Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

RIWAYA YA KIDAGAA KIMEMWOZEA. Mtoto ni mtoto hata likiwa bonge la nyama. Mtu hupata ajaliwalo sio alitakalo.

RIWAYA YA KIDAGAA KIMEMWOZEA.
Mtoto ni mtoto hata likiwa bonge la nyama. Mtu hupata ajaliwalo sio alitakalo.
(a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
(b) Eleza tamathali ya lugha iliyotumika katika usemi huu.
(c) Ukirejelea riwaya thibitisha kuwa mtu hupata ajaliwalo silo alitakalo.

Answers


sharon
a)i) Maneno haya yalisemwa na Dora.
ii) Msemewa ni Majisifu
iii) Walikuwa nyumbani mwao
iv) Majisifu alikuwa anataka kuwatupa watoto waliozaliwa majini kwa kuwa hawakuwa na uwezo wa kutembea lakini Dora akamzuia.
b) Methali - mtu hupata ajaliwalo sio alitakalo
Istiara - likiwa bonge la nyama.
c)- Imani alikuwa na ndoto ya kuwa daktarii lakini anakosa kusoma na kuishia kuwa kijakazi
- Nasaba Bora alikuwa na Imani kuwa mazishi yake yangehudhuriwa na wengi lakini baada ya kifo chake mazishi yalihudhuriwa na wachache mno
- Majisifu alitamani kupata watoto wazima kama wenzake badala yake watoto wake wanazaliwa wakiwa vilema
- Mashaka alisema badala ya Mungu kumpa kilema chochote afadhali ampe kifo. Hata hivyo anaishia kuwa kichaa
- Nasaba Bora alitarajia madhubuti aweze kuendeleza kazi yake lakini madhubuti anamgeuka na kuwa hasidi wake
- Bi Zuhura alitamani kupata mapenzi kutoka kwa mumewe lakini anachopata ni upweke na majonzi na hatimaye kupewa talaka
- Amani licha ya kusoma hadi chuo kikuu anasingiziwa uchochezi na kutokamilisha masomo yake hapati umaarufii wowote. Badala yake Majisifu anapata Sifa kemkem huku Amani akiwa mchungaji
sharon kalunda answered the question on September 25, 2019 at 07:25

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions

  • Fafanua jinsi maudhui ya unafiki yamejidhihirisha katika tamthilia ya Mstahiki Meya, ukirejelea wahusika wowote watano. (Solved)

    Fafanua jinsi maudhui ya unafiki yamejidhihirisha katika tamthilia ya Mstahiki Meya, ukirejelea wahusika wowote watano.

    Date posted: September 25, 2019 .    Answers (1)

  • Mbona isiwe kweli? Wewe panga uwalete tule matunda ya jasho letu nao watoto.(Kwa kurejelea tamthilia "Mstahiki Meya") (Solved)

    Mbona isiwe kweli? Wewe panga uwalete tule matunda ya jasho letu nao watoto.(Kwa kurejelea tamthilia "Mstahiki Meya")
    (a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    (b) Eleza mbinu mbili za uandishi katika dondoo hili.
    (c) Eleza yaliyopangwa baada ya usemi huu.

    Date posted: September 25, 2019 .    Answers (1)

  • Ole wangu! Ole wangu, nisikize Mola wangu, (Solved)

    Ole wangu! Ole wangu, nisikize Mola wangu,
    Lipokee ombi langu, wanisikize wenzangu,
    Washike ujumbe wangu, uloleta Mola kwangu,
    Nyakati tunazoishi, ni Sodoma na Gomora.

    Amri kumi za Mola, mumekwisha zikiuka
    Ndipo hamuwezi lala, mumekwisha vurugika,
    Mumemsahau Mola, ndipo nanyi mwasumbuka,
    Nyakati tunazoishi, ni Sodoma na Gomora.

    Mwaabudu mashetani, ushirikina ni mwingi,
    Munaiba hadharani, waongo nao ni wengi,
    Mwajawa na taraghani, na wazimu mwingi,
    Nyakati tunazoishi, ni Sodoma na Gomora,

    Mwauana ovyoovyo, mwasemana ndivyo sivyo,
    Fitina nazo zilivyo, mwarogana vivyo hivyo,
    Matusi ni vile sivyo, munaisha ka isivyo,
    Nyakati tunazoishi, ni Sodoma na Gomora.

    Kuna dawa za kulevya, na hata pembe haramu,
    Na ukimwi nakujuvya, unaua wanadamu,
    Na mimba nazo kuavya, watoto ni marehemu,
    Nyakati tunazoishi, ni Sodoma na Gomora.

    Wengine nao hudai, waoe jinisi moja,
    Ati mwingine hafai, heri sawia ya mja,
    Haya maoni ni hoi, tupinge kila mmoja,
    Nyakati tunazoishi, ni Sodoma na Gomora.

    Ploti mwazinyakua, na viwanja vya mipira,
    Makaburi mwala pia, mabibi mwateka nyara,
    Ibada zikifikia, mwafurika kwa majira
    Nyakati tunazoishi, ni Sodoma na Gomora.

    Wengi tuwachaguao, si viongozi ni waizi,
    Tamaa walio nao, yaongoza maamuzi,
    Mishahara ile yao, huongezwa kila mwezi,
    Nyakati tunazoishi, ni Sodoma na Gomora.

    Usalama hatunao, wasiwasi umezidi,
    Waja kiwa makazio, huogopa magaidi,
    Mabomu walipuao, huruma wamekaidi,
    Nyakati tunazoishi, ni Sodoma na Gomora.

    Beti kumi namaliza, dua yangu imetimu,
    Mungu amekwisha anza, kuhukumu mwanadamu,
    Wote walojipotoza.waiepuke hukumu,
    Nyakati tunazoishi, ni Sodoma na Gomora.

    MASWALI
    (a) Lipe shairi hili kichwa mwafaka.
    (b) Shairi hili linaweza kuwekwa katika bahari kadhaa. Taja na ueleze bahari zozote tatu.
    (c) Taja na ueleze mbinu tatu za lugha zilizotumiwa katika ubeti wa kwanza.
    (d) Eleza sababu ya mshairi kutumia alama ya ritifaa katika ubeti wa nne
    (e) Tambua uhuru wa kishairi uliotumika katika ubeti wa tisa mshororo wa tatu na ueleze umuhimu wake.
    (f) Andika ubeti wa sita kwa lugha tutumbi.
    (g) Taja mifano mitatu ya uozo anaolalamikia mwandishi.
    (h) Eleza toni ya mwandishi.

    Date posted: September 25, 2019 .    Answers (1)

  • Kanusha sentensi ifuatayo bila kutumia kiunganishi. Iwapo mvua itanyesha wakulima watapanda mapema. (Solved)

    Kanusha sentensi ifuatayo bila kutumia kiunganishi.
    Iwapo mvua itanyesha wakulima watapanda mapema.

    Date posted: September 25, 2019 .    Answers (1)

  • Andika kwa wingi. Seremala huyo alikula ndizi kwa uma. (Solved)

    Andika kwa wingi.
    Seremala huyo alikula ndizi kwa uma.

    Date posted: September 25, 2019 .    Answers (1)

  • Tunga sentensi kwa kutumia kivumishi cha sifa kisichoambishika. (Solved)

    Tunga sentensi kwa kutumia kivumishi cha sifa kisichoambishika.

    Date posted: September 25, 2019 .    Answers (1)

  • Unda nomino dhahania kutokana na kitenzi - abudu. (Solved)

    Unda nomino dhahania kutokana na kitenzi - abudu.

    Date posted: September 25, 2019 .    Answers (1)

  • Ainisha shamirisho katika sentensi ifuatayo . Jane alitengenezewa kiti na fundi kwa nyundo (Solved)

    Ainisha shamirisho katika sentensi ifuatayo .
    Jane alitengenezewa kiti na fundi kwa nyundo

    Date posted: September 25, 2019 .    Answers (1)

  • Tunga sentensi mbili kudhihirisha maana ya vitate rika na lika. (Solved)

    Tunga sentensi mbili kudhihirisha maana ya vitate rika na lika.

    Date posted: September 25, 2019 .    Answers (1)

  • Bainisha matumizi ya 'ni' Kimbieni! Huyu ni mnyama aliyeniuma mguuni. (Solved)

    Bainisha matumizi ya 'ni'
    Kimbieni! Huyu ni mnyama aliyeniuma mguuni.

    Date posted: September 25, 2019 .    Answers (1)

  • Bainisha matumizi ya 'po' katika sentensi ifuatayo. Alipowasili alionyeshwa walipo. (Solved)

    Bainisha matumizi ya 'po' katika sentensi ifuatayo.
    Alipowasili alionyeshwa walipo.

    Date posted: September 25, 2019 .    Answers (1)

  • Tunga sentensi ukitumia kiwakilishi cha pekee cha kusisitiza katika ngeli ya U-U (Solved)

    Tunga sentensi ukitumia kiwakilishi cha pekee cha kusisitiza katika ngeli ya U-U

    Date posted: September 25, 2019 .    Answers (1)

  • Taja msemo mwingine wenye maana sawa na : piga maji (Solved)

    Taja msemo mwingine wenye maana sawa na :
    piga maji.

    Date posted: September 25, 2019 .    Answers (1)

  • Akifisha sentensi ifuatayo: Je ni nani alingoa mti wa kiprono (Solved)

    Akifisha sentensi ifuatayo:
    Je ni nani alingoa mti wa kiprono

    Date posted: September 25, 2019 .    Answers (1)

  • Changanua kwa kutumia jedwali. Yeye alifaulu ingawa hana adabu (Solved)

    Changanua kwa kutumia jedwali.
    Yeye alifaulu ingawa hana adabu

    Date posted: September 25, 2019 .    Answers (1)

  • Nyambua kitenzi 'chwa' katika kauli ya kutendea kisha ukitungie sentensi. (Solved)

    Nyambua kitenzi 'chwa' katika kauli ya kutendea kisha ukitungie sentensi.

    Date posted: September 25, 2019 .    Answers (1)

  • Andika kinyume cha sentensi ifuatayo . Mahindi ya mama yamekua kwa kupata mvua ya kutosha. (Solved)

    Andika kinyume cha sentensi ifuatayo .
    Mahindi ya mama yamekua kwa kupata mvua ya kutosha.

    Date posted: September 25, 2019 .    Answers (1)

  • Ainisha vitenzi katika sentensi ifutayo. Wao watakuja kuwa waandishi maarufu. (Solved)

    Ainisha vitenzi katika sentensi ifutayo.
    Wao watakuja kuwa waandishi maarufu.

    Date posted: September 25, 2019 .    Answers (1)

  • Ainisha mofimu katika neno lifuatalo: Milangoni (Solved)

    Ainisha mofimu katika neno lifuatalo:
    Milangoni

    Date posted: September 25, 2019 .    Answers (1)

  • Upo msemo usemao kuwa kuvunjika kwa mwiko si mwisho wa upishi. (Solved)

    Soma kifungu kisha ujibu maswali
    Upo msemo usemao kuwa kuvunjika kwa mwiko si mwisho wa upishi. Msemo huu unaafiki kabisa ari ya watu wazima wengi ambao licha ya umri wao, wamo mbioni kutafuta elimu ili mbali na kupata nuru, wajiunge na wasomi wengine katika kuikuza na kuiendeleza jamii. Ni kwa sababu hii ndipo serikali, kwa ushirikiano na mashirika mengi yasiyokuwa ya kiserikali, imekuwa mstari wa mbele kutoa tunu hii kwa wazee ili kukata kiu yao ya elimu.
    Watu wengi wa umri wa makamo ambao labda walikosa kumaliza masomo ya kiwango fulani au walikosa kabisa kwenda shuleni kwa sababu mbalimbali, hasa za kifedha, wamekuwa wakiweka elimu kama mojawapo ya majukumu yao ya utuuzima. Hii imekuwa dhahiri hasa baada ya serikali ya Kenya kuanzisha mpango wa elimu bila malipo katika shule za msingi, kwani idadi ya watu wazima ambao wamejitokeza kunufaika na mpango huo haisemeki. Pamoja na mpango huo, wapo wale ambao walikosa kusoma au kumaliza masomo kwa sababu ya karo, na kwa sababu sasa wana mapato, wameazimia kujiendeleza ili wapate vyeti. Hii ndiyo maana si ajabu kuona hata wafungwa kwenye magereza wakifanya mitihani ya kitaifa.
    Elimu ya watu wazima hutekelezwa kwa njia mbalimbali. Kunayo elimu ambayo inalenga kuwapa watu hawa ujuzi wa kujiendeleza kiuchumi. Kutokana na ufundi wanaofundishwa, ambao huwa ni kazi kama useremala, umekanika, ushoni, usonara na kadhalika, huwawezesha kujitegemea kimapato, kwa hivyo wakaweza kuwapa wanao fursa ya kufaidi kile ambacho wao walikikosa.
    Kunayo pia aina ya elimu ya watu wazima ambayo inaegemea maslahi ya watu hawa, hasa mafunzo kuhusu afya na usafi, masuala ya kifamilia na mahusiano na pia suala la ulezi. Kwa kufanya hivi, watu hawa hupata motisha ya kutangamana na watu wengine na kubadilishana nao mawazo kuhusu masuala yanayoathiri maisha yao Ndiyo sababu utapata watu wa aina hii wana ujuzi mkubwa wa kila kitu kinachoendelea katika kila kona ya nchi.
    Aina nyingine ya elimu kwa watu wazima ni ile ya umma, inayohusu hasa masuala ya kisiasa. Mara nyingi, utawaona wakongwe wakipishwa kwenve foleni ili kwenda kupiga kura. Hii ni kwa sababu, mbali na kuwa huenda wakawa wamestaafu kikazi, bado wana jukumu muhimu sana katika kufanya maamuzi ya kisiasa kwa ajili ya vizazi vyao. Hivyo basi, serikali hufanya kila juhudi kuhakikisha kuwa hamasisho imetolewa kwa kila mwananchi, pamoja na kutoa mafunzo ya namna ya kupiga kura ili kura zisiharibike, hasa baada ya mtu kupitia utaratibu mrefu na wenye kuchosha wa kupiga kura. Kwa hili la kisiasa, watu wazima wengi hushangaza kwa jinsi wasivyoweza kushawishika kufanya maamuzi yanayokwenda kinyume na maazimio yao.
    Maswali
    (a) Eleza masuala muhimu katika aya mbili za kwanza kwa maneno 60.
    (b) Fafanua jinsi elimu ya watu wazima hutekelezwa ukitumia maneno 60

    Date posted: September 25, 2019 .    Answers (1)