Trusted since 2008
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Fafanua sifa zozote nne za ngomezi.

Fafanua sifa zozote nne za ngomezi.

Answers


Maurice
(i) Si rahisi kupata ujumbe wa ngomezi kama wewe si mshiriki wa utamaduni husika

(ii) Ngoma ni muhimu kupitishia ujumbe

(iii) Wanajamii tu ndio wanaoweza kufasiri mdundo wa ngoma na kufasiri maana

(iv) Ujumbe wa dharura huwasilishwa kwa njia ambayo si ghali ikilinganishwa na njia nyingine

(v) Mapigo yanayotolewa kwa maana maalumu huambatana na ngoma inayoeleweka kwa ujumbe mahsusi

(vi) Huongozwa na watu teule katika jamii.
maurice.mutuku answered the question on August 6, 2019 at 05:29

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions

  • Eleza ujumbe uliowasilishwa na ngomezi katika fasihi simulizi. (Solved)

    Eleza ujumbe uliowasilishwa na ngomezi katika fasihi simulizi.

    Date posted: August 6, 2019 .    Answers (1)

  • Taja aina zozote tatu za vitendawili (Solved)

    Taja aina zozote tatu za vitendawili

    Date posted: August 6, 2019 .    Answers (1)

  • Mbinu zifuatazo zina umuhimu gani katika uwasilishaji wa fasihi simulizi. (i) Uradidi (ii) Uigaji sauti (Solved)

    Mbinu zifuatazo zina umuhimu gani katika uwasilishaji wa fasihi simulizi.

    (i) Uradidi

    (ii) Uigaji sauti

    Date posted: August 5, 2019 .    Answers (1)

  • Fafanua majukumu yoyote sita ya maigizo katika jamii ya kisasa. (Solved)

    Fafanua majukumu yoyote sita ya maigizo katika jamii ya kisasa.

    Date posted: August 5, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza jinsi maudhui ya unafiki yameshughulikiwa katika hadithi hii. (Solved)

    “Wamelaa?’
    “Enh wamelala”
    “Basi wamelala tu?’

    Eleza jinsi maudhui ya unafiki yameshughulikiwa katika hadithi hii.

    Date posted: August 5, 2019 .    Answers (1)

  • “ulitaka wahamie wapi siku kama hizi?....Fafanua sifa za msemaji wa dondoo hii. (Solved)

    TAMTHLIA: KIGOGO

    “ulitaka wahamie wapi siku kama hizi? Wamekuja kuuguza majeraha yao ya kufungiwa soko?”

    Fafanua sifa za msemaji wa dondoo hii.

    Date posted: August 5, 2019 .    Answers (1)

  • Tambua mbinu mbili za lugha katika dondoo hili. (Solved)

    “ulitaka wahamie wapi siku kama hizi? Wamekuja kuuguza majeraha yao ya kufungiwa soko?”

    Tambua mbinu mbili za lugha katika dondoo hili.

    Date posted: August 5, 2019 .    Answers (1)

  • Weka maneno haya katika muktadha wake (Solved)

    “ulitaka wahamie wapi siku kama hizi? Wamekuja kuuguza majeraha yao ya kufungiwa soko?”

    Weka maneno haya katika muktadha wake

    Date posted: August 5, 2019 .    Answers (1)

  • Kwa kurejelea tamthlia ya KIGOGO, Thibitisha ukweli wa dondoo hili. (Solved)

    “Kitabu si jalada, fungua ndani usome mambo. Kitanda usichokilalia kunguni mwake huwajui.”

    Kwa kurejelea tamthlia ya KIGOGO, Thibitisha ukweli wa dondoo hili.

    Date posted: August 5, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza muktadha wa dondoo hili (Solved)

    TAMTHLIA: KIGOGO



    “Kitabu si jalada, fungua ndani usome mambo. Kitanda usichokilalia kunguni mwake huwajui.”

    Eleza muktadha wa dondoo hili

    Date posted: August 5, 2019 .    Answers (1)

  • Kwa kurejelea riwaya nzima eleza changamoto zinazoikumba jinsia ya “mwanagenzi” (Solved)

    RIWAYA: CHOZI LA HERI

    Kwa kurejelea riwaya nzima eleza changamoto zinazoikumba jinsia ya “mwanagenzi”

    Date posted: August 5, 2019 .    Answers (1)

  • Taja na ueleze mbinu mbili za lugha zinazijitokekeza katika dondoo hili. (Solved)

    Riwaya-Chozi la Heri

    Taja na ueleze mbinu mbili za lugha zinazijitokekeza katika dondoo hili.

    Date posted: August 5, 2019 .    Answers (1)

  • Weka dondoo hili katika muktadha wake. (Solved)

    RIWAYA: CHOZI LA HERI

    “……kama mataifa hayakushinda majabali miaka kumi iliyopita itakuwa huyu mwanagenzi ambaye hata mgwisho sisi ndio tulimfunza.”

    Weka dondoo hili katika muktadha wake.

    Date posted: August 5, 2019 .    Answers (1)

  • Bainisha shamirisho kipozi na shamisisho kitondo katika sentensi ifuatayo: Onyango alimnunulia simu mpenzi wake. (Solved)

    Bainisha shamirisho kipozi na shamisisho kitondo katika sentensi ifuatayo:
    Onyango alimnunulia simu mpenzi wake.

    Date posted: August 5, 2019 .    Answers (1)

  • Andika ngeli za maneno haya: (i) Kawa (ii) Baridi (Solved)

    Andika ngeli za maneno haya:

    (i) Kawa

    (ii) Baridi

    Date posted: August 5, 2019 .    Answers (1)

  • Majina mengi katika ngeli ya U-ZI huchukua kiambishi U katika umoja lakini viambishi tofauti katika wingi. Andika majina mawili ukionyesha viambishi hivyo tofauti katika umoja... (Solved)

    Majina mengi katika ngeli ya U-ZI huchukua kiambishi U katika umoja lakini viambishi tofauti katika wingi. Andika majina mawili ukionyesha viambishi hivyo tofauti katika umoja na wingi.

    Date posted: August 5, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza sifa za konsonanti zifuatazo: (i) /h/ (ii) /r/ (Solved)

    Eleza sifa za konsonanti zifuatazo:

    (i) /h/

    (ii) /r/

    Date posted: August 5, 2019 .    Answers (1)

  • Ni mambo gani yanayochangia kuanguka kwa mwanafunzi katika swali la ushairi? (Solved)

    Katika kila kiwango, wanafunzi huonekana kama wana shida kubwa sana katika kuyachambua mashairi. Hali hii ni matokeo ya mambo mengi. Yaweza kuwa mashairi waliyokutana nayo mara ya kwanza yalikuwa magumu, au yalikuwa yamechanganya Kiswahili sanifu na lahaja zingine ambazo wasomi hawangezielewa moja kwa moja.

    Jambo hili huwakatisha wanagenzi tamaa hasa wanapokosa kulipata katika kamusi msamiati uliotumika. Wanapotamauka, wao huwa hawataki kujishughulisha na mashairi. Huu ndio mwanzo wa kuanguka kwao katika mtihani kwa vile wengi wao hulazimika kukutana na mashairi kwa mara ya kwanza katika chumba cha mtihani. Hiki ni kinyume cha jinsi mambo yanavyostahili kuwa. Ukweli ni kuwa mashairi yanastahili kuwaburudisha wasomi pindi wakutanapo nayo.


    Madai kuwa mashairi ya Kiswahili ni magumu kufahamika isipokuwa kwa watu maalum wenye vipawa maalum hayafai. Mwanafunzi ambaye anataka kufanya vizuri katika swali la mashairi ni lazima aanze kuyapenda mapema iwezekanavyo. Ni muhimu aazimie kuyapenda hasa ajuapo kuwa atatahiniwa katika sehemu hii. Kwa vile hana njia ya kuyaepuka,azingatie msemoi wa wazungu usemao kuwa kama hupati upendacho, anza kupenda kile ukipatacho. Ili kuchochea upendo ndani yake, asijishughulishe nayale mashairi ambayo anayaona kama ni magumu. Ajaribu kuyaelewa yale ambayo anayaelewa na kuudondoa ule ujumbe ambao yameubeba na vile vile ajaribu kuufurahia utamu wa maneno yaliyotumika. Atalipata hili kwa kuyasoma kwa sauti. Kila mara, akumbuke kwamba kadiri atakavyokutana na mashairi mengi ndivyo atakavyofurahia na kuyaelewa.


    Pili, akikutana na shairi, asishtushwe na msamiati au lahaja iliyotumika. Hata kama haelewi msamiati uliotumika, ajaribu kuelewa ujumbe uliomo katika shairi. Hata hivyo, lazima ajihami na msamiati mwingi iwezakanavyo. Isitoshe, ni muhimu katika mazoezi yake kujaribu kuandika mashairi yake mwenyewe ili aelewe ni kwa nini waandishi huyaandika mashairi jinsi wanavyoandika;Atagundua kwa nini waandishi huyarefusha, huyafupisha au huyabadilisha maana ya maneno mbalimbali.


    Ni mambo gani yanayochangia kuanguka kwa mwanafunzi katika swali la ushairi?

    Date posted: August 5, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika mashairi. (i) Ja (ii) Sharuti (iii) Utukufu (iv) Baidi (Solved)

    SHAIRI A: HOFU YA BIN-ADAMU

    Hofu za wanyonge, ni nguvu za matajiri,

    Ambazo zinawaponda, wanapotaka usawa.


    Hofu ya watawala, ni kupoteza uhuru,

    Wa kutawala kwa mbavu, pamoja na utukutu.



    Hofu za mwanamke ,mwanamke wa sasa,

    Ni kutumiwa ja rungu, daima kuwekwa nyuma.


    Hofu za mmcha-mungu, ni maisha ya baadaye,

    Maana hana hakika, ndio aogopa kifo.


    Hofu za wasomi, ni kwamba wako baidi,

    Na wale wateteao, ambao ni sawa nao.




    SHAIRI B: AMANI

    Uhuru pia Amani
    Usifikirie ni zawadi
    Ambayo inapeanwa
    Pasipo mikwaruzano



    Kama wataka hakiyo
    Shariti uwe tayari Kupokeza roho yako
    Pamoja na ya mwingine



    Uhuru ja ini la fani
    Ambalo kulifikia
    Sharti uwe jasiri
    Jasiri aso kifani



    Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika mashairi.

    (i) Ja

    (ii) Sharuti

    (iii) Utukufu

    (iv) Baidi

    Date posted: August 3, 2019 .    Answers (1)

  • Andika ubeti wa pili wa shairi B kati lugha nathari. (Solved)

    SHAIRI A: HOFU YA BIN-ADAMU

    Hofu za wanyonge, ni nguvu za matajiri,

    Ambazo zinawaponda, wanapotaka usawa.


    Hofu ya watawala, ni kupoteza uhuru,

    Wa kutawala kwa mbavu, pamoja na utukutu.



    Hofu za mwanamke ,mwanamke wa sasa,

    Ni kutumiwa ja rungu, daima kuwekwa nyuma.


    Hofu za mmcha-mungu, ni maisha ya baadaye,

    Maana hana hakika, ndio aogopa kifo.


    Hofu za wasomi, ni kwamba wako baidi,

    Na wale wateteao, ambao ni sawa nao.




    SHAIRI B: AMANI

    Uhuru pia Amani
    Usifikirie ni zawadi
    Ambayo inapeanwa
    Pasipo mikwaruzano



    Kama wataka hakiyo
    Shariti uwe tayari Kupokeza roho yako
    Pamoja na ya mwingine



    Uhuru ja ini la fani
    Ambalo kulifikia
    Sharti uwe jasiri
    Jasiri aso kifani

    Andika ubeti wa pili wa shairi B kati lugha nathari.

    Date posted: August 3, 2019 .    Answers (1)