Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

“Hebu sikiza jo! Pana hasara gani nzi kufia kidondani?” a) Eleza muktadha wa dondoo hili. b) Taja na utoe mifano ya mbinu nne za lugha zilizotumika katika...

“Hebu sikiza jo! Pana hasara gani nzi kufia kidondani?”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Taja na utoe mifano ya mbinu nne za lugha zilizotumika katika dondoo
c) Onyesha ukweli wa kauli “ nzi kufia kidondani” unavyodhihirishwa na wahusika katika hadithi.

Answers


Kavungya
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
• Hii ni kauli ya Otii. Akimjibu rafiki yake anayejaribu kumtahadharisha kuhusu vimanzi warembo anapotambua ana uhusiano na Rehema. Otii anatamka kauli hii akijitetea na kuuhalalisha uhusiano wake anapojilinganisha na nzi anayefia juu ya kidonda, kitendo ambacho sio hasara kamwe. Walikuwa kwenye baa

b) Taja na utoe mifano ya mbinu nne za lugha zilizotumika katika dondoo
• Nidaa kwa mfano “ sikiza jo!”
• Balagha K.M “ pana hasara gani inzi kufia kidondani?”
• Methali K.M nzi kufa juu ya kidonda si hasara
• Sitiari/Jazanda K.M nzi inasimamia Otii na Kidondani ni rahani/ starehe .

c) Onyesha ukweli wa kauli “ nzi kufia kidondani” unavyodhihirishwa na wahusika katika hadithi.
• Otii anaugua maradhi ya ukimwi na kuishia kujutia kitendo chake.
• Rehema Wanjiru anaangamia kwa UKIMWI katika harakati za kujitafutia raha
• Otii anaishia kuvunjika muundi wake akiwa katika raha za kuicheza kandanda
• Otii anaconda kama ng’onda na kubakia mwembamba kama sindano.
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 06:15

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions