Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Nairobi , mji mkuu wa Kenya, ni jiji la maajabu na mastaajabu chungu nzima. Nadhari ya mtu anayewahi kuingia jiji hili...

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
Nairobi , mji mkuu wa Kenya, ni jiji la maajabu na mastaajabu chungu nzima. Nadhari
ya mtu anayewahi kuingia jiji hili kwa mara ya kwanza huvutiwa na huo msheheneko wa
majumba ya fahari, marefu ajabu, kiasi cha minazi mitano- sita iliyounganishwa
kuelekea juu mbinguni.

Jumba linalowavutia watu wengi ni lile la makongamano ya kimataifa liitwalo kwa
kiingereza Kenyatta International Conference Centre. Jumba hili, hadi miaka michache
ilipopita, ndilo lililokuwa refu zaidi mjini. Jumba lenyewe lina ghorofa ishirini na tisa
hivi, Usipohesabu hilo pambo kama kofia kileleni mwake, linalojulikana kama
mwavuli. Hata hivyo, miaka michache iliyopita jingo hili lilipitwa kwa urefu na mnara
wa Nyakati ( Times Tower) Mnara huo hasa ni jumba linaloafiki lakabu yake ya
kikwaruza mawingu. Jumba hili lina ghorofa zisizopungua thelathini na mbili.

Mbali na majumba haya mawili, kuna majumba mengine zaidi ya ishirini katikati ya jiji
ambayo, japo mengine ni mafupi kiasi, maumbo ya kustaajabisha kweli kweli. Hebu
zingatia mwenyewe jumba liitwalo “mdomo wa kengele” au bell - bottom” ambalo ni
vioo vitupu, toka chini hadi juu. Fauka ya haya, umbo lake ni la kipekee ulimwenguni
kote. Jumba hili lina kama miguu, kisha kiuno mithili ya kinu hivi japo si mviringo.
Linapaa juu, mbali sana, likichukua umbo pana kuliko lilivyo chini. Umbo la fua pana
kama kengele.

Halafu rudia barabara. Hizi hazina hesabu katikati ya jiji ni pona, tena safi sana. Magari
yanayotumia barabara hizi ni kochokocho, ya kila aina na yanashindania nafasi.

Ajabu kubwa ya Nairobi hata hivyo ni idadi ya watu. Hakuna hasa anayejua idadi kamili
ya watu wa Nairobi, lakini sio kupiga chuku ninaposema kwamba, hasa nyakati za
kuelekea kazini asubuhi, kwenda kula chakula cha mchana, kuelekea nyumbani baada
ya kazi na kuvuka barabara wakati wa msongamano, watu hukanyagana. Mtu anayesema
kwamba watu wa Nairobi ni wengi kama chungu, au kama mchanga wa ufuo wa bahari,
hatii chumvi

Watu wa Nairobi, kwa tabia na mavazi, si kama watu wa kwingineko nchini Kenya.
Watu hawa kuvalia nadhifu sana. Wanawake ni warembo ajabu na hutengeneza nywele
zao mithili ya hurulaini peponi. Wengi huvaa suruali ndefu! Kucha zao na midomo yao
hupata rangi maridadi sana. Huzungumza Kiswahili na kiingereza takriban wakati wote.
Wanawake wengi ajabu huendesha magari yao wenyewe, jambo ambalo litakushangaza
mara tu uingiapo jijini, hasa kama ulilelewa ukidhani maskani mwafaka ya wanawake ni
jikoni peke yake, yaani kuzingatia ile falsafa kuwa “ kuoa ni kupata jiko”. Wanaume
nao huvaa suti safi, maridadi na shingoni wamefunga tai stahiki yao. Wanaume hao huendesha magari ya kuyaegesha karibu na afisi zao. Huingia afisini mwao kwa maringo
na madaha, huku funguo za magari yao zikining’inia vidoleni. Hawa nao husema
Kiswahili na kiingereza kupitia puani, utadhani ni waingereza hasa.

Kwa upande mwingine, watoto ni nadhifu kweli hasa watoto wa shule. Hawa huvalia sare
zilizofuliwa na kunyoshwa vizuri kwa pasi. Wake kwa waume, shingoni huvalia tai.
Watoto wa shule Nairobi huongea Kiswahili, kiingereza na Sheng, ambayo ni “lahja” yao
waliyoibuni.
“Lugha” hii ni mchanganyiko wa Kiswahili. Kiingereza na msamiati mchache wa lugha
nyingine za wakenya zisemwazo jijini Nairobi na vitongoji vyake.

Kwa jumla, watu wote wa Nairobi hutembea kasi sana. Hawana hata wakati wa kutembea
pole pole na kuangazaanga huku na huko. Iwapo wewe ni mgeni jijini, ukizubaa
utapigwa kumbo na waendelee na hamsini zao kama vile hapakutokea jambo. Hili
linapojiri, usidhani limefanywa maksudi. La, hasha ni vile tu kwamba Wanairobi hawana
muda wa kupoteza.

(a) Kwa nini majumba ya jiji la Nairobi yana majina au lakabu za kiingereza?
(b) (i) Baadhi ya maajabu ya Nairobi ni barabara safi, msongamano wa magari
na majumba marefu. Ongezea maajabu mengine manne
(ii) Watu wa Nairobi wanajipenda kweli kweli. Fafanua
(c) (i) Je, unadhani watu wa Nairobi kweli hukanyagana? Eleza ni kwa nini
msimulizi ametoa maelezo hayo
(ii) Unafikiri ni kwa nini hasa wanawake wa Nairobi wanaonekana nadhifu?
(d) Kwa nini neno “lahja” limewekwa alama za mtajo?
(e) Eleza maana ya maneno na tamathali za usemi zifuatazo:
(i) Nadhari
(ii) Linaloafiki
(iii) Kikwaruza mawingu
(iv) Waendelee na hamsini zao

Answers


Kavungya
a) - Kiingereza ni lugha ya kimataif
- Kiingereza ni lugha rasmi nchini
- Kiingereza ni mojawapo ya lugha zitumiwazo Nairobi
- Ni athari ya waingereza walioitawala nchi hii

b) i) - Idadi ya watu ni kubwa/watu ni wengi
- Watu huvalia nadhifu/wanawake ni warembo/wanawake
huvaa suraali ndefu /wanawake hutengeza nywele
zao/wanawake hupaka rangi kucha zao na midomo yao
Watu huzungumza Kiswahili na Kiingereza karibu kila
wakati. Wanawake wengi hendesha magari yao wenyewe
- Majumba mengine yana maumbo ya kipekee
- Barabara ni nyingi na pana
- Kuna magari mengi ya kila aina
- Wanaume husema Kiswahili na Kiingereza kupitia puani
- Wanaume hutembea kwa maringo wakining’iniza funguo
za magari mikononi
- Watoto wa shule husema Kiswahili, Kiingereza na sheng’
- Watu wa Nairobi hutembea Kwa kasi sana bila simile
ii) - Watu huvalia nadhaifu
- Huzungumza Kiswahili na Kiingereza karibu kila wakati
- Wanawake wengi huendesha magari yao
- Wanaume husema Kiswahili na Kiingerexa kupitia puani
- Watu hutembea kwa kasi sana bila simile
- Watoto huzungumza Kiswahili, Kiingereza na sheng’

c) i) - Ndio kwa sababu watu wa Nairobi ni wengi sana
- La. Anapiga chukukuonyesha wingi wa watu wa Nairobi
ii) Ili wapendeze
- Kazi wafanyazo haziwachafui
- Wanajiweza kifedha
- Ili waafiki heshima zao.

d) - Limetumika nje ya muktadha/sheng si lahaja

e) i) Fikira/fikra/mawazo/mtazamo
ii) Linalofaa/linalolingana na/linalopatana
na/linaloakisi/linalostahiki/linlosadifu
iii) Jumba refu
iv) Waendelee na shughuli/kazi/plikapilka/harakati zao
Kavungya answered the question on June 28, 2019 at 05:34

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions