Trusted since 2008
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Yakinisha sentensi hii Mpishi asipokuwa mwangalifu chakula hakitaiva vizuri

Yakinisha sentensi hii
Mpishi asipokuwa mwangalifu chakula hakitaiva vizuri

Answers


Kavungya
Mpishi akiwa mwangalifu chakula kitaiva vizuri
Kavungya answered the question on October 4, 2019 at 13:09

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions

  • Uchumi wa soko huria ni hali ya kiuchumi ambapo itokeapo amali, shughuli na harakati zote za kiuchumi ghairi ya zile... (Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali

    Uchumi wa soko huria ni hali ya kiuchumi ambapo itokeapo amali, shughuli na harakati zote za kiuchumi ghairi ya zile ambazo ni za lazima kwa serikali au dola kama ulinzi, sheria na
    mpangilio wa jamii huwa huria kwa watu binafsi. Msingi wa soko huria, sifa kuu ya utandawazi, ni kuibua na kudumisha mazingira na hali zinazochochea na kumruhusu mtu yeyote kuongozwa na hawaa, au matamanio ya kibiashara anayoyaona sawa pasi na hofu ya kuingilia na udhibiti wa serikali.
    Mazingira hayo yanawapa watu satua ya kufanya maamuzi kuhusu hatima yao ya kiuchumi, uamuzi kuhusu suala la ajira yao, matumizi ya mtaji kipato na harija zake, na uwekezaji mzima. Suala mojawapo linaloibuka kuhusiana na mfano wa soko huria ni kuweka mipaka bainifu na wazi baina ya amali na shughuli zinazohusishwa na serikali na zile ambazo huachwa huria kwa watu. Kwa mfano, inaaminiwa kuwa haki ya kuishi na kulindwa dhidi ya shambulizi, liwe la kijambazi au la kigaidi, ni ya kimsingi ambayo haiwezi kuhusishwa na uwezo wa kiuchumi wa mtu binafsi. Aidha huduma za kimsingi za afya nazo zinaingia katika kumbo hili. Ikiwa huduma hizi zitaachwa huria pana uwezekano mkubwa kuwa zitaishia kuwa istihaki ya wenye mtaji na kipato cha juu tu.
    Licha ya kuwepo kwa sheria au kanuni huria kutoka nyanja maalum, hutokea hali ambapo adhibiti wa kiserikali ni lazima. Hii hutokea pale ambapo ipo haja ya kuyalinda mazingira hasa kutokana na uchafuzi wa viwanda au tasnia. Aidha udhibiti huo ni lazima pale ambapo haki za watu wengine zinahusika: yaani ikiwa uhuru wa hata mtu mmoja unaadhirika kutokana na sera hizo pana haja ya kuingilia ili kuisawazisha hali yenyewe.
    (a) Andika kwa muhtasari maana ya uchumi wa soko huria kulingana na taarifa hii.
    (maneno 25-30)
    (b) Eleza mawazo makuu yanayojitokeza katika aya ya pili na ya tatu.
    (maneno 70-75)

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Toa maana ya semi Shupaa mwili. (Solved)

    Toa maana ya semi Shupaa mwili.

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Taja dhamira ya sentensi ifuatayo Kimbia mbio ulete sahani (Solved)

    Taja dhamira ya sentensi ifuatayo
    Kimbia mbio ulete sahani

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Akifisha sentensi ifuatayo iii ilete dhana tatu tofauti; Fatuma Khamisi mjukuu wa Rashid na Rehema wametoroka shule (Solved)

    Akifisha sentensi ifuatayo iii ilete dhana tatu tofauti;
    Fatuma Khamisi mjukuu wa Rashid na Rehema wametoroka shule

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Tunga sentensi yenye muundo ufuatao KN(N+S)+KT(T+E+E) (Solved)

    Tunga sentensi yenye muundo ufuatao
    KN(N+S)+KT(T+E+E)

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Iandike sentensi ifuatayo upya katika hali yakinishi. Hapo napo sipo nitakapo. (Solved)

    Iandike sentensi ifuatayo upya katika hali yakinishi.
    Hapo napo sipo nitakapo.

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Tumia maneno yafuatayo katika sentensi moja ili kubainisha tofauti zao kimaana; i) Chuuza ii) Chuza (Solved)

    Tumia maneno yafuatayo katika sentensi moja ili kubainisha tofauti zao kimaana;
    i) Chuuza
    ii) Chuza

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza tofauti kati ya ama za vielezi vifuatavyo; i) Vielezi vya namna mfanano na; Vielezi vya namna hali. ii) Tunga sentensi mbili tofauti ukitumia vielezi vya hapo... (Solved)

    Eleza tofauti kati ya ama za vielezi vifuatavyo;
    i) Vielezi vya namna mfanano na;
    Vielezi vya namna hali.
    ii) Tunga sentensi mbili tofauti ukitumia vielezi vya hapo juu.

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Andika sentensi moja ukitumia kivumishi cha nomino. (Solved)

    Andika sentensi moja ukitumia kivumishi cha nomino.

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Jadili sababu tano zinazofanya "sheng" isiwe lugha ya taifa. (Solved)

    Jadili sababu tano zinazofanya "sheng" isiwe lugha ya taifa.

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza maana ya; i).Mkembe. ii).mkebe. (Solved)

    Eleza maana ya;
    i).Mkembe.
    ii).mkebe.

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Uwezo wa kuyakumbuka mambo ni hazina kuu kutoka kwa mtu yeyote yule aliye hai. Uwezo huu wa kukumbuka ni mojawapo ya... (Solved)

    Soma taarifa kisha fupisha kwa mujibu wa maswali yafuatayo.

    Uwezo wa kuyakumbuka mambo ni hazina kuu kutoka kwa mtu yeyote yule aliye hai. Uwezo huu wa kukumbuka ni mojawapo ya shughuli changamano za ubongo. Ubongo wa mwanadamu hutekeleza shughuli hii kwa namna tatu. Kwanza ubongo hunasa jambo kisha
    huliihifadhi. Baadaye huanzisha mfumo wa kutoa kilicho hifadhiwa. Ubongo ukiathirika kwa
    namna yeyote katika moja wapo ya njia hizi, basi uwezo wa kuyakumbuka mambo huvurugika.
    Ingawa inaaminika kuwa uwezo wa kukumbuka hurithishwa toka kizazi kimoja hadi kingine, wataalamu wa maswala ya kiakili wanabaini kuwa uwezo huu unaweza kuimarishwa.
    Uimarishaji huu huhitajika mikakati madhubuti.
    Njia mojawapo ya kustawisha uwezo wa kukumbuka ni kupitia kwa lishe. Vyakula vilivyosheheni vitamini B vyenye amino asidi husaidia kuimarisha uwezo wa kukumbuka. Vyakula kama hivi ni mboga, nyama (hasa maini), bidhaaa za soya, matunda, maziwa, ,bidhaa za ngano, samaki, pamoja na mayai. Vyakula vingine muhimu katika ustawishaji huu ni vile vyenye madini ya chuma. Madini haya huwezesha usambazaji wa hewa katika ubongo kwa wepesi. Vyakula ambavyo vina madina haya ni mboga za kijani, mawele, ndengu, soya, matunda kama maembe, ufuta (simsim) pamoja na nyama, hasa maini na mayai.
    Ubongo wa mwanadamu aliye hai hufanya kazi kila wakati awe macho au amelala. Utendaji kazi wake huendeshwa na glukosi mwilini. Kwa hivyo, vyakula vyenye sukari hii ni muhimu kuliwa. Hata hivyo, lazima mtu awe mwangalifu na kuhakikisha kuwa mwili una kiwango cha sukari kisicho hatarisha maisha. Haya yanawezekana kwa kula vyakula vyenye nyuzinyuzi kama vile mboga na matunda.
    Njia ya pili ni kupiga marufuku vileo kama pombe na nikotini. Vileo hivi huathiri utaratibu wa kunasa, kuhifadhi na kutoa yaliyo ubongoni.
    Iwapo mtu ana tatizo la kuyakumbuka majina ya watu, ni muhimu kufanya mazoezi ya
    kusikiliza kisha kurudia majina hayo wakati wa mazungumzo. Ni bora kulihusisha jina na sura
    ya mtu. Kwa njia hii ubongo utanasa jina na kile kinacholengwa.
    Woga na kuvurugika kiakili ni mambo mengine tunayopaswa kuepuka kila wakati. Ni kawaida mtu kupata woga wakati anapokabili jambo asilokuwa na uhakika na matokeo yake kama mtihani au mahojiano. Lakini anapaswa kuwa makini. Woga huo usikiuke mpaka na kumvuruga kiakili. Vurugu hizi huathiri kilichohifadhiwa ubongoni na pia namna ya kukitoa.
    Halikadhalika, mwili wenye siha nzuri huhakikisha kuwa ubongo ni timamu. Wataalamu wengi wa siha wanakubali kuwa na mazoezi ya kunyoosha viungo hustawisha ubongo na hivyo kuhakikisha kuweko kwa uwezo wa kukumbuka mambo. Ni muhimu kuwa na taratibu ya kunyoosha viungo kila wakati. Fauka ya hayo, mazoezi ya kiakili, kama vile kusoma makala yanayovutia, kujaza mraba na michezo mingine kama mafumbo, vitenzi ndimi ni muhimu katika kustawisha uwezo wa kukumbuka.
    Jamii ya watu wenye uwezo kuyakumbuka mambo ni ya jamii iliyopiga hatua kimaendeleo. Ni jukumu la kila mmoja wetu kuimarisha uwezo wa kukumbuka kila wakati.

    a) Kwa maneno 60 – 65 fupisha mchango wa chakula katika uimarishaji wa uwezo wa
    kukumbuka.
    b) Fupisha aya tatu za mwisho kwa maneno 80 – 90

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Toa maneno yenye maana sawa na haya. i. Izara ii. Anisi (Solved)

    Toa maneno yenye maana sawa na haya.
    i. Izara
    ii. Anisi

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya matawi. Atanishughulikia vizuri. (Solved)

    Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya matawi.
    Atanishughulikia vizuri.

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza maana ya nahau zifuatazo: i) Furaha ghaya ii) Maneo yalimkata maini. (Solved)

    Eleza maana ya nahau zifuatazo:
    i) Furaha ghaya
    ii) Maneo yalimkata maini.

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Umaskini ni tatizo sugu katika jamii. Binadamu wengi hujikuta katika hali hii kwa sababu hawakubahatika kusoma. Baadhi yao huenda... (Solved)

    Soma taarifa hii kisha ujibu maswali

    Umaskini ni tatizo sugu katika jamii. Binadamu wengi hujikuta katika hali hii kwa sababu hawakubahatika kusoma. Baadhi yao huenda walijaribu kusoma wakashindwa mapema kujipandisha kielimu. Ukosaji wa elimu huchangia sana katika kukuza ukata. Elimu huweza mtu kupata tonge kwa kujipatia kazi za kumwezesha kuyakidhi mahitaji ya maisha. Hali kadhalika, elimu humsaidia binadamu kupata maarifa mengi ya kutendea shughuli zake za kimaendeleo. Kwa mfano, kama ni wakulima wanaweza kutumia pembejeo zifaazo ili kuboresha uzalishaji wa mazao. Wakulima wenye elimu hawatapendelea njia duni za kuendeleza kilimo kama vile kutumia visagilima na mbinu nyingine za kijadi. Badala yake watatumia njia za kisasa za kuvunia mazao yao.
    Umaskini mwingine huwa mwiba wa kujichoma. Baadhi ya watu ni mikunguni. Kulaza damu kwao kunawafanya kuwa wategemezi katika familia na jamii kwa jumla. Kwa vile hawajazoea kuinamia cha mvunguni, hata wakifunzwa kuchakura hawawezi. Ili kujaribu kuutibu uwele wao na ufukara baadhi yao hutafuta njia za mkato kama vile upwekuzi wa vitu vya wale waliojitahidi. Wakifanikiwa huweza kufurisha vibindo vyao. Hata hivyo mkono mrefu wa walinda usalama ukiwakumbatia wao hubakia kusagika kwa dhiki isiyomithilika ndani ya magereza.
    Majanga ya kimaumbile kama vile mitetemeko ya ardhi, mikurupuko ya maradhi hatari, moto, ukame na mafuriko huchangia na kuzidisha umaskini. Matukio hayo yakiandama kidindia watu wengi huhasirika. Licha ya mali nyingi kupotea, manusura huachwa wakiwa maskini hohehahe. Matumizi yao hupotea kwani wengi huhitajika kuanza maisha upya.
    Vijana ni nguzo muhimu katika maendeleo ya nchi yoyote ile. Endapo watajiingiza katika uraibu wa dawa za kulevya, wataathirika wao wenyewe na jamii kwa jumla. Pamoja na kuwa vijana hawa hufuja pesa nyingi katika ununuzi wa dawa hizi, dawa zenyewe huwadhoofisha na kuwapoka nguvu za kushiriki katika uzalishaji mali. Kutokana na hali hii,umaskini hupaliliwa na kushamiri zaidi.
    Umaskini huzua matatizo mbalimbali katika jamii. Ufukara huchachawiza juhudi za serikali za kuwapa raia wake mahitaji ya kimsingi kama vile huduma za afya. Pia umaskini husababisha maovu mbalimbali ya kijamii kama vile mauaji na ukahaba.
    Baadhi ya wanajamii huona kwamba njia ya kipekee ya kukabiliana na changamoto zinazosababishwa na hali ya ulitima ni kupitia kwa biashara haramu. Hali hii huchochea zaidi kudorora kwa maadili ya kijamii.
    Mataifa mbalimbali ulimwenguni yamezua mikakati mahsusi ya kukabiliana na umaskini. Baadhi ya mataifa yamebuni utaratibu maalum wa kupunguza mwanya mkubwa uliopo kati ya matajiri na maskini. Mojawapo ya mipango hiyo ni kupandisha viwango vya kodi inayotozwa wenye mishahara minono na wafanyibiashara wenye pato kubwa. Aidha huduma za burudani hutozwa kodi ya kiwango cha juu. Kupitia kwa kodi hizo, na njia nyinginezo, serikali za nchi hizo hupata pesa za kuwahudumia maskini.
    Mataifa yanayoendelea yanaweza kuwakwamua wananchi kiuchumi kwa kuwapa wahitaji mitaji ya kuanzisha miradi mbalimbali ya kimaendeleo. Mifano ya miradi hiyo ni viwanda vya ‘Jua kali’, ususi wa vikapu na uchongaji wa vinyago. Hali kadhalika, serikali inaweza kuwatafutia masoko ya nje wafanyi biashara wadogo wadogo. Aidha, serikali inaweza kupunguza ushuru kwa bidhaa zinazoagizwa na masoko ya nje wafanyibiashara wa aina hiyo. Mathalan, ushuru unaotozwa nguo kuukuu zinazoingizwa nchini ukipunguzwa, wauzaji wa nguo hizi watafaidika zaidi na hali ya umaskini itaendelea kupungua.
    Sehemu za mashambani ni mhimili mkubwa wa uchumi. Ingawa kumekuwa na juhudi za kuzistawisha sehemu hizi kwa kusambaza huduma za umeme na maji kwa gharama nafuu, bado hali haijawa ya kuridhirisha. Ili kuimarisha sehemu hizi na kukabiliana vilivyo na tatizo la umaskini, hatuna budi kusambaza huduma hizi hasa katika sehemu kame. Sehemu hizi zikipata maji, kilimo chenye natija kitaendelezwa na umaskini utakuwa karibu kuzikwa katika kaburi la sahau. Ikiwa tutazitekeleza sehemu hizi, vijana wanaoweza kusistawisha watahamia mjini kutafuta maisha ‘bora’. Hali hii itazidisha msongomano wa watu mjini.
    Umaskini ni nduli ambaye lazima aangamizwe ima fa ima. Vijana hawana budi kubadili mtazamo wao hasa kuhusu kazi za mashambani na kujitahidi kuimarisha kilimo. Fauka ya hayo, mifumo mwafaka ya elimu ibuniwe ili kukidhi mahitaji ya kiuchumi ya taifa. Badala ya kuhimiza elimu ya kinadharia, elimu tekelezi isisitizwe zaidi ili wale wanaokosa kazi za kiafisi waweze kujiajiri katika kazi za kiufundi. Ukusanyaji wa ushuru uimarishwe zaidi. Hali ya usalama iendelee kustawishwa ili kuzidi kuwavutia wawekezaji, na hivyo kubuni nafasi zaidi za kazi.


    (a)Kulingana na kifungu ‘umasikini ni hali inayoletwa na udhaifu wa mtu binafsi’. Jadili
    (maneno 30-40)
    (b)Jamii ina uwezo wa kukabiliana na hali ya umaskini inayowakumba raia wake. Thibitisha
    kwa mujibu wa kifungu (maneno 40-50)

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Andika wingi wa sentensi zifuatazo; i) Sokwe aliukwea mti huo kwa kasi.ii) Mshale mkali ulitumiwa kumwua samba. (Solved)

    Andika wingi wa sentensi zifuatazo;
    i) Sokwe aliukwea mti huo kwa kasi.
    ii) Mshale mkali ulitumiwa kumwua samba.

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Tumia neno "vile" kama. i) Kivumishi … ii) Kiwakilishi iii) Kielezi (Solved)

    Tumia neno "vile" kama.
    i) Kivumishi …
    ii) Kiwakilishi
    iii) Kielezi

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza maana mbili za sentensi ifuatayo (Solved)

    Eleza maana mbili za sentensi ifuatayo.
    Nitakuja kukagua kazi hiyo baada ya saa mbili.

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)

  • Waajiri wengi wanazilaumu taasisi za elimu kwa kukosa kutoa wafanya kazi wenye ujuzi tosha, hasa wa kiteknolojia za kisasa kama kutumia... (Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha kisha ujibu maswali:-

    Waajiri wengi wanazilaumu taasisi za elimu kwa kukosa kutoa wafanya kazi wenye ujuzi tosha, hasa wa kiteknolojia za kisasa kama kutumia kompyuta kutenda kazi mbalimbali. Hali hii imekuwa ya kuhuzunisha sana.
    Ujuzi wa kuweza kutumia Kompyuta unaweza kumfaa mwanafunzi hata anapokosa nafasi ya kujiunga na chuo kikuu kwa vile anaweza kuendelea na elimu yake kupitia kwa elimu mtandao. Pia anaweza kufanya utafiti wa kina kupitia intaneti na kwa njia hii akaimarisha elimu yake.
    Mojawapo ya njia ya kuimarisha elimu kuhusu maswala ya teknolojia ni kuanzishwa kwa mikakati mipya ya kufunza. Somo la Kompyuta laweza kuimarika mashuleni endapo kwanza walimu watahamasishwa juu ya faida za ujuzi huu.
    Kwa kutumia Kompyuta kufunza, walimu wanaweza kufunza madarasa kadhaa katika kipindi kimoja bila kulazimika kuyahudhuria. Hii itapunguza kiwango cha kazi kwa walimu kwa vile watapata muda wa kufanya utafiti mpana. Aidha, watapata habari na ufahamu zaidi wa mambo kwa kutumia mitambo ya Kompyuta kutoka kwenye intaneti, kupitia tovuti.

    Hata hivyo mipango hii inakabiliwa na changamoto kama vile bei za juu za mitambo na vifaa vya Kompyuta, ukosefu wa miundo msingi itakayowezesha utumiaji wa mitambo hii na ukosefu wa walimu waliohitimu somo la Kompyuta.
    Pia, kuna tatizo la ukosefu wa nguvu za umeme hasa maeneo ya mashambani; vile vile, katika maeneo yaya haya, wanafunzi na wazazi wengi huvichukulia somo la Kompyuta kuwa gumu na linalofaa wakaazi na wanafunzi kutoka maeneo ya mijini na linalofaa wakaazi muhimu kwao mashambani.



    Maswali
    (a) Ipe taarifa uliyoisoma anwani inayoifaa
    (b) “Hali hii imekuwa ya kuhuzunisha.” Ni hali gani inayozungumziwa katika aya ya 1?
    (c) Ujuzi wa kutumia Kompyuta unaweza kumfaidi vipi mwanafunzi?
    (d) Mikakati mipya ya kuimarisha elimu kuhusu maswala ya teknolojia inakabiliwa na
    vizingiti vipi?
    (e) Taja manufaa mawili ambayo mwalimu anaweza kupata kutokana na ujuzi wa teknolojia
    ya Kompyuta
    (f) Andika msamiati mwafaka zaidi kwa maneno yafuatayo:
    (i) Kompyuta
    (ii) Intaneti

    Date posted: October 4, 2019 .    Answers (1)