Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Taja sifa nne za lakabu

      

Taja sifa nne za lakabu

  

Answers


KELVIN
a) Lakabu si jina la mtu ni jina tu la kupangwa.
b) Lakabu aghalau huwa neno au fugu la maneno lililo na maana iliyofumbwa.
c) Lakabu huoana na sifa za mhusika inaweza kusifu kukejeli au kufanyia tashtiti tabia hasi ya mhusika lakabu baba wa taifa moja kwa moja inaashiria sifa nzuri za mhusika na kumsifu kwa upande mwingine lakabu kama kangumu inaashiria tabia ya uchoyo.
d) Lakabu hupatikana katika tanzu na vipera vingine nya fasihi simulizi kama vile sifo, malumbano ya utani na majigambo (vivugo) ambapo wahusika hujipa majina ya kupanga ya kujitapa.
e) Lakabu huundwa kwa lugha ya picha au taswira na sitiari kwa mfano, lakabu ‘nyayo’ ya Raisi mstaafu inatumia sitiari inamfananisha na nyayo za mtu hivyo kutupa taswira ya kujipata kufuata falsafa ya mtu mwingine.
f) Ingawa lakabu si jina halisi la mtu, huweza kudumu na kufanya jina halisi la mtu kusahaulika kwa mfano Sonko.
kalvinspartan answered the question on October 24, 2017 at 14:29


Next: Taja asili nne za lakabu.
Previous: Misemo ina umuhimu upi katika jamii?

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions