Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

“Huyu ambaye mama alimwona kuwa gae, kumbe sasa ndiye chombo cha kunivisha bahari hii ya dhiki?” (Chozi la Heri)(a) Weka dondoo hili katika muktadha...

      

1. “Huyu ambaye mama alimwona kuwa gae, kumbe sasa ndiye chombo cha kunivisha bahari hii ya dhiki?” (Chozi la Heri)
(a) Weka dondoo hili katika muktadha wake faafu.
(b) Eleza mbinu mbili za lugha zinazojitokeza katika dondoo hili.
(c) Eleza jinsi mrejelewa alivyomsaidia nafsineni.

  

Answers


Francis
(a) Weka dondoo hili katika muktadha wake faafu.
? Umu anajisemea maneno haya
? Anamrejelea Hazina
? Ni barabarani, akiwa anaelekea sehemu za kanisa
? Hii ni baada ya kukutana na Hazina, kijana ombaomba ambaye waliwahi kukutana naye akiwa na mamake akamsaidia. Kwa sasa Hazina amebadilika, ni mhudumu hotelini na ndiye anamsaidia Umulkheri.

(b) Eleza mbinu mbili za lugha zinazojitokeza katika dondoo hili.
? Uzungumzi nafsi – Umulkheri anajisemea maneno haya
? Swali balagha - ...chombo cha kunivisha bahari hii ya dhiki?
? Istiara – gae kumrejelea Hazina.

(c) Eleza jinsi mrejelewa alivyomsaidia nafsineni.
? Alimpeleka hotelini alikokuwa akihudumu akala shibe yake.
? Alimtambulisha kwa Julida, mama aliyesimamia makao ya watoto ili apate msaada. Ni hapa ambapo Umulkheri alijiunga na Shule ya Tangamano.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 05:12


Next: Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata. WASAKATONGE 1. Wasakatonge na juakali Wabeba zege ya maroshani, Ni msukuma mikokoteni, Pia makuli bandarini, Ni wachimbaji wa migodini, Lakini...
Previous: “Sasa nitajuaje walichokuwa wamevalia nami sikuwaona? Mtu hukwambia anapotoroka au kutoroshwa?” (Chozi la Heri) (a) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (b) Ni mbinu zipi za lugha zinazotawala...

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions