Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Kwa kutoa mifano fafanua vipengele vitano vya kiisimu vinavyothibitisha kwamba kiswahili ni lugha ya kibantu

Kwa kutoa mifano fafanua vipengele vitano vya kiisimu vinavyothibitisha kwamba kiswahili ni lugha ya kibantu

Answers


Faith
Kiswahili ni moja Kati ya lahaja za kibantu.imethibitishwa kuwa kiswahili Ina maneno asilimia kubwa ya maneno ya kibantu.Tunaweza kuthibitisha hii kwa kuangalia ushahidi wa kiisimu unaotokana na utafiti wa sayansi ya lugha.
• Msamiati wa kiswahili.Guthrie(1967) alionyesha uhusiano uliopo katibya kiswahili na lugha zingine za kibantu.Alionyesha uhusiano wa mashina mengi ambayo yamezagaa katika lugha zingine za kibantu Alichunguza asili ya neno 'Bantu' au watu.Shina hili linapatikana katika lugha nyingi za kibantu na hii inaonyesha kuwa kiswahili ni mojawapo ya lahaja za kiswahili.
• Mnyambuliko wa vitenzi.Lugha za kibantu Kama ilivyo lugha ya kiswahili hudhihirisha mnyambuliko wa vitenzi. Kwa mfano;
Kutenda-lima
Kutendana-limana
Kutendeka-limika
Kutendatenda-limalima
Kulingana na myambuliko huo wa pamoja Basi kiswahili ni kibantu.
• Mfumo wa silabi wazi.Lugha za kibantu Kama ilivyo kiswahili hudhihirisha mfumo wa silabi wazi.Yaani Kila silabi ya neno lenye asili ya kibantu huishia kwa vokali.Hii pia inafanyika kwa lugha za kibantu.Maneno mengi ya kibantu huwa na muundo wa konsonanti vokali konsonanti vokali.Kwa mfano 'lima',kisu,meza na kadhalika.pia Kuna yasiyofuata muundo huu Kama vile cheka,mbuzi n.k
• Lugha za kibantu Kama ilivyo kiswahili huunganisha mofimu ili kuunda sentensi ya neno moja.Mfano 'alicheza' inaweza kuainishwa hivi.
A-kiambishi cha nafsi
Li-kiambishi Cha wakati uliopita
Chez-mzizi wa kitenzi
a-kiishio
• Katika lugha za kibantu na kiswahili Kuna uwezekano was kuunda nomino kutokana na vitenzi,vitenzi kutokana na nomino, vitenzi kwa vivumishi.kwa mfano
Kitenzi–nomino
Cheza-mchezo
Imba wimbo
Kivumishi–kitenzi
Bora-boresha
Safi-safisha

Titany answered the question on December 6, 2021 at 08:14

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions