Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Mtoto anapozaliwa huwa ni malaika wa Mungu. Hutaraji kuongozwa kwa kila njia ili awe mwana mwelekea. Jukumu la kulea mtoto huanzia nyumbani. Wako baadhi ya...

      

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali.

Mtoto anapozaliwa huwa ni malaika wa Mungu. Hutaraji kuongozwa kwa kila njia ili awe mwana mwelekea. Jukumu la kulea mtoto huanzia nyumbani. Wako baadhi ya watu ambao wanaamini kuwa jukumu hili muhimu hutekeleezwa bora na mama; wengine husema kuwa ni jukumu la baba. Ni kweli kwamba mtoto huwa na mama yake kwa muda mrefu zaidi ya baba lakini kivuli cha baba hakikosi kumwandama na kumwathiri maisha yake.
Uongozi wa mama huanzia siku ya mwanawe kuingia ulimwenguni. Kwa hivyo, mama zaidi ya baba huwa ndiye chanzo cha chemichemi ya maisha ya mwanawe. Mtoto kwa kawaida ana tabia ya kuiga kila jambo analoliona na kusikia na mambo ya awali ajifunzayo hutokana na mamaye.

Je; mtoto huiga kutokana na mama pekee? Kila utamaduni hasa huku kwetu Afrika, una taratibu zake zilizopangwa kuhusu malezi ya watoto. Kwa mfano; akina baba wengine wanaoishi maisha ya kijadi huonelea kwamba ni jukumu lao kuwalea watoto wa kiume. Kwa hivyo mvulana anayekulia katika mazingira haya akishachuchuka kiasi cha kujua lipi zuri lipi baya huanzia kuwa mtoto wa baba zaidi ya kuwa wa mama. Baba humuathiri mtoto wake kwa kumshauri kuhusu maneno ya kiada ya wanaume. Hupenda kukaa naye katika uga wake kwa kumshauri kuhusu maneno ya kiada ya wanaume huku akimkataza kukaa jikoni na kumsisitizia kuwa wanawake ni tofauti naye. Aidha, humfunza sifa kama vile ushujaa na uvumilivu kwa namna ambayo huona kuwa ni ya kiume. Pindi mtoto anapoonyesha tabia za kikekike, baba hujiandaa kuzitadaruki kwa kumkaripia. Baba hutaka kujiona mwenyewe katika hulka ya mwanawe.

Baba kama huyu humpa nafasi ndogo sana mkewe ya kumwongoza mtoto wake wa kiume kwa jambo lolote hata kama wakati mwingine ni la heri. Kwa upande mwngine baba huyu huwa na machache ya kuzungumza na bintiye kwa kuwa huona kuwa si stahili yake kufanya hivyo. Mtoto wa kike huachiwa mamake. Lakini kutokeapo jambo la kulipima mama huona linampita kimo, humwita baba kuingilia kati na aghalabu baba naye humwagiza dadake aje atoe suluhisho mwafaka.

Ulezi kama huu una nafasi yake katika jamii, lakini ni lazima tukiri kuwa pia unaendeleza maisha ya fawaishi na kuanzisha taasubi ambayo hatima yake ni mwanamke kukandamizwa na mwanaume. Wazazi walio na mwelekeo huu katika malezi yao hufikiri kuwa wataishi na watoto wao katika mazingira finyu na kwa hivyo waendelee kuwapulizia pumzi za kuhilikisha. Lakini ni sharti wakumbuke kuwa wao sio walezi peke yao na wala mtoto hawezi kuishi peke yake na kuwa na tabia ya kipekee. Leo ataishi kwao lakini kesho itambidi atoke aone ulimwengu. Kila atakapotia mguu ataona mambo mapya yatakayompa tajriba mpya na mawazo mapya ambayo aghalabu yataendelea kuiathiri hulka yake. Iwapo tabia alizozipata kwa wazazi wake hapo awali zilikuwa na misingi isiyokuwa madhubuti na mielekeo finyu, zinaweza kuwa pingamizi katika maingiliano yake na watu wengine. Mambo haya yanatuelekeza katika kufikiri kwamba maisha ya siku hizi hayaruhusu ugawaji wa kazi ya malezi ya namna ya baba na mama wa kijadi. Baba na mama ni walezi wa kwanza ambao kwa pamoja wanapaswa kuwaelekeza watoto wao katika maisha ya ulimwengu uliojaa bughudha na ghururi. Ni lazima wazazi watambue tangu awali kuwa katika malezi hakuna cha ubaguzi. Hakuna, mambo ajifunzayo mtoto wa kiume ambayo hayamhusu mtoto wa kike. Uvumilivu, bidii, utiifu na kadhalika ni sifa zinazomwajibikia kila mtoto kama vile upishi, ukulima na usafi. Mwanamke tangu azali ameumbwa kuwa mama na haipasi kulazimishwa kuchagua baina ya mtoto wa kike na kiume. Mapenzi na wajibu wa wazazi yapaswa yasiwe na mipaka bali yawe maridhawa kwa watoto wote.

Maswali
(a) Toa kichwa mwafaka cha makala haya
(b) Kulingana na kifungu hiki, taja mambo mawili ambayo yanaweza kuwa hatari kwa
malezi ya watoto
(c) Kwa nini baba humpa nafasi ndogo sana mkewe ya kumwongoza mtoto wa kiume katika
jambo lolote hata kama wakati mwingine ni la heri
(d) Eleza mambo mawili ambayo ni ya manufaa katika ulezi jadi
(e) Kulingana na makala haya, ushahidi gani unaonyesha kwamba kuna kutegemeana
katika ulezi jadi?
(f) Taja sifa mbili ambazo baba humfundisha mwana wa kiume
(g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika kaktika kifungu hiki:
(i) Chanzo cha chemichemi...
(ii) Akishachuchuka...
(iii) Hulka.

  

Answers


Maurice
(a) – malezi
- Wajibu wa wazazi katika malezi
- Jawabu lolote linalogusia juu ya malezi

(b) (i) – Baba kuona kuwa wajibu wake ni kulea watoto wa kiume tu
(ii) – Watoto wa kiume kuonyesha kuwa wao ni tofauti na watoto wa kike

(c) Kwa kuhofia kuwa stamfunza tabia za kike

(d) (i) Palikuwa na ugawaji wa kazi ya malezi
(ii) Watoto walifunzwa sifa kama vile uvumilivu, bidii , utii
(iii) Watoto wa kike walifunzwa upishi, ukulima , usafi

(e) Palipotokea jambo ambalo kwa kulipima mama aliona linampita kimo, alimwita baba
kuingilia naye alimwagiza dadake aje atoe suluhisho.

(f) Sifa- (i) Ushujaa
(ii) uvumilivu

(g) (i) Chanzo cha chemichemi – kitovu cha maisha/asili
(ii) Akishachuchuka – ongeza kimo /kua
(iii) Hulka – tabia/mwenendo/sifa
maurice.mutuku answered the question on October 4, 2019 at 05:52


Next: Discuss the factors that have contributed to declining population growth rate in some developing Countries.
Previous: Kwa kutumika njia ya jedwali, changanua sentensi ifuatayo: Gofu hushabikiwa na watu wengi sana.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • Fafanua aina ya hali iliyotumika katika sentensi hii. Wanasiasa wengi hulalamika kila mara. (Solved)

    Fafanua aina ya hali iliyotumika katika sentensi hii.
    Wanasiasa wengi hulalamika kila mara.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Bainisha shamirisho katika sentensi ifutayo: Maimuna alimtumia babake barua ndefu.(Solved)

    Bainisha shamirisho katika sentensi ifutayo:
    Maimuna alimtumia babake barua ndefu.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Sahihisha sentensi ifuatayo: Mwalimu mwenye ako nabidii amepeana mazoezi katika darasa yetu.(Solved)

    Sahihisha sentensi ifuatayo:
    Mwalimu mwenye ako nabidii amepeana mazoezi katika darasa yetu.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Ilikuwa Jumamosi. Nilifika nyumbani kwangu saa moja jioni. Tangu nistaafu miakamiwili awali sikupenda kuchelewa Taarifa ya Habari. Mwezi mmoja...(Solved)

    Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali.

    Ilikuwa Jumamosi. Nilifika nyumbani kwangu saa moja jioni. Tangu nistaafu miaka
    miwili awali sikupenda kuchelewa Taarifa ya Habari. Mwezi mmoja ukawa umepita tangu nipewe pesa za kiinua mgongo. Mwezi mmoja mzima nilikuwa katika shughuli za kulipa deni hapa na kulipa karo huku. Kuwekeza kwenye mradi ule na kununua hili. Sasa shilingi laki mbili tu zilikuwa zimesalia katika benki. Watu wengi walinishawishi nijaribu kilimo cha mahindi. Bei ilikuwa imeanza kuimarika. Katika taarifa ya habari jioni hiyo, Waziri wa Kilimo alitangaza bei mpya. Shilingi 1,500 kwa kila gunia. Nami nilikuwa naanza kuumakinikia mradi huu. Baaada ya taarifa, nilikoga, nikala na nikaenda kulala. Kwa sababu ya uchovu, usingizi ulinichukua mara moja.. Usingizini niliota. Katika ndoto niliutekeleza mradi wangu. Msimu huo wa kilimo nilitenga ekari kumu za shamba langu. Wataalamu walinishauri kuwa wakati mzuri wa kulima ni wa kiangazi. Mwezi wa Januari ulipoanza tu nilitafuta trekta na kulima. Malipo yalikuwa shilingi 1,200 kila ekari. Katikakati ya mwezi wa Machi, nilitafuta trekta la kutifua shamba tena kwa gharama ya shilingi 15,000 ekari zote kumi. Kufuatia ushauri wa manyakanga wa kilimo, nilipa shilingi elfu kumi na tatu kupiga shamba lote haro. Mwishoni mwa mwezi huo, nilienda mjini kutafuta pembejeo. Kwanza, nililipa shilingi 20,500 kwa magunia 15 ya mbolea. Kisha nilinunua magunia manne ya mbegu ya mahindi yenye uzani wa kilo 25 kwa shilingi 3,300 kila gunia. Mwezi wa Aprili ulipotimia tu, niliamua kupanda. Ili nipate mazao bora, nilipanda kwa tandazi. Gharama ilikuwa shilingi 1,000 kila ekari. Mvua ilinyesha vizuri na baada ya siku saba mahindi yalianza kuota. Ilifurahisha kuhesabu mistari ya kijani iliyonyooka. Hali hii iliwezekana tu baada ya kuajiri vijana wa kuwafukuza korongo na vidiri ili wasifukue mbegu mchangani. Baada ya mwezi mmoja, hatua ya kupalilia ilifika. Nilitafuta vibarua wa kupalilia. Malipo yalikuwa shilingi 700 kila ekari. Kumbe kupalilia kulichochea mtifuko wa mahindi. Punde yakawa yananifikia magotini. Hii ikawa ishara kuwa yanahitaji kumwagiwa mbolea ya kunawirisha iitwayo ‘amonia.’ Gharama yake ikawa shilingi1,300 kila gunia. Hivyo, nikalipa shilingi 19,500 kwa magunia kumi na matano.. Mahindi yalibadilika kimiujiza. Ghafla tu yalirefuka na kunenepa mashina. Yalibadilika rangi yakapiga weusi. Shamba liligeuka likawa kama msitu wa rangi ya kijani iliyokolea. Wapita njia waliajabia mimea na juhudi zangu. Shamba langu sasa likawa kielelezo. Maafisa wa kilimo wakawa kila siwanawaleta wakulima wengine kujifunza siri ya ufanis wangu. Hapo nikaanza kuhesabu mavuno nitakayopata kukadiria faida. Nilipuuza kabisa ushauri wa wahenga kuwa ‘Usikate majani, mnyama hajauawa.’
    Bila taarifa wala tahadhari mvua ikatoweka. Hayakupita majuma mawili mahindi yakaanza kubadilika. Juma moja baadaye mahindi yalinyauka. Badala ya mahindi, shamba likageuka la vitunguu vilivyochomwa na jua. Makasio yangu ya faida yaliyeyuka jinsi ufanyavyo moshi. Lakini ‘Muumba ndiye Muumbua.’ Siku moja mawingu yalitanda na mvua ikanyesha. Muda is muda mahindi yalianza kunawiri. Kumbe tukio lililonivunja moyo lilikuwa laja. Siku moja mvua kubwa ilinyesha. Asubuhi nilipotoka nje nilipigwa na butwaa. Barafu ilitapakaa pote. Shamba lilikuwa limetapakaa barafhuku majani ya mahindi yamechanika kama nyuzi. Niliugua. Baada ya wiki moja, nilipata nafuu. Nilipotazama upande wa shamba nikaona dalili za majani mapya ya mahindi yakianza kuchomoza. Maumbile ni kitu cha ajabu kweli. Muda si mrefu mahindi yalirudi hali yake tena, kisha yakakomaa. Harakati za kutafuta watu wa kuyakata na kuyakusanya zilianza. Gharama ya shughuli hii ikawa shilingi 5,000. Kuvuna, kusafirisha kutoka shamba na kukoboa kwa mashine magunia 200 yakachukua shilingi 20,500. Kufikia hapo nilikuwa nimetumia takribani shilingi 192,700. Gharama nyingine zilikuwa za usafiri, gharama ya dharura na usimamizi, usumbufu wangu binafsi, gharama ya magunia na kadhalika. Mahindi yalipokuwa tayari kwenye magunia nilifunga safari kwenda mjini kutafuta soko. Niliposhuka tu niliona gazeti. Habari motomoto siku hiyo ilikuwa: ‘MAHINDI GUNIA 900/=.’ Niligutuka usingizini.


    Maswali:
    a) Andika kichwa mwafaka kwa kifungu hiki cha habari.
    b) Msimulizi alikuwa na kiasi gani cha pesa katika benki baada ya mradi kukamilika?
    c) Taja matatizo matatu yaliyotisha mradi wa msimulizi wa kukuza mahindi.
    d) Eleza maana ya methali zifuatazo:
    (i) Usikate majani, mnyama hajauawa.
    e) Eleza mambo mawili yaliyosababisha msimulizi asipate faida alivyotarajia.
    f) Kwa nini msimulizi alisema maumbile ni kitu cha ajabu?
    g) Eleza maana ya:
    (i) kiinua mgongo.
    (ii) manyakanga wa kilimo.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Andika sentensi hii katika usemi wa taarifa" Nitampokea mjomba iwapo nitampata," Rehema alimwambia shangazi yake.(Solved)

    Andika sentensi hii katika usemi wa taarifa
    " Nitampokea mjomba iwapo nitampata," Rehema alimwambia shangazi yake.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Ainisha maneno yaliyopigiwa mstari. Naam! Amekaa kabla ya mkurungezi mkuu yule.(Solved)

    Ainisha maneno yaliyopigiwa mstari.
    Naam! Amekaa kabla ya mkurungezi mkuu yule.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Yakinisha sentensi hii: Hajanivunjia mlango wala kuniibia(Solved)

    Yakinisha sentensi hii:
    Hajanivunjia mlango wala kuniibia

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Onyesha mofimu katika: kilichopewa(Solved)

    Onyesha mofimu katika:
    kilichopewa

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Zingatia picha ifuatayo kisha ujibu maswali.(Solved)

    Zingatia picha ifuatayo kisha ujibu maswali.
    pic31020191638.png
    (a) Tambua kipera cha fasihi simulizi kinachowakilishwa na muktadha wa picha hii.
    (b) Toa sababu mbili za jawabu lako katika swali la (a).
    (c) Jadili sifa zozote tano zinazotambulisha kipera hiki.
    (d) Jadili udhaifu wa kipera hiki katika jamii ya kisasa.

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Kamilisha jedwali (Solved)

    Kamilisha jedwali
    fig3831020191616.png

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Bainisha kiima na chagizo katika sentensi ifuatayo. Walimu hao walifanya kazi yao kwa bidii. (Solved)

    Bainisha kiima na chagizo katika sentensi ifuatayo.
    Walimu hao walifanya kazi yao kwa bidii.

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Eleza matumizi ya “na” katika sentensi ifuatayo. Wageni na wenyeji walikimbiliana. (Solved)

    Eleza matumizi ya “na” katika sentensi ifuatayo.
    Wageni na wenyeji walikimbiliana.

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia jedwali. Ouma alianguka mtihani ila Kamau alifuzu vizuri. (Solved)

    Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia jedwali.
    Ouma alianguka mtihani ila Kamau alifuzu vizuri.

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Ainisha vielezi katika sentensi zifuatazo. (i)Jaribu kujitahidi kisabuni usianguke mtihani. (ii)Wachezaji wote wameingia uwanjani.(Solved)

    Ainisha vielezi katika sentensi zifuatazo.
    (i)Jaribu kujitahidi kisabuni usianguke mtihani.
    (ii)Wachezaji wote wameingia uwanjani.

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana mbili za sentensi ifuatayo. Wanafunzi waliandikiana barua. (Solved)

    Eleza maana mbili za sentensi ifuatayo.
    Wanafunzi waliandikiana barua.

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Unda nomino mbili kutokana na neno "kudhulumu".(Solved)

    Unda nomino mbili kutokana na neno "kudhulumu".

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Ainisha shamirisho katika sentensi ifuatayo Juma alimchinjia mamake mbuzi mzuri kwa kisu. (Solved)

    Ainisha shamirisho katika sentensi ifuatayo
    Juma alimchinjia mamake mbuzi mzuri kwa kisu.

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Andika katika usemi wa taarifa “Nitawatuza watahiniwa wote watakaopita mtihani mwaka huu”. Mwalimu aliwaahidi wazazi.(Solved)

    Andika katika usemi wa taarifa
    “Nitawatuza watahiniwa wote watakaopita mtihani mwaka huu”. Mwalimu aliwaahidi wazazi.

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Andika sentensi yakinishi kutokana na sentensi ifuatayo. Utawala mkubwa wa meya haukuzuilika. (Solved)

    Andika sentensi yakinishi kutokana na sentensi ifuatayo.
    Utawala mkubwa wa meya haukuzuilika.

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Andika kwa ukubwa na udogo Sahani zote zimepelekwa nyumbani (Solved)

    Andika kwa ukubwa na udogo
    Sahani zote zimepelekwa nyumbani

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)