Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Questions and answers: Kiswahili

Q&A Categories


Do you have Q&A pairs? Post them here

2287 Questions  View: All | Solved | UnsolvedSearch Results...
 • Nilitazama jua likichwa Matumaini yangu yakizama pamoja Na miale miekundu Nilidhani lilikuwa jinamizi tu Kwamba ulikuwa kesha n’acha(Solved)

  Nilitazama jua likichwa Matumaini yangu yakizama pamoja Na miale miekundu Nilidhani lilikuwa jinamizi tu Kwamba ulikuwa kesha n’acha Walikuwa wameisha n’ambia Walimwengu Ela nilikataa katakata walosema Nikajitia kuamini waloamba yalikuwa Uzushi Hadi siku hii nilopokea waraka, Waraka ambao ulikuwa jeneza ka kuzikia Pendo letu la miongo miwili. a. Taja aina ya wimbo ufuatao. b. Taja sifa tano za utanzu huu wa fasihi simulizi. c. Eleza umuhimu wa utanzu huu. d. Taja na ueleze aina zingine tano za nyimbo.

  Date posted: November 26, 2022.  

 • Soma makala haya kisha ujibu maswali. Kwani mnauza salamu? Sina time ya kuwaste hapa. Am a busy person leta order yako haraka... Nimesema samaki wa kupaka. Mimi...(Solved)

  Soma makala haya kisha ujibu maswali. Kwani mnauza salamu? Sina time ya kuwaste hapa. Am a busy person leta order yako haraka... Nimesema samaki wa kupaka. Mimi ng’ombe na chicken. a. Tambua sajili hii. b. Fafanua sifa tisa za sajili hii.

  Date posted: November 26, 2022.  

 • Kanusha: Asha aliwapelekea wageni chakula na akawanavya mikono.(Solved)

  Kanusha: Asha aliwapelekea wageni chakula na akawanavya mikono.

  Date posted: November 26, 2022.  

 • Tumia neno ‘kuwa’ kama kitenzi kishirikishi kikamilifu katika sentensi.(Solved)

  Tumia neno ‘kuwa’ kama kitenzi kishirikishi kikamilifu katika sentensi.

  Date posted: November 26, 2022.  

 • Eleza matumizi ya neno ‘mzee’ katika sentensi zifuatazo: Baba mzee amelewa Mzee amelewa(Solved)

  Eleza matumizi ya neno ‘mzee’ katika sentensi zifuatazo: -Baba mzee amelewa -Mzee amelewa

  Date posted: November 26, 2022.  

 • Andika katika usemi wa taarifa. “Tafadhali nifungulie mlango sasa. Nitanyeshewa.” Mtoto akamwambia(Solved)

  Andika katika usemi wa taarifa. “Tafadhali nifungulie mlango sasa. Nitanyeshewa.” Mtoto akamwambia

  Date posted: November 26, 2022.  

 • Eleza matumizi matatu ya viambishi awali.(Solved)

  Eleza matumizi matatu ya viambishi awali.

  Date posted: November 26, 2022.  

 • Andika sifa za sauti zifuatazo: /m/ /gh/(Solved)

  Andika sifa za sauti zifuatazo: /m/ /gh/

  Date posted: November 26, 2022.  

 • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali. Dawa za kulevya ni donda ndugu katika taifa letu. Ni zimwi linalotesa na kufisha wazee kwa vijana.(Solved)

  Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali. Dawa za kulevya ni donda ndugu katika taifa letu. Ni zimwi linalotesa na kufisha wazee kwa vijana. Halichagui jinsia, tabaka, rangi wala umri. Uraibu wa dawa hizi hauna faida yoyote. Wanaotumia dawa za kulevya huzitia mwili kwa kunusa, kuvuta, kumeza na kujidunga sindano. Zinapoingia katika miili ya watu madhara huwa mengi. Kuna wale wanaokosa hamu ya kula, wengine huambukizwa maradhi kama vile ukimwi wanapotumia sindano zilizotumiwa na watu wenye virusi vya maradhi hayo kujidunga sindano na kutia dawa mwilini. Mihadarati pia inaweza kufanya mtu awe mwendawazimu. Vifo pia hutokea ikiwa uraibu utazidi na mtu akose kupata matibabu. Mtu anayetumia dawa za kulevya huathirika akili. Yeye huwa hana uamuzi wenye hekima katika maisha yake .wengi wao hushiriki katika vitendo vya uhayawani. Wao hukosa fikra za utu. Baadhi yao wamebaka kina mama na watoto wadogo na wengine wamezua vita katika familia na kusababisha madhara makubwa katika jamii zao kwa sababu ya ulevi. Familia za wanaotumia mihadarati hazina amani. Jamaa zao hutumia hala nyingi kuwalipia ada ya hospitali ili wapate matibabu baada ya kuzidiwa na uraibu. Mali hufujwa na watu wenye uraibu wa dawa hizo pale wanapohakikisha hawazikosi kila siku. Mzazi kwa mfano anaweza kutumia hela kununua dawa za kulevya badala ya kumlipia mwanawe karo. Kuna wale wanaowaibia majirani na marafiki ili wakidhi mahitaji yao. Ajali barabarani pia husababishwa na malevi. Dereva yeyote awe wa matatu au gari la kibinafsi anapoedesha gari akiwa mlevi huwa anahatarisha maisha yake mwenyewe, abiria na wananchi wanaopiga miguu barabarani .Uchumi wa taifa huzorota baada ya wananchi kutumia mihadarati. Watu wenye uraibu hukaa mbumbumbu bila kufanya lolote hasa kutokana na kudhoofika kwa afya yao au ulegevu unaosababishwa na ulevi. Watu wa aina hiyo huwa wanamchango haba katika ukuzi wa uchumi wa taifa. Dawa hizi zimesambaa kila mahali utapata zinauzwa masokoni, shuleni, njiani na hata pahali popote pale penye watu. Dawa za kulevya haziuzwi hadharani nchini Kenya kwa sababu serikali imepiga marufuku uuzaji wa bidhaa hiyo. Waja wanaoziuza hufanya hivyo kisiri. Walanguzi wa mihadarati aghalabu hutumia watu wengine kuuza kwa niaba yao. Kuna wale wanaotumia watoto , wanaorandaranda almaarufu chokoraa na wengine hutumia vijana katika shule za misingi, upili na vyuo vikuu kama mawakala. Vijana hasa wamejipata katika mtego huu kwa kuwafanyia walanguzi biashara hii haramu hili waweze kupata hela za kukidhi matakwa yao ukweli ni kuwa pesa wanazo patiwa na waajiri wao ni chache mno na hatimaye wao hutumia daw zile na kuishia kuwa na uraibu unaosababisha wao wenyewe kuwa wateja wa mabwenyenye hao wasio na utu. Watu maarufu kama vile wafanyabiashara, wanamuziki na wanasiasa wametuhumiwa kushiriki katika biashara hii . washukiwa hawa mara nyingi hukosa kufikishwa mahakamani kwa sababu jamii hukosa ushahidi wa kutosha dhidi ya tabia hiyo. Ni nani hasa muhusika katika kuingiza sumu hii katika nchi yetu ? hakuna mtu anayeweza kusimama kadamnasi na kusema hiyo ndiyo kazi yake. Mbona tushiriki katika biashara tusiyoweza kujivunia? Ni mwito wangu kwa kila mwananchi mzalendo kuungana na wenzake ili kupinga biashara hii haramu. Tuhubiri makanisani, shuleni misikitini, hekaluni na mahali popote pale. Tukemee adui huyu, wa afya na mali. Washauri nasaha washike usukani wawashauri wazee kwa vijana, wakubwa kwa wadogo, weusi kwa weupe tuizike mihadarati katika kaburi la sahau. Maswali 1. Yape makala haya anwani mwafaka. 2. Mwandishi anamaanisha nini anaposema kuwa dawa za kulevya ni donda ndugu katika taifa letu. 3. Taja namna ambavyo dawa za kulevya zinavyotumiwa. 4. Eleza athari ya dawa za kulevya kwa familia za wanaotumia . 5. Kuna changamoto gani katika kupiga vita matumizi ya mihadararati. 6. Eleza sera ya serikali kuhusu dawa za kulevya. 7. Msamiati ufuatao umetumika kumaanisha nini kwa mjibu wa taarifa. i. mawakala ii. kadamnasi iii. washauri nasaha

  Date posted: November 26, 2022.  

 • Eleza sifa za sajili ya maabadani.(Solved)

  Eleza sifa za sajili ya maabadani.

  Date posted: November 26, 2022.  

 • Unda nomino mbilimbili kutokana na mizizi ifuatayo. i) -f- ii) -l-(Solved)

  Unda nomino mbilimbili kutokana na mizizi ifuatayo. i) -f- ii) -l-

  Date posted: November 26, 2022.  

 • Bainisha kirai nomino na kirai kivumishi katika sentensi hizi. i) Nguo aliyonunua mzazi ni mpya. ii) Kondoo mwenye manyoya mengi hupendeza.(Solved)

  Bainisha kirai nomino na kirai kivumishi katika sentensi hizi. i) Nguo aliyonunua mzazi ni mpya. ii) Kondoo mwenye manyoya mengi hupendeza.

  Date posted: November 26, 2022.  

 • Tunga sentensi ya neno moja yenye visehemu vifuatavyo vya sarufi. i) Kiambishi kiwakilishi cha kiima ii) Kiambishi kiwakilishi cha wakati uliopo iii) Kiambishi kiwakilishi cha kitendewa/mtendewa iv) Shina la...(Solved)

  Tunga sentensi ya neno moja yenye visehemu vifuatavyo vya sarufi. i) Kiambishi kiwakilishi cha kiima ii) Kiambishi kiwakilishi cha wakati uliopo iii) Kiambishi kiwakilishi cha kitendewa/mtendewa iv) Shina la kitenzi v) Kiambishi cha kauli ya kutendesha vi) Kiishio

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Tumia neno dhahiri katika setensi kulingana na maagizo Kama: i) Kiambishi ii) Kivumishi(Solved)

  Tumia neno dhahiri katika setensi kulingana na maagizo Kama: i) Kiambishi ii) Kivumishi

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Bainisha yambwa tendwa na yambwa tendewa katika sentensi hii. Mbunge wa Mtondo Kaskazini atawajengea wanakijiji josho kisha aghurie mjini.(Solved)

  Bainisha yambwa tendwa na yambwa tendewa katika sentensi hii. Mbunge wa Mtondo Kaskazini atawajengea wanakijiji josho kisha aghurie mjini.

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Tunga sentensi ukitumia nomino zifuatazo pamoja na kivumishi __ingine i) dau ii) urembo(Solved)

  Tunga sentensi ukitumia nomino zifuatazo pamoja na kivumishi __ingine i) dau ii) urembo

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Andika katika usemi taarifa. “Tutawatembelea wazazi wetu leo jioni” Leo alimwambia Asha.(Solved)

  Andika katika usemi taarifa. “Tutawatembelea wazazi wetu leo jioni” Leo alimwambia Asha.

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Andika katika ukubwa wingi. Kitoto kijeuri kikiletwa kitarejeshwa kwao.(Solved)

  Andika katika ukubwa wingi. Kitoto kijeuri kikiletwa kitarejeshwa kwao.

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia mbinu ya matawi. Mwanafunzi stadi amenunua kitabu kizuri.(Solved)

  Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia mbinu ya matawi. Mwanafunzi stadi amenunua kitabu kizuri.

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Yakinisha sentensi hii. Simba asiponguruma wanyama wote hawababaiki.(Solved)

  Yakinisha sentensi hii. Simba asiponguruma wanyama wote hawababaiki.

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Taja sifa mbili bainifu za vokali 'U'(Solved)

  Taja sifa mbili bainifu za vokali 'U'

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Taja sauti mbili ambazo ni vikwamizo na hutamkiwa kwenye ufizi.(Solved)

  Taja sauti mbili ambazo ni vikwamizo na hutamkiwa kwenye ufizi.

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata Wakaazi wengi wa maeneo ya kitajiri miji yetu hawajui wapo chini ya utawala wa machifu.(Solved)

  Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata Wakaazi wengi wa maeneo ya kitajiri miji yetu hawajui wapo chini ya utawala wa machifu.Huenda wakasalia katika hali hii ya kutojua hadi wanapokosa kulipa ujira wa watumishi wao wa nyumbani halafu maskini mwajiriwa huyu anaripoti kwa chifu, kwa kuwa ni hali yake. Chifu ni uzi muhimu katika vazi Ia kijamii. Bila hawa maafisa, jamii kama tunavyoijua ingeporomoka. Wakati mwingine hawaungwi mkono. Mfano mzuri ni kukataliwa kwa katiba kielelezo cha Wako, Novembe 2005, wakati wa kura ya maoni. Kwa sababu jukumu la chifu au kibadala chake halikudhihirishwa wazi wazi katika kielelezo, wengi walikataa stakabadhi hiyo, wakihofia sasa hawataweza kufikia mtawala wao kushughulikia malalamishi yao. Nimeishi mtaa wa Nairobi West miaka mingi na kuhudhuria kamati nyingi za lokesheni, chini ya uwenye kiti wa chifu akisaidiwa na naibu na wazee. Mikutano, pia inahudhuriwa na madiwani, inspekta wa askari tawala na wawakilishi wengi na washia dau katika lokesheni. Takribani kila swali linalogusia maslahi ya jamii linajadiliwa na kuchunguzwa na maazimio kupitishwa. Mada muhimu wakati wa mikutano hii ni usalama, taa za barabarani, ulanguzi wa mihadarati hasa karibu na taasisi za elimu, kudumisha usafi wa vyoo vya umma, kudumisha usalama kupitia kwa raia na swala nyeti la vioski. Kazi ngumu ya chifu ni kuwazia kila kju. Kwa mfano, mwenye kioski ni sharti apate mkate wa kila siku na sehemu ya biashara yake iliyoko ni muhimu. Ikiwa kioski kitajengwa na kukiuka sheria za baraza la jiji au ikiwa wizi usiofahamika na utumizi wa dawa za kulevya unatokea kufuatia kukua kwa idadi ya vioski katika eneo, shinikizo zinaelekezwa kukuwa kwa wenye vioski. Chifu lazima azingatie shinikizo za umma hatari za kiusalama na hofu za wenye vioski kabla ya kufanya uamuzi ikiwa mijengo hiyo ibomolewe. Tatizo jingine ni watoto wa barabarani. Makao ya kuwakimu ni machache kama walivyo wahudumu wa kijamii, suluhu ni nini? Tuwatupe katika ukumbi wa kijamii, ambao watahepa pindi tu, wapatapo fürsa ndogo au wapelekwe huduma kwa vijana wa Taifa, ambapo wachache wanaweza kutunzwa kwa wakati mmoja. Ili kufaulu kwa wengine, sharti wawe katika vituo vya urekebishaji tabia za matumizi ya dawa za kulevya. Tuwakabidhi polisi kwa sababu wanaranda au tujaribu kuungana na vituo vya urekebishaji tabia kuhakikisha hawatarudi barabarani. Mazingira ya lokesheni pia huibuka katika ajenda. Hali ya barabara, juhudi za kusafisha mazingira, wizi wa maji na umeme, usafiri wa umma, uchafuzi wa mazingira, hewa na kelele, hii inatokea kupitia malalamishi ya watu wanaoishi karibu na mabaa na uzingativu wa saa ya biashara hujadiliwa kila mara. Chifu ni sharti afahamu sheria na kanuni zinazotawala hali hizo, halafu ajadili na wahusika kabla ya kutoa mwelekeo. Usawa na uwazi katika kugawa fedha za Hazina ya maendeleo ya maeneo Bunge, pia hujadiliwa. Katika maswala haya mengine, chifu ndiye aliye nyanjani. Anawajibikia jamii na wakubwa wake na hatarajii shukrani au kutambuliwa kwa kazi njema aliyofanya. Isipokuwa hukashifiwa anapofeli. Watu wengine wana taswira ya Chifu kama mtu kwenye jukwa, kofia yake. na kifimbo kinachompa mamlaka ya kuhutubia baraza, Kajubu tyji zaidi ya hivyo. Kwa mujibu wa kitabu cha mafunzo ya machifu na Naibu wao (Januari 2004), wajibu wa chifu ni kuwakilisha sera na mipango ya serikali kwa wananchi. Chifu ni ajenti wa “mabadiliko” mwenye wajibu Wa kuhamasisha watu katika maendeleo. Anajishughulisha na kujua ni nani maskini katika lokesheni, mkoa, mgonjwa asiyeweza kupata tiba na kupanga jinsi mhasiriwa atakavyopelekwa hospitali kama anavyoweza. Ni sharti ashughulikie ugomvi wa kinyumbani, uhalifu wa watoto, dhuluma za watoto, agawe chakula na mavazi kwa wahitaji na kuhukumu kesi ndogo za wizi na uharibifu. Chifu hutatua kesi za kisheria kwa wasioweza kumudu wakili. Wakati wananchi wanapohisi mbunge wao hafikiliki na hawana imani na polisi, chifu ndiye suluhisho. Lakini kuna machifu wachache ambao hawafanyi kazi yao vyema. Kwa ufupi, chifu ni mkusanyiko wa kushngaza; mfalme katika himaya yake, pasta, baba msikivu, wanasaikolojia, mtunga sheria na mdumisha sheria, balozi mchaguzi, mama, mlumbi na askari asiyechelewa. Ingawa halipwi vyema, anafanya kazi bila tarakilishi, na aghalabu hujilipia gharama ya kodi ya afisi yake kutoka mfuko wake. Kwa sababu ni mtumishi wa umma, tunataraji afanye kazi mufti. Hiyo haimaanishi tusishukuru kwa kazi njema aliyofanya. Serikali inaweza kufanya hivi kwa kuimarisha hali yake ya kazi, mazingira yake ya kikazi, na kuhakikisha yana tarakilishi, anapata mafunzo ya uongozi na usimamizi. Wananchi sharti washukuru watu hawa kwa kujitolea sabili. Maswali a) Fupisha aya nne za kwanza (Maneno 60) Matayarisho Jibu b) Kwa maneno kati ya 80-90 fupisha aya ya tano hadi mwisho. Matayarisho Jibu

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Soma taarifa ifuatayo halafu ujibu maswali Kama kuna jambo ambalo limeiparaganya akili yamahuluki ni kuielewa dhana ya demokrasia. Kiumbe huyu heshi kuuliza mkururo wa maswali. Demokrasia ni...(Solved)

  Soma taarifa ifuatayo halafu ujibu maswali Kama kuna jambo ambalo limeiparaganya akili yamahuluki ni kuielewa dhana ya demokrasia. Kiumbe huyu heshi kuuliza mkururo wa maswali. Demokrasia ni nini hasa? Tunaweza kula demokrasia? Ni dude gani hili lina kichwa au mkia pekee yake? Je demokrasia inazuia njaa? Demokrasia ni himaya ya wasomi tu au vilevile ni haki ya mafalahi? Kwa muda mrefu kumekuwa na kinyang‟anyiro kikubwa katika jamii ambacho azma na. matokeo yake yamekuwa ya kutatanisha. Baadhi ya watu wamejitokeza kama mchuzi wa ugali na kuzusha zahama ambazo si za kuyumkinika. Vichwa vya adinasi vikafyekwa kwa miundo na maparange na matumbo yakapasuliwa na kuapakaza utumbo na vijusi kila mahali. Shingo zikapigiwa vigingi na kukomewa ardhini. Demokrasia si mchezo wa lelemama. Ni sharti tujifunge vibwebwe tumwage damu na tufe ili tupate demokrasia ya kweli!” Mmoja wa mibabe wa demokrasia alinguruma kadamnasi ya umati huku ngoma za vita zikirindima.” Hata Marekani na ulaya walimwaga damu. Mamilioni ya watu walipukutishwa na kimbunga cha demokrasia. Chini walilaliana kama Vimatu na tunutu. Hawa manafiki wanafikiri hatuwajui. Katu hatutakubali porojo zao. Wanatupikia majungu kisha wakatoweka. Kuna demokrasia ya Afrika na ile ya Ulaya „ mkereketwa wa Uafrika akachanganua. Demokrasia ya Afrika basi imefuata mkondo huu wa umwagikaji damu. Kila kukijiri uchaguzi zahama hutawala. Walio madarakani hawataki kubanduka. Hutaruta visababu vya kukwepa wimbi la ushinde. Demokrasia ni mchezo wa mizengwe tu ati. Hali hil imesababisha maafa makubwa, uharibifu mkubwa wa mali, majeraha, ukimbizi wa raia ndani na nje ya mataifa husika, dhuluma za kimapenzi dhidi ya wanawake, kuzagaa kwa magonjwa ainati, uhasama wa kikabila. Jambo la kusikitisha ni kwamba raia na viongozi hawaelekei kujifundisha chochote kutokana na hali. Huku mataifa mengi Ulayani na Asia yakikwea daraja moja baada ya nyingine kimaendeleo, Afrika imedumaa tu. Imesalia kuimba ule wimbo wake wa kutokea azali„ Tutaendelea vipi na tunadhulimiwa na kaka wakubwa”. Siasa ya demokrasia katika bara la Afrika ina tija kubwa hususan kwa wale wachache wanaofanikiwa kudhibiti nyenzo za kutia tonge kinywani. Ulitima wa umma husalia miradi hewa ya tabaka la viongozi ambayo hutumiwa kujinadi zamu nyingine ifikapo tena. Demokrasia ya kweli imo mikononi mwa umma pale utakapojikomboa kimawazo na kwa ujasiri kudai huduma bora, uajibikaji na kuheshimiwa kwa mkataba wa kijamii uliosisiwa na Jean Jacques Rousseau. Maswali a) Binadamu amechanganyika kwa njia ipi? b) Ni vipi Demokrasia ya kweli inaweza kufikiwa c) Kwa nini inasemekana kuwa „Demokrasia ni mchezo wa mizengwe? d) Ni athari gani hutokana na kinyang‟anyiro cha Demokrasia? e) “Dhiki za raia zimesalia kuwa mradi-hewa wa wanasiasa” Eleza. f) Fafanua maana ya maneno na mafungu yafuatayo jinsi yalivyotumika katika taarifa. i) Mafahali ii) Wanatupikia majungu iii) Ukarabati

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Toa maana mbili ya sentensi ifuatayo: Laleni!(Solved)

  Toa maana mbili ya sentensi ifuatayo: Laleni!

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Nomino zifuatazo ziko katika ngeli gani? i. Nyasi ii. Furaha(Solved)

  Nomino zifuatazo ziko katika ngeli gani? i. Nyasi ii. Furaha

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Tunga sentensi mbili ukitumia mzizi uliopewa ili kuonyesha mwingiliano wa maneno katika mabano. -baya (kivumishi kuwa kiwakilishi)(Solved)

  Tunga sentensi mbili ukitumia mzizi uliopewa ili kuonyesha mwingiliano wa maneno katika mabano. -baya (kivumishi kuwa kiwakilishi)

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Tofautisha maana ya sentensi zifuatazo. i. Ningeenda leo ningefika mapema. ii. Ningalienda ningalifika mapema.(Solved)

  Tofautisha maana ya sentensi zifuatazo. i. Ningeenda leo ningefika mapema. ii. Ningalienda ningalifika mapema.

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Andika maana mbili za sentensi ifuatayo. Wanafunzi walipigia wazazi wao simu.(Solved)

  Andika maana mbili za sentensi ifuatayo. Wanafunzi walipigia wazazi wao simu.

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Tunga sentensi uliyopewa upya bila matumizi ya ‘amba’ Ndoo ambayo ilinunuliwa ilivunjwa jana.(Solved)

  Tunga sentensi uliyopewa upya bila matumizi ya ‘amba’ Ndoo ambayo ilinunuliwa ilivunjwa jana.

  Date posted: November 25, 2022.