Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.
Got a question or eager to learn? Discover limitless learning on WhatsApp now - Start Now!

Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali FADHILA ZA PUNDA Rita na Evelyn walikuwa marafiki wa chanda na pete kwa muda mrefu.

      

Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali
FADHILA ZA PUNDA
Rita na Evelyn walikuwa marafiki wa chanda na pete kwa muda mrefu. Waliishi katika mtaa wa Kibokoni
jijini Mombasa. Evelyn alikuwa mwanafunzi wa masomo ya uhazili katika chuo kimoja pale mjini. Naye
Rita alifanya kazi ya ukarani papo hapo mjini. Waliishi kidugu katika chumba kimoja walichopanga pale
mtaani. Ingawa marafiki hawa walishirikiana kwa kila njia katika shughuli za upishi, kupiga deki, kufagia,
kufua na kazi nyinginezo za nyumbani, aliyekuwa akitoa msaada mkubwa zaidi alikuwa ni Rita. Rita
alikuwa na mazoea ya kutunza pesa zake vyema. Aidha alijua maana ya haba na haba hujaza kibaba.
Alijua kuwa Evelyn, kama mwanafunzi, hakuwa na uwezo wa kuyakidhi baadhi ya mahitaji yake.
Alijitolea sabili hata kumnunulia Evelyn nguo, viatu na vim vingine alivyohitaji. Mara nyingine ilibidi Rita
kulipa kodi ya nyumba peke yake kwa vile mwenzake hangeweza kupata pesa kwa wakati. Hakuwahi
hata siku moja kumkera wala kumtesa Evelyn kwa jinsi yoyote ile. Fauka ya hayo, hakuwahi
kumsemesha vibaya wala kuonyesha dharau kwake. Aliamini kama wanavyosema watu kuwa dunia
rangi rangile, huenda siku moja atahitaji kusaidiwa yeye pia. Siku kama hiyo atamtegemea Evelyn,
mwandani wake. Evelyn alipomaliza masomo yake alikuwa na bahati ya mtende. Alipata kazi nzuri mara
moja katika kampuni moja ya maffita papo hapo jijini. Lakini muda si muda, mambo ya ajabu yalianza
kutokea. Baada ya kupata kazi yenye kipato kizuri, kichwa cha Evelyn kilianza kufura mfano wa kaimati.
Badala ya kunisaidia mwenzake katika kazi za pale nyumbani pamoja na gharama za maisha, alifhatilia
raha za jijini kwa kuamini ule msemo wa ponda raha kufa kwaja. Rita alipomwuliza alimjibu kwa ukali,
“Nikusaidie nini? Sasa si kama wakati nilipokuwa mwanafunzi. Kila mtu ana pesa zake.Ala!” Rita
hakumwelewa tena Evelyn.Isistoshe, alianza kumwibia Rita vitu vyake wakati alipokuwa hayupo
nyubani. Mara kwa mara Rita aligundua kuwa pesa alizokuwa ameficha sehemu Fulani nyumbani
zimedokolewa. Alipomwuliza, Evelyn alikujajuu, “Unafikiri mimi sina pesa? Unadhani ni wewe tu
uliyeajiriwa?” Rita alizidi kushangaa, Muda wote alioishi na kumfadhili rafiki yake aliamini kuwa atamlipa
mema. “Kumbe fadhila za punda ni mateke?” Alijiuliza Rita. Baada ya muda, urafiki wao ulivunjika na
Evelyn akahamia mtaa wa Furaha alikoendelea na maisha yake ya starehe na ureda. Hata hivyo mambo
yalianza kumwendea mrama Evelyn. Wakubwa wake kazini hawakupendezwa najinsi alivyoendesha
shughuli zake pale ofisini. Mara nyingi alifika kazini akiwa amechelewa na kila wakati alitoa vijisababu
mbalimbali ambavyo havikumridhisha yeyote. Aidha, alipokuwa ofisini hakufanya mengi isipokuwa
kutembea kutoka ofisi hii hadi nyingine akiwasumbua watu kazini mwao. Mara kwa mara alionekana
akisinzia wakati wenzake walipokuwa wakichapa kazi. Lakini lililowakera zaidi wakuu wa kampuni hiyo
ya mafuta ni jambo fulani lililoanza kutendeka pale. Vitu vya watu vilianza kupoteapotea.Mara
mfanyikazi huyu anapoteza saa yake, mara mwingine anapoteza pesa, mara hiki mara kile. Wakuu
walipoyatupa mawazo yao nyuma wakagundua kuwa mambo haya yalianza kutendeka mara tu
alipowasili Evelyn. Wakaamua kumwekea mtego. Evelyn alioshikwa kimasomaso akidokoa mkoba wa
msichana mwenzake. Mkoba huo ulikuwa umeaehwa juu ya dawati kimakusudi ili kumvuta Evelyn.
Evelyn alifutwa kazi papo hapo. Fauka ya hayo, alitiwa mikononi na kukabidhiwa poisi waliomtupa
korokoroni. Kesho yake Evelyn alifikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kosa la wizi. Alitozwa faini ya
shilingi elfu tano au kifungo cha miezi sita. Hakuwa na pesa zozote za kulipia faini hii. Akawekwa
rumande. Hata rafiki mmoja hakuwa naye wa kumuauni katika wakati huo wa majaribu. Kwa bahati, Rita
alisikia kuhusu kadhia hiyo.Hakupoteza muda. Akashika njia moja kwa moja hadi kituo cha polisi.
Mpango ukafanywa na akamlipia. Evelyn ile faini. Evelyn alipoachiliwa hum akashangaa. “Yaani
nimesamehewa ama nini?”Aliuliza.“La. Hujasamehewa.Faini uliyotozwa imelipwa na msichana yule.”
Evelyn akageuka na kumwona Rita. Alimtazama kwa muda bila kujua la kusema. Mwishowe alimsogea
kisha wakakaribiana polepole na kukumbatiana. Machozi yakaanza kumdondoka Evelyn, nde! Nde! Nde!
Akalia kilio cha uchungu na soni. Akamwomba Rita msamaha, “Nisamehe, sikujua nililokuwa
nikifanya.Nilidhani kuwa baada ya kupata kazi sitahitaji tena urafiki wako. Haya yaliyonipata
yamenifunza,” alisema kwa masikitiko. “Evelyn, kijengacho mtu ni uth na tabia,” alisema Rita.“Ni kweli
rafiki yangu” alitamka Evelyn, Sasa nimejitia kwenye shida.Hata kazi yangu nzuri nimeipoteza.Sina
mahali pa kuishi. Itabidi nirudi kijijini kwa baba na mama. Kwaheri rafiki yangu naasante kwa yote
uliyofanya.”“La! Hutaondoka”. Rita alimwambia lcwa dhati, “Tutakwenda nawe nyumbani mwangu
tukaishi pamoja kama zamani. Nitayagharamia mahitaji yako yote hadi utakapopata kazi”. Basi Rita na
Evelyn wakaungana tena na kuishi vizuri katika nyumba ile ile mtaani Kibokoni. Kweli akufaaye kwa dhiki
ndiye rafiki.

MASWALI:
1. Maisha ya Evelyn na Rita yalikuwaje kabla ya Evelyn kupata kazi?
2. Kutokana na jinsi Rita alivyomtunza Evelyn, unafikiri yeye alikuwa ni mtu wa ama gani?
3. Eleza baadhi ya mambo ambayo Rita alimtendea mwenzake.
4. Baada ya kupata kazi Evelyn alikuwa mtu mkarimu. Je, unakubali?Eleza ilivyokuwa.
5. Evelyn alipokuwa mwanafunzi hakuwa na tabia ya udokozi. Unafikiri ni kwa nini alianza tabia
hiyo baada ya kuajiriwa?
6. ‘Asiyefunzwa na mama hufunzwa na ulimwengu.’ Methali hii inahusianaje na Evelyn?
7. ‘Akufaaye ukiwa dhiki ndiye rafiki.’ Methali hii inahusianaje na Rita?
8. Eleza maana ya misemo ifuatayo kama ilivyotumika kwenye kifungu: (alama 3)
(a) marafiki wa chanda na pete
(b) enda mrama
(c) jitolea sabili

  

Answers


Kavungya
1. Maisha ya Evelyn na Rita yalikuwa aje kabla ya Evelyn kupata kazi?
i. Walikua marafiki wa chanda na pete
ii. ii. Walishirikiana kwa kila njia

2. Kutokana na jinsi Rita alivyomtunza Evelyn, unafikiri yeye alikuwa ni mtu wa namna gani?
i. Alikua mwenye ukarimu
ii. Alijawa na wema
iii. Alikua na mapenzi ya dhati

3. Eleza baadhi ya mambo ambayo Rita alimtendea mwenzake.
i. Alimnunulia mahitaji kama nguo na viatu
ii. Alilipa kodi kwa niaba ya Evelyn
iv. Alimlipia faini alipokua kizuizini

4. Baada ya kupata kazi Evelyn alikuwa mtu mkarimu. Je, unakubali?Eleza ilivyokuwa.
- La.
- Evelyn alifuatilia raha za jijini na kukosa kumsaidia Rita katika kazi na gharama za maisha

5.Evelyn alipokuwa mwanafunzi hakuwa na tabia ya udokozi. Unafikiri ni kwanini alianza tabia
hiyo baada ya kuajiriwa?
- Aliona kuwa alikuwa na pesa zake na angeweza kujikimu mwenyewe
- Alidhani kuwa tayari alikuwa mtu mzima na hivyo hakuhitaji kuelekezwa

6. ‘Asiyefunzwa na mama hufunzwa na ulimwengu.’ Methali hii inahusiana aje na Evelyn?
- Evelyn alikataakumskiza Rita nabaadayeakatendakosalililomtiakorokoroni

7. ‘Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki.’ Methali hii inahusiana aje na Rita?
- Rita alimsadia rafikiye Evelyn alipokuwa mwanafunzi na hata baadaye alipokuwa korokoroni

8. Eleza maana ya misemo ifuatayo kama ilivyotumika kwenye kifungu:
(a) marafiki wa chanda na pete- Marafiki wasioachana kwa vyovyote vile
(b) enda mrama -Kuharibika
(c) jitolea sabili –Kuamua kikamilifu
Kavungya answered the question on November 22, 2022 at 08:59


Next: Fill in the blanks with the most appropriate preposition i) The candidates are very good ............ languages. ii) Give us the details ............ your courses....
Previous: Eleza sifa za sauti zifuatazo: /e/ /p/

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions