
Wanacheneo walichukua hatua kama:
- Kugoma – ili kushurutisha viongozi kuwalipa mishahara yao.
- Kuandamana – maandamano yaliwawezesha kuonyesha uongozi wa Sosi kuwa wanacheneo walikuwa wamechoka.
- Dkt. Siki alimtembelea Meya kumjuza shida ambazo wanacheneo walikumbana nazo.
- Diwani III aliwaomba wenzake kushughulikia maslahi ya wanacheneo.
- Watetezi wa wafanyakazi, Tatu, Medi na Beka walimwarifu Meya shida ambazo walikumbana nazo.
- Waridi aliwacha kazi ili kuonyesha kuwa aliudhika na jinsi wanacheneo walivyoshughulikiwa.
- Mamake Dadaruo, kumlisha mtoto chakula kilicholala ili angaa kuepuka na athari ya njaa.
- Ili Meya kuwadhibiti polisi, aliwaongezea mshahara na hivyo aliweza kuwatumikia alivyopenda.
- Meya anaombwa kuunda kamati nyingi ili aweze kuwapa viongozi wanaompinga na hivyo kupata utulivu katika baraza.
- Meya kuwapeleka watoto wake kusomea ng‘ambo kwani elimu ya Cheneo ni ya kawaida mno.
- Meya angependa mtoto wako apate uraia wa kule ng‘ambo, jambo linalomfanya ampeleke mkewe ng‘ambo kujifungulia huko.
- Meya ananyakua vipande vya ardhi ili kuweza kujitajirisha na kuwapeleka watoto na mke wake ng‘ambo.
- Meya anamtaka mhubiri awe upande wake na kwa hivyo anapendekeza kumpa sadaka ya laki kila mwezi.
- Wanacheneo kumripoti Meya kwa makao makuu jambo linalofanya Meya kushikwa.
- Diwani I na II kumdanganya Meya kuhusu uongozi wake, jambo linalowafanya kunufaika kutokana na ujinga wa Meya.
- Meya kuandaa kongamano la mameya ili wampe msaada wa kukidhi nakisikitika bajeti.
- Diwani III kumrahi Dkt. Siki kuingia siasani ili kuleta uadilifu.
sharon kalunda answered the question on October 3, 2019 at 05:56
-
"Mtu huvuna alichopanda, ukipanda pojo huwezi kuvuna kunazi."
(Solved)
Mstahiki Meya
"Mtu huvuna alichopanda, ukipanda pojo huwezi kuvuna kunazi."
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Anayeambiwa alisema nini baada ya kuambiwa haya?
c) Thibitisha kuwa wanacheneo walipanda pojo.
Date posted:
October 3, 2019
.
Answers (1)
-
Taja aina nne za hadithi.
(Solved)
Taja aina nne za hadithi.
Date posted:
October 3, 2019
.
Answers (1)
-
Mtemi Nasaba Bora ni kielelezo cha viongozi wa kiafrika wanaondeleza uongozi mbaya. Jadili kauli hii.
(Solved)
Kidagaa kimemwozea
Mtemi Nasaba Bora ni kielelezo cha viongozi wa kiafrika wanaondeleza uongozi mbaya. Jadili kauli hii.
Date posted:
October 3, 2019
.
Answers (1)
-
Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika Diwani Damu Nyeusi, jadili namna ambavyo wahusika wa kike wamesawiriwa.
(Solved)
Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika Diwani Damu Nyeusi, jadili namna ambavyo wahusika wa kike wamesawiriwa.
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
"Hizi kurani zako ndizo zifanyazo nisije huku …"
(Solved)
Riwaya ya Kidaa Kimemwozea.
"Hizi kurani zako ndizo zifanyazo nisije huku …"
a) Eleza muktadha wa maneno haya.
b) Eleza umuhimu wa mrejelewa katika dondoo hili kwenye riwaya.
c) Eleza maisha ya msemaji yalivyokuwa kwa mujibu wa Riwaya ya Kidaa Kimemwozea.
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
"Leo ni siku, siku ya nyani kufa ambapo miti yote huteleza"
(Solved)
Damu nyeusi na hadithi zingine
"Leo ni siku, siku ya nyani kufa ambapo miti yote huteleza"
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Bainisha tamathali mbili za usemi zinazojitokeza katika dondoo hili.
c) Huku ukitoa mifano, thibitisha maudhui sita ambayo yamejitokeza katika hadithi ya Damu Nyeusi na wanayoyaendeleza.
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
"Umenena ndipo ndugu yangu. Hiyo ndiyo tanzia ya Afrika huru."
(Solved)
Kidagaa kimemwozea
"Umenena ndipo ndugu yangu. Hiyo ndiyo tanzia ya Afrika huru."
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Ni nini sifa za mvuto zinazowaleta pamoja mzungumzaji na mzungumziwa.
c) Tambua na ufafanue mbinu inayotumika katika dondoo.
d) Kwa mifano mwafaka fafanua tanzia hiyo inayorejelewa katika dondoo.
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
Jadili mbinu zifuatazo kama zilivyotumika katika Mstahiki Meya.
(Solved)
Jadili mbinu zifuatazo kama zilivyotumika katika Mstahiki Meya.
(a) Jazanda
(b) Uzungumzi nafsia
(c) Majazi
(d) Methali
(e) Taharuki
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
Eleza dhima ya lakabu kwa kurejelea hoja tano.
(Solved)
Eleza dhima ya lakabu kwa kurejelea hoja tano.
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
Eleza maudhui ya ukengeushi ukirejea hadithi zifuatazo katika diwani ya Damu nyeusi na hadithi nyingine
(Solved)
Eleza maudhui ya ukengeushi ukirejea hadithi zifuatazo katika diwani ya Damu nyeusi na hadithi nyingine
(i) Mke wangu
(ii) Damu Nyeusi
(iii) Tazamana na Mauti
(iv) Mizizi na matawi
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
"Wanyonge ndio wanyongwao" ni kauli inayodhihirika vyema kupitia wahusika tofauti katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.
(Solved)
"Wanyonge ndio wanyongwao" ni kauli inayodhihirika vyema kupitia wahusika tofauti katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.
Jadili.
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
Kama ningefuga ng‘ombe, mafahali na vindama,
(Solved)
Soma mashairi yafuatayo kisha ujibu maswali.
SIKUJUA!
1. Kama ningefuga ng‘ombe, mafahali na vindama,
Zisingenidhuru pembe, ngeu kuniandama,
Samli ni lembelembe, na minofu ya minyama.
2. Kama ningefuga mbuzi, na kondoo kundi zima,
Ningewajengea zizi, na maziwa nikakama,
Ningewachuna na ngozi, kutengenezea ngoma.
3. Kama ningefuga bata, nao kuku kwa ujima,
Chakula siyo matata, ni machicha na mtama,
Mayai ningeyapata, na kitoweo kizima.
4. Kumbe nimefuga punda, mashuzi ndio heshima,
Ni ukaidi na inda, mateke kurusha nyuma,
Nyama limekuwa nunda, mfugaji humuuma.
Kiitikio
Sikujua wa kufuga, mnyama mwenye faida
SHAIRI B
Afrika na Watu Wake
Mimi ninaona mgonjwa
Bado amelala kitandani.
Kama hatutamtoa miiba iliyobaki
Mgonjwa hataweka miguu yake chini
Ili kutembea bila ya kujiegemeza.
Miiba iliyomo ndani mwetu lazima
Pia iondolewe upesi kabla haijaingia
Kati ya mfupa na kufa pamoja nasi.
Baada ya kuitoa tuvae viatu vya chuma
Halafu tucheze nao mchezo wa siasa na uchumi.
Lakini kuitoa miiba hii
Tunahitaji macho makali
Mikono isiyotetemeka
Moyo usio na huruma
Na kuona miiba ilipoingilia.
MASWALI
(a) Onyesha jinsi ujumbe unaopatikana katika ubeti wa nne wa Shairi A na Shairi la B unavyokatisha tamaa.
(b) Eleza maana ya mshororo huu kama unavyojitokeza kwenye ubeti wa pili wa shairi B.
Baada ya kuitoa tuvae viatu vya chuma.
(c) Linganua sifa za kimuundo ukizingatia ubeti wa pili wa Shairi A na Shairi B.
(d) Ukizingatia Mshororo wa kwanza kwenye ubeti wa pili wa Shairi A, onyesha jinsi Mshairi alivyotumia kibali chake.
(e) Onyesha sifa moja ambayo inadhihirika kwenye shairi la B na ambayo hutawala tungo za aina hii.
(f) Nafsi neni amedhihirisha toni gani kwenye shairi A?
(g) Taja nafsi mbili nenwa kwenye shairi la B.
(h) Andika ubeti wa mwisho wa shairi B kwa lugha ya nadhari.
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
Ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia?
(Solved)
SABUNI YA ROHO
Ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia?
Ndiwe suluhu za zama, waja wakukimbilia,
Waja wanakutazama, madeni wakalipia,
Ndiwa sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Ndiwe mafuta ya roho, walisema wa zamani,
Utanunua majoho, majumba na nyumbani,
Umezitakasa roho, umekuwa mhisani,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvinja mlima.
Matajiri wanakujua, wema wako wameonja,
Nguo zao umefua, wakupata kwa ujanja,
Sura zao ‗mefufua, wanazuru kila njanja,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Ndiwe mvunja mlima, onana na maskini,
Watazame mayatima, kwao kumekua duni,
Webebe waliokuwa, wainue walio chini,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Ndiwe mvunja mlima, wapi kapata uwezo,
Umezua uhasama, waja kupata mizozo,
Ndiwe chanzo cha zahama, umewatia vikwazo,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Umevunja usuhuba, familia zazozana,
Waliokuwa mahabuba, kila mara wagombana,
Roho zao umekaba, majumbani wachinjana,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Nakutafuta kwa hamu, sabuni unirehemu,
Sinilipue ja bomu, sije kawa marehemu,
Niondoe jahanamu, ya ufukara wa simu,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Naondoka wangu moyo, nikuitapo itika,
Fulusi wacha uchoyo, tatua yalonifika,
Nichekeshe kibogoyo, nami nipate kuwika,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Date posted:
October 1, 2019
.
Answers (1)
-
Jadili matumizi ya mbinu ya ishara katika tamthilia hii.
(Solved)
Mstahiki Meya
Jadili matumizi ya mbinu ya ishara katika tamthilia hii.
Date posted:
October 1, 2019
.
Answers (1)
-
Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea imesheheni hali zinazotukia bila kutarajiwa. Fafanua.
(Solved)
Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea imesheheni hali zinazotukia bila kutarajiwa. Fafanua.
Date posted:
October 1, 2019
.
Answers (1)
-
"………Alimaliza kwa kuandika, "yajayo yapokee"
(Solved)
Damu Nveusi na Hadithi nyingine
"………Alimaliza kwa kuandika, "yajayo yapokee"
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Thibitisha ufaafu wa anwani ya hadithi hii.
Date posted:
October 1, 2019
.
Answers (1)
-
"Alikuwa na kiu lakini si ya maji, kadhalika alikuwa na njaa lakini si ya chakula Habebeki mwanamume habebeki……."
(Solved)
Kidagaa kimemwozea
"Alikuwa na kiu lakini si ya maji, kadhalika alikuwa na njaa lakini si ya chakula Habebeki mwanamume habebeki……."
(a) Weka dondoo hili katika muktadha wake .
(b) Eleza tamathali mbili zilizotumika katika dondoo hili.
(c) Eleza aina za kiu na njaa zilizomkumba mrejelewa wa kwanza.
(d) Mrejelewa wa pili alishindwa mtihani wa maisha. Jadili.
Date posted:
October 1, 2019
.
Answers (1)
-
"Duniani kuna watu na viatu"
(Solved)
Tamthilia nzima ya Mstahiki Meya.
"Duniani kuna watu na viatu"
(a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
(b) Thibitisha ukweli wa kauli hii ukirejelea tamthilia nzima ya Mstahiki Meya.
Date posted:
October 1, 2019
.
Answers (1)
-
Mwandishi wa tamthilia ya Mstahiki Meya ametumia wahusika kukuza kazi yake, Thibitisha kauii hili kwa kuwarejelea wahusika wafuatao.
(Solved)
Mwandishi wa tamthilia ya Mstahiki Meya ametumia wahusika kukuza kazi yake, Thibitisha kauii hili kwa kuwarejelea wahusika wafuatao.
(i) Diwani wa tatu
(ii) Bili
(iii) Mhubiri
(iv) Diwani I na II
Date posted:
October 1, 2019
.
Answers (1)
-
Kila nikaapo hushika tama.
(Solved)
Kila nikaapo hushika tama
Na kuwazia hali inayonizunguka.
Huyawazia madhila
Huziwazia shida
Huiwazia dhiki
Dhiki ya ulezi
Shida ya kudhalilishwa kazini.
Madhila ya kufanyiwa dharau
Kwa sababu ya jinsia ya kike.
Hukaa na kujidadisi
Hujidadisi kujua kwa nini
Jamii haikisikii kilio changu
Wenzangu hawanishiki mikono
Bali wananidharau kwa kuukosoa utamaduni
Hukaa na kujiuliza
I wapi raha yangu uiimwengu huu?
I wapi jamaa nzima ya wanawake?
MASWALI
(a) Shairi hili ni la aina. gani? Eleza
(b) Eleza dhamira ya mtunzi wa shairi hili.
(c) Kwa kutolea mifano eleza maana ya mistari mishata.
(d) Taja na ueleze tamathali mbili zilizotumika katika shairi hili.
(e) Tambulisha nafsi-neni katika shairi hili.
(f) Fafanua toni ya shairi hili.
(g) Fafanua maudhui mawili ya shairi hili.
(h) Onyesha namna nafasi neni anavyosalitiwa.
(i) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika shairi.
(i) Madhila
(ii) Kudhalilishwa.
Date posted:
October 1, 2019
.
Answers (1)