popote, ujumbe hukamilika.

    Afrika ndipo petu, pa wabantu halisi
    Baba na mama ni Bantu, shina la wangu ukwasi
    Warabu na wengi wetu, sio wangu Adinasi
    Kwao ‘meomba kiasi, ili kujizidisha

    Mfumo mpya hongera, wa elimu humu Kenya
    Lugha takuwa imara, ukabila tutafinya
    Kiswahili ni ibara, kila mtu kiimanya
    Methali imetuonya, mtumwa si mwasilia.

    Tamati lugha yalia, yabaguliwa bayana
    Kukua imeridhia, msamiati kufana
    Wengine wataijulia, kwa marefu na mapana
    Lugha yetu ya maana, mwaipuuza yalia.


    Maswali
    (a) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu
    (b) Kwa kutoa hoja nne, eleza kwa nini shairi hililikaitwa kilio cha lugha.
    (c) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari.
    (d) Eleza toni ya shairi hili.
    (e) Tambua uhuru wa kishairi uliotumiwa kwa kurejelea mifano mitatu.
    (f) Bainisha nafsineni katika shairi.
    (g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kwa mujibu wa shairi.
    i. nasongwa
    ii. kuriaria
    iii. adinasi

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Lau dunia nanena, tuseme si ati ati, Mauti kawa hakuna, katika wote wakati, Vipi tungelisongana, tunaoishi tiati? Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana? Dunia ingetatana, na kizazi katikati, Huku kwazaliwa bwana,...(Solved)

    Lau dunia nanena, tuseme si ati ati,
    Mauti kawa hakuna, katika wote wakati,
    Vipi tungelisongana, tunaoishi tiati?
    Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

    Dunia ingetatana, na kizazi katikati,
    Huku kwazaliwa bwana, kule kwazawa binti,
    Vipi tungelioana, na kuzaa hatuwati?
    Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

    Lau mauti hakuna, tungesongana sharuti,
    Kwa viumbe kukazana, wanadamu na manyati,
    Vipi tungelijazana, kwa kusitawi umati?

    Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
    Walakini Subuhana, kapanga sisi na miti,
    Ili tusizidi sana, si wengi na si katiti
    Maisha ya kupishana, yule ende yule keti,
    Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

    Ndipo dunia kufana, ikawa kama yakuti,
    Kwa uwezowe Rabana, kaipanga madhubuti,
    Maisha kugawiana, kayagawa kwa mauti,
    Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

    Njia ingekuwa hapana, pembeni na katikati,
    Sote tungeambatana, kama ukosi na shati,
    Na njaa ingetutafuna, pa kulima hatupati,
    Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

    Peleleza utaona, hayataki utafiti,
    Kama tungelikongana, ingekuwa ni bahati,
    Vipi tungesukumana, katika hiyo hayati?
    Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

    Mbele sitokwenda tena, hapa mwisho nasukuti,
    Yaoleni waungwana, shauri yake Jabaruti,
    Yote tuloelezana, katenda bila senti,
    Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
    (Abdalla Said Kizere)


    Maswali
    a) Pendekeza anwani mwafaka la shairi hili.
    b) Je, hili ni shairi la bahari gani? Eleza
    c) Eleza vile mwandishi alivyotumia uhuru wa kishairi.
    d) Eleza umbo la shairi hili.
    e) Fafanua ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa tano.
    f) Andika majina mawili ya Mungu kwa mujibu wa shairi.
    g) Kwa kutolea mifano, eleza mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika shairi hili

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Eleza mambo yanayozingatiwa katika uhuru wa kishairi (Solved)

    Eleza mambo yanayozingatiwa katika uhuru wa kishairi

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Taja baadhi ya masuala muhimu katika uchambuzi wa mashairi(Solved)

    Taja baadhi ya masuala muhimu katika uchambuzi wa mashairi

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Taja aina mbalimbali za takriri katika ushairi(Solved)

    Taja aina mbalimbali za takriri katika ushairi

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Katika ikisiri yake, Joseph Nyehita anaangazia kuwa matumizi ya methali yanapozingatiwa, ushairi wa Kiswahili unaweza kuainishwa zaidi kwa kuzingatia kutumiwa au kutotumiwa kwa methali. Anasema...(Solved)

    Katika ikisiri yake, Joseph Nyehita anaangazia kuwa matumizi ya methali yanapozingatiwa, ushairi wa Kiswahili unaweza kuainishwa zaidi kwa kuzingatia kutumiwa au kutotumiwa kwa methali. Anasema kuwa kila kikundi cha ushairi kinaweza kupendekezewa jina mahususi kuwa kitambulisho chake. Taja majina yanayopendekezwa

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Taja huku ukitoa mfano, aina kadha za taswira katika ushairi(Solved)

    Taja huku ukitoa mfano, aina kadha za taswira katika ushairi

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Taja na ueleze tamathali tofauti za usemi(Solved)

    Taja na ueleze tamathali tofauti za usemi

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)