Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

"Penzi lenu na nani? . . Mgomba changaraweni haupandwi ukamea. Potelea mbali mkate wee!" (a) Eleza muktadha wa dondoo hii...

      

. "Penzi lenu na nani? . . . . Mgomba changaraweni haupandwi ukamea. Potelea mbali mkate wee!"
a) Eleza muktadha wa dondoo hii. (alama 4)
b) Taja naufafanue mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili. (alama 4)
c) Onyesha vile maudhui ya utabaka yanavyo jitokeza katika hadithi nzima. (alama 6)
d) Eleza sifa sita za mzugumzaji kwenye dondoo. (alama 6)

  

Answers


ESTHER
a)1. Mzungumzaji ni Penina.
2. Anamzungumzia Dennis Machora
(msimulizi)
3. Wako nyumbani kwao (Machora na Penina)
katika mtaa wa New. Zealand.
4. Dennis Machora alikuwa amerudi nyumbani
kutoka kampuni ya kuchapisha magazeti
alikoenda kutafuta kazi lakini akaambulia
patupu. (Alama 4)
b)1 Methali - Mgomba Changaraweni haupandwi
ukamea
2. Swali balagha - penzi lenu na nani?
3. Nidaa . . . Mkata wee!
4. Msemo - potelea mbali.
5. Mdokezo (.....)
zozote mbili 2 x 2 (Alama 4)

c) Maudhui ya Utabaka.
1. Wazazi wa Dennis walijitahidi kumsomesha
kwa kuwalimia matajiri mashamba.
2. Wazazi wa Penina walipinga uhusiano wa
Dennis na Penina kwa kuwa laitoka tabaka la
chini ilhali wao walikuwa matajiri.
3. Dennis anakunywa uji kama chamcha kwa
kukosa chakula ilhali Penina hupokea
shilingi elfu tano kila wiki.
4. Dennis hangejiunga na shule aliyoalikwa
kwa umaskni ilhali wenzake walisomea
shule za hadhi kubwa.
5. Penina anapangiwa nyumba katika mtaa wa
New Zedand. wanakoishi watu wenye
mapato ya Kadri.
6. Penina anamkataa Dennis kwa kuwa hana
uwezo wa kifedha kwa kukosa kazi na
hangeweza kudumisha maisha yake ya
kifahari.
7. Wazazi wa Dennis walimtegemea asome ili
kuwatoa umaskinini ilhali wazazi wa Penina
wanamkimu hata baada ya kumaliza
masomo. zozote 6 × 1
d) Sifa za mzungumzaji.
1. Msaliti - Alimsaliti mchumba wake Dennis
kwa kumfukuza na kuwaibisha sababu ya
umaskini.
2. Mwenye dharau - alimfokea Dennis kwa
dharau akimwita mkata.
3. Mwenye tamaa - ana tamaa ya mapenzi na
akatafuta mchumba kwa bidii.
4. Mwenye bidii masomoni - alikuwa
mwanafunzi wa chuo kikuu cha kivukoni.
5. Ni jasiri - alimwendea Dennis kutafata
mapenzi na uchumba na mambo
yanapokwenda kombo anamfukuza bila
woga.
6. Mpyaro - alimtusi Dennis akimwita mkata
6 × 1 = 6

ESTHER STEVE answered the question on November 12, 2018 at 09:52


Next: "Mapenzi ya Kifaurongo",Kenna Wasike Mapenzi ya Kifaurongo" Mimi sijui hata kidogo ,huwa nayaona mapenzi kama ule mmea wa Kifaurongo.Huwa hai hali ikiwa shwari,na shari ikitokea ...
Previous: In details describe the sets of capabilities of handling Geo-referenced data in Geographic information system.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions