Trusted since 2008
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Bainisha aina za vishazi katika sentensi hii Watoto walioachwa mayatima wamesaidiwa

Bainisha aina za vishazi katika sentensi hii
Watoto walioachwa mayatima wamesaidiwa

Answers


Kavungya
Watoto wamesaidiwa – kishazi huru
Watoto waliachwa mayatima – kishazi tegemezi
Kavungya answered the question on October 3, 2019 at 12:54

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions

  • Ainisha viambishi na mzizi katika kitenzi Hawakunichokoza (Solved)

    Ainisha viambishi na mzizi katika kitenzi
    Hawakunichokoza

    Date posted: October 3, 2019 .    Answers (1)

  • Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya jedwali. Sisi tulipokuwa shuleni tulisoma kwa bidii. (Solved)

    Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya jedwali.
    Sisi tulipokuwa shuleni tulisoma kwa bidii.

    Date posted: October 3, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza tofauti ya kisarufi ya maneno yaliyopigiwa mstari. i)Hiki ni kitabu cha mwalimu ii)Hiki ni cha mwalimu (Solved)

    Eleza tofauti ya kisarufi ya maneno yaliyopigiwa mstari.
    i)Hiki ni kitabu cha mwalimu
    ii)Hiki ni cha mwalimu

    Date posted: October 3, 2019 .    Answers (1)

  • Andika sifa mbili mbili bainifu za sauti. i)/e/ ii)/n/ (Solved)

    Andika sifa mbili mbili bainifu za sauti.
    i)/e/
    ii)/n/

    Date posted: October 3, 2019 .    Answers (1)

  • UFAHAMUSoma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.Mojawapo kati ya misingi na nguzo za maendeleo uliwenguni ni viwanda. Viwanda ni muhimu kwa kuwa ndivyo vinavyoigeuza malighafi inayopatikana... (Solved)

    UFAHAMU
    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.

    Mojawapo kati ya misingi na nguzo za maendeleo uliwenguni ni viwanda. Viwanda ni muhimu kwa kuwa ndivyo vinavyoigeuza malighafi inayopatikana na kuwa bidhaa zinazoweza kutumiwa na watu. Katika nchi zinazoendelea, ambazo hazina uwezo mkubwa wa mitaji viwanda vinavyoimarika ni vile vidogo. Hivi ni viwanda ambavyo huhusisha amali za mikono. Kuimarika kwa viwanda hivi vidogo kunatokana na sababu mbalimbali.

    Nchi zinazoendelea huwa na masoko finyu sana kwa kuzingatia uwezo wa ununuzi wa wanaolengwa na bidhaa za viwanda . Katika msingi huu viwanda vikubwa vitawiwa ugumu kufanya biashara katika mazingira ambako masoko yake ni finyu au utashi wa bidhaa zake sio mkubwa. Viwanda vidogo pia vinao uwezo wa kuwaajiri wafanyikazi wengi hasa kwa kuwa havina uwezo wa kugharamia mashine. Uajiri huu wa wafanyikazi wengi ni muhimu katika maeneo mengi ambako tatizo la ajira ni mojawapo wa matatizo sugu. Tofauti na mataifa ya kitasmia (yenye viwanda vingi) mataifa mengi yanayoendelea hayana mifumo imara ya kuwakimu watu wasiokuwa na kazi. Utegemezi wa jamaa wanaofanya kazi kwa hivyo unakuwa nyenzo ya pekee ya kuyamudu maisha.

    Kuanzisha viwanda vidogo vidogo hakuhitaji mtaji mkubwa tofauti na viwanda vikubwa. Hali hii inasahilisha uwezekano wa watu wengi kujasurisha shughuli yoyote ile. Sambamba na suala hili ni kuwa ni rahisi kujarisha bidhaa mpya kwa kiwango kidogo cha kiwanda kidogo. Ikiwa mzalishaji yeyote atazalisha bidhaa mpya kwa mapanu, kwa mfano kama ilivyo kwa viwanda vikubwa, pana uwezekano wa kupata hasara kubwa. Huenda utashi wa bidhaa hiyo uwe mdogo ukilinganishwa na ugavi wa bidhaa yenyewe. Majaribio mazuri huwa ni kwa kiwango kidogo.

    Kuwepo kwa viwanda vidogo huwa chocheo kubwa la usambazaji wa viwanda hadi maeneo ya mashambani. Hali hii inahakikisha kuwa nafasi za ajira zimezambazwa nchini hali ambayo inasaidia kuhakikisha kuwa pana mweneo mzuri wa kimapato nchini. Mweneo huo wa mapato unachangia katika kuboresha uwezo wa kiununuzi wa umma. Huu ni msingi muhimu wa maendeleo. Upanuzi na ueneaji wa viwanda vidogo vidogo ni msingi mkubwa wa kujitegemea kiuchumi. Aghalabu viwanda vikubwa huegemea kwenye mitaji ya mashirika ya kimataifa na huwa msingi wa kuendelezwa kwa utegemezi wa kiuchumi.

    Maswali
    a)Kwa nini viwanda ni muhimu?
    b)Ni nini kiini cha matatizo ya uuzaji wa bidhaa katika nchi zinazoendelea?
    c)Eleza faida zinazotokana na kuwepo kwa viwanda vidogo vidogo.
    d)Usambazaji wa viwanda katika maeneo ya mashambani una faida gani?
    e)Fafanua maana ya msamiati huu kama ulivyotumika katika kifungu.
    i)Kujasurisha
    ii)Amali
    iii)Utashi

    Date posted: October 3, 2019 .    Answers (1)

  • Onyesha aina za virai katika sentensi hii. Wazazi wetu watawasili kesho saa tatu. (Solved)

    Onyesha aina za virai katika sentensi hii.
    Wazazi wetu watawasili kesho saa tatu.

    Date posted: October 3, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza matumizi mawili ya "ka". (Solved)

    Eleza matumizi mawili ya "ka".

    Date posted: October 3, 2019 .    Answers (1)

  • Tambua hali katika sentensi ifuatayo. Vyungu vya aina hii vyafinyangwa na huyu. (Solved)

    Tambua hali katika sentensi ifuatayo.
    Vyungu vya aina hii vyafinyangwa na huyu.

    Date posted: October 3, 2019 .    Answers (1)

  • Tumia kitenzi "amerudi" kuonyesha dhana tatu za kiimbo. (Solved)

    Tumia kitenzi "amerudi" kuonyesha dhana tatu za kiimbo.

    Date posted: October 3, 2019 .    Answers (1)

  • Tunga sentensi ukitumia yambwa tendwa na yambwa tendewa. (Solved)

    Tunga sentensi ukitumia yambwa tendwa na yambwa tendewa.

    Date posted: October 3, 2019 .    Answers (1)

  • Onyesha matumizi ya kiambishi "ni" katika sentensi ifuatayo: Maria ni mpole ndio maana ninapenda kwenda kwao. (Solved)

    Onyesha matumizi ya kiambishi "ni" katika sentensi ifuatayo:
    Maria ni mpole ndio maana ninapenda kwenda kwao.

    Date posted: October 3, 2019 .    Answers (1)

  • Andika sentensi ifuatayo katika wakati ujao hali ya kuendelea. Juma anafundisha katika shule hii. (Solved)

    Andika sentensi ifuatayo katika wakati ujao hali ya kuendelea.
    Juma anafundisha katika shule hii.

    Date posted: October 3, 2019 .    Answers (1)

  • Uzi iko kwa ngeli gani? (Solved)

    Uzi iko kwa ngeli gani?

    Date posted: October 3, 2019 .    Answers (1)

  • Weka "kiziwi" kwa ngeli yake. (Solved)

    Weka "kiziwi" kwa ngeli yake.

    Date posted: October 3, 2019 .    Answers (1)

  • Tumia neno "Nairobi" katika sentensi kama : (Solved)

    Tumia neno "Nairobi" katika sentensi kama :
    i) Nomino
    ii) Kielezi

    Date posted: October 3, 2019 .    Answers (1)

  • Tunga sentesi moja kutofautisha maana ya: ngoma goma (Solved)

    Tunga sentesi moja kutofautisha maana ya:
    ngoma
    goma

    Date posted: October 3, 2019 .    Answers (1)

  • Ainisha viambishi katika kitenzi kifuatacho. Walimtembelea (Solved)

    Ainisha viambishi katika kitenzi kifuatacho.
    Walimtembelea

    Date posted: October 3, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza maana ya sentensi ya masharti. (Solved)

    Eleza maana ya sentensi ya masharti.

    Date posted: October 3, 2019 .    Answers (1)

  • Andika sifa mbili za irabu / u / (Solved)

    Andika sifa mbili za irabu / u /

    Date posted: October 3, 2019 .    Answers (1)

  • Aibu kubwa ya taifa kushindwa kukabiliana na tatizo sugu la ajali za barabarani bado inaendelea kuwafedhehesha wahusika katika sekta ya uchukuzi na mawasiliano licha ya... (Solved)

    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
    Aibu kubwa ya taifa kushindwa kukabiliana na tatizo sugu la ajali za barabarani bado inaendelea kuwafedhehesha wahusika katika sekta ya uchukuzi na mawasiliano licha ya matumizi ya vidhibiti mwendo na kanda za usalama.
    Ajali za barabarani zinaangamiza idadi kubwa ya watu kila mwaka wakiwemo viongozi na watu mashuhuri. Miongoni mwa sababu ambazo zinaleta maafa barabarani pamoja na uendeshaji kasi kupita inavyotakikana, yaani kukiuka masharti yaliyowekwa na wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano. Madereva wengi hung‘oa vidhibiti mwendo vilivyowekwa, hawarekebishi mikanda ya usalama, wala hawayapeleki magari yao kukaguliwa mara kwa mara kama inavyopaswa. Yale yanayopelekwa kwa ukaguzi, mengi hushindwa kutekeleza kanuni zilizoweka kwa hivyo hutegemea hongo kuwa barabarani. Fauka ya hayo, madereva wa malori na matrela mara nyingi huendesha magari hayo wakiwa walevi. Dawa za kulevya kama miraa na bangi hutumiwa sana na hawa na matokeo yake huwa ajali mbaya.
    Hata hivyo, lawama haiwezi kuelekezewa madereva pekee. Ukiangazia barabara nchini Kenya utapata kuwa barabara haziko katika hali nzuri. Zile za lami zimekuwa na mashimo makubwa ambapo mvua ikinyesha hufanya vidimbwi mithili ya michimbo ya madini yaliyojaa maji baada ya kuachwa wazi. Na zile barabara zisizokuwa na lami zimeharibika kiasi kwamba
    ni vigumu kuzitofautisha na njia za ng‘ombe kwenye maeneo kame. Kinachohitajika ni kuzirudisha katika kiwango ambacho zinaweza kufaa tena.
    Wananchi pia inafaa waelimishwe ili wasikubali kupanda magari ambayo tayari yamejaa. Hili litawasaidia wananchi wenyewe kudumisha usalama wao barabarani. Pia inawafaa watambue ya kwamba wana jukumu la kuwaarifu walinda usalama endapo dereva anaendesha kwa kasi kuliko ile ya kilomita themanini kwa saa iliyokubaliwa. Inafahamika kuwa maafia wa usalama ndio wafisadi zaidi, hivyo basi huchangia katika kuongeza idadi ya vifo barabarani. Katika vita vya ufisadi na ajali za barabarani ni mwanachi mwenyewe ambaye atawezesha kukomesha hali hii. Kwa mfano, afisa wa usalama akipatikana akichukua hongo, yeye pamoja na yule aliyetoa hongo wakamatwe na kupelekwa kwenye vituo vya kukabiliana na ufisadi na kuchukuliwa hatua kali, matatizo haya yataisha. Lakini kabla kufikia hapo, ni muhimu kumhamasisha mwananchi kuhusu haki zake na namna ya kukabiliana na suala hili la ufisadi. Hali hii inatuonyesha kwamba mipango maalum inapaswa kufanywa na serikali ili kuwaelimisha wananchi kama hatua ya kwanza kukabiliana na ufisadi, hatimaye izilainishe sekta zote wala si ya uchukuzi na mawasiliano pekee.
    (a) Kwa kurejelea aya ya pili na ya tatu, eleza mambo yanayochangia ajali za barabarani. (Maneno 45-50)
    (b) Fupisha ujumbe wa aya ya mwisho. (maneno 50-55)
    (c) Mbali na ajali za barabarani, taja, tatizo lingine sugu ambalo linakumba nchi ya Kenya
    (d) Mwandishi anapendekeza hatua zipi zichukuliwe na serikali ili suluhisho la kudumu
    lipatikane?
    (e) Taja hatua ambazo serikali imechukua ili kuimarisha uchukuzi
    (f) Ni kitu gani ambacho kinaonyesha kuwa serikali imeshindwa kukabiliana na ajali
    barabarani?
    (g) Eleza maana ya maneno haya:-
    (i) Tatizo sugu.
    (ii) Vithibiti mwendo.
    (iii) Machimbo.
    (iv) Ukarabati.
    (v) Hongo.
    (vi) Kuhamasisha..

    Date posted: October 3, 2019 .    Answers (1)