Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Andika sentensi zifuatazo kwa wingi. i) Ukuta ambao ulianguka ni huu. ii) Mwanagenzi yule amepita mtihani vizuri.

      

Andika sentensi zifuatazo kwa wingi.
i) Ukuta ambao ulianguka ni huu.

ii) Mwanagenzi yule amepita mtihani vizuri.

  

Answers


Kavungya
[i] Kuta ambazo zilianguka ni hizi.

[ii] Wanagenzi wale wamepita mitihani vizuri .
Kavungya answered the question on November 21, 2022 at 11:46


Next: Indicate the appropriate intonation at the end of each sentence. i) Have all the students been registered? ii) Stop wasting time. iii) That was superb! iv) There is hope...
Previous: Mary cannot bear children i) Identify the above genre. ii) Give the two possible meanings of the above. iii) Give one function of the above genre.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • Tenganisha neno lifuatalo katika viambiu vyake mbalimbali. Aliyempigia(Solved)

    Tenganisha neno lifuatalo katika viambiu vyake mbalimbali.
    Aliyempigia

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Sauti mwambatano ni nini?(Solved)

    Sauti mwambatano ni nini?

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Toa mifano miwili ya sauti za nazali/ving’ong’o.(Solved)

    Toa mifano miwili ya sauti za nazali/ving’ong’o.

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Andika konsonanti tatu ambazo ni vipasuo.(Solved)

    Andika konsonanti tatu ambazo ni vipasuo.

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Taja aina mbili za konsonanti.(Solved)

    Taja aina mbili za konsonanti.

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Viungo ambavyo hutumika katika utamkaji wa sauti huitwa aje?(Solved)

    Viungo ambavyo hutumika katika utamkaji wa sauti huitwa aje?

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Kiungo ambacho hutetemeka na kutoa sauti huitwaje?(Solved)

    Kiungo ambacho hutetemeka na kutoa sauti huitwaje?

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Taja: i) Irabu za mbele. ii) Irabu ya kati iii) Irabu za nyuma(Solved)

    Taja:
    i) Irabu za mbele.

    ii) Irabu ya kati

    iii) Irabu za nyuma

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Taja aina mbili kuu za sauti katika kiswahili.(Solved)

    Taja aina mbili kuu za sauti katika kiswahili.

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Soma Ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali. Beata alikuwa msichana mrembo lakini alikuwa haambiliki, hasemezeki . Fauka ya hayo, alikuwa na tamaa isiyo na kifani.(Solved)

    Soma Ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali.
    Beata alikuwa msichana mrembo lakini alikuwa haambiliki, hasemezeki . Fauka ya hayo, alikuwa na tamaa
    isiyo na kifani.
    Alipokuwa katika shule ya msingi, walimu na wazazi walimfunza umuhimu wa kuwa na maadili.
    Isitoshe, alifunzwa masomo vyema lakini akili yake ilikuwa butu. Akawa haingizi chochote cha maana ila
    uchafu wa fikira. Nyumbani nako hakuzingatia maonyo. Alikuwa hatulii.
    Wakati fulani wa krismasi, Beata alipomaliza tu shule ya msingi, alikutana na mwanamume mmoja
    mliliwa na wasichana wengi; mtajika kwa mali na jina lake ni Mshikaji . Beata akadanganywa akadanganyika.
    Akatorokea kwa huyu Mshikaji ambaye alikuwa ameshawataliki wake wawili tayari. Akawa mke mlezi. Ikabidi
    awalee watoto waliobaki na baba yao baada ya mamazao kutanzuka. Beata mwanzoni aliona raha, ingawa
    alikereka kuitwa mama kabla hata ya kumpokea mwana wake mwenyewe. Aliwabeza waliokuwepo awali na
    akajiona kuwa yeye ndiye mchukuzi bora. Akadharau kuwa pakacha likivuja, nafuu huwa ni kwa yule
    mchukuzi. Aliwaona wenzake kama maua yaliyonyauka na lake ndilo kwanza linaonana na jua.
    Muda si muda, akajikuta ana wana watatu kwa kipindi kifupi. Mumewe naye hakutulia na mambo ya
    nje. Akaimarisha nyendo zake za kiguu na njia, akipochoka, akiingia garini na kuikata mitaa. Beata aende wapi?
    Alifungika nyumbani ndi ndi Akamlea mwana huyu na yule; wake na wale wa kambo. Vijisenenesenene
    vikazidi. Lakini akajaribu kuvumilia akidhani atazila mbivu, wapi! Alipoligema ilibidi alinywe. Siku zikaja na
    kupita. Beata akajuta kwa kutosikiliza wakuu na kumkimbilia mtu ambaye hata hakuwa anamuelewa vizuri.
    Pesa na raha alizokuwa amezikimbilia akawa anazisikia kama hadithi ndotoni. Kwao nako kukawa hakurudiki.
    Beata akawa majamzito tena kama kawaida akawa anaenda kliniki za wajawazito. Alipopimwa ikabainika
    kuwa ana ukimwi. Mtoto alipozaliwa akafariki. Yule mumewe akaanza kumnyanyasa.
    Baada ya miaka mitatu, bwana Mshikaji, aliyekuwa akijitapa kwa unene na mali, akaanza kupotelewa na
    kiriba chake cha tumbo. Homa za hapa na pale zikaanza kumyemelea. Vipelevipele vikamsambaa mwilini. Hata
    akamsingizia Beata kuwa ni yeye aliyeuleta huo ukimwi Ilikuwa ni wazi kuwa msambazaji alikuwa ni yeye
    bwana. Waliokuwa pembe za chaki waliujua ukweli ulipokuwa . Baadhi ya vidosho wake walishaanza
    kupukutika kama majani yafanyavyo wakati wa mapukutiko. Isitoshe, wengine walikuwa hoi vitandani wakiwa
    hawajui waingiao wala watokao. Ugonjwa wa kamata ulishawakamata. Mwisho akawa ni wa kulazwa na
    kutoka hospitali hizi na zile. Pesa zikawaishia, wakawa waya. Beata akawa hana budi kuviuguza vidonda
    ndugu vyake na vya mumewe. Hatimaye, mumewe akabwagwa chini na ukimwi na akafafo!
    Si ndugu si marafiki, hawakumuelewa Beata. Waliamuona kama pweza aliyejipalia makaa makubwa ya
    moto makali. Ada za shule zikawa ni shida. Huruma ikwaingia watu. Watu wakasema. “Lisilobudi hutendwa.”
    Wakaubeba mzigo kwa hiari yao. Wakawafanyia watoto harambee ya ada na peza za matibabu. Mwishowe
    Beata naye aliaga dunia akiwa bado mbichi kwa umri. Hata miaka ishirini alikuwa bado hajafikisha. Watoto
    ikabidi walelewe na wahisani.
    Hapo walimwengu wakaja kutambua ukweli kwamba, uzuri si hoja hoja ni tabia. Isitoshe mtu
    akikimbiliwa na kila mtu, ukimwi hatauepuka. Mtu akiupata, hufa. Anadidimiza watu wengi pamoja na familia
    yake. Jamii ilifunzwa pia kuwa unene si hoja. Hata watu vibonge huweza kuleta ukimwi. Basi, jamii hiyo
    ikaazimia kuwa wao hawatakuwa watumwa wa tabia iletayo ukimwi. Walitambua kuwa ukimwi unarudisha
    nyuma maendeleo na kuipakaza jamii mizigo isiyo tarajiwa. Nasi tutahadhari kabla ya hatari

    1. Andika kichwa kifaacho kisa hiki
    2. Ni jambo gani lililomkera Beata baada ya kuolewa na Mshikaji?
    3. Toa sababu moja iliyomfanya Beata kuwadharau wenzake waliomtangulia kwa mshikaji?
    4. Ni kwa nini Beata alianza kujuta?
    5. Toa sababu moja kuonysha kuwa Mshikaji ndiye aliyeusambza ukimwi
    6. Kulingana na kifungu hiki taja hasara zinazoletwa na ukimwi.
    7. Kwa nini walimu na wazazi hawangelaumiwa kwa yale yaliyompata Beata?
    8. Andika maana ya:
    i) butu
    ii) Kope zikawa si zake
    iii) Akiwa bado mbichi
    iv) Kuzanzuka
    v) Vijisenensenene.

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Tambua kielezi katika sentensi ifuatayo. Kijana mkorofi ameadhibiwa vibaya(Solved)

    Tambua kielezi katika sentensi ifuatayo.
    Kijana mkorofi ameadhibiwa vibaya

    Date posted: August 17, 2020.  Answers (1)

  • Tambua kivumishi katika sentensi ifuatayo. Mwanafunzi mdogo amezungumza taratibu.(Solved)

    Tambua kivumishi katika sentensi ifuatayo.
    Mwanafunzi mdogo amezungumza taratibu.

    Date posted: August 17, 2020.  Answers (1)

  • Vita vina athari nyingi katika maisha ya binadamu, dhibitisha ukweli wa kauli hii ukiangazia riwaya ya chozi la heri.(Solved)

    Athari za vita katika riwaya ya Chozi la heri.

    Date posted: June 15, 2020.  Answers (1)

  • "Maisha yangu yalijaa shubiri tangu utotoni." Rejelea Chozi la heri.(Solved)

    a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    b) Bainisha tamathali ya usemi iliyotumika katika dondoo hili.

    Date posted: June 15, 2020.  Answers (1)

  • Nini maana ya kishazi?toa mifano ya vishazi(Solved)

    Nini maana ya kishazi?toa mifano ya vishazi.

    Date posted: May 10, 2020.  Answers (1)

  • Toa sababu nne zinazosababisha watu kufanya makosa katika matumizi ya lugha.(Solved)

    Toa sababu nne zinazosababisha watu kufanya makosa katika matumizi ya lugha.

    Date posted: November 20, 2019.  Answers (1)

  • Fafanua mambo manne yaliyochochea usanifishaji wa Kiswahili wakati wa ukoloni nchini.(Solved)

    Fafanua mambo manne yaliyochochea usanifishaji wa Kiswahili wakati wa ukoloni nchini.

    Date posted: November 20, 2019.  Answers (1)

  • Tambua aina za shamirisho katika sentensi ifuatayo. Gaidi aliyepigwa risasi alikuwa amebeba bunduki.(Solved)

    Tambua aina za shamirisho katika sentensi ifuatayo.

    Gaidi aliyepigwa risasi alikuwa amebeba bunduki.

    Date posted: November 20, 2019.  Answers (1)

  • Ni hisia zipi zinazodhihirika katika matumizi haya ya vihisishi. (i) Maskini! Alinyimwa msaada na serikali (ii) Wallahi! Nikikutana naye atajuta kwa nini kazaliwa.(Solved)

    Ni hisia zipi zinazodhihirika katika matumizi haya ya vihisishi.

    (i) Maskini! Alinyimwa msaada na serikali
    (ii) Wallahi! Nikikutana naye atajuta kwa nini kazaliwa.

    Date posted: November 20, 2019.  Answers (1)

  • Ondoa ‘o’ rejeshi bila kubadilisha maana. Kuimba kulikosifika siku nyingi sasa kunatia shaka(Solved)

    Ondoa ‘o’ rejeshi bila kubadilisha maana.

    Kuimba kulikosifika siku nyingi sasa kunatia shaka

    Date posted: November 20, 2019.  Answers (1)