Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Kitabu kinaeleza Mungu kamuumba mwanamke kutokana na ubavu tu wa mwanamume. Na hapa bila shaka ndipo linapojisalimishia shina lisilokuwa na mzizi thabiti...

      

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali:-

Kitabu kinaeleza Mungu kamuumba mwanamke kutokana na ubavu tu wa mwanamume. Na hapa bila shaka ndipo linapojisalimishia shina lisilokuwa na mzizi thabiti la ubinafsi wa kiume – mwanamume akijijadilia kimoyomoyo. Ikiwa huyu mwanamke alitokana na ubavu wangu, yeye awe nani kwangu? Hakuna shaka ni wangu, mali yangu. Kwa sababu hii, miaka nenda miaka rudi mwanamke amekuwa akiugua na kuguna chini ya uonevu wa mwanamume.
Swala la kitabu kumleta duniani mwanamke kupitia ubavu wa mwanamume laweza kueleweka katika muktadha wa kile ambacho kimekuja kujulikana kama taasubi ya kiume. Na ili tuelewane barabara kuhusu maoni haya, tujisitishe kidogo katika kunusa tumbako huku tukijiuliza: ni nani au ni kina nani walihusika katika kubuni au kuandika hadithi ya asili ya mwanamke kitabuni? Ni kawaida ya binadamu kutazama na kueleza jambo kibinafsi. Asili ya mwanamke ilivyoelezwa kitabuni katika mkururo wa fikra hii yaweza kutambulikana kama uzushi tu.
Kiutamaduni, hasa wa Kiafrika, huku akiwa yuakua, mtoto wa kike husombezewa kasumba ya mawazo akilini, na kwa bahati mbaya sana, aghalabu na mamake au nyanyake, kuhusu namna anavyotarajiwa kutabasamu, kujinyenyekeza, na jumla kujidunisha mbele ya mvulana. Ni mwiko kwake kudhihirisha tabia za kimabavu, sitaji kujitetea, ili asije akatiwa mdomoni mitaani! Msichana atacharazwa na wazazi wake kwa ujasiri licha ya kuthubutu kupigana na mvulana. Na hapo ndipo ilipojificha siri ya kuwa anapoolewa na akosane na mumewe, daima yeye hutolewa makosa na kupatikana na hatia mbele ya wazee.
Wavulana kwa upande wao ni wanaume na lazima afanye mambo kiume. Si ajabu kuwa kinyume cha yale yanayowafika wasichana, wavulana wengi huonyeshwa mbovu na baba zao kwa sababu wamepigwa na wenzao. Ni vibaya baba kusikia mtoto (mvulana) wake amepigwa.
Nyumbani msichana hutarajiwa kujilindia heshima kimwili hasa kwa kuhifadhi ubikira mpaka aolewe. Anapotembea na wanaume huitwa Malaya. Ni ajabu kuwa hakuna bikira wala Malaya mwanaume. Mvulana ambaye hajajuana kimwili na mwanamke kabla ya ndoa huchukuliwa kuwa zuzu; ilhali anayetembea ovyo na wanawake ndiye dume.
Fauka ya hayo, inasikitisha kabisa kuwa mwanamke hana mahali pa kutua kikamilifu duniani. Kabla hajaolewa nyumbani, huchukuliwa kuwa mpita njia tu. Na anapoolewa ni poa kaolewa. Isitoshe mwanamke huolewa, haoi wala yeye na mume hawaoani. Mwanamke mahali pake ni jikoni pia anaonekana tu; ni hatia kwake kujaribu kusikika.
Mkutano kuhusu mwongo wa wanawake uliofanyika miaka miwili iliyopita jijini Nairobi ilinuiwa kupalilia vizuri mwamko juu ya ukweli kuwa binadamu ni binadamu na hakuna haja ya wao kubaguana. Tofauti za kimaumbile haziwezi kuwa hoja. Tusiupigie makelele ubaguzi wa rangi huko Afrika kusini ilhali kwetu tuna ubaguzi wa kimaumbile. Tusipozingatia ushauri huu daima tutakuwa kwenye kile kinaya cha kuchekwa katika muktadha wa methali kuwa nyani haoni ngokoye.
Ni kweli kosa lilifanyika tangu awali ambapo kufumba na kufumbua, mwanamke akapigwa jeki na kuachwa akilewalewa katika hali ambayo hangeweza kujitetea hivyo basi akachukuliwa kuwa kiumbe duni. Lakini haidhuru, yaliyopita si ndwele, tugange yajayo. Kinachohitajika ni wanawake kuwa na nia na msimamo imara. Ni lazima wajifunge kibwebwe na kujitoa mhanga na kupambana dhidi ya taasubi ya kiume.


(a) Andika kichwa kinachofaa kutokana na taarifa uliyoisoma
(b) Taasubi ya kiume ilianzaje?
(c) Katika utamaduni wa mwafrika ni kasumba gani anayosombezewa mtoto wa kike anapokua?
(d) “Wavulana walidekezwa na utamaduni”. Eleza
(e) Taja kwa ufupi mambo muhimu yaliyoshughulikiwa katika mkutano wa mwongo wa wanawake mjini Nairobi
(f) Eleza maana ya semi zifuatazo kama zilivyotumiwa katika taarifa uliyosoma:-
(i) Nyani haoni ngokoye .
(ii) Akatiwa midomoni
(iii) Huonyeshwa mbovu
(iv) Wajifunge kibwebwe
(v) Yaliyopita si ndwele ganga yajayo

  

Answers


Maurice
(a) - Haki za wanawake
- Taasubi ya kiume

(b -Mwanamke kuumbwa kutokana na ubavu tu wa mwanaume

(c) - Ya mawazo akilini, kujinyenyekeza na kujidunisha mbele ya mwanamume
- Ni mwiko kudhihirisha tabia za kimabavu
- Hutarajiwa kujilinda heshima kimwili kwa kuhifadhi ubikira wake
- Mahali pake ni jikoni, hasikiki bali aonekanalo

(d) – Kuhifadhi ubikira mpaka aolewe
- Mwanamke huolewa haoi
- Ndiye mkosaji kila mara
- Nyumbani aonekana tu, asisikike

(e) - Wana uhuru wa kutembea na wanawake ovyo
-Wana uhuru wa kujitetea na kupigana
- Mwanamume ndiye huoa


(f)(i) Twawashtumu wengine ilhali sisi twabaguana kimaumbile
(ii) Akasemwa vibaya mtaani
(iii) Hupigwa /hushutumiwa
(iv) Wajitolee
(v) Yeye hahesabiwi makosa ila mkewe tu kila wakati hulaumiwa kutuze ufahamu
maurice.mutuku answered the question on October 4, 2019 at 07:42


Next: State two disadvantages of traditional house designs.
Previous: State two qualities of travel wear.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • Uundaji wa istilahi – hasa za lugha ya Kiswahili ni shughuli nyeti na nzito hivi kwamba, haipaswi kupapiwa na mtu yeyote. Hii...(Solved)

    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali:-

    Uundaji wa istilahi – hasa za lugha ya Kiswahili ni shughuli nyeti na nzito hivi
    kwamba, haipaswi kupapiwa na mtu yeyote. Hii ni shughuli inayohitaji umakinifu zaidi kwa wanaoshiriki katika mchakato wa uundaji istilahi za kutufaa katika mawasiliano na kukuza Kiswahili kwa jumla. Ufanisi wa watu binafsi, vyombo vya habari kama vile Shirika la Habari la Kenya (KBC), Taifa Leo na mashirika mengineyo katika ukuzaji wa lugha hutegemea mno sera na utayarishaji wa serikali katika kugharamia shughuli hii. Aidha, shughuli za kukuza lugha hukwama kwa sababu ya ukosefu wa fedha pamoja na sera maalum ya serikali kuhusu lugha.
    Hata hivyo, katika kuyakwepa matatizo haya, pamekuwepo na hatua za kimataifa za kujaribu kusawazisha shughuli ya uundaji wa maneno. Hatua hii ilichochea kubuniwa kwa shirikisho la kimataifa la vyama vya usanifishaji istilahi mnamo 1936. Lengo la kitengo hiki lilikuwa ni kufafanua msingi madhubuti ya uundaji wa istilahi duniani. Kwa hakika, shirikisho hilo limesaidia mno katika kuweka misingi ya shughuli za ukuzaji wa istilahi. Misingi hiyo ni ya jumla na haihusu taaluma yoyote mahususi. Katika makala hii, tunapiga darubini baadhi ya misingi hiyo pamoja na mapendekezo yake.
    Mosi, uundaji istilahi unafaa uanzie kwenye dhana na wala sio neno. Hii ina maana kwamba, kwanza pawepo na dhana au hali ambayo inahitaji itafutiwe neno au istilahi ya kuielezea. Inasikitisha sana kwamba pana wataalamu ambao wanaukaidi au kuukiuka msingi huu. Wanataaluma hawa hufanya mambo kinyume kwa kujibunia maneno yao na kuyahifadhi kwenye mikoba yao – halafu wakasubiri dhana izuke ndiposa waipachike istilahi yao. Pili, dhana zinabuniwa au kutolea istilahi au maneo ni muhimu zielezwe kwa ukamilifu na uwazi. Istilahi zinazoundwa zinafaa ziwe fupi iwezekanavyo na ziwe na uwezo wa kuelezea dhana kwa njia inayoeleweka bila utata. Tatu, maneno yanayoundwa sharti yawe na uhusiano wa aina fulani na dhana zinazowakilishwa na maneno hayo.
    Uhusiano huo unaweza kuwa ama ni wa kimaumbile au wa kiutendaji. kwa mfano, Mzee Sheikh Nanhany wa Mombasa alipobuni istilahi ‘uka’ kwa maana ya ‘ray’. Neno hili latokana na kupambauka au (kupambazuka kwa lafudhi ya kiamu. Neno ‘image’ ni jazanda kwa Kiswahili. ‘Mirage’ kwa Kiswahili ni ‘mangati’ (kutoka kwa mang’aanti) – yaani kung’aa kwa nchi. Mtaalamu mwingine aliyewazia uendajikazi wa kifaa na kubuni istilahi inayokubalika mpaka sasa ni Prof. Rocha Chimerah ambaye alibuni istilahi ‘tarakilishi’. Pengine Prof. Chimerah alifikiria kazi ni kifaa husika na kuunda neno la Kiswahili linaloakisi kazi hiyo. Tunajua kwamba kompyuta hufanya kazi inayohusu tarakimu kwa haraka kama umeme. Labda Chimerah ameegemea sifa hii kuibuka na istilahi hii.
    Maneno mengine ambayo yamebuniwa kufuatana na msingi huu ni ya Mzee Nabhany-mathalan ‘barua pepe’ (e-mail), na wavuti (website). Tukiegemea maumbile, neno ‘kifaru’ lina maana ya vita ilihali tuna zana ya vita iliyopewa jina hilo kwa sababu ya labda kuwa na maumbile sawa na kifarumnyama. Nne, istilahi zinaweza kukopwa kutoka lugha nyingine. Yamkini hakuna lugha hata moja ulimwenguni-zikiwemo lugha duniani kama vile kiingereza zinazoweza kujitosheleza. Takriban asilimia 80 ya maneno katika kiingereza ni ya kukopwa. Kwa hivyo, lugha ya Kiswahili inapokopa, hali hiyo haipaswi kuchukuliwa kuwa ni lugha dhaifu.
    Hata hivyo, istilahi zinazokopwa zi-nafaa zichukuliwe zilivyo katika umbo lao asili. Umbo hili linaweza kufanyiwa marekebisho machache tu, kulingana na sarufi na matumizi ya lugha kopaji. Mifano ya istilahi kama hizi ni ‘televisheni’ (television), kopmpyuta (computer), kioski (kutokana na jina ‘kiosk’ la Kijerumani) na redio (radio), Tano, pale istilahi haiwezi kukopwa, lugha husika ijaribu kubuni msamiati ufaao, kufanya hivyo ni kuhakikisha kwamba, lugha inastawi. Lakini tahadhari inapaswa kuchukuliwa hivi kwamba, Kiswahili kisikope maneno kiasi cha kupoteza upekee wake. Mwisho, uundaji wa istilahi uzingatie mofolojia ya kawaida ya lugha. Istilahi zinazoundwa kwa kuzingatia mofolojia huwa rahisi kuiua maneno yenye uhusiano wa istilahi asili kwa njia ya mnyambuliko.



    (i) Taja mambo ambayo huchangia ukuaji na ufanisi wa jumla wa lugha ya Kiswahili
    (ii) “Lugha ya Kiswahili ni dhaifu na isiyotosheleza” Je, mwandishi wa makala haya
    ana msimamo upi kuhusu kauli hii?
    (iii) Tahadhari zipi zinazofaa kuchukuliwa kabla ya kukopa istilahi kutoka lugha zingine?
    (iv) Yape makala haya anwani mwafaka
    (v) Eleza maana ya maneno yafuatayo:
    (a) Dhana-
    (b) Takribani –
    (c) Istilahi – .
    (d) Mofolojia –...

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Kuna fikra inayotawala siku hizi kuwa jela si mahali pa adhabu bali matibabu.(Solved)

    Kuna fikra inayotawala siku hizi kuwa jela si mahali pa adhabu bali matibabu. Yaani lengo la kumfunga mhalifu si kumuadhibu bali kumtibu kwa njia ya kurekebisha tabia ili aweze kuchangia katika maendeleo ya jamii yake anapoachiliwa.Wataalamu wa masuala ya urekebishaji tabia wanasema kuwa mhalifu akiadhibiwa sana na kufanyishwa kazi ngumu anapokuwa kifungoni, huisha kuwa sugu zaidi kuliko alipofungwa. Kwa hivyo, wataalamu wanasisitiza umuhimu wa kutilia mkazo lengo la kumtia mtu jela kuwa ni kumjenga kitabia. Mijizi, minyang‘anyi na wauaji wanapotoka gerezani kama hawakubadilishwa hurejelea tabia zao za kuhatarisha zaidi maisha ya watu wengi.Ajabu na kinaya ni kwamba baadhi ya wahalifu nchini na kwingineko wametokea kupata faida kuu kutokana na vifungo vyao. Kuna wagungwa ambao wamewahi kuandika hadithi za kusisimua kuhusu maisha yao na kutokea kuwa mabilionea.Magazeti na vyombo vya habari pia huvutiwa na habari kuhusu maisha yao. Mara kwa mara, magazeti hujaa habari kuhusu mambo kama haya. Pia kuna sinema nyingi ambazo zimetungwa kufuata maisha ya wahalifu Fulani.Watetezi wa haki za kibinadamu wanadai kuwa yale wafungwa walikuwa wakitendewa, nab ado wanatendewa katika nchi nyingine ni kinyume nah akin za kimsingi za binadamu. Hali hii imepelekea magereza mengi kukarabatiwa ili kuweza kukidhi mahitaji ya "uibinadamu."
    Nchini kenya, wafungwa sasa wameanza kushughulikiwa kwa kila hali. Sikwambii wanapata chakula kizuri chenye viini lishe bora, malazi bora, maji safi na mazingira nadhifu kwa jumla. Kumeanzishwa pia mpango wa elimu ambao ni maalum kwa wafungwa magerezani. Sasa wafungwa wanapata elimu na kuhudhuria madarasa na hata kuufanya mtihani wa kitaifa.Vile vile magereza nchini wameanzisha pia mpango wa kuwa na mashindano ya kila aina, ya kati ya magereza mbalimbali.Kuna mashindano ya michezo mathalan kandanda, voliboli, na michezo mingine na juu ya yote majuzi magereza yalianzisha mashindano ya urembo baina ya wafungwa wa kike.
    Kilele cha kuboresha kwa hali ya magereza nchini Kenya ni kuanzishwa kwa huduma za kuwastarehesha wafungwa hao. Sasa wafungwa wa humu nchini wanaweza kusoma magazeti na hata kutazama runinga ili kupata habari kuhusu
    yanayotendeka nchini wanapoendelea kutumikia vifungo vyao.
    Hata ingawa serikali imeanzisha mipango hii ya kuboresha hali katika magereza ya kenya, kuna matatizo mbalimbali ambayo yanaendelea kukumba taasisi hii. Kwanza, ni msongamano wa wafungwa uliopo. Magereza mengi yana wafungwa maradufu ikilinganishwa na idadi yanayofaa kuwa nayo. Hali hii imepelekea kuzuka kwa magonjwa na madhara mengine.
    Hii imewafanya watetezi wa haki za kibinadamu kuitaka serikali ianzishe mpango wa kutoa vifungo vya nje kwa wahalifu wenye makosa madogo madogo kuondoka msongamano huo.

    Maswali
    a) Eleza ujumbe muhimu unaojitokeza katika aya nne za kwanza. (maneno 50-60)
    b) Eleza mabadiliko ambayo yamefanywa katika idara ya magereza nchini Kenya

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Nchini Kenya, pamoja na kuwa mwanamke amepewa hadhi kubwa ikilinganishwa na hapo awali, kumetokea visa vingi vya unyanyasajiwa wanawake. Visa hivi haviwakati...(Solved)

    Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali

    Nchini Kenya, pamoja na kuwa mwanamke amepewa hadhi kubwa ikilinganishwa na hapo awali, kumetokea visa vingi vya unyanyasajiwa wanawake. Visa hivi haviwakati wengi maini, bali ni vyombo vya kuwazindua viongozi kuona kwamba hali haijafika kiwango cha kuridhisha. Visa vya ubakaji wa watoto wa kike na wazee, na wakati mwingine baba zao, vimetokea katika miaka ya hivi karibuni. Isitoshe, akina mama wengi wamekuwa wahasiriwa wa mivua ya makonde kutoka kwa waume zao, hata kwa makosa madogo madogo. Hivi majuzi mmoja wa wanawake hawa, ambao maisha kwao ni shairi tu, alichomwa vibaya na mumewe, kisa na maanaamejitia kujua kuwa kuna siku ya wapenzi, yaani Valentine day. Mwanamke huyu, baada ya kutoa mashambani kuja kujumuika na mumewe kusherehekea siku ya wapenzi, alipata sherehe za kuchoma moto huku mumewe akilalamika kuingiliwa uhuruwake. Mama huyu bado anauguza majeraha ya mwili na moyo!
    Mwanamke aliyesoma na kupewa fursa ya kufanya kazi na ajira ofisini naye amekabiliwa na changamoto nyingi. Huyu lazima atekeleze majukumu yake kama mama, mke na mfayikazi. Wengi wa wanawake wanaofanya kazi mjini hulalamika wanafanya kazi maradufu ya wanaume. Mwanamke kama huyu, kama alivyolalamika mmoja wao ambaye ni afisa wa utawala wa mikoa, huanza siku yake alfajiri na mapema kuitayarishia familia staftahi, kisha kuelekea ofisisni ambapo anakabiliwa na migogoro mingi ya kusuluhisha. Arejeapo nyumbani jioni, hali huwa hiyo hiyo, kutayarisha chajio, kushughulikia kazi za shule za watoto na kuichangamsha familia. Maisha yake huwa hivyo, siku nenda siku rudi. Utashangaa mja huyu atayabeba mangapi?
    Hali huwa mbaya zaidi kwa wanawake ambao wameingia siasa. Hawa mikasa yao haihesabiki. Mara watupiwe mabezo ya kila aina na wanasiasa wenzao, mara washutumiwe na kutiwa midomoni na wanajamii kwa kuonekana wakichapa kazi na kuwa na uhusiano wa karibu na wazalendo wenzao wa kiume. Maisha yake hupigwa darubini hata nyakati ambazo hayahitaji kuangazwa.
    Mwanamke amekuwa kinyago cha kufanyiwa mzaha. Juzi karibu mbingu zianguke alipojitokeza mwana vitimbi mmoja aliyejitia kufanyia utani yasiyohitaji. Alimwasiri mwanamke kama aliyechangia kukosewa heshima kwake kwa kule kutamani kufanywa hivyo. Ingawa wanawake walimshinikiza mhusika huyu kuomba msamaha, upayukaji wake haupaswi kuchukuliwa kama mzaha. Ni ishara ya hisia ya ndani za watu wengi kuhusu mwanamke; kwamba ingawa wakenya wamejitahidi kupigania haki za wanawake; baadhi yetu bado wana zile fikira za kijadi kuhusu wanawake.
    Uchumi wa nchi kamwe hauwezi kuendelea bila kumhusisha kila mtu. Nchini humu, baada ya kutambua haya, mwanamke amepewa nyadhifa mbalimbali katika serikali. Ingawa kuna baadhi ya wanawake waliohusika na kashfa mbalimbali za kifisadi, Kuna wale ambao wametumia nyadhifa zao kuhifadhi nchi. Mmoja wa wanawake amejaribu kwa jino na ukucha kuyalinda mazingira dhidi ya mapapa. Nani asiyekumbuka matusi na mabezo aliyopata mwanamke huyu anayejitoa mhanga kuikinga sehemu Fulani ya burudani dhidi ya kunyakuliwa na wanaostahili? Hakuyajutia yaliyompata. Aliowatisha walijaribu kummeza mzimamzima lakini mwishowe walisalimu amri na kuliacha eneo hilo. Hiki kilikuwa kitendo cha ujasiri na uzalendo mkubwa. Matunda yake yamewafaidi wengi, vijana kwa wazee. Kila mwisho wa wiki huwaona watu wakimiminika kwenye eneo hili kujipumbaza. Hii si fahari kwake tu, bali kwa nchi kwa jumla. Wale waliompinga na kumwita punguani wakati huo wamebaki kuinamisha nyuso tu; bila shaka wamefunzwa mengi.
    Wanawake sasa wana haki ya kumiliki mali mathalani shamba. Kutokana na hili tumeshuhudia ongezeko kubwa la uzalishaji wa chakula mashambani na kwa hivyo kupunguza njaa na umaskini.
    Biashara ndogondogo zinazoendelezwa sokoni na mitaani, kwa kiasi kikubwa, huhusisha wanawake. Biashara hizi huchangia pakubwa katika kuimarisha uchumi wa nchi kwani hutoa ajira ya kibinafsi kwa maelfu ya watu. Ushuru na leseni zinazokatiwa biashara hizi huongezea serikali pato la ndani.
    Mgala muuwe na haki umpe. Ni ukweli kwamba tumekuwa na visa vya hapa na pale vya ukiukaji wa haki za wanawake. Hata hivyo, ni dhahiri kwamba nchi hii imejitahidi mno kuendelea kumkwamua mwanamke kwayo. Hata mashirika ambayo hapo awali hayakupenda kuwaajiri wanawake, sasa yanawapa nafasi sawa na wanaume. Vyuo vikuu vya kibinafsi vimeanzishwa kuwasajili wanawake. Jijini humu, mna chuo kikuu cha sayansi cha wanawake. Aidha kumeanzishwa kituo (shule) cha kuwasajili wasichana kutoka familia maskini kujiunga na kidato cha kwanza. Wasichana hawa watapata wadhamini kutoka mashrika na watu mbalimbali ili kujiendeleza kimasomo.
    Kumheshimu mwanamke ni miongoni mwa haki za kibinadamu ambazo shart zitekelezwe. Hata hivyo, wanawake wakumbuke kwamba hata wanapopuliza siwa kuhusu pupewa haki, lazima wao pia wawajibike. Wao ndio walimu wa kwanza wa wanao; ikiwa basi wataonekana kwenye vyombo vya habari wakining’inia juu ya magari ya wachunga magereza kwa kuzitafutia pesa za mayatima maumizi bora, watakuwa wanapotosha watoto wao. Wawe watu wa vitendo zaidi ya upayukaji.


    a) Kwa mujibu wa taarifa, ni mambo yapi yanayoonyesha ukiukaji wa haki za wanawake
    b) Fafanua jinsi mwanamke aliyesoma huteseka maradufu zaidi ya mwanamme
    c) Ni faida gani ambazo zimepatikana kutokana na wanawake kupigania haki zao?
    d) Hatimaye wanawake wanahimizwa kufanya nini?
    e) Eleza maana ya msamiati ufuatao jinsi ulivyotumiwa katika nakala
    Kinyago…
    Mabezo
    f) Andika mfano wa mbalagha na uhuishi uliotumiwa katika makala haya
    i) Mbalagha
    ii) Uhuishi

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Ufisadi ni uhalifu unaohusu kuzitumia njia za ulaghai kujipatia pesa, mali au vitu hasa vya umma. Nchini Kenya ufisadi hujitokeza...(Solved)

    Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali.

    Ufisadi ni uhalifu unaohusu kuzitumia njia za ulaghai kujipatia pesa, mali au vitu hasa vya umma.
    Nchini Kenya ufisadi hujitokeza kwa njia mbalimbali na kila mojawapo ina athari zake. Kwa mfano kuna maafisa wa serikali wajipatiao pesa kwa kuuza stakabadhi za serikali kama vile pasi, vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya kumiliki mashamba, vitambulisho n.k. kwa raia, kuna hatari kubwa kwa sababu watu wasio raia wa Kenya wameweza kusajiliwa kama wakenya na kuendeleza uhalifu kama ugaidi, wizi na ulanguzi wa dawa za kulevya.
    Wengine hujipatia vibali vya kufanya kazi na kuajiriwa kazi ambazo zingefanywa na wakenya. Hii imechangia ongezeko la uhaba wa kazi nchini.
    Watumizi wengine wa umma huuza mali ya serikali kama vile magari nyumba na ardhi na kufutika pesa za mauzo mifukoni mwao. Wengine wao hujinyakulia na kufanya vitu hivyo kuwa mali yao. Ufisadi wa aina hii umegharibu serikali kiasi kikubwa cha fedha. Serikali imelazimika kununulia maafisa wake magari baada ya muda mfupi, kulipia wafanyi kazi wake kodi za nyumba na kukosa viwanja vya upanuzi na ujenzi wa shule hospitali, vituo vya polisi na taasisi zingine maalumu.
    Baadhi ya wataalamu kama madaktari huiba dawa kutoka hospitali za umma kupeleka vituo vyao vyaafya. Pia hutumia wakati wao mwingi katika kazi zao za kibinafsi na kuwaacha wagonjwa katika hospitali za umaa wakihangaika. Sio madaktari tu, kuna masoroveya, whandisi, mawakili, walimu na mahesibu ambao hukwepa majukumu yao serikalini na kufanya kazi za kibinafsi.. Wengine wasio wataalam huendesha biashara za aina tofauti, na huku wanaendelea kupokea mishahara.
    Wanafunzi wanaotaka kujiunga na vyuo na shule bora za umma na hawakuhitimu wakati mwinginehulazimika kusalimu amri na kutoa hongo hili wapate nafasi za kusoma. Kiasi cha pesa kinachohitajika huwa kikubwa hivi kwamba ni wachache humudu hizo rushwa. Wale wasiojimudu kifedha hubaki wakilia ngoa. Kuna wazazi ambao hutumia vyeo vyao na ‘undugu’ kupata nafasi zilizotajwa, jambo ambalo huwanyima wanafunzi werevu kutoka jamii maskini nafasi ya kupata elimu. Matokeo huwa ni kuelimisha watu wasiostahili na ambao mwishowe hawaziwezi kazi wanazosomea wakihitimu na kuanza hudumia jamii.
    Ufisadi umekita mizizi na kushamiri katika sekta za umma za kibinafsi kwa upande wa kuajiri wafanyikazi. Ni vigumu kupata kazi ikiwa hujui mtu mkubwa katika shirika linalohusika au uzunguke mbuyu. Matokeo ni kuajiri wafanyikazi wasiohitimu na wasiohitimu na wasiowajibika kazini.
    Vyeo na madaraka katika baadhi ya mashirika hutolewa kwa njia ya mapendeleo na ufisadi. Kwa hivyo, wafanyikazi wenye biddi hufa moyo kwa sababu hawasaidiwi ipasavyo. Badala yake wale wasioleta bidii hupandishwa vyeo na kuwaacha palepale.

    Hata hivyo, mbio za sakafuni huishaia ukingoni. Serikali imetangaza vita dhidi ya ufisadi. Tayari tume kadhaa zimeteuliwa kuchunguza visa vya ufisadi uliotekelezwa hapo mbeleni. Mojawapo ya tume hizo ni Tume ya Kuchunguzavisa vya ufisadi uliotekelezwa hapo mbeleni. Mojawapo ya tume hizo ni Tume ya kuchunguza Kashfa ya “Goldenberg” ambapo pesa za umma (mabilioni ya shilingi) ziliporwa na mashirika na watu binafsi kwa njia siziso halali. Watakaopatikana na hatia ya kushiriki ufisadi huo watahitajika kurudisha pesa hizo.
    Serikali pia imeunda kamati ya kupikea malalamiko kutoka kwa wananchi waliohasiriwa na mawakili walaghai ambao hupokea ridhaa kwa niaba ya wateja wao na kukosa wakalipa, au wakilipwa kuwatetea mahakamani wanakwepa jukumu hilo ilhali wamekwishalipwa. Ni matumaini yetu kuwa ulaghai huu utaangamizwa kabisa kwani hakuna refu lisilokuwa na ncha.


    1. Eleza aina nne za ufisadi zilizotajwa katika kifungu ulichosoma
    2. Kulingana na kifungu ulichosoma, ufisadi umeathiri nchi yetu kwa njia gani?
    3. Serikali inafanya jitihada gani ili kukomesha ufisadi?
    4. Kwa maoni yako, unafikiri ufisadi husababishwa na nini?
    5. Toa msamiati mwingine wenye maana sawa na rushwa
    6. Eleza mana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa kifunguni;
    (a) Majukumu
    (b) Kashfa
    (c) Shamiri
    (d) wakilia ngoa
    (e) Waliohasiriwa
    (f) Kita mizizi

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • HADITHI FUPI DAMU NYEUSI NA HADITHI ZINGINEZO (KEN WALIBORA NA SAID A. MOHAMED) Mwana wa Darubini (Kristina Mwende Mbai) “Ulijuaje alikuwa anaangalia kwetu? a.Eleza muktadha wa dondoo hili. b.Hadithi...(Solved)

    HADITHI FUPI
    DAMU NYEUSI NA HADITHI ZINGINEZO
    (KEN WALIBORA NA SAID A. MOHAMED)

    Mwana wa Darubini (Kristina Mwende Mbai)
    “Ulijuaje alikuwa anaangalia kwetu?
    a.Eleza muktadha wa dondoo hili.
    b.Hadithi hii inaonyesha matatizo ya kijamii. Fafanua.
    c.Eleza yaliyotokea baada ya mazungumzo haya.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Kimya changu kimezidi, navunja yangu subira,(Solved)

    Soma shairi ifuatayo kisha ujibu maswali yatakayofuata.
    Kimya changu kimezidi, navunja yangu subira,
    Marejeya ya miradi, kuhitimisha dhamira,
    Kukejeli sina budi, niwafunze utu bora,
    Nani aali zaidi, Wakenya au vinara?

    Serikali bila hadi, ndo kiini cha madhara,
    Yanopiga kama radi, isokuwa na ishara,
    Yamini kuwa gaidi, wakitupora mishahara,
    Nani aali zaidi, Wakenya au vinara?

    Wamejifanya hasidi, wasopatana kifikira,
    Wana yao maksuudi, kijisombea ujira,
    Wakilenga kufaidi, tumbo zao za kichura,
    Nani aali zaidi, Wakenya au vinara?

    Nchi yetu kufisidi, ni jambo linonikera,
    Tangia siku za jadi, ufukara ndo king‘ora,
    Kutujazeni ahadi, nyie mkitia for a,
    Nani aali zaidi, Wakenya au vinara?

    Maskini watozwa kodi, wapwani na walo bara,
    Kwa uvumba na uudi, mwawalipa kwa hasara,
    Hamudhamini miradi, mejihisi masongora,
    Nani aali zaidi, Wakenya au vinara?

    Mesema kazi ni chudi, basi sirikali gura,
    Nafsi zenu mzirudi, mkubali kuchakura,
    Makondeni mkirudi, muondoe ufukara,
    Nani aali zaidi, Wakenya au vinara?

    Ujanjenu umezidi, demokrasia bakora,
    Debeni takaporudi, michirizi kwenye sura,
    Kuwachuja a! muradi, kwa za mkizi hasira
    Nani aali zaidi, Wakenya au vinara?

    Maswali
    a) Toa anwani mwafaka kwa shairi hili.
    b) Ainisha shairi hili kwa jinsi tatu huku ukitoa sababu.
    c) Onyesha Mbinu mbili za lugha katika shairi hili.
    d) Bainisha matumizi matatu ya uhuru wa mshairi katika shairi hii.
    e) Andika ubeti wa nne katika mtindo tutumbi.
    f) Fafanua maudhui matatu yanayojitokeza katika shairi hili.
    g) Taja mpango mmoja unaotajwa kama njia ya kutatua matatizo ya nchi.
    h) Eleza muhudo wa shairi hili.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • USHAIRI Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali: Hakika siku ya leo, ni siku ya majivuno Basi pasiwe na choyo, na usonono Tulekezane yaliyo, unawiri Muungano. Tuzisafisheni nyoyo, pasiwe na...(Solved)

    USHAIRI

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali:

    Hakika siku ya leo, ni siku ya majivuno
    Basi pasiwe na choyo, na usonono
    Tulekezane yaliyo, unawiri Muungano.

    Tuzisafisheni nyoyo, pasiwe na miguguno
    Yaongoke tutakayo, kusiwe na mabishano
    Mbegu hii tupandayo, ilete mema mavuno.

    Tufungulie upeo, Mola usiye mfano
    Pa kitasa na komeo, tupite bila kinzano
    Tupitishe njia hiyo, pasina masongamano

    Twakuomba uumbao, mkono vyanda vitano
    Tushikane hii leo, tuwe moja tangamano
    Tupendane kwa pumbao, hali na maridhiano

    Aliye ana machukiyo, adui wa Muungano
    Naazibe masikiyo, asisikie maneno
    Kisha awe kibogoyo, asiwe na moja jino.

    Ya Ilahi ujalie, juu wetu Muungano
    Nuru yake izagae, na nguvu za mapigano
    Hasidi mpe hakie, mateso yaso mfano

    Watamati komeleo, kuimba kwangu hukuno
    Nataka maendeleo, yasiyo na malumbano
    Daima tuwe ni ngao, palipo msagurano

    (i) Lipe shairi hili anwani yake.
    (ii) Liweke shairi hili katika bahari mbili ukitumia:
    Idadi ya
    (i)Mishororo
    (ii)Vina
    (iii) Onyesha muundo wa shairi hili.
    (iv) Andika ubeti wa pili kwa lugha ya nathari.
    (v) Toa mifano ya idhini ya kishairi iliyotumika katika shairi hili.
    (vi) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi.
    (i)Usonono –
    (ii)Msagurano –

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi moja kubainisha tofauti kati ya: i) Samani ii) Zamani(Solved)

    Tunga sentensi moja kubainisha tofauti kati ya:
    i) Samani
    ii) Zamani

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • RIWAYA Kidagaa kimemwozea Ken Walibora Angewezaje kumwambia kwamba mifugo wake walikuwa katika ukalifu tangu Amani kutiwa mbaroni?” a)Eleza muktadha wa dondoo hili? b)Mzungumziwa hakuwa na utu. Fafanua. c)Toa mifano...(Solved)

    RIWAYA
    Kidagaa kimemwozea
    Ken Walibora

    Angewezaje kumwambia kwamba mifugo wake walikuwa katika ukalifu tangu Amani kutiwa mbaroni?”
    a)Eleza muktadha wa dondoo hili?
    b)Mzungumziwa hakuwa na utu. Fafanua.
    c)Toa mifano ya maudhui ya ukatili katika Riwaya ya kidagaa kimemwezea inayofaa.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Habari kuwa watoto chini ya miaka mitatu ‘huwindwa’ kitandani na kuraushwa na wazazi wao waende shuleni mwendo wa saa kumi na moja asubuhi...(Solved)

    Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali.

    Habari kuwa watoto chini ya miaka mitatu ‘huwindwa’ kitandani na kuraushwa na wazazi wao waende shuleni mwendo wa saa kumi na moja asubuhi ni za kusikitisha.
    Kwa mujibu wa ripoti za wataalamu wa elimu ya watoto wachanga (ECD), watoto hao hutakikana kuwa darasani kabla ya saa kumi na mbili asubuhi.
    Wanapowasili wao huanza kufukuza ratiba ya masomo ambayo huwapatia muda mfupi mno wa kula, kucheza, kupumzika na hata kuchunguza afya na usalama wao.
    Badala ya kuondoka mapema kuelekea nyumbani, wengi wao hufika saa za usiku pamoja na wazazi wao wakitoka kazini. Wanapowasili nyumbani wanapaswa kuoga na kupata chakula cha jioni kwa pupa ili wafanye mazoezi waliyopewa na walimu wao.
    Mazoezi hayo huwa ya masomo yote matano huku kila somo likiwa na zaidi ya maswali thelathini. Badala ya kupumzika mwishoni mwa juma, watoto hao huhitjika kuhudhuria shule siku nzima ya Jumamosi. Jumapili wanatakiwa Kanisani na hali hii hujirudia mpaka muhula umalizike. Ikiwa ulidhani watapewa nafasi ya kupumzika wakati wa likizo , umekosea kwa sababu watoto hao huhitajika kuhudhuria shule. Hili limekuwa likiendelea hata baada ya Wizara ya Elimu kupiga marufuku kusomesha wakati wa likizo.
    Wazazi-hasa wale wanaofanya kazi mijini- wamekuwa wakiunga mkono mtindo huu kwa sababu unawaondolea mzigo wa malezi na gharama ya kuwaajiri walezi.
    Wataalamu wanasema matokeo ya hali hii ni watoto wakembe wenye afya na maadili mabaya kutokana na kuchanganyishwa akili na walimu wanaowataka wajue kila kitu wakiwa na umri mdogo.
    Kuwashinikiza watoto wakembe wahudhurie shule na zaidi ya hayo wajue kila kitu kuna madhara mengi. Kwanza kabisa, kuraushwa kwa watoto macheo waende shule kunawanyima fursa ya kulala na kupumzika. Utafiti unaonyesha kuwa watoto wanahitaji kulala na kupumzika kwa zaidi ya saa 12 kwa siku. Hii ina maana kuwa mbali na muda mfupi wanaolala na kupumzika mchana kutwa, watoto wanapaswa kutumia usiku mzima kwa usingizi.
    Hii huwasaidia kukua wakiwa na afya nzuri hasa kiakili. Matokeo ya kuwarausha watoto hao waende shule saa hizo huwafanya wakose furaha mbali na kuwafanya wachanganyikiwe kiakili.
    Pili, kuwalazimisha watoto wakae darasani kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni huwa kunawanyima fursa ya kucheza na kutangamana. Wataalamu wa afya ya watoto wanapendekeza kuwa watoto wachanga wanapaswa kucheza ili viungo vya miili yao kama moyo, akili, mapafu na kadhalika vifanye kazi vizuri.
    Kinyume na watu wazima ambao hufanya kazi nzito nzito na kuwawezesha kufanya mazoezi, watoto huwa hawafanyi kazi hizo. Wazazi na walimu wanapaswa kufahamu kuwa kazi ya watoto ni mchezo na wana kila haki ya kupewa furaha ya kucheza wakiwa shuleni na hata nyumbani.
    Tatu, wazazi wengi ambao hufurahia kuwaachia walimu jukumu la kuwalea watoto wao huku wao wakiwa kazini huwa wanasahau kuwa sio kila mwalimu ana maadili yanayopaswa kuigwa na mwanawe. Ingawa tunawatarajia walimu wawe mifano bora ambayo inaweza kuigwa na kila mtu, ukweli ni kwamba baadhi ya walimu hawajui maana wala hawana maadili. Hatari ni kwamba watoto wakembe husoma kwa kuiga wakubwa wao na ikiwa walimu wanaoshinda nao shule wamepotoka kimaadili, kuna uwezekano mkubwa wa watoto hao kupotoka pia. Hii ndiyo sababu wazazi wengi wamekuwa wakilalamika kuwa wanawao tabia mbaya ambazo hawaelewi zilipotoka.
    Kila mzazi anayejali maisha ya mwanawe anapaswa kutekeleza jukumu lake la kumlea na kumwelekeza jinsi anavyotaka akue. Ni kinaya kuwa wanawatarajia wanawao wawe na tabia na maadili kama yao ilhali hawachukui muda wa kukaa nao na kuwaelekeza.
    Nne, kuwawinda, kuwaamsha, kuwaosha na kuwalazimisha watoto waende shule kila siku hata ingawa hawataki huwa kunawafanya wawe wategemezi wasioweza kujipangia na kutekeleza mambo kivyao.

    (a) Ipe taarifa anwani mwafaka
    (b) Mwandishi anatoa maoni gani kuhusu ratiba ya masomo?
    (c) Eleza athari za mfumo wa elimu unaoangaziwa hapa
    (d) Ni ushauri upi unaotolewa kwa wazazi ?
    (e)Taja mbinu zozote mbili za lugha alizotumia mwandishi
    (f) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika taarifa.
    (i) ‘huwindwa’ kitandani
    (ii) Maadili
    (iii) Kuwashinikiza…
    (iv) Wakembe…

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Weka dagaa kwa ngeli yake.(Solved)

    Weka dagaa kwa ngeli yake.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Tamthilia; Mstahiki Meya Timothy M. Arege Au unafikiri pakawa na fursa nyingine hii leo ya kuchagua viongozi matokeo yatakuwa tofauti sana?...................Ukipanda huwezi kuvuna kunazi. a)Eleza muktadha wa...(Solved)

    Tamthilia; Mstahiki Meya
    Timothy M. Arege

    Au unafikiri pakawa na fursa nyingine hii leo ya kuchagua viongozi matokeo yatakuwa tofauti sana?...................Ukipanda huwezi kuvuna kunazi.
    a)Eleza muktadha wa maneno haya?
    b)Mzungumzaji na mzungumziwa wanafanana. Thibitisha.
    c)Taja mbinu za kifasihi zinazojitokeza katika muktadha huu.
    d)Eleza maovu yoyote manne yanayokumba wanacheneo.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Unda nomino kutokana na kitenzi nena.(Solved)

    Unda nomino kutokana na kitenzi nena.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi ukitumia kauli iliyobanwa ya kitenzi ulichopewa. i) soma (kutendeshwa) ii) –ja (kutendewa)(Solved)

    Tunga sentensi ukitumia kauli iliyobanwa ya kitenzi ulichopewa.
    i) soma (kutendeshwa)
    ii) –ja (kutendewa)

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Eleza matumizi ya "ki" katika sentensi hii. Ukikata kipira kitapotea.(Solved)

    Eleza matumizi ya "ki" katika sentensi hii.
    Ukikata kipira kitapotea.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Andika udogo wa: Ndege huyu ana miguu midogo(Solved)

    Andika udogo wa:
    Ndege huyu ana miguu midogo

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Bainisha aina za virai vilivyopigiwa mstari katika sentensi ifuatayo:(Solved)

    Bainisha aina za virai vilivyopigiwa mstari katika sentensi ifuatayo:
    Uchochole wa kinjinsia umepigwa marufuku na kiongozi mwenye msimamo thabiti mno.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yafuatayo ................napinga hoja iliyotolewa na waziri wa Finance ya kupiga marufuku matumizi ya plastic bags. Baada ya kumsikiza...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yafuatayo
    ................napinga hoja iliyotolewa na waziri wa Finance ya kupiga marufuku matumizi ya plastic bags. Baada ya kumsikiza kwa makini, napenda kumkosoa kwa kudhihirisha kuwa.................. kulingana na kifungu nambari ...................
    i)Bainisha sajili ya mazungumzo hayo.
    ii)Huku ukitoa mifano mwafaka, eleza sifa nne za sajili hii kwa mujibu wa kifungu hiki.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Geuza katika wingi ukizingatia nafasi ya pili. Nitasafiri kuelekea kwake kesho kutwa(Solved)

    Geuza katika wingi ukizingatia nafasi ya pili.
    Nitasafiri kuelekea kwake kesho kutwa

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Kwa kutumika njia ya jedwali, changanua sentensi ifuatayo: Gofu hushabikiwa na watu wengi sana.(Solved)

    Kwa kutumika njia ya jedwali, changanua sentensi ifuatayo:
    Gofu hushabikiwa na watu wengi sana.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)