Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

“Kutazamia shule za vijijini kumwibua bingwa katika mtihani wa kitaifa ni kama kutarajia kupata maziwa kutoka kwa kuku.” (Shibe Inatumaliza) a) Eleza muktadha wa dondoo hili. b)...

      

“Kutazamia shule za vijijini kumwibua bingwa katika mtihani wa kitaifa ni kama kutarajia kupata maziwa kutoka kwa kuku.” (Shibe Inatumaliza)
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Tambua mbinu moja ya lugha kutoka kwenye dondoo hili.
c) Eleza maudhui yafuatayo katika hadithi hii:
i) Mabadiliko
ii) Uozo
iii) Shaka

  

Answers


Francis
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
? Ni maneno ya Dennis
? Anajizungumzia
? Ni baada ya kuona tofauti ya kitabaka iliyopo baina ya wanafunzi chuoni Kivukoni.
? Anahisi uchungu moyoni anapowatazama wenzake na kuhisi laiti angeweza kusomea shule za kifahari na za hadhi ya juu.


b) Tambua mbinu moja ya lugha kutoka kwenye dondoo hili.
? Tashbihi- ni kama kutarajia maziwa kutoka kwa kuku


c) Eleza maudhui yafuatayo katika hadithi hii:
i) Mabadiliko
? Hata ingawa mwanzoni Penina alimrai Dennis wawe wapenzi, anapobadilisha mawazo yake anamwuliza ni penzi lao gani analouliza limekwenda wapi.
? Dennis anabadilisha msimamo wake wa kukosa kujirekibisha na uhusiano anapotembelewa na Penina. Mwanzoni alilenga kusoma aweze kupata ajira angalau awasaidie wazazi wake ambao ni maskini.
? Penina anamkomesha Dennis asimwite mpenzi wake tena na asije akamwambia mtu kuwa aliwahi kuwa mpenzi wake kinyume na walivyozoeana.
? Penina anamwuliza Dennis kuwa atakula chakula cha nani kwani hajachangia chochote hata senti moja kinyume na walivyozoea.

ii) Uozo
? Dkt. Mabonga anakejeli uozo wa wanafunzi kutofanya utafiti na wao ni kama binadamu waliogeuka kuwa kupe, kulaza damu usiku na mchana, kutegemea vya bure au rushwa au msaada kutoka kwa wafadhili.
? Daktari Mabonga anawatamkia wanafunzi maneno machungu kama shubiri wanapomwuliza maswali ya fasihi.
? Wachapishaji wa vitabu wanafumbia macho kazi za wasanii wanaoibuka zikiishia ‘kapuni”.
? Chuoni, wanafunzi wa kitajiri na wa kimaskini wanatengana kama ardhi na mbigu na kuzuia kusaidiana.
? Pennina anamfukuza Dennis chumbani akimlaumu kukosa kuchangia chakula baada ya kukosa kazi kinyume na awali walivyoishi.

iii) Shaka
? Dennis ana shaka iwapo ndiye au Pennina kupe wa kumtegemea mwenzake.
? Dennis ana shaka iwapo asimame au ageuke nyuma, asonge au aendelee kusimama baada ya kusikia sauti ya kike.
? Dennis ana shaka iwapo atafanikiwa kupata kazi - amekaa mbele ya wakurugenzi akisubiri uamuzi wao.
? Dennis ana shaka nani atawafisidi nguvu na jasho wazazi wake lililomwagika wakikusuru kumsomesha kwani anakosa kujieleza kwa maofisa ili apate ajira.
? Ana shaka na sababu za kicheko cha wanafunzi na minongono yao darasani.
? Shaka ya ufanifu wao na Pennina kutokana na toauti ya kitabaka inayowatia kiwewe mno wazazi.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 09:02


Next: Jadili jazanda za anwani katika hadithi zifuatazo. a) Shibe Inatumaliza b) Mtihani wa Maisha c) Mkubwa
Previous: Jadili suala la mikosi maishani ukirejelea hadithi zifuatazo: i) Nizikeni Papa Hapa ii) Ndoto ya Mashaka

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions