Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Jadili usemi halisi wa sentensi

Jadili usemi halisi wa sentensi.

Answers


kelvin
? Maneno halisi kama yanavyotamkwa na msemaji.
a) Huandikwa bila kugeuza chochote.
b) Huanzia kwa herufi kubwa.
c) Hunukuliwa kwa alama za usemi ambazo huandikwa zikiwa mbili mbili na moja moja katika dondoo ndogo k.m. “Mwambie ‘ugua pole’ ukimuona,” baba aliniambia.
d) Koma hutumiwa mwanzoni au mwishoni mwake.
e) Msemaji mpya anapoanza kusema, unapaswa kufungua aya mpya k.m.
Alimuuliza, “Huendi kwa nini?”
“Sikupewa ruhusa,” alijibu Zahara.
f) Baada ya (?) na (!) na (.) maneno huanzia kwa herufi kubwa k.m. Lo! Unatoka wapi saa hii? Aliniuliza.

kevowmuchiri answered the question on August 10, 2018 at 09:59

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions