Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

"Ndoto za uhuru barani Afrika imegeuka kuwa jinamizi, jinamizi inayowafanya wazalendo kulia Kidagaa kimetuozea". Ukirejelea riwaya ya kidagaa kimemwozea eleza sababu za wazalendo kulia Kidagaa...

"Ndoto za uhuru barani Afrika imegeuka kuwa jinamizi, jinamizi inayowafanya wazalendo kulia Kidagaa kimetuozea". Ukirejelea riwaya ya kidagaa kimemwozea eleza sababu za wazalendo kulia Kidagaa kimetuozea.

Answers


sharon
- Unyakuzi wa ardhi - Nasaba Bora anabadilisha hatimiliki ya shamba la chichiri Hamadi
- Mauaji - Nasaba Bora anapanga njama Chichiri Hamadi auawe
- Umaskini- Imani anakosa kuendelea na masomo kwa ukosefu wa pesa
- Matumizi mabaya ya pesa za umma - Nasaba Bora na washirika wake wanatumia pesa zilizonuiwa kujengea hospitali na kuishia kujenga zahanati
- Huduma duni za afya - nduguye Imani anakufa kutokana na utepetevu wa madaktari / uhuru
- Umma kulazimishwa kumchangia Madhubuti ili aende akasomee Urusi
- Kufungwa jela bila. sababu - Amani na Imani / Yusufu, Matuko Weye
- Maskini kunyimwa nafasi za masomo huku pesa zikiwaendea watoto wa matajiri k.m.
- Fao kufadhiliwa kwa pesa za mahawinde
- Viongozi kama Nasaba kuwa na uhusiano na watoto wa shule kama vile Lowela
- Udangan yifu katika mtihani. Fao anafanyiwa mtihani
- Wiziwa miswaada - mwalimu Majisifu anaiiba miswaada na kuichapisha kwa jina lake
- Kutowajibika - Majisifu hafiki shuleni
sharon kalunda answered the question on September 25, 2019 at 07:29

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions