Trusted since 2008
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Alipokuwa akiukemea utamaduni na dhana za kikabila katika nyimbo zake, marehemu Bob Marley aliufananisha ubepari na "wanyama wala watu."

Soma taarifa hii kisha ujibu maswali yanayofuata.

Alipokuwa akiukemea utamaduni na dhana za kikabila katika nyimbo zake, marehemu Bob Marley aliufananisha ubepari na "wanyama wala watu." Katika wimbo "Babylon System" (yaani mfumo wa kibepari), Marley alisema kuwa utamaduni huo ndio mzawa wa matatizo yote ya kiutawala ambayo yalikuwa yakiyakumba mataifa ya Weusi katika karne ya 20, wakati nchi zao zilikuwa zikitawaliwa na nchi za mataifa ya Ulaya.
Kwa mantiki hiyo, pengine Marley alikuwa na maono kuwa Afrika haingejikomboa kutoka kwa utumwa wa Kizungu, ikiwa ingeendelea kuziabudu na kuzishadidia tamaduni za Kimagharibi.
Utabiri huo nauoanisha na yanayoendelea nchini, ambapo serikali ya Jubilee imeonekana kushindwa kabisa kuikabili saratani ya ufisadi, ambayo inahatarisha kuliangamiza taifa hili lenye uchumi dhalili.
Donda hili linazidi kuyatandaza mabawa yake kutoka, tisho kuu likiwa ni uvamizi wa taasisi ―takatifu‖ ambazo tunazitegemea kulikabili donda hilo.
Ni nani tutategemea kukabiliana na rushwa ikiwa taasisi kama Bunge, Tume ya Maadili na Kukabiliana na Ufisadi (EACC) kati ya zingine muhimu zimepakwa tope na saratani hiyo?
Kimsingi yote tunayopitia ni matunda ya uasi wa tamaduni za Kiafrika na uegemezi wa mifumo ya Kizungu kama mihimili ya jamii na nchi zetu.
Ndoto za watetezi wa Uafrika na nafasi ya Weusi kama marehemu Malcom X na Martin Luther King, zilikuwa ni kuona kuwa wameungana kabisa kukabiliana na matatizo yaliyowakabili bila kuzingatia mazingara waliyokuwemo.
Pindi tu baada ya mataifa mengi ya Kiafrika kujinyakulia uhuru wao katika miaka ya hamsini na sitini, viongozi wakuu walioziongoza nchi hizo kama Kwame Nkrumah, Jomo Kenyatta, Mwalimu Julius Kibarage Nyerere kati ya wengine walianza harakati za kuliunganisha bara hili na kubuni Muungano wa Nchi za Kiafrika (OAU) japo ndoto hiyo haikufikia.
Kwa msingi huo, mhimili mkuu wa kiutawala ungekuwa ni mfumo wa kisosholisti, ambao ungekuwa nguzo kuu ya kuyaunganisha mataifa hayo.
Hata hivyo, migawanyiko mikubwa ilianza kushuhudiwa, huku baadhi ya mataifa yakianza kukabiliwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe. Huo ndio ulikuwa mwanzo wa kutaasisika kwa maovu yote tunayoshuhudia sasa: ufisadi na tamaa ya kuogofya kutoka kwa viongozi wetu.

Maswali
a. Ipe taarifa hii anwani mwafaka.
b. Onyesha mambo mawili makuu ambayo msanii aliyapinga .
c. Kwa nini ubepari umelinganishwa na "wanyama wala watu"?
d. Kwa mujibu wa taarifa eleza sifa za Bob Marley.
e. Swala linalozungumziwa limerejelewa kama "Donda".
i) Eleza mbinu ya lugha iliyotumika..
ii) Ni kweli kuwa donda hili laelekea kuwa gumu? Thibitisha.
f. Tatizo hili la "donda" ni kama kujipalia makaa. Fafanua.
g. Eleza maana ya maneno yafuatayo kwa mujibu wa taarifa.
i) Mhimili
ii). Taasisi

Answers


sharon
a) Ufisadi
b) i) Utamaduni
ii) Dhana za kikabila
c) Ndiyo mzawa wa matatizo yote ya kiutawala.
d) i) Mwenye maono
ii) Mtetezi
e) i) Jazanda – ufisadi kurejelewa kuwa donda.
ii) Donda linatandaza mbawa zake kwenye 'taasisi takatifu' zinazopaswa kuupinga ufisadi.
f) Uasi wa tamaduni za kiafrika
Kuegemea mifumo ya kizungu
g) i) Mhimili - nguzo / tegemeo / iliyoimara
ii) Taasisi – kituo maalum cha kustawisha / kutoa mafunzo.
sharon kalunda answered the question on October 2, 2019 at 09:51

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions