Trusted since 2008
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Liandikwalo ndilo liwalo? Since when has man ever changed his destiny? Eleza muktadha wa dondoo hili.....

Chozi la heri
Liandikwalo ndilo liwalo? Since when has man ever changed his destiny?
Eleza muktadha wa dondoo hili.
Bainisha mbinu tatu za kimtindo zinazojitokeza katika dondoo hili.
Kwa kuzingatia hoja kumi, jadili jinsi ambavyo hali ya, liandikwalo ndilo liwalo, inavyojitokeza katika Chozi la Heri.

Answers


ESTHER
Liandikwalo ndilo liwalo? Since when has man ever changed his destiny?
Eleza muktadha wa dondoo hili. Alama 4
Maneno ya Terry
Akimwambia Ridhaa
Nyumbani kwao
Baada ya kugundua kuwa anaamini ushirikina
Au
Ni mawazo ya Ridhaa akikumbuka maneno aliyoambiwa na mkewe Terry
Kwa sababu ya kuamini kuwa milio ya bundi na kerengende huashiria jambo Fulani lingefanyika.
Yuko kando ya vifusi vya nyumba yake iliyochomwa
Baada ya familia yake kuchomewa ndani
4x1 =4
Bainisha mbinu tatu za kimtindo zinazojitokeza katika dondoo hili. Alama 6
Methali-liandikwalo ndilo liwalo
Kuhamisha ndimi/msimbo-kauli ya kutumia sentensi nzima kwa lugha nyingine.
Since when has man ever changed his destiny?
Tanbihi: mbinu hii si kuchanganya ndimi.Atakayeandika hivi asituzwe.
Swali la balagha- liandikwalo ndilo liwalo?
Since when has man ever changed his destiny?
3x2=6
Kwa kuzingatia hoja kumi, jadili jinsi ambavyo hali ya, liandikwalo ndilo liwalo, inavyojitokeza katika Chozi la Heri. Alama 10.
-Neema na Mwangemi wanajitahidi kupata mtoto lakini hawafanikiwi na wanaishia kumpanga Mwaliko.
-Wafuasi wa Mwanzi wanajaribu kushinda ushindi wa Mwekevu lakini wanashindwa.
-Kaizari anajitahidi kuzuia wahuni wasiwabake binti zake lakini wanamzidi nguvu na kuwabaka.
-Lunga anajitahidi kumrithia na kumpendeza mkewe Naomi lakini hatimaye anamtoroka na kumwachia Watoto
-Kiriri anampinga Annette asiende ughaibuni lakini anampuuza na kuhamia huko.
-Kiriri anawasihi wanawe warudi nyumbani lakini waliendelea kuishi ughaibuni hata baada ya kukamilisha masomo yao.
-nyanyake Pete anajizatiti kupinga ndoa ya Pete lakini hatimaye Pete anaozwa.
-Kipanga anataka kuambiwa babake halisi baada ya aliyemdhania kuwa babake kumkana lakini mamake hakumwambia.
-hata baada ya mabwanyenye kutoa hongo ili nyumba zao zisibomolewe katika mtaa wa Tononokeni, zianbomolewa.
-Dick anakataa kutumiwa na Buda kulangua dawa za kulevya lakini anamtishia na baadaye kuuza dawa za kulevya.
-Naomi alimtoroka Lunga kwa sababu ya umaskini lakini anaishia kuteseka Zaidi na baadaye kufa
-Amize Lucia wanajizatiti kupinga ndoa ya Lucia lakini baadaye Lucia anaolewa.
-Wanaume wanatishia kumtusi Mwekevu anapojitosa siasani ili kumvunja moyo lakini anavumilia mpaka anachaguliwa kuwa kiongozi wa Wahafidhina.
-Pete anakunywa dawa ya kuua panya ili afe lakini anapelekwa katika kituo cha afya cha Mwanzo Mpya na kuendelea kuishi.
-Pete anajaribu kuavya mimba ya mtoto wake wa pili na wa tatu lakini anaishia kuwazaa Watoto hawa.
ESTHER STEVE answered the question on April 1, 2020 at 01:23

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions

  • "...wanahofia kusema wasije wakavikata viganja vinavyowalisha..." a. Eleza muktadha wa dondoo hili. b. Taja maudhui yanayojitokeza katika dondoo hili na ueleze. c. Kwa kutoa hoja kumi, eleza namna... (Solved)

    "...wanahofia kusema wasije wakavikata viganja vinavyowalisha..."

    a. Eleza muktadha wa dondoo hili.

    b. Taja maudhui yanayojitokeza katika dondoo hili na ueleze.

    c. Kwa kutoa hoja kumi, eleza namna maudhui uliyotaja hapo juu (2b) yanavyojitokeza katika riwaya.

    d. Eleza sifa nne za msemaji

    Date posted: October 15, 2019 .    Answers (1)

  • "Na mwamba ngoma huvuta wapi?" a. Eleza muktadha wa dondoo hili. b. Tambua tamathali mbili za sauti zilizotumika katika muktadha huo. c. Fafanua sifa za msemewa wa... (Solved)

    "Na mwamba ngoma huvuta wapi?"

    a. Eleza muktadha wa dondoo hili.

    b. Tambua tamathali mbili za sauti zilizotumika katika muktadha huo.

    c. Fafanua sifa za msemewa wa maneno.

    d. Thibitisha ukweli kuwa kila mwamba ngoma huvuta kwake ukirejelea Tamthilia nzima ya Kigogo.

    Date posted: October 15, 2019 .    Answers (1)

  • Nina jambo muhimu, nyi wakubwa kwa wadogo, Kuwa tabia alimu, usiubwage gogo, Mtu kukosa nidhamu, ja mtu akili ndogo, Tabia... (Solved)

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali

    Nina jambo muhimu, nyi wakubwa kwa wadogo,
    Kuwa tabia alimu, usiubwage gogo,
    Mtu kukosa nidhamu, ja mtu akili ndogo,
    Tabia njema ni utu.

    Walezi nawaambia, wafunze tabia wana,
    Ili wanapokua, wenye heshima maana,
    Mtu kukosa tabia, ni kama mti bila shina,
    Tabia njema ni utu.

    Hutuzidisha hisia, kufurahisha roho,
    Gumu tuepushia, linalotumiza roho,
    Mtu kukosa twabia, nikiumbe bila roho,
    Tabia njema ni utu.

    Wanafunzi nao pia, shuleni sizushe bala,
    Ili masomo kubia, bila mambo ya kifala,
    Mtu kukosa twabia, dereva toroli bila,
    Tabia njema ni utu.

    Mahabani walioa, sio urembo mwingi,
    Bali hasa ni tabia, utu mapenzi mengi,
    Mtu kukosa tabia, kama nyumba bila msingi,
    Tabia njema ni utu.

    Shuleni vijijinia, amani dumu kujali,
    Sababu kuwa tabia, lizingatiwa aali,
    Mtu kukosa tabia, ni kisu bila makali,
    Tabia njema ni utu.

    Rafiki kukupendea, sio kwa uzuri eti,
    Bali ni hasa tabia, ndani yako wima uti,
    Mtu kukosa tabia, ni kiumbe bila uti,
    Tabia njema ni utu.

    Tamati kuachia, kwamba jambo aali,
    Mengi ningewambia, lakini metoshekali,
    Mtu kukosa tabia, ni kiatu bila soli,
    Tabia njema ni utu.

    Maswali
    1.Pendekeza kichwa mwafaka cha ushairi uliosoma.
    2.Toa bahari tatu tofauti za ushairi huu na uzifafanue.
    3.Fafanua muundo wa shairi hili.
    4. Onyesha jinsi idhini ya mshairi imetumika.
    5. Taja na ueleze mbinu za lugha zilizotumika katika shairi hili.
    6. Andika ubeti wa sita katika lugha ya tutumbi.
    7. Eleza maana ya maneno haya kwa mujibu wa shairi ulilosoma.
    i) Shina.
    ii)Wima.

    Date posted: October 8, 2019 .    Answers (1)

  • Jadili jinsi mwigizaji anaweza kuboresha utanzu wake jukwaani (Solved)

    Jadili jinsi mwigizaji anaweza kuboresha utanzu wake jukwaani

    Date posted: October 8, 2019 .    Answers (1)

  • Kwa kurejelea hadithi ya Mke Wangu eleza mambo yanayochangia kuimarika kwa ndoa (Solved)

    Kwa kurejelea hadithi ya Mke Wangu eleza mambo yanayochangia kuimarika kwa ndoa

    Date posted: October 5, 2019 .    Answers (1)

  • Tamthilia ya Mstahiki Meya ni taswira kamili ya mataifa mengi barani Afrika. Thibitisha kauli hii (Solved)

    Tamthilia ya Mstahiki Meya ni taswira kamili ya mataifa mengi barani Afrika. Thibitisha kauli hii

    Date posted: October 5, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza jinsi mbinu ya tabaini inavyojitokeza katika riwaya ya kidagaa kimemwozea (Solved)

    Eleza jinsi mbinu ya tabaini inavyojitokeza katika riwaya ya kidagaa kimemwozea

    Date posted: October 5, 2019 .    Answers (1)

  • “Hawa ndio watu muhimu katika ulimwengu wa sasa” (Solved)

    “Hawa ndio watu muhimu katika ulimwengu wa sasa”

    a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    b) Fafanua mchango wa mrejelewa katika kusambaratisha baraza la Cheneo.
    c) Cheneo imekandamizwa kutokana na wakazi wake kutotumia akili. Fafanua kauli hii kwa kurejelea tamthilia nzima.

    Date posted: October 5, 2019 .    Answers (1)

  • …unaa…seema mimiiii sipakui?...wataka mimi nipike? Ehee? Ati mimi nalaza damu? Wewe unaiamsha damu? (Solved)

    …unaa…seema mimiiii sipakui?...wataka mimi nipike? Ehee? Ati mimi nalaza damu? Wewe unaiamsha damu?

    a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
    b) Eleza mbinu zozote tatu za lugha zilizotumika katika dondoo hili.
    c) Jadili ufaafu wa anwani kwa kurejelea mnenaji.

    Date posted: October 5, 2019 .    Answers (1)

  • Vile lelo walalama, kwa yale ulotendewa, Huyakumbuki ya nyuma, pindi ulipochachawa, (Solved)

    Vile lelo walalama, kwa yale ulotendewa,
    Huyakumbuki ya nyuma, pindi ulipochachawa,
    Ulipotenda unyama, uliona ndiyo sawa,
    Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa!

    Ulizusha uhasama, leo wewe wapagawa,
    Walia bila kukoma, tungadhani umefiwa,
    Sasa huna usalama, huwezi kujiopowa
    Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa!

    Tenda mambo kwa kupima, usiruke huna mbawa,
    Una macho kutazama, na akili umepewa,
    Matendo hurudi nyuma, atendaye hurudiwa,
    Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa!

    Dunia haishi njama, sijione umepewa,
    Ukadhani usalama, binadamu kuwagawa,
    Ukahisi ni wanyama, waso hali kama ngawa,
    Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa!

    Unapotenda zahama, siku yako itakuwa,
    Ambapo utaungama, useme umechachiwa,
    Na uanze kutetema, ulie umeonewa,
    Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa.


    Maswali
    a) Lipe shairi hili kichwa mwafaka.
    b) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu.
    c) Eleza muundo wa ubeti wa pili.
    d) Ni kaida zipi za utunzi zilizozingatiwa na mshairi?
    e) Andika ubeti wa kwanza kwa lugha ya mjazo.
    f) Toa mifano miwili ya idhini ya mshairi.
    g) Kwa nini msemewa hafai kulalamika ?
    h) Eleza maana ya maneno yafuatayo.
    i) Uhasama
    ii) Umepowa

    Date posted: October 5, 2019 .    Answers (1)

  • Tafautisha kati ya; Ngonjera za ushairi na za maigizo. (Solved)

    Tafautisha kati ya;
    Ngonjera za ushairi na za maigizo.

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Onyesha kwa kutolea mifano minne, jinsi misimu huzuka. (Solved)

    Onyesha kwa kutolea mifano minne, jinsi misimu huzuka.

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Thibitisha kauli kuwa, "Mla naye huliwa zamu yake ifukapo". Ukirejelea riwaya ya Kidagaa Kimemwozea. (Solved)

    Thibitisha kauli kuwa, "Mla naye huliwa zamu yake ifukapo". Ukirejelea riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • "Siku moja kabla ya kufika kwa wageni. Meya ana mkutano na wawakilishi wa wafanyikaziambao wameketi mkabala naye". (Solved)

    Mtahiki Meya; Timothy Arege
    "Siku moja kabla ya kufika kwa wageni. Meya ana mkutano na wawakilishi wa wafanyikazi ambao wameketi mkabala naye".
    (a) Fafanua madai yaliyotolewa na wafanyakazi katika mkutano huu.
    (b) Eleza jinsi Meya alivyojibu madai ya wawakilishi wa wafanyakazi.

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Wanawake, wanaoishi katika maeneo ya mashambani katika nchi ambazo zinazoendelea ni baadhi ya watu waliotopea na kubobea katika uchochole mkubwa. (Solved)

    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yafuatayo.
    Wanawake, wanaoishi katika maeneo ya mashambani katika nchi ambazo zinazoendelea ni baadhi ya watu waliotopea na kubobea katika uchochole mkubwa. Jumla ya idadi kubwa ya wanawake hawa wanaoishi chini ya kiwango cha chini, cha umaskini inakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 600. Hii ni idadi kubwa hasa ikikumbukwa kuwa ni asilimia kubwa ya wanawake inayoishi kwa maeneo haya. Ulimwengu umeshuhudia ongezeko kubwa la idadi ya watu pamoja na kuwako kwa matatizo ya kiuchumi duniani.Kadhalika matatizo mengine ni mitarafuku na vita vya kikabila, majanga ya kiasili mathalani mafuriko , ukame na milipuko ya volkano. Usisahau kuwa pia kina uharibifu wa kimazingira, mabadiliko ya desturi na kusambaratika kwa familia na misingi yake. Tatizo lingine ni kuwa kuna kuongezeka kwa hali ya wanawake kuwa wazazi pekee na hivyo kuongeza familia zinazosimamiwa na wanawake ( ambao tumewataja kuwa wanakumbwa na umaskini mkubwa).Wanawake wanaoishi mashambani wanakumbwa na makubwa. Kwanza, kama maskini wanaishi katika mazingiramagumu. Vile vile kama wanawake wanakabiliana na mapendeleo ya kisera na kitamaduni yanayowadharau na kuwapuuza wanawake na mchango wao katika maendeleo. Tatu, kama viongozi wa familia hasa wanaolea na kutunza jamaa na mzazi mmoja, wanapambana na uogonzi wa familia pamoja na uzalishaji. Aghalabu hawapati usaidizi wowote katika majukumu kama haya bali wanalazimika kupambana nayo peke yao. Kutokana na hayo yote wanawake hawapati nafasi nzuri kushiriki katika maamuzi ya maswala yanayowahusu. Maswala mengi yanaamuliwa na wanaume pasipokuwahusisha wanawake. Licha ya dhiki yao kubwa, wanawake hawa wanachangia katika maendeleo ya jammi na kiuchumi kwa njia mbalimbali. Mchango huu unaonekana katika kiwango cha jamii,taifa na familia. Katika kiwango cha kijamii na kitaifa wanawake ndio chazo cha nguvukazi kwani ni wao na watoto wao wanatekeleza kazi nyingi hasa za nyumbani na mashambani. Mara nyingi huwa na uwezo bora wa kutunza chochote walichonacho kuliko wenzao wanaume.
    Kifamilia wanawake wa shambani wanashughulika mchana kutwa katika hali ngumu ya hewa aidha jua kali au mvua huku wameeleka wanao migongoni wakilima mashamba ili kupata chakula kwa familia zao. Jukumu la kuandaa chakula nyumbani bado linaachiwa wale wale wanawake wanaokizalisha mashambani.
    Jambo lisilopingika ni kwamba wanawake wanatekeleza majuku makubwa na muhimu katika kizazi cha binadamu na ndio hasa miimili ya jamii yoyote staarabu. Kwa hivyo, ni kinaya kitupu kudhalilisha wanawake. Mataifa mengi yaliyoendelea ni yale yaliyoondoa vikwazo vyote mbele ya wanawake na kuwaacha watekeleze wajibu wao. Kadhalika wanaume wa huko wanawaona wanawake kama wenzao katika kujenga jamii wala sio watumwa au watumishi wao wanaoumia na kutumikishwa kama vifaa na bidhaa. Inafaa jamii zinazodinisha wanawake zitambue kuwa ubaya wa tendo hili sio tu kudumaza maendeleo yake bali pia kutoa mfano mbaya kwa vijana ambao wataendeleza Ukandamizaji huu kwa vizazi vijavyo. Kwa hivyo, jamii inawajibika kutenda lililo sawa kwa kuwapa hadhi wanawake wote.

    Maswali
    a) Ipe taarifa hii anwani mwafaka
    b) Nakili maafa matatu ya kimaumbile yaliyotajwa katika kifungu hiki.
    c) Eleza sababu tatu zinazowazuia wanawake kushiriki katika maamuzi ya masuala yanayowahusu kulingana na makala haya.
    d) Wanawake hutekeleza majukumu gani katika jamii na taifa kutokana na makala haya?
    e) Kuna tofauti gani baina ya wanawake wa mataifa yaliyoendelea nay ale ambayo hayajastawi.
    f) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa kwenye taarifa:
    i) uchochole
    ii) kudhalilisha
    iii) mitafuruku

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Jadili changamoto za elimu katika hadithi ya Kanda la Usufi. (Solved)

    Jadili changamoto za elimu katika hadithi ya Kanda la Usufi.

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Uongozi mbaya una athari kadhaa. Thibitisha madai haya kwa kurejelea Tamthili ya Mstahiki Meya. (Solved)

    Uongozi mbaya una athari kadhaa. Thibitisha madai haya kwa kurejelea Tamthili ya Mstahiki Meya.

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Ndiyo yale ya "ngome in‘tuumiza naswi tu mumo ngomeni.‘ (Solved)

    Mshtahiki Meya: T. Arege
    Ndiyo yale ya "ngome in‘tuumiza naswi tu mumo ngomeni.‘
    a) Weka dondoo hili katika muktadha wake.
    b) Tambua tamathali mbili za usemi zilizo tumika latika dondoo hili.
    c) Kwa kurejelea tamthilia onyesha jinsi ngome inavyowaumiza wanacheneo.
    d) Wanacheneo wanatumia mikakati gani kukabiliana na hali ya (c) hapo juu.

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Onyesha jinsi mwandishi wa Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea alivyoshughulikia Nafasi ya mwanamke. (Solved)

    Onyesha jinsi mwandishi wa Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea alivyoshughulikia Nafasi ya mwanamke.

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Onyesha jinsi mwandishi wa Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea alivyoshughulikia Nafasi ya vijana. (Solved)

    Onyesha jinsi mwandishi wa Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea alivyoshughulikia Nafasi ya vijana.

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)