Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Soma shairi hili kasha ujibu maswali yanayofuata.

      

Soma shairi hili kasha ujibu maswali yanayofuata.

SABUNI YA ROHO
Ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia?
Ndiwe suluhu la zama, waja wa kukimbilia,
Waja wana kutazama, madeni wakalipia,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

Ndiwe mafuta ya roho, walisema wa zamani,
Utanunua majoho, majumba na nyumbani
Umezitakasa roho, umekuwa mhisani,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Matajiri wakujua, wema wako wameonja,

Nguo zao umefua, wakupata kwa ujanja,
Sura zao mefufua,wanazuru kila Nyanja,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

Ndiwe mvunja mlima, onana na maskini,
Watazame mayatima, kwao kumekua wa duni,
Wabebe waliokwama, wainue waliochini,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

Ndiwe mvunja mlima, wapi kupata uwezo?
Umezua uhasama, waja kupata mizozo
Ndiwe chanzo cha zahama, umewaitia vikwamizo,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

Umevunja usuhuba, familia zazozana,
Walokuwama habuba, kila mara wagombana,
Roho zao umekaba, majumbani wa chinjana,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

Nakutafuta kwa hamu, sabuni unirehemu,
Sinilipue ja bomu, sije kawa marehemu,

Niondoe jehanamu, ya ufukara wa sumu,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

Naondoka wangu moyo, nikuitapo itika,
Fulusi wacha uchoyo, tatua yalonifika,
Nichekeshe kibogoyo, name nipate kuwika,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima

Maswali

a) Mshairi anaongea na nani katika shairi hili?
.
b) Taja majina mengine matatu aliyopewa huyu anayesemeshwa

c) Anayezungumziwa katika shairi hili anasababisha balaa gani?

d) Mshairi anatoa mwito gani kwa mwenziwe?

e) Fafanua maudhui ya ubeti wa sita.

f) Mbinu kadha za uandishi zimetumiwa na msanii kuwasilisha ujumbe wake. Taja mbinu zozote tatu na uzitolee mifano katika shairi.

g) Fafanua maana ya : sura zao ’mefufua, wanazuru kila nyanja’

h) Andika ubeti wa saba katika lugha nathari.

  

Answers


Martin
a)Pesa

b)Sabuni ya royo
- Mvunja milima
- Mafuta ya roho
- Fulusi
- Tu ya ntima
- Suluhu la zama

c)-Amesababisha uhasama/uadui
- Ugomvi kati ya wapanzi
- vifo

d)
-Awaarike maskini na mayatima.
- Asimwangamize bali bali amwandoe ufukara
- Amwitapo uchoyo/amtatulie shida zake
- Amechekeshe/ amfurahishe

e)Pesa zimezua uhasama katika ndoa nyingi na kusababisha vifo

f)
- Semi –mvunja mlima
-sabuni ya roho
- Tashhisi- umevuna usuhubai
-Umezua uhasama
- Balagha- kwa nini wanikimbia?
-Wapi kapata uwezo?
- Takriri- ndiwe mvunja mlima

g)Pesa zimewaletea furaha hata wanatalii sehemu zozote wanazotaka

h)Mshairi anasema kuwa anamtafuta pesa sana ili amsaidie. Anamsihi asimpige kwa kumtoroka na kumwacha hoi bila uwezo. Anamwomba amuondoe katika lindi hili la umaskini kwa vile yeye ndiye anayetuliza watu na kuwaondolea matatizo ya kila namna
marto answered the question on October 2, 2019 at 11:44


Next: "Hizi kurani zako ndizo zifanyazo nisije huku …"
Previous: Explain four factors that are frustrating the fight against drug abuse in Kenya today.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • Lugha inaweza kuelezwa kwa jumla kuwa ni mfumo wa mawasiliano.(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
    Lugha inaweza kuelezwa kwa jumla kuwa ni mfumo wa mawasiliano.Haiyamkiniki kwa mtu yeyote kueleza chanzo au kiini cha lugha na sote tunakubalina kuwa matumizi yake yameanza tangu kuumbwa kwa binadamu kwani ni vigumu kukisia kuwepo kwa jamii ya watu bila lugha ya mawasiliano yoyote ile.
    Katika taifa lolote,huwapo na lugha moja au hata zaidi ya moja ambayo huwa ndicho chombo zatika cha mawasiliano ya taifa katika nyanja za:elimu maandishi,siasa na biashara.Kwa mfano mataifa ya Kanada hutumia lugha mbili kwa usawa kama lugha za taifa na za kikazi.Maana ya lugha ya taifa ni lugha moja ambayo huteuliwa kutumika katika shughuli zote za taifa hasa katika nchi yenye lugha nyingi za kikabila.Lugha ya taifa ni muhimu sana kwa maisha na maendeleo ya taifa lolote lile.Lugha hii huwa ndiyo kiungo cha kueneza umoja na uelewano miongoni mwa jamii nyingi tofauti na huwa kama kitambulisho kwao kwa kuwa wao ni ndugu wa jamii moja kubwa,yaani taifa lao.
    Kenya ni mfano mzuri wa taifa lenye lugha nyingi zinazozidi 40 za vikundi vidogo vidogo vya kikabila.Hapo kabla ya miaka mia moja hivi iliyopita kila kimojawapo cha vikundi hivi kilijitambulisha kama kabila huru.Baada ya kuja kwa serikali ya kikoloni na hasa baada ya Kenya kujinyakulia uhuru,haja ya kuunganisha raia wote chini ya taifa moja lenye uongozi na shabaha moja ilikuwa ndilo jambo lililozingatiwa sana.Kwa hivyo utamaduni wa taifa Kenya ni mchanganyiko wa tamaduni za watu wengi wenye mila,desturi,imani na itikadi tofauti.Utamaduni humaanisha jumla ya amali na tabia za watu wa jamii fulani.Amali hizi zinafungamanisha fikira,ustaarabu,mila,taasisi na sanaa za aina zote za jamii inayohusika.
    Ili kujieneza na kujiimarisha,taifa huhitaji chombo hicho kuwasiliana na kuwaunganisha watu wake wenye asili mbalimbali. Chombo hicho huwa ni lugha ambayo siyo tu kwamba ni sehemu ya utamaduni wa jamii bali pia ni njia muhimu sana ya kutawanyia na kustawishia ule utamaduni.
    Katika taifa lenye lugha nyingi kama Kenya kwa mfano,lugha ya taifa inayozungumzwa na kueleweka na baadhi kubwa ya raia ambayo imekiuka mipaka na tofauti za kikabila ni njia muhimu sana ya kueneza maongozi ya taifa na kuleta ufahamikiano bora kote nchini.Kama
    zilivyo taasisi kama wimbo wa taifa,bendera ya taifa au bunge la taifa, lugha ya taifa ndicho kielelezo cha taifa lolote lile.Lugha kama hiyo huvunja na hukomesha hisia za kibinafsi na kikabila na badala yake kuunda moyo wa uaminifu wa kitaifa.
    Zaidi ya kuwa chombo cha mawasiliano,lugha ni kielelezo cha fikira na hisia za binadamu.Lugha ya watu fulani haituelezi tu ujuzi au maarifa yao bali pia mtazamo wao kimaisha,falsafa na mawazo yao.Kwa ufupi lugha hutufahamisha namna akili za watu waizungumzayo ile lugha zinavyofikiri na kufanya maazimio.Lugha ni sehemu ya utamaduni wa taifa tulimozaliwa na lazima lugha hiyo ifunzwe katika muktadha wa maisha ya jamii ihusikayo.Utamaduni wa jamii havitenganiki na lugha yake.

    Maswali
    (a) Huku ukirejelea kifungu, eleza fasiri na chanzo cha lugha.
    (b) Tofautisha baina ya lugha ya taifa na lugha ya kikazi.
    (c) Kwa nini lugha ya taifa huhitajika sana katika nchi kama Kenya.
    (d) Eleza kazi nne kuu zinazotekelezwa na lugha ya taifa.
    (e) Eleza maana ya mafungu yafuatayo kama yalivyotumiwa katika taarifa:
    (i) Amali na tabia za watu:
    (ii) Muktadha wa maisha ya jamii:
    (iii) Haiyamkiniki:
    (f)Eleza majukumu mawili ya lugha kwa ujumla

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Taja madhumuni ya kusanifisha lugha ya Kiswahili nchini(Solved)

    Taja madhumuni ya kusanifisha lugha ya Kiswahili nchini

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Changanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha jedwali(Solved)

    Changanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha jedwali

    Mwanafunzi aliyeondoka jana alishindwa kumwona

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Kanusha Akimaliza kucheza mwite(Solved)

    Kanusha
    Akimaliza kucheza mwite

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Bainisha matumizi ya viambishi vilivyopigiwa mistari katika sentensi(Solved)

    Bainisha matumizi ya viambishi vilivyopigiwa mistari katika sentensi

    i)Yego ana ujuzi mwingi
    ii) Yule mfanyibiashara aliyejidanganya amepata hasara

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi sahihi kuonyesha wakati uliopo usiodhihirika(Solved)

    Tunga sentensi sahihi kuonyesha wakati uliopo usiodhihirika

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Akifisha sentensi: lo unaweza kuubeba mzigo huo pekeyo mzee alishangaa(Solved)

    Akifisha sentensi:
    lo unaweza kuubeba mzigo huo pekeyo mzee alishangaa

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli kwenye mabano(Solved)

    Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli kwenye mabano

    1. Oa (kufanyiza)
    2. -la- (kufanyana )
    3. Dhuru (fanyika)

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Andika upya sentensi zifuatazo kwa kutumia jina jingine lililo na maana sawa na lililopigiwa mstari(Solved)

    Andika upya sentensi zifuatazo kwa kutumia jina jingine lililo na maana sawa na lililopigiwa mstari

    i. Ni nadra sana kumpata msichana asiyetoga masikio siku hizi

    ii. Zahama ilizuka wafanyikazi walipogoma

    iii. Lengo la kila mwanafunzi ni kupasi mtihani

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Tumia neno vizuri kama:(Solved)

    Tumia neno vizuri kama:
    i) Kielezi

    ii)Kiwakilishi

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Weka shadda kwa neno WALAKINI ili kuonyesha maana mbili(Solved)

    Weka shadda kwa neno WALAKINI ili kuonyesha maana mbili

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Tumia ‘po’ kutunga sentensi ya kuleta dhana ya wakati maalum(Solved)

    Tumia ‘po’ kutunga sentensi ya kuleta dhana ya wakati maalum

    i) Wakati maalum
    ii) Wakati usiodhihirika

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi yenye maneno N + V + E + E + T + N(Solved)

    Tunga sentensi yenye maneno N + V + E + E + T + N

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Toa mifano miwili ya aina za nomino zifuatazo(Solved)

    Toa mifano miwili ya aina za nomino zifuatazo
    i)nomino mseto
    ii) nomino za wingi
    iii) nomino za fikra

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Tumia kivumishi cha a- unganifu pamoja na nomino katika ngeli ya I-I kutunga sentensi(Solved)

    Tumia kivumishi cha a- unganifu pamoja na nomino katika ngeli ya I-I kutunga sentensi

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Andika sentensi ifuatayo katika usemi wa taarifa.(Solved)

    Andika sentensi ifuatayo katika usemi wa taarifa.
    “Mimi nitawakaribisha wageni leo jioni. Kisha nitaondoka kwenda kwangu kesho.” Fatuma alimwambia juma.

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Ainisha viambishi katika neno HAKUJULIKANA(Solved)

    Ainisha viambishi katika neno HAKUJULIKANA

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana ya kiambishi(Solved)

    Eleza maana ya kiambishi

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Sisi vijana wa Kenya inatupasa tuwajibike kufanya kazi kwa bidii, na kwa dhati ya mioyo yetu tuweze kupata ufanisi, na uwezekano wa kuinua nchi yetu...(Solved)

    Sisi vijana wa Kenya inatupasa tuwajibike kufanya kazi kwa bidii, na kwa dhati ya mioyo yetu tuweze kupata ufanisi, na uwezekano wa kuinua nchi yetu changa katika kiwango cha juu. Tukumbuke, “Ajizi ni nyumba ya njaa” Kwa hivyo basi haifai kulaza damu ikiwa matatizo nchini mwetu yametuzonga. Lazima tufanye kazi kwa busara, adabu njema na jitihada kwa moyo mmoja. Sharti tutilie maanani zaidi elimu ya vijana na watu wazima,kilimo,uchumi na amani katika nchi yetu vigumu sana kuweza kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo. Tupende tusipende lazima tizidishe mazao kilimo, uchumi na amani katika nchi yetu. Tunahitaji taifa lenye watu walioelimika, kwani bila elimu itakuwa vigumu sana kuweza kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo. Tupende tusipende lazima tuzidishe mazao mashambani kwani kila kukicha idadi ya watu inaongezeka, Ni sharti tuweze kujitosheleza katika vyakula. Zaidi ya haya pia lazima tujishughulishe na biashara ambapo kwa sasa ni Wakenya wachache sana ambao wanatambua umuhimu wa biashara. Wengi ni wale wenye mawazo ya kwamba, lazima kila mmoja aajiriwe maishani. Yatupasa tujitahidi kuleta uchumi katika mikono ya wananchi wa Kenya badala ya kuwaachia wengine ambao hawahusiki.

    Mafunzo tunayopata majumbani, shuleni na hata katika jamii, lazima yatuwezeshe kutambua mbinu za kupitia. Tunahitaji elimu tambuzi ambayo itamfanya Mwanakena kujua wajibu wake katika jamii. Tumesinywa na elimu pumbao; inayotupumbaza na kutufanya tusione mbele. Sisi vijana tukiwa viongozi wa ‘utengano ni uvundo’, lugha ya taifa ndicho chombo cha pekee ambacho kinatuunganisha na kuweza kutuwasilishia mapendekeza, mawaidha ni hisia zetu. Kukosa ndiko binadamu, wakati tunapokosea, lazima tukubali tumekosea na kufanya masahihisho mara moja. “Kwani usipoziba ufa, utajenga ukuta”. Tusikasirike kwa sababu tumesahihishwa makosa yetu tukiwa wazalendo halisi.

    Sisi tukiwa vijana sharti tujishughukishe na kuyaangalia matatizo ya nchi, pia kutafuta njia za kutatua matatizo hayo. Siku zote tutekeleze nidhamu.Ni jambo la kusikitisha kwamba sisi vijana twashutumiwa mara kwa mara kwa kutokuwa na nidhamu shuileni na majumbani mwetu.Utamaduni wa assili unanakariri sana kuwa tuwe na nidhamu shuleni na majumbani mwetu.Ili watu waweze kuishi maisha bora na kuwa na maendeleo,amani na upendo lazima tuwe na bidii,ushirikiano mwema na kuchagua viongozi wenye mioyo ya maendeleo.Tukiwa viongozi ambao hawajishughulishi na maendeleo,basi tutabaki nyuma kama mkia kila siku zote.Bahati mbaya ni kwamba wananchi wengi siku hizi huchagua viongozi wao kwa kufuata ukoo ama kama kwa utajiri wake.Kwa hivyo basi tuchagueni viongozi ambao watatuletea ufanisi badala ya viongozi wanaotokana na sababu kubwa au ya utajiri.


    a) Ni nini dhamira ya mwandishi?
    b) Katika aya ya kwanza, mwandishi anawahimiza vijana kufanya nini ili kuleta maendeleo nchini?
    c) Ni mambo gani yaliyochangia, kuzorota kwa maendeleo nchini Kenya kwa mujibu wa taarifa?

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Siku ya kuzungumza gharama za serikali katika bunge hungojewa kwa pashau kubwa.(Solved)

    Siku ya kuzungumza gharama za serikali katika bunge hungojewa kwa pashau kubwa. Maana kwa hakika siku hiyo ndiyo inayomuathiri kila mtu kwani ndipo serikali inapomchakuria mifuko na vibindo vyake. Wiki nzima kabla ya hapo huwa Waziri wa Hazina na Maendeleo ya Uchumi amekwisha onyesha kiasi kadha wa kadha kitahitajiwa katika mwaka kuikuza elimu ya wananchi – kwa idadi ya skuli zilioko mpaka sasa, vifaa na ala zihitajiwazo, waalimu watakiwao, shule gani mpya za aina gani zataka kujengwa na zitagharimu Serikali kiasi gani, na kadhalika. Wizara ya Afya itahitajia milioni kadha wa kadha kuongeza mavuno ya konde na mazao ya nyanyangu. Basi hivyo Waziri anaendelea kudondoa makisio ya kila wizara kinaganaga na viwango vya fedha zinazodhamiriwa kutumiwa kutosheleza kila kinacholazimu.

    Basi juma hilo lote huwa wafanyibiashara wanavuna kwa wanunuzi; namna biashara inayokwenda ni ajabu maana wanunuzi huwa wananunua kila kitu ambacho wanachelea kitabandikwa ushuru. Wafanyi biashara ndio wanaowatia hofu kuwa bidhaa zitapanda bei.Wachuuzi wa magari huwa wanatangaza kuwa wamepata fununu ‘mwaka huu ushuru wa magari utapandishwa mpaka thalathini katika mia. Basi patilizeni kabla siku hiyo maana baada ya hapo bei itakuwa haishikiki.’

    Wauzaji mapombe nao huwa na vishindo vyao: “Kodi ya forodha ya kila aina ya mvinyo itokayo ugenini itaongezwa ishirini kila mia, na pombe za kienyeji zitapandishwa peni kila chupa.’ Sigara nazo pia zaambiwa zitapanda: Fulani amedokezwa kuwa kila pakiti itazidishwa bei kwa mapeni mawili.

    Mradi, mlolongo wa bidhaa hupandishwa ushuru mkubwa kabla ya siku yenyewe haijafika.Basi angalia kufundika huko! Kande za vyakula na vifaa aina aina hununuliwa vikawekwa kwa kuchelea kuwa vitaongezwa bei au pengine vitakuwa adimu. Wafanyi biashara nao huwa wamekwisha ‘piga pua’ kuwa vitu fulani vitaekewa ushuru. Basi huvinunua kwa wingi wakavitutiza maghalani mwao kwa bei ya tahafifu kabla ya kuongezwa ushuru na baada ya kupandishwa kodi, huviuza kwa bei mpya.

    Ikifikia hiyo siku kila mtu mwenye hamu ya mambo ya kilimwengu huwa amechachawa kukimbilia penye redio kusikiliza hotuba ya waziri wa Fedha.Ikishamalizika huwa kila mtu akishusha pumzi,maana huwa mbichi na mbivu ishajulikana na kwa upande wake anaona hakuelemewa sana.


    a) Toa anwani mwafaka kwa taarifa uliyoisoma
    b) Taja wizara ambazo zimetajwa kwenye taarifa
    c) Ni mambo gani huzingatiwa katika makisio ya masomo
    d) Unadhani ni sababu zipi zichangiazo mavuno ya wafanya biashara kabla ya kusomwa makadirio ya fedha
    e) Wafanyi biashara hutumia mbinu gani ili kujipa faida zaidi
    f) Kuvumbika bidhaa maghalani si ufanyaji biashara halali. Toa maoni yako
    g) Eleza maana ya vifungu hivi kama vilivyotumiwa katika muktadha wa habari hii
    i. Fununu
    ii. Siha
    iii. Mbichi na mbivu

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)