Trusted since 2008
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

"Mtu huvuna alichopanda, ukipanda pojo huwezi kuvuna kunazi."

Mstahiki Meya
"Mtu huvuna alichopanda, ukipanda pojo huwezi kuvuna kunazi."
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Anayeambiwa alisema nini baada ya kuambiwa haya?
c) Thibitisha kuwa wanacheneo walipanda pojo.

Answers


sharon
(a)
- Msemaji ni Diwani III
- Alikuwa akimwambia Dkt. Siki
- Walikuwa nyumbani kwa Diwani III.
- Daktari Siki alikuwa amemtembelea Diwani III kutaka kujua hali ya mji wa Cheneo.
(b) Dkt. Siki alikiri kuwa hakuwa akiyaona mambo kwa mtazamo huo. Mtazamo kuwa viongozi wabaya ni zao la uchaguzi uliofanywa na wanacheneo.
(c) Walichagua viongozi wabaya, waovu na hatma yake walivuna machungu.
- Hawana madawa – Meya anadanganya kuwa madawa yameagizwa, hatma yake ni vifo vya wanacheneo.
- Uchafuzi wa mazingira kwani Meya amekataa kuwalipa wafanyakazi wanaogoma .
- Mishahara duni kwa wafanyakazi wa Cheneo, huku madiwani wakijiongezea na hatakutolipa kodi.
- Mishahara ya wafanyakazi kucheleweshwa na hivyo kutokuwa na uwezo wa kukidhi mahitaji yao.
- Mali ya umma kunyakuliwa. Mali ambayo ilikuwa inufaishe wanacheneo, inawanufaisha viongozi wachache.
- Meya kumnyang‘anya mwanakandarasi, kandarasi yake na hivyo kuwafanya wanacheneo kutushughulikiwa mahitaji .
- Meya kushirikiana na madiwani wa I na II na Bili kuiba fimbo ya Meya ambayo ni ishara ya mamlaka ya Baraza la Cheneo.
- Kiwango cha elimu kuzoteka. Wanaofuzu hawawezi kupata kazi. Inambidi Meya kumpeleka mtoto wake ng‘ambo.
- Kuzoroteka kwa hali ya maisha. Umaskini unakithiri wanacheneo, hawawezi kununua chakula wala kulipia matibabu.
-Kusababisha migomo na maandamano ya wafanyakazi wa Cheneo.
sharon kalunda answered the question on October 3, 2019 at 05:50

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions

  • Taja aina nne za hadithi. (Solved)

    Taja aina nne za hadithi.

    Date posted: October 3, 2019 .    Answers (1)

  • Mtemi Nasaba Bora ni kielelezo cha viongozi wa kiafrika wanaondeleza uongozi mbaya. Jadili kauli hii. (Solved)

    Kidagaa kimemwozea
    Mtemi Nasaba Bora ni kielelezo cha viongozi wa kiafrika wanaondeleza uongozi mbaya. Jadili kauli hii.

    Date posted: October 3, 2019 .    Answers (1)

  • Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika Diwani Damu Nyeusi, jadili namna ambavyo wahusika wa kike wamesawiriwa. (Solved)

    Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika Diwani Damu Nyeusi, jadili namna ambavyo wahusika wa kike wamesawiriwa.

    Date posted: October 2, 2019 .    Answers (1)

  • "Hizi kurani zako ndizo zifanyazo nisije huku …" (Solved)

    Riwaya ya Kidaa Kimemwozea.
    "Hizi kurani zako ndizo zifanyazo nisije huku …"
    a) Eleza muktadha wa maneno haya.
    b) Eleza umuhimu wa mrejelewa katika dondoo hili kwenye riwaya.
    c) Eleza maisha ya msemaji yalivyokuwa kwa mujibu wa Riwaya ya Kidaa Kimemwozea.

    Date posted: October 2, 2019 .    Answers (1)

  • "Leo ni siku, siku ya nyani kufa ambapo miti yote huteleza" (Solved)

    Damu nyeusi na hadithi zingine
    "Leo ni siku, siku ya nyani kufa ambapo miti yote huteleza"
    a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    b) Bainisha tamathali mbili za usemi zinazojitokeza katika dondoo hili.
    c) Huku ukitoa mifano, thibitisha maudhui sita ambayo yamejitokeza katika hadithi ya Damu Nyeusi na wanayoyaendeleza.

    Date posted: October 2, 2019 .    Answers (1)

  • "Umenena ndipo ndugu yangu. Hiyo ndiyo tanzia ya Afrika huru." (Solved)

    Kidagaa kimemwozea
    "Umenena ndipo ndugu yangu. Hiyo ndiyo tanzia ya Afrika huru."
    a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    b) Ni nini sifa za mvuto zinazowaleta pamoja mzungumzaji na mzungumziwa.
    c) Tambua na ufafanue mbinu inayotumika katika dondoo.
    d) Kwa mifano mwafaka fafanua tanzia hiyo inayorejelewa katika dondoo.

    Date posted: October 2, 2019 .    Answers (1)

  • Jadili mbinu zifuatazo kama zilivyotumika katika Mstahiki Meya. (Solved)

    Jadili mbinu zifuatazo kama zilivyotumika katika Mstahiki Meya.
    (a) Jazanda
    (b) Uzungumzi nafsia
    (c) Majazi
    (d) Methali
    (e) Taharuki

    Date posted: October 2, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza dhima ya lakabu kwa kurejelea hoja tano. (Solved)

    Eleza dhima ya lakabu kwa kurejelea hoja tano.

    Date posted: October 2, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza maudhui ya ukengeushi ukirejea hadithi zifuatazo katika diwani ya Damu nyeusi na hadithi nyingine (Solved)

    Eleza maudhui ya ukengeushi ukirejea hadithi zifuatazo katika diwani ya Damu nyeusi na hadithi nyingine
    (i) Mke wangu
    (ii) Damu Nyeusi
    (iii) Tazamana na Mauti
    (iv) Mizizi na matawi

    Date posted: October 2, 2019 .    Answers (1)

  • "Wanyonge ndio wanyongwao" ni kauli inayodhihirika vyema kupitia wahusika tofauti katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea. (Solved)

    "Wanyonge ndio wanyongwao" ni kauli inayodhihirika vyema kupitia wahusika tofauti katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.
    Jadili.

    Date posted: October 2, 2019 .    Answers (1)

  • Kama ningefuga ng‘ombe, mafahali na vindama, (Solved)

    Soma mashairi yafuatayo kisha ujibu maswali.

    SIKUJUA!
    1. Kama ningefuga ng‘ombe, mafahali na vindama,
    Zisingenidhuru pembe, ngeu kuniandama,
    Samli ni lembelembe, na minofu ya minyama.

    2. Kama ningefuga mbuzi, na kondoo kundi zima,
    Ningewajengea zizi, na maziwa nikakama,
    Ningewachuna na ngozi, kutengenezea ngoma.

    3. Kama ningefuga bata, nao kuku kwa ujima,
    Chakula siyo matata, ni machicha na mtama,
    Mayai ningeyapata, na kitoweo kizima.

    4. Kumbe nimefuga punda, mashuzi ndio heshima,
    Ni ukaidi na inda, mateke kurusha nyuma,
    Nyama limekuwa nunda, mfugaji humuuma.

    Kiitikio
    Sikujua wa kufuga, mnyama mwenye faida

    SHAIRI B
    Afrika na Watu Wake

    Mimi ninaona mgonjwa
    Bado amelala kitandani.
    Kama hatutamtoa miiba iliyobaki
    Mgonjwa hataweka miguu yake chini
    Ili kutembea bila ya kujiegemeza.

    Miiba iliyomo ndani mwetu lazima
    Pia iondolewe upesi kabla haijaingia
    Kati ya mfupa na kufa pamoja nasi.
    Baada ya kuitoa tuvae viatu vya chuma
    Halafu tucheze nao mchezo wa siasa na uchumi.

    Lakini kuitoa miiba hii
    Tunahitaji macho makali
    Mikono isiyotetemeka
    Moyo usio na huruma
    Na kuona miiba ilipoingilia.

    MASWALI
    (a) Onyesha jinsi ujumbe unaopatikana katika ubeti wa nne wa Shairi A na Shairi la B unavyokatisha tamaa.
    (b) Eleza maana ya mshororo huu kama unavyojitokeza kwenye ubeti wa pili wa shairi B.
    Baada ya kuitoa tuvae viatu vya chuma.
    (c) Linganua sifa za kimuundo ukizingatia ubeti wa pili wa Shairi A na Shairi B.
    (d) Ukizingatia Mshororo wa kwanza kwenye ubeti wa pili wa Shairi A, onyesha jinsi Mshairi alivyotumia kibali chake.
    (e) Onyesha sifa moja ambayo inadhihirika kwenye shairi la B na ambayo hutawala tungo za aina hii.
    (f) Nafsi neni amedhihirisha toni gani kwenye shairi A?
    (g) Taja nafsi mbili nenwa kwenye shairi la B.
    (h) Andika ubeti wa mwisho wa shairi B kwa lugha ya nadhari.

    Date posted: October 2, 2019 .    Answers (1)

  • Ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia? (Solved)

    SABUNI YA ROHO
    Ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia?
    Ndiwe suluhu za zama, waja wakukimbilia,
    Waja wanakutazama, madeni wakalipia,
    Ndiwa sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
    Ndiwe mafuta ya roho, walisema wa zamani,
    Utanunua majoho, majumba na nyumbani,
    Umezitakasa roho, umekuwa mhisani,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvinja mlima.
    Matajiri wanakujua, wema wako wameonja,
    Nguo zao umefua, wakupata kwa ujanja,
    Sura zao ‗mefufua, wanazuru kila njanja,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
    Ndiwe mvunja mlima, onana na maskini,
    Watazame mayatima, kwao kumekua duni,
    Webebe waliokuwa, wainue walio chini,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
    Ndiwe mvunja mlima, wapi kapata uwezo,
    Umezua uhasama, waja kupata mizozo,
    Ndiwe chanzo cha zahama, umewatia vikwazo,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
    Umevunja usuhuba, familia zazozana,
    Waliokuwa mahabuba, kila mara wagombana,
    Roho zao umekaba, majumbani wachinjana,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
    Nakutafuta kwa hamu, sabuni unirehemu,
    Sinilipue ja bomu, sije kawa marehemu,
    Niondoe jahanamu, ya ufukara wa simu,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
    Naondoka wangu moyo, nikuitapo itika,
    Fulusi wacha uchoyo, tatua yalonifika,
    Nichekeshe kibogoyo, nami nipate kuwika,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)

  • Jadili matumizi ya mbinu ya ishara katika tamthilia hii. (Solved)

    Mstahiki Meya
    Jadili matumizi ya mbinu ya ishara katika tamthilia hii.

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)

  • Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea imesheheni hali zinazotukia bila kutarajiwa. Fafanua. (Solved)

    Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea imesheheni hali zinazotukia bila kutarajiwa. Fafanua.

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)

  • "………Alimaliza kwa kuandika, "yajayo yapokee" (Solved)

    Damu Nveusi na Hadithi nyingine
    "………Alimaliza kwa kuandika, "yajayo yapokee"
    (a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    (b) Thibitisha ufaafu wa anwani ya hadithi hii.

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)

  • "Alikuwa na kiu lakini si ya maji, kadhalika alikuwa na njaa lakini si ya chakula Habebeki mwanamume habebeki……." (Solved)

    Kidagaa kimemwozea
    "Alikuwa na kiu lakini si ya maji, kadhalika alikuwa na njaa lakini si ya chakula Habebeki mwanamume habebeki……."
    (a) Weka dondoo hili katika muktadha wake .
    (b) Eleza tamathali mbili zilizotumika katika dondoo hili.
    (c) Eleza aina za kiu na njaa zilizomkumba mrejelewa wa kwanza.
    (d) Mrejelewa wa pili alishindwa mtihani wa maisha. Jadili.

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)

  • "Duniani kuna watu na viatu" (Solved)

    Tamthilia nzima ya Mstahiki Meya.
    "Duniani kuna watu na viatu"
    (a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
    (b) Thibitisha ukweli wa kauli hii ukirejelea tamthilia nzima ya Mstahiki Meya.

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)

  • Mwandishi wa tamthilia ya Mstahiki Meya ametumia wahusika kukuza kazi yake, Thibitisha kauii hili kwa kuwarejelea wahusika wafuatao. (Solved)

    Mwandishi wa tamthilia ya Mstahiki Meya ametumia wahusika kukuza kazi yake, Thibitisha kauii hili kwa kuwarejelea wahusika wafuatao.
    (i) Diwani wa tatu
    (ii) Bili
    (iii) Mhubiri
    (iv) Diwani I na II

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)

  • Kila nikaapo hushika tama. (Solved)

    Kila nikaapo hushika tama
    Na kuwazia hali inayonizunguka.
    Huyawazia madhila
    Huziwazia shida
    Huiwazia dhiki

    Dhiki ya ulezi
    Shida ya kudhalilishwa kazini.
    Madhila ya kufanyiwa dharau
    Kwa sababu ya jinsia ya kike.

    Hukaa na kujidadisi
    Hujidadisi kujua kwa nini
    Jamii haikisikii kilio changu
    Wenzangu hawanishiki mikono
    Bali wananidharau kwa kuukosoa utamaduni

    Hukaa na kujiuliza
    I wapi raha yangu uiimwengu huu?
    I wapi jamaa nzima ya wanawake?

    MASWALI
    (a) Shairi hili ni la aina. gani? Eleza
    (b) Eleza dhamira ya mtunzi wa shairi hili.
    (c) Kwa kutolea mifano eleza maana ya mistari mishata.
    (d) Taja na ueleze tamathali mbili zilizotumika katika shairi hili.
    (e) Tambulisha nafsi-neni katika shairi hili.
    (f) Fafanua toni ya shairi hili.
    (g) Fafanua maudhui mawili ya shairi hili.
    (h) Onyesha namna nafasi neni anavyosalitiwa.
    (i) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika shairi.
    (i) Madhila
    (ii) Kudhalilishwa.

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)

  • Wasiwasi n‘ondokeya, ondoka enenda zako, (Solved)

    Soma ushairi ufuatao kisha ujibu maswali.
    1. Wasiwasi n‘ondokeya, ondoka enenda zako,
    Ondoka andama ndiya, nondosheya uso wako,
    Ondoka wanisikiya, ziwate jeuri zako,
    Jishughulishe na yako, yangu wayatakiyani?

    2. Wasiwasi siitaki, suhuba yako si nzuri,
    Haistahamilikii, uovu umekithiri,
    Inganyoshwa hainyoki, ikukutene kikiri,
    Sikati yako shari, enda zako wasiwasi.

    3. Huna kazi ufanyayo, ela kuwafitinisha,
    Viumbe na zao nyoyo, vitina kuwagotanisha,
    Hiino ndio kaziyo, yenye kukufurahisha,
    Ni kazi isiyokuchosha, mno umeizoeya.

    4. Mara waja na habari, mambo yalivyo nyumbani,
    Ati mambo si mazuri, mambo yote tatashani,
    Wanitaka nifikiri, usemayo ni yakini,
    Nisononeke moyoni, upate kufurahika.

    5. Au mara hunijiya, na kingine kisahani,
    Kuhusu zao afiya, hao waliyo nyumbani,
    Huwa husishi nambiya, hali zao taabani,
    Zingawa wakati gani? Ni zako au ni zao?

    6. Na mara kuja mambiya, nitakapotoka humu,
    Na kwamba yaningojea, nde maisha magumu,
    Uliloni kusudiya, ni kunitiya wazimu,
    Kama ndiyo yako hamu, basi unshatahayari.

    (a) Eleza ujumbe uliojitokeza katika shairi hili.
    (b) Fafanua muundo wa ubeti wa tatu.
    (c) Eleza aina ya shairi hili.
    (d) Fafanua arudhi za utunzi alizozingatia mshairi.
    (e) Eleza toni ya mshairi.
    (f) Andika ubeti wa tano katika lugha ya kinathari.
    (g) Eleza mifano mitatu ya uhuru wa mshairi.
    (h) Eleza maana ya misamiati ifuatayokama ilivyotumika katika shairi.
    (i) ndiya
    (ii) kisahani
    (iii) nde

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)