Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Jadili suala la mikosi maishani ukirejelea hadithi zifuatazo: i) Nizikeni Papa Hapa ii) Ndoto ya Mashaka

      

Jadili suala la mikosi maishani ukirejelea hadithi zifuatazo:
i) Nizikeni Papa Hapa
ii) Ndoto ya Mashaka

  

Answers


Francis
i) Nizikeni Papa Hapa
? Otii alivunjika mguu wake akichezea timu ya Bandari FC.
? Licha ya sifa kemkem alizoletea taifa lake alitelekezwa na maofisa wasimamizi wa timu hizi.
? Otii alipopata nafuu alikosa kazi bora ya kufanya akarejelea kazi yake duni katika Halmashauri ya bandari iliyokuwa na malipo duni.
? Mkosi wa kukutana na mpenzi mnafiki na kuambukizwa UKIMWI naye - Rehema Wanjiru.
? Marafiki wake walitayarisha mazishi yake akiwa hai huku akiwasikia.
? Hata baada ya kifo mkosi wa ajali ulimwandama – Mtito Andei.
? Otii aliugua maradhi yasiyo na tiba. Madaktari walimkataa hospitalini wakasema arejeshwe nyumbani.


ii) Ndoto ya Mashaka
? Mamake Mashaka alifariki tu baada ya kumzaa.
? Babake Mashaka naye alifariki muda mfupi tu baada ya mkewe kufa. Mashaka akawa yatima.
? Mamake mlezi naye Biti Kidebe daima alikuwa na maumivu ya mguu hivyo ilibidi waleane.
? Mashaka alikulia katika mazingira magumu ya kufanya kazi za kijungu jiko k.m kufua, kufyeka nk.
? Licha ya bidii yao kuna wakati walikosa ikamlazimu Kidebe atumie akiba aliyokuwa nayo.
? Mashaka alifungishwa ndoa ya mkeka na mzee Rubeya - hakuwa tayari.
? Mkosi wa kudharauliwa na wazazi wa Waridi kwa ajili ya umaskini - wanatorokea Yemeni kuondokea aibu ati.
? Walipooana Mashaka anasema ni kama ndoa yao iliingia nuksi moja kwa moja. Wanaendelea kuishi katika chumba kile kile kimoja na watoto wao kwani wasingeweza kuhamia chumba kingine. (fedha)
? Familia ya Mashaka iliishi katika mtaa usiokuwa na mpangilio. Chumba chao kilikuwa karibu na choo cha jirani kilichojaza uvundo kwao. Udhia ulizidi maradufu wakati wa mvua.
? Mkosi wa paa lao kuvuja nyakati za mvua.
? Mkosi wa kupata pacha mara tatu wakaishia kuwa na watoto wengi. Hawatoshelezi malazi hivyo anaombea wavulana mahali jikoni kwa jirani.
? Mshahara aliopewa na kampuni ya ZWS ulikuwa mdogo sana.
? Mkewe (Waridi) alimtoroka, akaenda na watoto wote bila taarifa.
? Ni mkosi kwamba mambo ya Mashaka yanatengenea ndotoni tu. Anapoamka anajipata katika mashaka yale yale na maisha yale duni tu.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 09:05


Next: “Kutazamia shule za vijijini kumwibua bingwa katika mtihani wa kitaifa ni kama kutarajia kupata maziwa kutoka kwa kuku.” (Shibe Inatumaliza) a) Eleza muktadha wa dondoo hili. b)...
Previous: “Hebu kwanza kanawe hilo dongo jekundu miguuni.” (Shibe Inatumaliza) (a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (b) Fafanua sifa za wandani wa msemaji. (c) Jadili jinsi hadithi hii inavyoafiki...

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions