Trusted since 2008
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

"Na mwamba ngoma huvuta wapi?" a. Eleza muktadha wa dondoo hili. b. Tambua tamathali mbili za sauti zilizotumika katika muktadha huo. c. Fafanua sifa za msemewa wa...

"Na mwamba ngoma huvuta wapi?"

a. Eleza muktadha wa dondoo hili.

b. Tambua tamathali mbili za sauti zilizotumika katika muktadha huo.

c. Fafanua sifa za msemewa wa maneno.

d. Thibitisha ukweli kuwa kila mwamba ngoma huvuta kwake ukirejelea Tamthilia nzima ya Kigogo.

Answers


Martin
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili

(i) Msemajio ni Kenga
(ii) Msemewa ni Majoka
(iii) Wako katika ofisi ya Majoka
(iv) Ni baada ya Majoka kumwelezea kuhusu habari gazetini kuhus umaarufu wa Tunu


(b) Tambua tamathali mbili za semi zilizotumika katika muktadha huu

(i) Methali – mwamba ngoma huvuta……
(ii) Swala la balagha - huvuta wapi?


(c) Fafanua sifa sita za msemewa wa maneno haya

Msemewa ni Majoka
(i) Ni katili – alishiriki katika mauaji ya Jabali
(ii) Ni mkware - Alikuwa amemuoa Husda lakini alitaka kujihusisha kimapenzi na Ashua
(iii) Ni mpyaro – aliwatukana wanasagamoyo wajinga
(iv) Ni fisadi – alinyakua mali ya uma kam vile soko la chapakazi
(v) Ni msaliti – Aliwasliti wanasagamoyo kwa kuwa walimchagua ilhali anajinufaisha yeye, pia anamsaliti Husda kimapenzi.
(vi) Ni mwenye dharau
(vii) Ni laghai
(viii) Ni dikteta
(ix) Ni mwoga

d) Thibitisha ukweli kuwa kila mwamba ngoma huvuta kwake ukirejelea Tamthilia nzima ya Kigogo.
(i) Kenga anamfuata Majoka na uongozi dhalimu kwani ananufaika nao. Mfano ardhi
(ii) Ngurumo anaunga mkono uongozi thalimu wa Majoka ili aendelee kunufaika. Mfano pombe.
(iii) Mama pima anautetea uongozi wa Majoka kwa kuwa ananufaika nao, mfano. Kandarasi ya kuoka keki, kibali cha kuuza pombe haramu
(iv) Majoka ana ari ya kuwafurusha wafanyabiashara kutoka sokoni ili alinyakue kwa matumizi yake kibinafsi ya kujenga hoteli ya kifahari.
(v) Wafadhili wa kina Tunu wanatia habari chumvi kuhusu umaarufu wa Tunu.
(vi) Wanapolisi wanayafuata maagizo ya Majoka ya kuwashambulia wanasagamoyo ili walinde kazi yao.
(vii) Chopi anatekeleza uhuni wa Majoka ndiposa asije akamwaga unga wake. (Kufutwa kazi)
(viii) Husda anaolewa na Majoka kwa sababu ya utajiri wa Majoka.
Boza anajipendekeza kwa kenga ili apewe mradi wa kuchonga kinyago. Pia anasema mke wake ndiye aliyeioka keki
marto answered the question on October 15, 2019 at 07:36

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions

  • Nina jambo muhimu, nyi wakubwa kwa wadogo, Kuwa tabia alimu, usiubwage gogo, Mtu kukosa nidhamu, ja mtu akili ndogo, Tabia... (Solved)

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali

    Nina jambo muhimu, nyi wakubwa kwa wadogo,
    Kuwa tabia alimu, usiubwage gogo,
    Mtu kukosa nidhamu, ja mtu akili ndogo,
    Tabia njema ni utu.

    Walezi nawaambia, wafunze tabia wana,
    Ili wanapokua, wenye heshima maana,
    Mtu kukosa tabia, ni kama mti bila shina,
    Tabia njema ni utu.

    Hutuzidisha hisia, kufurahisha roho,
    Gumu tuepushia, linalotumiza roho,
    Mtu kukosa twabia, nikiumbe bila roho,
    Tabia njema ni utu.

    Wanafunzi nao pia, shuleni sizushe bala,
    Ili masomo kubia, bila mambo ya kifala,
    Mtu kukosa twabia, dereva toroli bila,
    Tabia njema ni utu.

    Mahabani walioa, sio urembo mwingi,
    Bali hasa ni tabia, utu mapenzi mengi,
    Mtu kukosa tabia, kama nyumba bila msingi,
    Tabia njema ni utu.

    Shuleni vijijinia, amani dumu kujali,
    Sababu kuwa tabia, lizingatiwa aali,
    Mtu kukosa tabia, ni kisu bila makali,
    Tabia njema ni utu.

    Rafiki kukupendea, sio kwa uzuri eti,
    Bali ni hasa tabia, ndani yako wima uti,
    Mtu kukosa tabia, ni kiumbe bila uti,
    Tabia njema ni utu.

    Tamati kuachia, kwamba jambo aali,
    Mengi ningewambia, lakini metoshekali,
    Mtu kukosa tabia, ni kiatu bila soli,
    Tabia njema ni utu.

    Maswali
    1.Pendekeza kichwa mwafaka cha ushairi uliosoma.
    2.Toa bahari tatu tofauti za ushairi huu na uzifafanue.
    3.Fafanua muundo wa shairi hili.
    4. Onyesha jinsi idhini ya mshairi imetumika.
    5. Taja na ueleze mbinu za lugha zilizotumika katika shairi hili.
    6. Andika ubeti wa sita katika lugha ya tutumbi.
    7. Eleza maana ya maneno haya kwa mujibu wa shairi ulilosoma.
    i) Shina.
    ii)Wima.

    Date posted: October 8, 2019 .    Answers (1)

  • Jadili jinsi mwigizaji anaweza kuboresha utanzu wake jukwaani (Solved)

    Jadili jinsi mwigizaji anaweza kuboresha utanzu wake jukwaani

    Date posted: October 8, 2019 .    Answers (1)

  • Kwa kurejelea hadithi ya Mke Wangu eleza mambo yanayochangia kuimarika kwa ndoa (Solved)

    Kwa kurejelea hadithi ya Mke Wangu eleza mambo yanayochangia kuimarika kwa ndoa

    Date posted: October 5, 2019 .    Answers (1)

  • Tamthilia ya Mstahiki Meya ni taswira kamili ya mataifa mengi barani Afrika. Thibitisha kauli hii (Solved)

    Tamthilia ya Mstahiki Meya ni taswira kamili ya mataifa mengi barani Afrika. Thibitisha kauli hii

    Date posted: October 5, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza jinsi mbinu ya tabaini inavyojitokeza katika riwaya ya kidagaa kimemwozea (Solved)

    Eleza jinsi mbinu ya tabaini inavyojitokeza katika riwaya ya kidagaa kimemwozea

    Date posted: October 5, 2019 .    Answers (1)

  • “Hawa ndio watu muhimu katika ulimwengu wa sasa” (Solved)

    “Hawa ndio watu muhimu katika ulimwengu wa sasa”

    a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    b) Fafanua mchango wa mrejelewa katika kusambaratisha baraza la Cheneo.
    c) Cheneo imekandamizwa kutokana na wakazi wake kutotumia akili. Fafanua kauli hii kwa kurejelea tamthilia nzima.

    Date posted: October 5, 2019 .    Answers (1)

  • …unaa…seema mimiiii sipakui?...wataka mimi nipike? Ehee? Ati mimi nalaza damu? Wewe unaiamsha damu? (Solved)

    …unaa…seema mimiiii sipakui?...wataka mimi nipike? Ehee? Ati mimi nalaza damu? Wewe unaiamsha damu?

    a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
    b) Eleza mbinu zozote tatu za lugha zilizotumika katika dondoo hili.
    c) Jadili ufaafu wa anwani kwa kurejelea mnenaji.

    Date posted: October 5, 2019 .    Answers (1)

  • Vile lelo walalama, kwa yale ulotendewa, Huyakumbuki ya nyuma, pindi ulipochachawa, (Solved)

    Vile lelo walalama, kwa yale ulotendewa,
    Huyakumbuki ya nyuma, pindi ulipochachawa,
    Ulipotenda unyama, uliona ndiyo sawa,
    Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa!

    Ulizusha uhasama, leo wewe wapagawa,
    Walia bila kukoma, tungadhani umefiwa,
    Sasa huna usalama, huwezi kujiopowa
    Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa!

    Tenda mambo kwa kupima, usiruke huna mbawa,
    Una macho kutazama, na akili umepewa,
    Matendo hurudi nyuma, atendaye hurudiwa,
    Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa!

    Dunia haishi njama, sijione umepewa,
    Ukadhani usalama, binadamu kuwagawa,
    Ukahisi ni wanyama, waso hali kama ngawa,
    Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa!

    Unapotenda zahama, siku yako itakuwa,
    Ambapo utaungama, useme umechachiwa,
    Na uanze kutetema, ulie umeonewa,
    Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa.


    Maswali
    a) Lipe shairi hili kichwa mwafaka.
    b) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu.
    c) Eleza muundo wa ubeti wa pili.
    d) Ni kaida zipi za utunzi zilizozingatiwa na mshairi?
    e) Andika ubeti wa kwanza kwa lugha ya mjazo.
    f) Toa mifano miwili ya idhini ya mshairi.
    g) Kwa nini msemewa hafai kulalamika ?
    h) Eleza maana ya maneno yafuatayo.
    i) Uhasama
    ii) Umepowa

    Date posted: October 5, 2019 .    Answers (1)

  • Tafautisha kati ya; Ngonjera za ushairi na za maigizo. (Solved)

    Tafautisha kati ya;
    Ngonjera za ushairi na za maigizo.

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Onyesha kwa kutolea mifano minne, jinsi misimu huzuka. (Solved)

    Onyesha kwa kutolea mifano minne, jinsi misimu huzuka.

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Thibitisha kauli kuwa, "Mla naye huliwa zamu yake ifukapo". Ukirejelea riwaya ya Kidagaa Kimemwozea. (Solved)

    Thibitisha kauli kuwa, "Mla naye huliwa zamu yake ifukapo". Ukirejelea riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • "Siku moja kabla ya kufika kwa wageni. Meya ana mkutano na wawakilishi wa wafanyikaziambao wameketi mkabala naye". (Solved)

    Mtahiki Meya; Timothy Arege
    "Siku moja kabla ya kufika kwa wageni. Meya ana mkutano na wawakilishi wa wafanyikazi ambao wameketi mkabala naye".
    (a) Fafanua madai yaliyotolewa na wafanyakazi katika mkutano huu.
    (b) Eleza jinsi Meya alivyojibu madai ya wawakilishi wa wafanyakazi.

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Wanawake, wanaoishi katika maeneo ya mashambani katika nchi ambazo zinazoendelea ni baadhi ya watu waliotopea na kubobea katika uchochole mkubwa. (Solved)

    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yafuatayo.
    Wanawake, wanaoishi katika maeneo ya mashambani katika nchi ambazo zinazoendelea ni baadhi ya watu waliotopea na kubobea katika uchochole mkubwa. Jumla ya idadi kubwa ya wanawake hawa wanaoishi chini ya kiwango cha chini, cha umaskini inakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 600. Hii ni idadi kubwa hasa ikikumbukwa kuwa ni asilimia kubwa ya wanawake inayoishi kwa maeneo haya. Ulimwengu umeshuhudia ongezeko kubwa la idadi ya watu pamoja na kuwako kwa matatizo ya kiuchumi duniani.Kadhalika matatizo mengine ni mitarafuku na vita vya kikabila, majanga ya kiasili mathalani mafuriko , ukame na milipuko ya volkano. Usisahau kuwa pia kina uharibifu wa kimazingira, mabadiliko ya desturi na kusambaratika kwa familia na misingi yake. Tatizo lingine ni kuwa kuna kuongezeka kwa hali ya wanawake kuwa wazazi pekee na hivyo kuongeza familia zinazosimamiwa na wanawake ( ambao tumewataja kuwa wanakumbwa na umaskini mkubwa).Wanawake wanaoishi mashambani wanakumbwa na makubwa. Kwanza, kama maskini wanaishi katika mazingiramagumu. Vile vile kama wanawake wanakabiliana na mapendeleo ya kisera na kitamaduni yanayowadharau na kuwapuuza wanawake na mchango wao katika maendeleo. Tatu, kama viongozi wa familia hasa wanaolea na kutunza jamaa na mzazi mmoja, wanapambana na uogonzi wa familia pamoja na uzalishaji. Aghalabu hawapati usaidizi wowote katika majukumu kama haya bali wanalazimika kupambana nayo peke yao. Kutokana na hayo yote wanawake hawapati nafasi nzuri kushiriki katika maamuzi ya maswala yanayowahusu. Maswala mengi yanaamuliwa na wanaume pasipokuwahusisha wanawake. Licha ya dhiki yao kubwa, wanawake hawa wanachangia katika maendeleo ya jammi na kiuchumi kwa njia mbalimbali. Mchango huu unaonekana katika kiwango cha jamii,taifa na familia. Katika kiwango cha kijamii na kitaifa wanawake ndio chazo cha nguvukazi kwani ni wao na watoto wao wanatekeleza kazi nyingi hasa za nyumbani na mashambani. Mara nyingi huwa na uwezo bora wa kutunza chochote walichonacho kuliko wenzao wanaume.
    Kifamilia wanawake wa shambani wanashughulika mchana kutwa katika hali ngumu ya hewa aidha jua kali au mvua huku wameeleka wanao migongoni wakilima mashamba ili kupata chakula kwa familia zao. Jukumu la kuandaa chakula nyumbani bado linaachiwa wale wale wanawake wanaokizalisha mashambani.
    Jambo lisilopingika ni kwamba wanawake wanatekeleza majuku makubwa na muhimu katika kizazi cha binadamu na ndio hasa miimili ya jamii yoyote staarabu. Kwa hivyo, ni kinaya kitupu kudhalilisha wanawake. Mataifa mengi yaliyoendelea ni yale yaliyoondoa vikwazo vyote mbele ya wanawake na kuwaacha watekeleze wajibu wao. Kadhalika wanaume wa huko wanawaona wanawake kama wenzao katika kujenga jamii wala sio watumwa au watumishi wao wanaoumia na kutumikishwa kama vifaa na bidhaa. Inafaa jamii zinazodinisha wanawake zitambue kuwa ubaya wa tendo hili sio tu kudumaza maendeleo yake bali pia kutoa mfano mbaya kwa vijana ambao wataendeleza Ukandamizaji huu kwa vizazi vijavyo. Kwa hivyo, jamii inawajibika kutenda lililo sawa kwa kuwapa hadhi wanawake wote.

    Maswali
    a) Ipe taarifa hii anwani mwafaka
    b) Nakili maafa matatu ya kimaumbile yaliyotajwa katika kifungu hiki.
    c) Eleza sababu tatu zinazowazuia wanawake kushiriki katika maamuzi ya masuala yanayowahusu kulingana na makala haya.
    d) Wanawake hutekeleza majukumu gani katika jamii na taifa kutokana na makala haya?
    e) Kuna tofauti gani baina ya wanawake wa mataifa yaliyoendelea nay ale ambayo hayajastawi.
    f) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa kwenye taarifa:
    i) uchochole
    ii) kudhalilisha
    iii) mitafuruku

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Jadili changamoto za elimu katika hadithi ya Kanda la Usufi. (Solved)

    Jadili changamoto za elimu katika hadithi ya Kanda la Usufi.

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Uongozi mbaya una athari kadhaa. Thibitisha madai haya kwa kurejelea Tamthili ya Mstahiki Meya. (Solved)

    Uongozi mbaya una athari kadhaa. Thibitisha madai haya kwa kurejelea Tamthili ya Mstahiki Meya.

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Ndiyo yale ya "ngome in‘tuumiza naswi tu mumo ngomeni.‘ (Solved)

    Mshtahiki Meya: T. Arege
    Ndiyo yale ya "ngome in‘tuumiza naswi tu mumo ngomeni.‘
    a) Weka dondoo hili katika muktadha wake.
    b) Tambua tamathali mbili za usemi zilizo tumika latika dondoo hili.
    c) Kwa kurejelea tamthilia onyesha jinsi ngome inavyowaumiza wanacheneo.
    d) Wanacheneo wanatumia mikakati gani kukabiliana na hali ya (c) hapo juu.

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Onyesha jinsi mwandishi wa Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea alivyoshughulikia Nafasi ya mwanamke. (Solved)

    Onyesha jinsi mwandishi wa Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea alivyoshughulikia Nafasi ya mwanamke.

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Onyesha jinsi mwandishi wa Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea alivyoshughulikia Nafasi ya vijana. (Solved)

    Onyesha jinsi mwandishi wa Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea alivyoshughulikia Nafasi ya vijana.

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Kuna mfanano mkubwa kati ya ulumbi na hotuba. Thibitisha. (Solved)

    Kuna mfanano mkubwa kati ya ulumbi na hotuba. Thibitisha.

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • "Wema wako umeniua kabisa………Nina jishtaki mwenyewe kila siku kwa miaka na miaka". (Solved)

    KIDAGAA KIMEMWOZEA: Ken Walibora.
    "Wema wako umeniua kabisa………Nina jishtaki mwenyewe kila siku kwa miaka na miaka".
    (a) Eleza muktadha wa maneno haya.
    (b) Onyesha kwa kutoa mifano kuwa anayeambiwa maneno haya alikuwa na wema.
    (c) Eleza umuhimu wa mhusika mashaka katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.

    Date posted: October 3, 2019 .    Answers (1)