Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Utanzu wa ushairi umepitia matapo/vipindi vinne katika kukua na kusambaa kwake. Eleza vipindi kama vinavyoelezewa na Kitula King’ei na Amata Kemoli, katika Diwani yao ‘Taaluma...

      

Utanzu wa ushairi umepitia matapo/vipindi vinne katika kukua na kusambaa kwake. Eleza vipindi kama vinavyoelezewa na Kitula King’ei na Amata Kemoli, katika Diwani yao ‘Taaluma ya Ushairi’.

  

Answers


Francis
a) Tapo/Kipindi cha urasimi mkongwe
Dhana ya urasimi huwa na maana ya mkusanyo wa mikondo ya kifikra au kimtazamo ambayo chanzo chake ni sanaa na utamaduni wa Wayunani na Warumi. Matapo ni vipindi mbalimbali vya kihistoria ambavyo fasihi au sanaa kwa jumla imevipitia. Pia huweza kuelezwa kama mikondo au makundi makuu ya kinadharia ambayo yametawala katika fasihi au sanaa katika nyakati maalum. Katika karne ya kumi na nane na kumi na tisa ushairi ulianza kuandikwa.
Upande wa mashairi kimaandishi mshairi aliyejulikana sana ni Muyaka bin Haji (1776-1970). Ingawa kuna malenga wengine wa kipindi hiki, mashairi yao bado hayajakusanywa na kuwekwa katika vitabu. Mashairi yanayotambulika mno katika tapo hili ni pamoja na Utenzi wa Hamziya ambao uliandikwa na Sayyid Abdarus, Utenzi wa Al-Inkishafi wake Sayyid Abdalla, Utenzi wa Tambuka ulioandikwa na Mwengo na Utenzi wa Mwanakupona. Utenzi huu wa Mwanakupona ndio wa kipekee uliotungwa na mwanamke na ulioacha athari kubwa katika wakazi wa Pwani Kaskazini hasa katika maisha yao kindoa. Katika kipindi hiki pia, nyingi ya mashairi yalikuwa yenye maudhui ya kidini hasa dini la Kiislamu. Watunzi wengine wa kipindi hiki ni Bwana Mataka, Ali Kofi, Muhammad Kijumwa na Hemedi Abdallah.

b) Kipindi cha utasa (1885-1945)
Huenda kipindi hiki killitwa hivi kwa sababu maandishi machache yaliandikwa wakati huu.Huu ulikuwa ni wakati wa vita vya dunia, na mataifa mengi yakigawana Afrika. Sheria za utunzi wa mashairi zilianza kutozingatiwa.

c) Kipindi cha urasimi mpya (1945-1960)
Mashairi yaliyotungwa katika kipindi hiki aghalabu yalikuwa yanafuata kanuni/ arudhi. Washairi waliotawala kipindi hiki ni Amini Abedi, Shabaan Robert, Mathias Mnyampala miongoni mwa wengine mashuhuri. Wao walikuwa na itikadi kuwa ili utungo uitwe shairi, sharti liweze kuimbwa, hivyo lazima liwe na urari wa vina, mizani inayolingana pamoja na masuala mengine ya kiarudhi. Kipindi hiki pia kilishuhudia washairi chipukizi wapya kuanza kuibuka.

d) Kipindi cha sasa (1967 kuendelea)
Hiki ni kipindi cha leo hii ambapo pana mgogoro kati ya wanamapokeo na kundi nyingine la wanamapinduzi.Wanamapokeo wanashikilia mitazamo ya jadi kuwa shairi lazima lifuate arudhi, nao wanamapinduzi wanapinga suala hili. Kulingana na wao, muhimu ni ujumbe ambao shairi linabeba bali si muundo wa shairi. Mashairi mengi wanaotunga wanamapinduzi ni mashairi huru. Washairi wa kipindi hiki ni pamoja na Euphrase Kezilahabi, Kithaka wa Mberia, Alamin Mazrui, Mugyabuso Mulokozi kati ya wengineo.
francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 12:25


Next: Eleza mbinu zifuatazo zilivyotumika kwenye hadithi, Pupa, ukitolea mifano; i. Kinaya ii. Sadfa
Previous: Ni mambo gani yanayobainika wazi, yanayoelezea ushairi umekuwa sanaa ya umma katika kipindi cha sasa?

View More Ushairi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions