Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia?

      

SABUNI YA ROHO
Ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia?
Ndiwe suluhu za zama, waja wakukimbilia,
Waja wanakutazama, madeni wakalipia,
Ndiwa sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Ndiwe mafuta ya roho, walisema wa zamani,
Utanunua majoho, majumba na nyumbani,
Umezitakasa roho, umekuwa mhisani,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvinja mlima.
Matajiri wanakujua, wema wako wameonja,
Nguo zao umefua, wakupata kwa ujanja,
Sura zao ‗mefufua, wanazuru kila njanja,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Ndiwe mvunja mlima, onana na maskini,
Watazame mayatima, kwao kumekua duni,
Webebe waliokuwa, wainue walio chini,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Ndiwe mvunja mlima, wapi kapata uwezo,
Umezua uhasama, waja kupata mizozo,
Ndiwe chanzo cha zahama, umewatia vikwazo,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Umevunja usuhuba, familia zazozana,
Waliokuwa mahabuba, kila mara wagombana,
Roho zao umekaba, majumbani wachinjana,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Nakutafuta kwa hamu, sabuni unirehemu,
Sinilipue ja bomu, sije kawa marehemu,
Niondoe jahanamu, ya ufukara wa simu,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Naondoka wangu moyo, nikuitapo itika,
Fulusi wacha uchoyo, tatua yalonifika,
Nichekeshe kibogoyo, nami nipate kuwika,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

  

Answers


sharon
i) Taja nafsi nenewa. Thibitisha.
Nafsi nenewa ni pesa/fulusi- waja wanazitumiwa kusuluhusha matatizo mbalimbali kama vile kununulia vifaa kulipa madeni.
(ii) Eleza toni ya nafsi neni.
- Toni ya nafsi neni ni ya kulalamika. Analalamika kuwa pesa zimemkimbia.
- Toni ya kusifia – ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
(iii) Eleza arudhi zozote nne zilizozingatiwa katika utunzi wa shairi hili.
- Beti nne
- Mishororo mine katika kila mshororo
- Vina vinabadilika katika kila ubeti isipokuwa kibwagizo
- Mshororo wa mwisho ni kibwagizo- sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
(iv) Mshairi anawasilisha ujumbe gani katika mleo wa ubeti wa sita?
- Pesa zimeteka nyara roho za wapendanao na kuwafanya kuuana majumbani mwao.
(v) Ukitoa mfano eleza mbinu zozote tatu za lugha alizotumia mshairi.
- Balagha – ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia?
- Tashbihi – sinilipe ja bomu.
- Jazanda – jehanamu ni tatizo.
- Tashhisi – fulusi zinazoombwa kumwondoa mnenaji jehanamu, zina uchoyo.
- Takriri – ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
(vi) Andika ubeti wa nne katika lugha nathari.
Mshairi anamsihi mvunja mlima (pesa) kuwasaidia maskini na mayatima ambao hali zao duni. Awabebe waliokwama na kuwainua walio chini. Ndiye sabuni ya roho na mvunja mlima (mtimiza yote).
(vii) Jadili jinsi mshairi anatumia ruhusa ya mshairi.
- inkisari – mfano; sinilipue – usinilipue
'mefufua – umefufua
- kuboronga sarufi - mfano wema wako wameonja badala ya wameonja wema wako.
Naondoka wangu moyo badala ya naondoka moyo wangu.
(viii) Kwa kurejelea mpangilio wa vina eleza bahari ambamo shairi hili linaweza kuainishwa.
- Bahari; ukaraguni – kila ubeti una vina tofauti na vya ubeti mwingine.
(ix) Fafanua maana ya : )
(i) ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima
- ni wewe ambaye hufurahisha na kusuluhisha matatizo yote
(ii) Jehanamu
- tatizo
sharon kalunda answered the question on October 1, 2019 at 13:45


Next: Nitafukuzwa mbinguni Kwa ushairi wangu mbaya Lakini hata motoni nitaimba:
Previous: Identify the challenges that face the practice of circumcision in our society today.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • Nitafukuzwa mbinguni Kwa ushairi wangu mbaya Lakini hata motoni nitaimba:(Solved)

    Nitafukuzwa mbinguni
    Kwa ushairi wangu mbaya
    Lakini hata motoni nitaimba:
    Wanasema
    Wanasiasa ni kama jizi
    Lililosukuma mtoto pembeni
    Na kunyonya ziwa la mama
    Wakati amelala usingizi usiku.
    Wanasema
    Mwanasiasa afapo
    Tumejikomboa na domo
    Moja pana lizibwalo na mchanga
    Na kilima cha simenti ngumu
    Lisikike tena hadharani.
    Wanasema pia
    Kusema haki
    Kwa kawaida
    Wanasiasa hatuwapendi.
    Kupiga kura ni hasira za mkizi
    Ni basi tu. Ni Ah!
    Ah!
    Wanamalizia
    Nchi mmefiilisi waacheni walimu
    Wakajenga taifa jipya.
    Top grade predictor publishers Page | 63
    Kama hamwezi kuona mbali
    Bure kuweka mkono usoni,
    Bure hakuna kichwa
    Kama hamwezi kufikiri.
    Ng‘ombe amekamuliwa na wazungu
    Waarabu, wahindi na wao
    Sasa anatoa damu
    Vilivyobaki ni chai ya rangi
    Na madomo mapana zaidi
    Yaliyo bado hai.
    Kuimba nimeimba

    Maswali
    (a) Mshairi ana dhamira gani?
    (b) Shairi hili ni la kukatisha tama, tetea rai hii.
    (c) Onyesha matumizi mawili ya mishata.
    (d) Eleza mbinu zozote nne za lugha zilizotumika katika shairi hili.
    (e) Andika ubeti wa mwisho katika lugha tutumbi.
    (f) Fafanua umbo la shairi hili.
    (g) Eleza maana ya mafungu ya maneno ya maneno yafuatayo:
    (i) kupiga kura ni hasira ya mkizi
    (ii) kuweka mkono usoni
    (iii) ng‘ombe amekamuliwa.

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • Jadili matumizi ya mbinu ya ishara katika tamthilia hii.(Solved)

    Mstahiki Meya
    Jadili matumizi ya mbinu ya ishara katika tamthilia hii.

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • Hayawezi kulinganishwa na tendo hili ndogo. Walifanya vizuri kuja.(Solved)

    MSTAHIKI MEYA: Timothy Arege
    Hayawezi kulinganishwa na tendo hili ndogo. Walifanya vizuri kuja.
    Hayawezi kulinganishwa na tendo hili ndogo. Walifanya vizuri kuja.
    (a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    (b) Fafanua nafasi ya wanaorejelewa kuwa ―"walifanya vizuri kuja" katika tamthilia hii.
    (c) Migogoro katika tamthilia hii hazikusuluhishwa vyema. Jadili.

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea imesheheni hali zinazotukia bila kutarajiwa. Fafanua.(Solved)

    Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea imesheheni hali zinazotukia bila kutarajiwa. Fafanua.

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • "Nyamaza boza wewe. Wadhani sisi kazi tunaanza leo? Tumekutana na wauaji wangapi?(Solved)

    Kidagaa Kimemwozea:
    "Nyamaza boza wewe. Wadhani sisi kazi tunaanza leo? Tumekutana na wauaji wangapi?
    a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    b) Dondoo hili linadokeza maudhui gani? Kwa kutoa mifano saba kwenye riwaya, bainisha jinsi maudhui hayo yanavyojitokeza.

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • "Hakujua maisha yake yangechukua mkondo upi. Mzo wa majuto ulimwandama. Ulimwengu wake ulivurugika, akawa kama tiara inayopeperushwa na upepo ikaenda arijojo"(Solved)

    Kanda la Usufi
    "Hakujua maisha yake yangechukua mkondo upi. Mzo wa majuto ulimwandama. Ulimwengu wake ulivurugika, akawa kama tiara inayopeperushwa na upepo ikaenda arijojo"
    (a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    (b) Taja na kueleza tamathali ya usemi kwenye dondoo hili.
    (c) Kwa kutolea mifano, onyesha jinsi anwani Kanda la Usufi inavyoafiki hadithi husika.

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • "………Alimaliza kwa kuandika, "yajayo yapokee"(Solved)

    Damu Nveusi na Hadithi nyingine
    "………Alimaliza kwa kuandika, "yajayo yapokee"
    (a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    (b) Thibitisha ufaafu wa anwani ya hadithi hii.

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • Elimu imeshindwa kutimiza lengo la kuwapa vijana uwezo wa kukabiliana na maisha ya kisasa. Thibitisha kauli hii kwa kurejelea hadithi zifuatazo.(Solved)

    Elimu imeshindwa kutimiza lengo la kuwapa vijana uwezo wa kukabiliana na maisha ya kisasa. Thibitisha kauli hii kwa kurejelea hadithi zifuatazo.
    (a) Mke wangu
    (b) Samaki wanchi zajoto
    (c) Damu nyeusi.

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • "Alikuwa na kiu lakini si ya maji, kadhalika alikuwa na njaa lakini si ya chakula Habebeki mwanamume habebeki……."(Solved)

    Kidagaa kimemwozea
    "Alikuwa na kiu lakini si ya maji, kadhalika alikuwa na njaa lakini si ya chakula Habebeki mwanamume habebeki……."
    (a) Weka dondoo hili katika muktadha wake .
    (b) Eleza tamathali mbili zilizotumika katika dondoo hili.
    (c) Eleza aina za kiu na njaa zilizomkumba mrejelewa wa kwanza.
    (d) Mrejelewa wa pili alishindwa mtihani wa maisha. Jadili.

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • Kuvunjwa kwa haki na sheria lilikuwa jambo la kawaida chini ya uongozi wa Mtemi Nasaba bora. Thibitisha ukweli wa Kauli hii ukirejelea riwaya ya Kidagaa...(Solved)

    Kuvunjwa kwa haki na sheria lilikuwa jambo la kawaida chini ya uongozi wa Mtemi Nasaba bora. Thibitisha ukweli wa Kauli hii ukirejelea riwaya ya Kidagaa kimemwozea.

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • "Duniani kuna watu na viatu"(Solved)

    Tamthilia nzima ya Mstahiki Meya.
    "Duniani kuna watu na viatu"
    (a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
    (b) Thibitisha ukweli wa kauli hii ukirejelea tamthilia nzima ya Mstahiki Meya.

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • Mwandishi wa tamthilia ya Mstahiki Meya ametumia wahusika kukuza kazi yake, Thibitisha kauii hili kwa kuwarejelea wahusika wafuatao.(Solved)

    Mwandishi wa tamthilia ya Mstahiki Meya ametumia wahusika kukuza kazi yake, Thibitisha kauii hili kwa kuwarejelea wahusika wafuatao.
    (i) Diwani wa tatu
    (ii) Bili
    (iii) Mhubiri
    (iv) Diwani I na II

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • Kila nikaapo hushika tama.(Solved)

    Kila nikaapo hushika tama
    Na kuwazia hali inayonizunguka.
    Huyawazia madhila
    Huziwazia shida
    Huiwazia dhiki

    Dhiki ya ulezi
    Shida ya kudhalilishwa kazini.
    Madhila ya kufanyiwa dharau
    Kwa sababu ya jinsia ya kike.

    Hukaa na kujidadisi
    Hujidadisi kujua kwa nini
    Jamii haikisikii kilio changu
    Wenzangu hawanishiki mikono
    Bali wananidharau kwa kuukosoa utamaduni

    Hukaa na kujiuliza
    I wapi raha yangu uiimwengu huu?
    I wapi jamaa nzima ya wanawake?

    MASWALI
    (a) Shairi hili ni la aina. gani? Eleza
    (b) Eleza dhamira ya mtunzi wa shairi hili.
    (c) Kwa kutolea mifano eleza maana ya mistari mishata.
    (d) Taja na ueleze tamathali mbili zilizotumika katika shairi hili.
    (e) Tambulisha nafsi-neni katika shairi hili.
    (f) Fafanua toni ya shairi hili.
    (g) Fafanua maudhui mawili ya shairi hili.
    (h) Onyesha namna nafasi neni anavyosalitiwa.
    (i) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika shairi.
    (i) Madhila
    (ii) Kudhalilishwa.

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • Wasiwasi n‘ondokeya, ondoka enenda zako,(Solved)

    Soma ushairi ufuatao kisha ujibu maswali.
    1. Wasiwasi n‘ondokeya, ondoka enenda zako,
    Ondoka andama ndiya, nondosheya uso wako,
    Ondoka wanisikiya, ziwate jeuri zako,
    Jishughulishe na yako, yangu wayatakiyani?

    2. Wasiwasi siitaki, suhuba yako si nzuri,
    Haistahamilikii, uovu umekithiri,
    Inganyoshwa hainyoki, ikukutene kikiri,
    Sikati yako shari, enda zako wasiwasi.

    3. Huna kazi ufanyayo, ela kuwafitinisha,
    Viumbe na zao nyoyo, vitina kuwagotanisha,
    Hiino ndio kaziyo, yenye kukufurahisha,
    Ni kazi isiyokuchosha, mno umeizoeya.

    4. Mara waja na habari, mambo yalivyo nyumbani,
    Ati mambo si mazuri, mambo yote tatashani,
    Wanitaka nifikiri, usemayo ni yakini,
    Nisononeke moyoni, upate kufurahika.

    5. Au mara hunijiya, na kingine kisahani,
    Kuhusu zao afiya, hao waliyo nyumbani,
    Huwa husishi nambiya, hali zao taabani,
    Zingawa wakati gani? Ni zako au ni zao?

    6. Na mara kuja mambiya, nitakapotoka humu,
    Na kwamba yaningojea, nde maisha magumu,
    Uliloni kusudiya, ni kunitiya wazimu,
    Kama ndiyo yako hamu, basi unshatahayari.

    (a) Eleza ujumbe uliojitokeza katika shairi hili.
    (b) Fafanua muundo wa ubeti wa tatu.
    (c) Eleza aina ya shairi hili.
    (d) Fafanua arudhi za utunzi alizozingatia mshairi.
    (e) Eleza toni ya mshairi.
    (f) Andika ubeti wa tano katika lugha ya kinathari.
    (g) Eleza mifano mitatu ya uhuru wa mshairi.
    (h) Eleza maana ya misamiati ifuatayokama ilivyotumika katika shairi.
    (i) ndiya
    (ii) kisahani
    (iii) nde

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • Ajaye kisimani mbele hunywa maji maenge, (Solved)

    Soma ushairi ufuatao kisha ujibu maswali.
    1. Ajaye kisimani mbele hunywa maji maenge,
    Asinywe yalo na vunju,
    Yakampa kigegezi,
    Yakamkibua roho akaona na kinyaa,
    Awali ndio awali, awali mbovu hamna.

    2. Kiwa utalimatia.
    Utayaramba makombo,
    Utadata vitu cheche,
    Kisomo chenye dhamana kikakupa kisogo,
    Inajuzu ujihimu
    Mwanafuu darasani,
    Urauka po mapema,
    Katu hutayaramba makombo,
    Hutakosa kisebeho.

    3. Dereva hata utingo,
    Natija ni asubuhi,
    Wateja utawawahi,
    Wasaa kuzingatia,
    Uwafikishe kazini,
    Kwa wasaa ufaao,
    Wasije wakateteshwa,
    Na bosi wao kazini,
    Nao wakakuapiza.

    4. Na ewe mwanazaraa,
    Mpini uukamate,
    Kabla jua kuwaka sana,
    Majasho kutiririsha mwilini,
    Yang‘oe yote magugu,
    Kutoka kwa lako konde.

    5. Mhadimu mwenye ajizi,
    Yakujuza ujihimu,
    Ununue na maziwa,
    Majogoo uyawahi mapema,
    Usije ukayadata,
    Chai mkandaa ukaandaa,
    Wateja wakuambae mithili ya ibilisi.

    Maswali
    (a) Eleza nasaha yoyote inayotolewa kwa wafanyakazi wowote watatu kwenye shairi.
    (b) Taja sifa zozote za kimuundo zilizotumiwa na mtunzi.
    (c) Eleza toni ya mshairi.
    (d) Nafsi nenewa anahimizwa kufanya nini.
    (e) Andika ubeti wa tatu kwa lugha tutumbi.
    (f) Toa mifano miwili ya uhuru wa mshairi.
    (g) Eleza maana ya misamiati ifuatayo kama ilivyotumiwa kwenye shairi.
    (i) Maji maenge
    (ii) Natija
    (iii) Majogoo

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • Jumuiya ya "Mstahiki Meya" inaafiki kwa kiasi kikubwa jamii ya kisasa. Thibitisha.(Solved)

    Jumuiya ya "Mstahiki Meya" inaafiki kwa kiasi kikubwa jamii ya kisasa. Thibitisha.

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • "Huu ni ukoloni mamboleo"(Solved)

    Mstahiki Meya
    "Huu ni ukoloni mamboleo"
    (a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    (b) Eleza umuhimu wa msemewa katika tamthilia hii.
    (c) Jadili namna ukoloni mamboleo unavyojitokeza katika tamthilia.

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • Kufariki kwa kitoto Uhuru ni jazanda inayoashiria hali halisi ya mambo riwayani "kidagaa kimemwozea". Jadili(Solved)

    Kufariki kwa kitoto Uhuru ni jazanda inayoashiria hali halisi ya mambo riwayani "kidagaa kimemwozea". Jadili.

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • "Kwa nini mnaifunga mnyororo ile doggy mgonjwa? Mbona msiiwache free".(Solved)

    Kidagaa kimemwozea
    "Kwa nini mnaifunga mnyororo ile doggy mgonjwa? Mbona msiiwache free".
    (a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    (b) Onyesha jinsi wahusika riwayani wamefungwa minyororo.
    (c) Minyororo inayorejelewa katika (b) hapo juu ilifunguliwaje?

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • Onyesha jinsi ukatili unavyojitokeza kwa kurejelea hadithi zifuatazo. (Solved)

    Onyesha jinsi ukatili unavyojitokeza kwa kurejelea hadithi zifuatazo.
    (i) Kanda la usufi
    (ii) Shaka ya mambo
    (iii) Mwana wa darubini
    (iv) Ndoa ya Samani.

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)