Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Huku ukidondoa ushahidi wa kiisimu jadili madai kwamba kiswahili ni lugha asili ya kiafrika

Huku ukidondoa ushahidi wa kiisimu jadili madai kwamba kiswahili ni lugha asili ya kiafrika

Answers


Faith
Tunaposema kuwa kiswahili ni lugha ya kiafrika basi tunachosema ni kuwa kiswahili ni lahaja ya kibantu.Wanaisimu tajika Kama vile Guthrie, Greenberg na wengineo walifanya utafitiwa lugha zingine za kibantu ikiwemo kiswahili na kupata uhusiano huu wa kiisimu.Baadhi ya madai hayo ni;
• Msamiati was kiswahili.Guthrie (1967) alionyesha uhusiano uliopo Kati ya kiswahili na lugha zingine za kibantu.Alionyesha uhusiano wa mashina mengi ambayo yamezagaa katika lugha mbalimbali za kibantu.Alichunguza asili ya neno'Bantu' au watu .Shina hili linapatikana katika lugha zote za kibantu na hii unatuonyesha kuwa kiswahili ni kiafrika.kwa mfano
Kiswahili
Mtu - watu
Kimeru
Muntu - anti
Kikuyu
Mûndû - andû
• Mpangilio was majina katika ngeli.Lugha za kibantu Zina mpangilio wa majini katika makundi au ngeli.Pia kiswahili inaonyesha mpangilio huo kwa hivyo kiswahili ni kibantu.mfano
Kiswahili
Mtu - watu
Kikuyu
Mûndû - andû
• Mnyambuliko wa vitenzi.lugha za kibantu Kama ilivyo kiswahili hudhihirisha mnyambuliko wa vitenzi.Kwa hivyo kiswahili asili take ni Kiafrika.kwa mfano
Kutenda
Lima
Kutendana
Limana
Kutendeka
Limika
• Mfumo was silabi wazi.Lugha za kibantu hudhihirisha mfumo wa silabi wazi yaani Kila silabi ya neno lenye asili ya kibantu huishia kwa vokali.Hii pia huonekana kwa lugha mbalimbali za kibantu.
• Lugha za kibantu Kama ilivyo kiswahili huunganisha mofimu ili kuunda sentensi ya neno moja.kwa mfano 'alicheza'
A-kiambishi Cha nafsi
Li-kiambishi Cha wakati uliopita
Chez-mzizi wa kitenzi
a-kiishio

Titany answered the question on December 6, 2021 at 08:16

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions