Mahitaji Ya Kujiunga Na Shahada Ya B.A (Kiswahili Na Mawasiliano:-
Mahitaji ya kawaida ya shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Egerton pamoja na yale ya kitivo cha elimujamii na maendeleo, yatatumika:
Zaidi ya kutimiza mahitaji haya, mwanafunzi atahitaji kuwa na alama ya C+ katika Kiswahili ili kujiunga na shahada ya B.A (Kiswahili na Mawasiliano).
i) Mwanafunzi pia atakubaliwa kujiunga na shahada ya B.A (Kiswahili na Mawasiliano) iwapo ana stashahada ya Diploma katika elimu kutoka kwa chuo chochote kile kinachotambulika. Mwanafunzi huyu ataruhusiwa kuhamisha hadi asilimia 30% ya tuzo alizopata katika stashahada ya diploma, kama inavyoruhusiwa na kanuni za chuo kikuu cha Egerton.
ii) Waliohitimu kiumri pia wanaweza kujiunga na shahada ya B.A (Kiswahili na Mawasiliano) kutegemea vyeti vyao vya kiakademia vya awali pamoja na tajriba walizo nazo katika nyanja hii ya Kiswahili na mawasiliano kama itakavyopendekezwa na idara ya usomilugha na mawasiliano