Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Andika vinyume vya sentensi zifuatazo:- (i) Mama anaanika nguo (ii) Baba anaenda sokoni.

      

Andika vinyume vya sentensi zifuatazo:-
(i) Mama anaanika nguo
(ii) Baba anaenda sokoni.

  

Answers


Kavungya
(i) Mama anaanika nguo
Mama anaanua nguo

(ii) Baba anaenda sokoni.
Baba anatoka sokoni
Kavungya answered the question on November 21, 2022 at 12:49


Next: Bainisha maneno haya yanapatikana katika ngeli ipi? Ngoma – Ukuta – MachoUgonjwa – Mmea – Maiti –
Previous: Kanusha sentensi zifuatazo. (i) Mkulima analima shamba. (ii) Mwanafunzi anasoma kitabu.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • Bainisha maneno haya yanapatikana katika ngeli ipi? Ngoma – Ukuta – MachoUgonjwa – Mmea – Maiti –(Solved)

    Bainisha maneno haya yanapatikana katika ngeli ipi?
    Ngoma –
    Ukuta –
    MachoUgonjwa –
    Mmea –
    Maiti –

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Andika maneno yenya miundo ya silabi ifuatayo. KI (Konsonanti irabu) – KKI (Konsonanti, konsonanti, irabu) – II (irabu) –(Solved)

    Andika maneno yenya miundo ya silabi ifuatayo.
    KI (Konsonanti irabu) –
    KKI (Konsonanti, konsonanti, irabu) –
    II (irabu) –

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Andika majukumu tatu ya lugha.(Solved)

    Andika majukumu tatu ya lugha.

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Taja vigezo vitatu vinavyotumika kuainisha konsonati.(Solved)

    Taja vigezo vitatu vinavyotumika kuainisha konsonati.

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Jibu maswali yote kwenye nafasi zilizoachwa wazi. Mawasiliano ni neno ambalo asili yake ni wasili. Wasili lina maana ya kufika kwa mtu, kitu, au jambo fulani baada...(Solved)

    Jibu maswali yote kwenye nafasi zilizoachwa wazi.
    Mawasiliano ni neno ambalo asili yake ni wasili. Wasili lina maana ya kufika kwa mtu, kitu, au
    jambo fulani baada ya mwendo au safari. Kwa hivyo kuwasiliana kuna maana watu, kitu au
    mambo kufikiana kutoka mahali.
    Katika siku za jadi mawasiliano yalikuwepo lakini ya shida. Hata hivyo, watu waliwasiliana kwa
    kutumia moshi, ngomezi au kupiga mbiu. Mbinu hizi za jadi zilitumiwa baina ya vijiji ili
    kujulisha wanakijiji jambo la dharura au kuwajulisha jambo lingine lolote. Mbiu ilitumika kwa
    jambo la dharura. Njia za kusafirisha mizigo zilikuwa haba. Baadhi ya watu walitumia wanyama,
    kama fahali au farasi kukokotea mizigo yuao.
    Siku hizi mawasiliano yamepanuka sana. Mawasiliano ya kisasa yanahusisha simu, mtandao,
    televisheni na wavuti. Mawasiliano ya kisasa yamefanya ulimwengu wa kisasa kuwa kijiji kimoja
    kikubwa.
    Kwa kuzingatia maudhui haya, vyombo au njia kama redio, simu, waraka, ndege, meli, motokaa
    na wavuti vimepewa jina la vyombo vya mawasiliano. Hivyo basi yafaa tutathmini ni vipi
    vyombo au njia hizi hufanya kazi ya kuwasiliana na huwasilisha nini. Vyombo hivi vinaweza
    kuelezwa chini ya vichwa vitatu; usafiri, mazungumzo na picha. Vyombo mathalan baiskeli,
    ndege, meli na magari hufanya kazi ya kuwasafirisha watu kutoka janibu moja hadi nyingine.
    Watu wanaposafiri huwa wanasafirisha mali yao. Bidhaa kama kahawa, vyuma na mizigo
    mingine husafirishwa kwa meli, ndege na magari kupitia majini, hewani au barabarani.
    Bandari, viwanja vya ndege na barabara zimeimarishwa ili kukuza uchumi na kuleta maendeleo.
    Anayesafirisha bidhaa fulani na wakati huo anatakikana kukusanya nyingine, inamlazimisha
    asiambatane na bidhaa hizo lakini ahakikishe zimewasili alikozikusudia. Hivyo basi njia nyingine
    ya mawasiliano ilivumbuliwa.
    Njia hii ambayo ni mazungumzo hutumia vifaa kama barua, simu, barua pepe na kipepesi.
    Mtumiaji ataandika ujumbe na kuutuma kupitia shirika la posta au mashirika mengine ama
    mtandao. Yamkini ilihitajika kuweza kujibizana na kuulizana kati ya watu hao wawili ndipo simu
    ilipovumbuliwa na kumwezesha mtu kuzungumza na mwingine akiwa mbali sana. Watu
    huzungumza na kufahamiana. Ilipohitaji mtu kukiona kitu anachozungumzia ndipo ilibidi kuunda
    vifaa vya kuonyesha picha kama vile televisheni.
    Ilikuwa fahari kubwa sana kwa Wakenya kuwasiliana na nchi ya Ghana wakati wa michuano ya
    mpira ya kuwania kombe la taifa bingwa Afrika. Wakenya waliweza kuiona michezo hiyo moja
    kwa moja ingawa kijiografia Kenya na nchi hiyo zina majira tofauti.
    Mawasiliano tuliyotaja ni vyombo vya ufundi vilivyoundwa lakini kunayo maswasiliano ya ana
    kwa ana. Mwalimu na mwanafunzi darasani huwasiliana kutumia midomo, mikono, macho,
    kichwa na ishara nyinginezo. Wanapofanya hivyo huwa wanaelewana.
    Ndege kama kuku akihisi adui hufanya ishara au mlio fulani wa kutahadharisha viranga wakek
    katika michezo. Mwamuzi huwasiliana na wachezaji labda kwa kutumia firimbi au kipenga,
    kengelel au ishara za mkono. Kengele pia hutumiwa shuleni ili kuonyesha kukamilika kwa
    kipindi au kuhitajika mahali pengine.
    Kwa muhtasari, mawasiliano hutumia chochote ilimradi ujumbe utokao kwa mtu, kitu au mahali
    fulani ufike panapotarajiwa.

    MASWALI:
    (i) Taja anwani faafu ya kifungo hiki.

    (ii) Vyombo vya mawasiliano vimeleta manufaa gani katika maisha ya watu?

    (iii) Mawasiliano yameelezwa katika vipenge vitatu. Vitaje.

    (iv) Andika visawe vya:
    (a) Televisheni –
    (b) Waraka –

    (v) Nini maana ya:
    (a) Ana kwa Ana –
    (b) Ulimwengu umekuwa kijiji kimoja kikubwa –

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Taja majukumu matano ya fasihi simulizi.(Solved)

    Taja majukumu matano ya fasihi simulizi.

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Fasihi simulizi ni nini?(Solved)

    Fasihi simulizi ni nini?

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Kanusha sentensi ifuatayo. Nyumba hiyo itafunguliwa.(Solved)

    Kanusha sentensi ifuatayo.
    Nyumba hiyo itafunguliwa.

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Tambulisha maneno mbalimbali katika sentensi zifuatazo. i) Mwanafunzi mvumilivu alisoma vizuri. ii) Yule ameongea maneno mengi.(Solved)

    Tambulisha maneno mbalimbali katika sentensi zifuatazo.
    i) Mwanafunzi mvumilivu alisoma vizuri.

    ii) Yule ameongea maneno mengi.

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Sentensi zifuatazo ziko katika nyakati / hali gani? a) Otieno hula samaki kila siku b) Yeye anaandika tu kitabu(Solved)

    Sentensi zifuatazo ziko katika nyakati / hali gani?
    a) Otieno hula samaki kila siku

    b) Yeye anaandika tu kitabu

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Andika sentensi zifuatazo kwa wingi. i) Ukuta ambao ulianguka ni huu. ii) Mwanagenzi yule amepita mtihani vizuri.(Solved)

    Andika sentensi zifuatazo kwa wingi.
    i) Ukuta ambao ulianguka ni huu.

    ii) Mwanagenzi yule amepita mtihani vizuri.

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Tenganisha neno lifuatalo katika viambiu vyake mbalimbali. Aliyempigia(Solved)

    Tenganisha neno lifuatalo katika viambiu vyake mbalimbali.
    Aliyempigia

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Sauti mwambatano ni nini?(Solved)

    Sauti mwambatano ni nini?

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Toa mifano miwili ya sauti za nazali/ving’ong’o.(Solved)

    Toa mifano miwili ya sauti za nazali/ving’ong’o.

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Andika konsonanti tatu ambazo ni vipasuo.(Solved)

    Andika konsonanti tatu ambazo ni vipasuo.

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Taja aina mbili za konsonanti.(Solved)

    Taja aina mbili za konsonanti.

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Viungo ambavyo hutumika katika utamkaji wa sauti huitwa aje?(Solved)

    Viungo ambavyo hutumika katika utamkaji wa sauti huitwa aje?

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Kiungo ambacho hutetemeka na kutoa sauti huitwaje?(Solved)

    Kiungo ambacho hutetemeka na kutoa sauti huitwaje?

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Taja: i) Irabu za mbele. ii) Irabu ya kati iii) Irabu za nyuma(Solved)

    Taja:
    i) Irabu za mbele.

    ii) Irabu ya kati

    iii) Irabu za nyuma

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Taja aina mbili kuu za sauti katika kiswahili.(Solved)

    Taja aina mbili kuu za sauti katika kiswahili.

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)