Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Taja sifa mbili za mizizi wa kitenzi.

      

Taja sifa mbili za mizizi wa kitenzi.

  

Answers


Maurice
(i) Haubadiliki kitenzi kinaponyambuliwa.

(ii) Hubeba maana ya kimisingi ya kitenzi.
maurice.mutuku answered the question on November 20, 2019 at 08:22


Next:  Sekta za umma humu nchini hazina kifani katika uzembe. Unapohitaji huduma za posta, umeme, maji, mawasiliiano, utayarishaji wa mishahara na malipo mengine, utalazimika...
Previous: (b) Tofautisha vitamkwa vifuatavyo. (i) /ny/ (ii) /ng’/

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • Sekta za umma humu nchini hazina kifani katika uzembe. Unapohitaji huduma za posta, umeme, maji, mawasiliiano, utayarishaji wa mishahara na malipo mengine, utalazimika...(Solved)

    Sekta za umma humu nchini hazina kifani katika uzembe. Unapohitaji huduma za posta, umeme, maji, mawasiliiano, utayarishaji wa mishahara na malipo mengine, utalazimika kusubiri kwa siku, miezi na hata miaka ili upate haki yako, hata wakati mwingine ukakosa!


    Wafanyakazi wa sekta hii hukosa kutimiza majukumu yao ipasavyo kutokana na ukosefu wa motisha yaani mishahara duni, uhaba wa nyenzo za kutekeleza majukumu yao na kutozingatia kazi kwa wakaguzi na viongozi wa wafanyakazi.

    Minghairi ya hali hii, visa vya ufisadi ndiyo sifa inayopambanua huduma za umma. Baadhi ya wafanyakazi hupatikana ofisini na katika maeneo ya kazi kwa nadra sana kwa sababu huwa wanakimbilia kwingineko kutafuta malipo ya kujazia mishahara yao duni kujikimu kimaisha. Athari za matendo haya zimekuwa kukokota kukua kwa uchumi, ukosefu wa imani kwa huduma za umma na utoaji wa huduma hafifu.

    Kufuatia udhaifu huu, katika siku za majuzi, sekta za kibinafsi zimetambulika kuwa muhimu sana katika utoaji wa huduma kwa wananchi. Uchumi wa mataifa yanayopendelea sekta za kibinfasi yametambuliwa kukua kwa kasi kuliko yale yanayoandama mfumo kongwe wa serikali kutawala shughuli za uzalishaji mali.

    Lakini kwa kuwa mashirika ya kibinafsi, aidha, yamebainika kuwa na udhaifu wa aina yake, serikali inaposhirikiana kindakindaki na sekta hii, ustawishaji wa hali za kazi utajiri. Kwa kuwa dhamira kuu ya mashirika ya kibinafsi huwa kujizolea faida kemkem, yamekuwa yakifanyiza wafanyakazi wao kazi nyingi kupita kiasi ambayo mara nyingine huwadhuru kiafya. Japo mshahara wao ni afadhali kuliko wa sekta ya umma, baadhi ya sera huwa kandamizi na hutinga fursa za wafanyakazi kukuza majukumu yao binafsi, mengi yakiwa muhimu kwa jamii kijumla.

    Ushirikiano wa serikali na mashirika ya kibinafsi, kwa hivyo, una uwezo mkubwa wa kustawisha na kupanua mawanda ya uchumi. Utakuwa dawa mujarabu kwa udhaifu wa pande zote. Sekta za kibinafsi zikijizolea faida nyingi kwa upande mmoja, zitasaidia katika kuondoa uzembe, utepetevu na mapuuza yanayotamalaki huduma za serikali kwani yatalenga uzalishaji mwingi ili kutimiza malengo yao.

    (a) Eleza mawazo muhimu ya aya tatu za mwanzo kwa maneno 50 – 55.
    (b) Fupisho aya tatu za mwisho bila kubadilisha maana iliyokusudiwa kwa maneno 75 – 80.

    Date posted: November 20, 2019.  Answers (1)

  • Takwimu za tafiti za umaskini kila mara huonyesha kuwa bara la Afrika ndilo bara maskini kabisa kote duniani. Takriban wakaazi kiasi cha asilimia...(Solved)

    Takwimu za tafiti za umaskini kila mara huonyesha kuwa bara la Afrika ndilo bara maskini kabisa kote duniani. Takriban wakaazi kiasi cha asilimia themanini hawawezi kumudu kutumia dola moja kwa siku. Toka kaskazini hadi kusini. mashariki hadi magharibi mwa bara, makaazi ya vibanda yametamalaki. Wakaazi wengi hulala njaa kutokana na ukosefu wa chakula. Watu wa mitaani waliovaa mararuraru wamejaa katika miji ya bara hili. Swali ni: Je, kwa nini umaskini umeliganda bara la Afrika hivi mithili ya kupe? Kwa nini bara huselelea katika lindi la uchochole?

    Ili kuelewa sababu za umaskini kuganda barani Afrika, yampasa mtu ima fa ima kurejelea historia ya bara hili. Kwa kipindi cha karne nyingi, Afrika ilidhibitiwa na walowezi pamoja na mabeberu. Wanawake ambao wangelistwawisha bara hili kiuchumi walitwaliwa kimabavu na kupelekwa, huku wamefungwa minyororo, kustawisha uchumi wa mabara mengine. Afrika ikaporwa nguvu ambayo ni rasilmali kuu katika ustawishaji wa uchumi. La kusikitisha ni kuwa Afrika haikufidiwa kutokana na wizi huu. Badala yake iliongezewa mizigo mingine.

    Baada ya kipindi cha biashara ya utumwa kumalizika, Afrika ilijipata katika janga jingine. Wakoloni wakaliingilia bara kwa pupa. Wakaligawanya katika koloni mbalimbali miongoni mwao. Wakaingiwa na wendawazimu kuiba malighafi ya bara hili. Wakaiba mashamba, madini, miti na chochote cha maana walichokipata. Badala ya malighafi haya kutumika kunawirisha bara la Afrika, yalitwaliwa kustawisha chumi za walikotoka wakoloni. Afrika ikaachwa kuzidi kudidimia katika lindi la umaskini.

    Wakoloni walipotoka barani Afrika na kuzipa dola nyingi za Afrika ‘uhuru’, waliacha mkururo wa madhila. Madhila haya hayangeikubalia Afrika kujikomboa kutoka katika biwi la uchochole. Tatizo la kwanza na kubwa zaidi ni wakoloni kugawanya na kukatakata Afrika katika mataifa mengi. Mgawanyo huu ukawa haukufuata utaratibu wowote. Kwa sababu hii, watu wa nasaba moja wakawekwa katika nchi tofauti. Mathalani , watu wa nasaba ya Kisomali waligawanywa na kuwekwa chini ya nchi huru ya Somali, wengine chini ya dola la Uhabeshi, huku wengine wakiwa nchini Kenya na Jibuti. Watu kama hawa hawakutaka mpango huu. Waliokuwa Kenya na Uhabeshi wakachukua silaha na kupigana ili warejeshwe chini ya himaya moja ya taifa huru la Somali. Watu kama hawa wakatumia muda mwingi kupigana; muda ambao ungetumika kuinua Afrika kiuchumi. Mapigano haya ya wenyewe kwa wenyewe yamekithiri kote katika bara la Afrika.

    Halikadhalika, mkoloni hakufanya juhudi zozote za kuanzisha viwanda ambavyo vingenyanyua uchumi wa Afrika na kuwatoa Waafrika katika biwi la ufukara. Palipokuwa na ari yoyote ya kuanzisha kiwanda, kilipoanzishwa hakikusaidia Afrika kiuchumi. Vilikuwa viwanda vya kupunguza zigo la bidhaa na kuzifanya kuwa nyepesi ili zisafirishwe kwa ajili ya viwanda vya nchi walizotoka wakoloni.

    Kwa kipindi cha muda ambao mkoloni amekuwa na maingiliano na wakaazi wa Afrika, amehakikisha kuwa mwafrika amekuwa mtegemezi wake. Malighafi ya Afrika yalipelekwa kutayarishiwa viwanda vya wakoloni. Kisha mwafrika alirudishiwa zikiwa bidhaa kamili za kutumiwa. Mwafrika akaonyeshwa kuwa chochote kilichotoka kwa wakoloni ni bora zaidi ya chake alichozalisha. Hii ikawa ni mbinu moja ya wakoloni kuwafukarisha Waafrika. Hata sasa, kilichotoka Ulaya, hata kama ni cha hali ya chini, huonekana bora zaidi kuliko alichozalisha Mwafrika

    Kwa upande mwingine, inadhihirika kuwa wakoloni hawajawahi kuondoka na kuwaachia Waafrika jukumu kamili la kuendesha uhuru wao kisiasa, kijamii na kiuchumi. Waliondoka kupita mlango mmoja na kurudi kwa wa pili. Mlango wa pili ukawa ni ukoloni kuchukua sura nyingine, sura ya ukoloni mamboleo. Kupitia ukoloni huu, wakoloni hudhibiti uchumi na maendeleo ya Afrika kupitia asasi mbili walizozianzisha, yaani Benki Kuu ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani. Ili kupata mikopo ya maendeleo, asasi hizi hutoa masharti ambayo hukwamiza badala ya kuchangia kuleta maendeleo barani Afrika.

    Sasa hivi pana haja ya wana wa Afrika kufanya vikao vya dhurura ili kujadiliana kuhusu suluhisho la tatizo hili sugu la umaskini barani. Lazima wawahimize Waafrika wote kujikomboa kiakili na kung’amua kuwa maendeleo ya bara lazima yaongozwe na yadhibitiwe na Waafrika wenyewe. Wawahimize kuacha hulka za kukimbilia mataifa yaliyowafanya watumwa na kuwakalia kikoloni kwa misaada ya maendeleo. Misaada hii si ya dhati bali ni ya chati na hailengi kuondoa umaskini barani bali kuuendeleza.

    Pana haja pia Waafrika kuwa na miungano ya kiuchumi. Miungano hii husaidia katika uteteaji wa soko pamoja na bei za bidhaa zao ikilinganishwa na taifa moja kuyaendeleza mambo haya. Halikadhalika, Waafrika wanapaswa kutambua kile wanachotaka na kupanga mikakati ya kufikia mahitaji ya kimsingi kwa wananchi wake. Kwa mfano, uimarishaji wa mbinu msingi ambazo zitachangia kuimarisha uchumi wa mataifa wahitaji kuwa mstari wa mbele badala ya ununuzi wa magari na ndege za hadhi za kuwabebea viongozi.

    (a) Ipe taarifa uliyoisoma anwani mwafaka.

    (b) Kutamalaki kwa umaskini barani Afrika kunadhihirishwa na nini.

    (c) Onyesha jinsi ambavyo wakoloni wameendeleza umaskini barani Afrika.

    (d) Thibitisha kwa kutoa hoja tatu, dhana ya kuwa “Waafrika wenyewe ndio wamechangia kuwepo kwa umaskini wa bara la Afrika.”

    (e) Umaskini barani Afrika unaweza kukabiliwa vipi kwa mujibu wa makala haya?

    (f) Eleza msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika taarifa:
    (i) kuselelea……………
    (ii) mabeberu…………

    Date posted: November 20, 2019.  Answers (1)

  • Halleluyah… Mungu asifiwe sana… shetani ashindwe… Tambua na utoe sifa za sajili hii.(Solved)

    Halleluyah… Mungu asifiwe sana… shetani ashindwe…
    Tambua na utoe sifa za sajili hii.

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Eleza dhima ya sentensi hii. Rudi ulikotoka.(Solved)

    Eleza dhima ya sentensi hii.
    Rudi ulikotoka.

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Kanusha. Mwanafunzi alikuwa akilia alipojikwaa.(Solved)

    Kanusha.
    Mwanafunzi alikuwa akilia alipojikwaa.

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Onyesha aina ya vishazi katika sentensi hii. Isipokuwa ni kulewa kwake angeenda Kitui.(Solved)

    Onyesha aina ya vishazi katika sentensi hii.
    Isipokuwa ni kulewa kwake angeenda Kitui.

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Kosoa sentensi ifuatayo kwa njia mbili tofauti. Ningelima shamba langu kwa wakati ufaao ningalivuna sawasawa.(Solved)

    Kosoa sentensi ifuatayo kwa njia mbili tofauti.
    Ningelima shamba langu kwa wakati ufaao ningalivuna sawasawa.

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi kutofautisha maana ya majina haya. Nadhari Nathari(Solved)

    Tunga sentensi kutofautisha maana ya majina haya.
    Nadhari
    Nathari

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Onyesha shamirisho katika sentensi ifuatayo. Kakubwa alimjengea mama yake nyumba kwa mawe.(Solved)

    Onyesha shamirisho katika sentensi ifuatayo.
    Kakubwa alimjengea mama yake nyumba kwa mawe.

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Badilisha sentensi ifuatayo iwe katika kauli ya kutendwa. Simba mwenda pole alimla swara mnono sana.(Solved)

    Badilisha sentensi ifuatayo iwe katika kauli ya kutendwa.
    Simba mwenda pole alimla swara mnono sana.

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya matawi. Anampenda wake sana lakini alimpiga sana(Solved)

    Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya matawi.
    Anampenda wake sana lakini alimpiga sana

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Tumia neno msomi kama nomino na kama kivumishi katika sentensi.(Solved)

    Tumia neno msomi kama nomino na kama kivumishi katika sentensi.

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Andika kinyume cha sentensi hii. Mama alienda sokoni jana asubuhi.(Solved)

    Andika kinyume cha sentensi hii.
    Mama alienda sokoni jana asubuhi.

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Andika sentensi hii kwa udogo wingi. Mti ulikatwa ukatengeneze kiti.(Solved)

    Andika sentensi hii kwa udogo wingi.
    Mti ulikatwa ukatengeneze kiti.

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi moja ukitumia kiunganishi cha kuongeza.(Solved)

    Tunga sentensi moja ukitumia kiunganishi cha kuongeza.

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Tumia kiambishi ndi- pamoja na kiwakilishi huru cha nafsi ya kwanza wingi.(Solved)

    Tumia kiambishi ndi- pamoja na kiwakilishi huru cha nafsi ya kwanza wingi.

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Thibitisha kuwa neno moja linaweza kuwa katika ngeli mbili tofauti.(Solved)

    Thibitisha kuwa neno moja linaweza kuwa katika ngeli mbili tofauti.

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Onyesha mofimu mbalimbali katika neno kikikipikia.(Solved)

    Onyesha mofimu mbalimbali katika neno kikikipikia.

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Eleza kanuni ya kutia shadda katika lugha ya Kiswahili.(Solved)

    Eleza kanuni ya kutia shadda katika lugha ya Kiswahili.

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)

  • Toa mfano wa maneno mawili ambayo yana sauti mwambatano mbili.(Solved)

    Toa mfano wa maneno mawili ambayo yana sauti mwambatano mbili.

    Date posted: October 31, 2019.  Answers (1)