Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Andika maana ya msemo. Kuwa na mihayara.

      

Andika maana ya msemo.
Kuwa na mihayara.

  

Answers


sharon
Kuwa na maumivu.
sharon kalunda answered the question on October 4, 2019 at 08:34


Next: Andika upya sentensi hii kwa kutumia visuwe vya maneno yaliyopigwa mstri. Lupita ndiye alitakadamu upelelezi wa shamba hili.
Previous: A student was culturing E. coli (a bacterium) in a Petri-dish. He placed the Petri-dish in an incubator at 30oC.He removed it from the incubator...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • Andika upya sentensi hii kwa kutumia visuwe vya maneno yaliyopigwa mstri. Lupita ndiye alitakadamu upelelezi wa shamba hili.(Solved)

    Andika upya sentensi hii kwa kutumia visuwe vya maneno yaliyopigwa mstri.
    Lupita ndiye alitakadamu upelelezi wa shamba hili.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Andika kinyume. Ukipitia kwao utalaaniwa.(Solved)

    Andika kinyume.
    Ukipitia kwao utalaaniwa.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Mwanafunzi aliadhibiwa kwa uongo wake. (Anza kwa .......Uongo)(Solved)

    Mwanafunzi aliadhibiwa kwa uongo wake.
    (Anza kwa .......Uongo)

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Tambua kinai kilichopigwa mstari katika senensi hii; Watu wenye woga mwingi hukimbia ovyo.(Solved)

    Tambua kinai kilichopigwa mstari katika senensi hii;
    Watu wenye woga mwingi hukimbia ovyo.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Andika maana mbili za neno "mlango".(Solved)

    Andika maana mbili za neno "mlango".

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Jibu kulingana na maagizo. (i) Ufisadi (unda kitenzi) (ii) - pya (unda nomino)(Solved)

    Jibu kulingana na maagizo.
    (i) Ufisadi (unda kitenzi)
    (ii) - pya (unda nomino)

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Kanusha sentensi hii katika hali ya "a" Kibofu hupaa angani.(Solved)

    Kanusha sentensi hii katika hali ya "a"
    Kibofu hupaa angani.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • CHIMBUKO LA USHAIRI Ushairi ni fani kongwe kama mwanadamu mwenyewe alivyo mkongwe duniani. Na mashairi yamekuwepo kitambo sana hata kabla ya lugha...(Solved)

    CHIMBUKO LA USHAIRI
    Ushairi ni fani kongwe kama mwanadamu mwenyewe alivyo mkongwe duniani. Na mashairi yamekuwepo kitambo sana hata kabla ya lugha ya Kiswahili bado haijanawiri na kushamiri kama ilivyo hivi leo. Ndipo tunasikia kuna mashiri ya kipemba, mashairi ya kimvita, mashairi ya kivumba, mashairi ya kipate, mashairi ya kiyunani, ya kirumi na kadhalika,. Almradi kila jamii na kila kabila lilikuwa na mashairi yake.
    Katika utafiti na kongomano zao, wataalam wa arudhi za Kiswahili asili wamechambua na kufafanua kwamba mashairi ya Kiswahili asili yake ni nyimbo za jadi zilizokuwa zikiimbwa na manju, wangoi au waimbaji stadi wa tangu na tangu walipojumuika katika matukio na hafla mbalimbali kama za jando, arusi, matanga, ngoma na shangwe zao za maishani.
    Nyimbo hizi zilitumiwa na watangulizi wetu, kidhamira hazikuhitalafiana hata kidogo na mashairi ya Kiswahili tunayohimiza wakati huu. Farka iko katika lugha na umbo kwani kila jamii ilitumia lugha yake na lahaja ya mazingira yake. Na kwa upande wa umbo, tungo hizo za awali kabisa hazikuwa na sanaa kwa maana ya ushauri tunauona leo. Bali tungo hizo zilijengeka katika nguzo mbili kuu. Kwanza ni uzito wa mawazo maadilifu ambayo yalitaamaniwa sana. Na pili ni mizani ya sauti ya manju kulingana na lahani, pumzi zake pamoja na madoido katika uimbaji ambao ulikuwa burudani naathari katika noyo za wasikilizaji wake.
    Kwa kifupi ni kwamba, nyimbo hizo ziliuhifaid umma kwa njia mbili, mawaidha kwa mapana na taathira au jadhba kutokana na sauti tamu ya manju.
    Kama utakubalika, basi huo ndio ushairi wa awali kabisa ullioambatana na nyimbo zetu za kienyeji. Kila kabila katika nchi zetu lilikuwa na ushauri wake au nyimbo zake zenye undani uliolenga sababu maalum na tukio maalum katika jamii.
    Nyimbo kama hizo kwa jina la sasa tunaweza kuita mashairi ndizo zile zilizoitwa ‘mwali’ na wakamba; gichandi kwa ‘wakikuyu’; ‘gigia gi sigele’ kwa waluo na ‘wagashe’ kwa wasukuma zilikuwa na undani wa kipekee tena uliodidimia ambao si bure kutolewa hadharani.
    Aina za mashairi ya watu wa mwambao ni kama lelemama, misemele, gungu, nyiso, kongozi n.k.
    (Walla Bin Walla – Malenga wa Ziwa Kuu , E.A.E.P)



    1. Ni nini haswa chimbuko la ushairi?
    2. Kulingana na kifungu hiki, ni nini umuhimu wa ushairi ?
    3. Ni maswala gani yaliyowapendeza wasikilizaji wa tungo hizo za zama ?
    4. Tofauti kati ya nyimbo za zama na ushairi wa leo upo kwenye vipengele gani viwili ?
    5. Kifungu : ‘haijanawiri na kushamiri’ ina maana gani katika lugha nyepesi ?
    6. Eleza maana ya :
    (a) Kongamano …
    (b) Jadhiba
    (c) Farka
    (d) Awali..

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Andika katika msemo halisi. Mwalimu alishangaa ni kwa nini Juma hakuwa amebeba mkoba wake siku hiyo.(Solved)

    Andika katika msemo halisi.
    Mwalimu alishangaa ni kwa nini Juma hakuwa amebeba mkoba wake siku hiyo.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Andika sentensi ifuatayo kwa udogo wingi. Mtu yule haachi kuandamana na mbwa wake aliyedhoofika kiafya.(Solved)

    Andika sentensi ifuatayo kwa udogo wingi.
    Mtu yule haachi kuandamana na mbwa wake aliyedhoofika kiafya.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi moja yenye kishazi huru na kishazi kitegemezi ukitumia "O" rejeshi tamati.(Solved)

    Tunga sentensi moja yenye kishazi huru na kishazi kitegemezi ukitumia "O" rejeshi tamati.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Changanua sentensi hii kwa kutumia jedwali. Mama alilima kwa bidii ingawa hakupata faida.(Solved)

    Changanua sentensi hii kwa kutumia jedwali.
    Mama alilima kwa bidii ingawa hakupata faida.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi ukitumia kitenzi cha katika hali ya kutendwa.(Solved)

    Tunga sentensi ukitumia kitenzi cha katika hali ya kutendwa.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Bainisha shamirisho na chagizo katika sentensi ifuatayo. Kimathi alimwandikia babake barua kwa kalamu jana jioni.(Solved)

    Bainisha shamirisho na chagizo katika sentensi ifuatayo.
    Kimathi alimwandikia babake barua kwa kalamu jana jioni.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Asifuye mvua imemnyea. Huu ni msemo wenye hakika isiopingika, na kutilia shaka ni sawa na kudai jua linaweza kubadilika na kuchomozea upande...(Solved)

    Soma taarifa hii kisha ujibu maswali

    Asifuye mvua imemnyea. Huu ni msemo wenye hakika isiopingika, na kutilia shaka ni sawa na kudai jua linaweza kubadilika na kuchomozea upande wa magharibi badala ya mashariki. Huu ndio ukweli uliodhihirika juzi katika vyombo vyetu vya magazeti.
    Lisemwalo lipo, na kama halipo li njiani. Waama, pafukapo moshi pana moto. Mwanafunzi mmoja wa kike kwa jina P.N. katika chuo kikuu kimojawapo nchini alishangaza umma wa Kenya na ulimwengu kwa jumla alipodai kuwaambukiza wanafunzi wenzake wa kiume mia moja na ishirini na wanne virusi vya Ukimwi.
    Kisa na maana? Aliambukizwa Ukimwi na mwanafunzi mwenzake aliyekuwa akifanya majaribio ya ualimu katika shule yao ya upili. Baada ya kushawishika sana alijuana naye kimwili, na matokeo yakawa kifo ambacho sasa alikuwa anawagawia wenzake.
    Kisa kama hiki kinachangia kueleza kina kirefu cha kutamauka na upweke ambao maisha ya waja wengi yameingia kiasi cha kuwaacha wanyama ijapo wanaenda kwa miguu miwili bado. Katika mojawapo ya mafunzo ya kidini ambayo Padre alinifunza mimi na wanafunzi wenzangu, tuliambiwa kisasi ni chake Mola, sisi waja wetu ni kushukuru tu. Mbona basi mwanafunzi kama huyu kutaka kulipiza?
    Ima fa ima, na waswahili husema, “mlaumu nunda na kuku pia”. Huyu mwanafunzi hawezi kuachiwa atende alivyotenda. Aliyekula naye raha alikuwa mtu aliyefahamika vizuri sana kwake. Isitoshe, huenda wakati huo alikosana na mama na baba kulala nje. Huenda alikosana na ndugu zake kwa kuepa nyumbani usiku wa manane kwenda kumwona huyu kalameni. Huenda alikosana na mwalimu wake kwa sababu kiburi kilianza kuingia. Kwa vyovyote vile, alikula raha na hastahili kuwaadhibu watu wasio na hatia kufidia makosa yake. Je, kama yeye na huyo jamaa wasingekuwa na Ukimwi, raha kiasi gani wangezila hadi leo?
    Jamii na watu wote kwa jumla hawana budi basi kulaani vitendo vya P.N. vya kuambukiza wanafunzi wenzake virusi huku akijua. Hili ni kosa ambalo linastahili adhabu ya kifo. Dawa ya moto ni moto ni adhabu inastahili kuchukuliwa haraka ili P.N. ambaye tayari amekiri hatia, atiwe nguvuni na adhabu itolewe.
    Barua ya P.N. inafafanua jambo jingine sugu. Kwamba kiwango cha maadili katika vyuo vyetu kimezorota kiasi cha kufanyiana unyama usiosemeka. Vijana wengi siku hizi wanashiriki tendo la ndoa bila haya. Huu upotofu wa maadili katika jamii wapaswa kushutumiwa na wote. P.N. hana sababu yoyote ya kibinadamu, kidini au kitu chochote kile kudai haki kwa uovu huo wake.


    1.Taja kichwa kwa makala haya
    2. Katika aya mbili za kwanza, mwandishi anamlaumu mwanafunzi kwa kosa gani? Eleza chanzo cha tabia za P.N
    4. Mwandishi wa taarifa hii anataka P.N achukuliwe hatua gani? Kwa nini?
    5. Barua ya P.N. bila shaka imeonyesha uvumbuzi mpya. Utaje
    6. Eleza maana ya vifungu hivi kama vilivyotumiwa katika taarifa:
    (a) Kina kirefu cha kutamauka
    (b) Ima fa ima
    (c) Kufidia makosa yake

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi kwa kutumia. (i) Kivumishi cha "ki" ya mfanano. (ii) Kielezi cha kiasi cha jumla.(Solved)

    Tunga sentensi kwa kutumia.
    (i) Kivumishi cha "ki" ya mfanano.
    (ii) Kielezi cha kiasi cha jumla.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Onyesha matumizi ya "kwa" katika sentensi hii. Kwa kuwa alikuwa amechelewa kwenda kwa nyanyake alisafiri kwa baiskeli.(Solved)

    Onyesha matumizi ya "kwa" katika sentensi hii.
    Kwa kuwa alikuwa amechelewa kwenda kwa nyanyake alisafiri kwa baiskeli.

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Kiswahili lugha yenye asili yake katika ukanda wa Afrika Mashariki imeenea duniani ambako inafundishwa katika uyuo vikuu saba vya umma na vyuo vikuu viwili visivyo vya...(Solved)

    Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali.
    Kiswahili lugha yenye asili yake katika ukanda wa Afrika Mashariki imeenea duniani ambako inafundishwa
    katika uyuo vikuu saba vya umma na vyuo vikuu viwili visivyo vya umma. Hivi ni Baratoni na Chuo kikuu ch aKikatoliki. Katika kiwango hiki, watu wanafunzwa isimu na fasihi mafunzo haya yanatolewa kuanzia shahada ya kwanza, shahada ya uzamili na shahada ya uzamifu.Elimu ya juu ya Kiswahili inatiliwa mkazo katika vyuo vikuu nchini Tanzania na hasa Dar-es-Salaam. Chuo hiki ndicho mlezi wa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI). Kwa muda mrefu, TUKI imechapisha mararida, kuzua istilahi na kuandaa kamusi. Vyuo vikuu nchini Uganda vikiongozwa na Makerere vimeanzisha mikakati kabambe ya kufunza Kiswahili. Kwingineko barani Afrika, Kiswahili kinafunzwa nchini Msumbiji, Sudan, Misri, Lesotho, Ghana, Nigeria n.k lugha hii imepewa msisimko mkubwa katika mitaala kuambatana na sera ya Afrika Kusini kutukuza lugha za Kiafrika. Ikumbukwe kuwa lugha hii ilichangia pakubwa ukombozi wa Afrika Kusini.Ukitembelea baadhi ya vyuo vikuu katika nchi za mashariki ya mbali kama Japani, Kora Kusini na Uchina, utapata Kiswahili kwenye orodha ya masomo. Maandishi mengi yanatafsiriwa kwa Kiswahili katika vyuo hivi. Takribani nchi zote ulaya zina vyuo vikuu vinavyofunza Kiswahili. Lakini Uingereza, Ujeremani na nchi za Skandinevia zimetia fora, pamoja na kufunza lugha hii, vyuo vinafadhili utafiti na uchapishaji wa mambo kuhusu Kiswahili. aidha nchi hizo huwadhamini wengi kusomea huko. Muhimu zaidi ni kuwa vyuo vikuu katika nchi hizo zimehifadh maandishi mengi ya Kiswahili. Hivi sasa masomo mengi wanayatumia kufanya utafiti hasa hukusu ushairi. Moja ya asasi hizi ni School of Oriental and African studies. Jijini London. Wataalamu waliosomea vyuo hivi wamerudi nyumbani na sasa wanajihusisha na uchapishaji wa vitabu vya nadharia, isimu, surufi, fasihi andishi na fasihi simulizi.
    Hata hivyo, ni Marekani ambapo matumizi na mafunzo ya Kiswahili katika vyuo vikuu yamepanuka sana. Lugha hii inafunzwa katika majimbo kama Washington, New York, Chicago, Texas, California, New Jersey n.k. vyuo maarufu sana vile Cornel, Yale na Havard vinafunza Kiswahili. Hali hii imesaidia kuingizwa kwa lugha hii katika mtandao.Lugha hii inafunzwa kama ishara ya hisia za Uafrika. Wamerekani weusi wanaona fahari kuzungumza Kiswahili. Hii huwakumbusha kuwa wao wana asili ya barani Afrika. Kupitia mafunzo haya, Wamerekani wengi wanaiga utamaduni wa Kiafrika. Wengi wao wamejipa majina ya Kiswahili kama vile Baruti Katembo Maulana, Simba n.k. kwa hakika Kiswahili kinapata hadhi.

    Maswali.
    (a) Bila kupoteza maana illiyokusudiwa na mwandishi, fupisha aya ya kwanza na ya pili.
    (maneno 50 - 60)
    (b) Kwa kuzingatia aya zilizobaki, eleza mambo muhimu anayoeleza mwandishi kuhusu ufundishaji
    wa Kiswahili katika vyuo vikuu. (maneno 60 - 70)

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Kitabu kinaeleza Mungu kamuumba mwanamke kutokana na ubavu tu wa mwanamume. Na hapa bila shaka ndipo linapojisalimishia shina lisilokuwa na mzizi thabiti...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali:-

    Kitabu kinaeleza Mungu kamuumba mwanamke kutokana na ubavu tu wa mwanamume. Na hapa bila shaka ndipo linapojisalimishia shina lisilokuwa na mzizi thabiti la ubinafsi wa kiume – mwanamume akijijadilia kimoyomoyo. Ikiwa huyu mwanamke alitokana na ubavu wangu, yeye awe nani kwangu? Hakuna shaka ni wangu, mali yangu. Kwa sababu hii, miaka nenda miaka rudi mwanamke amekuwa akiugua na kuguna chini ya uonevu wa mwanamume.
    Swala la kitabu kumleta duniani mwanamke kupitia ubavu wa mwanamume laweza kueleweka katika muktadha wa kile ambacho kimekuja kujulikana kama taasubi ya kiume. Na ili tuelewane barabara kuhusu maoni haya, tujisitishe kidogo katika kunusa tumbako huku tukijiuliza: ni nani au ni kina nani walihusika katika kubuni au kuandika hadithi ya asili ya mwanamke kitabuni? Ni kawaida ya binadamu kutazama na kueleza jambo kibinafsi. Asili ya mwanamke ilivyoelezwa kitabuni katika mkururo wa fikra hii yaweza kutambulikana kama uzushi tu.
    Kiutamaduni, hasa wa Kiafrika, huku akiwa yuakua, mtoto wa kike husombezewa kasumba ya mawazo akilini, na kwa bahati mbaya sana, aghalabu na mamake au nyanyake, kuhusu namna anavyotarajiwa kutabasamu, kujinyenyekeza, na jumla kujidunisha mbele ya mvulana. Ni mwiko kwake kudhihirisha tabia za kimabavu, sitaji kujitetea, ili asije akatiwa mdomoni mitaani! Msichana atacharazwa na wazazi wake kwa ujasiri licha ya kuthubutu kupigana na mvulana. Na hapo ndipo ilipojificha siri ya kuwa anapoolewa na akosane na mumewe, daima yeye hutolewa makosa na kupatikana na hatia mbele ya wazee.
    Wavulana kwa upande wao ni wanaume na lazima afanye mambo kiume. Si ajabu kuwa kinyume cha yale yanayowafika wasichana, wavulana wengi huonyeshwa mbovu na baba zao kwa sababu wamepigwa na wenzao. Ni vibaya baba kusikia mtoto (mvulana) wake amepigwa.
    Nyumbani msichana hutarajiwa kujilindia heshima kimwili hasa kwa kuhifadhi ubikira mpaka aolewe. Anapotembea na wanaume huitwa Malaya. Ni ajabu kuwa hakuna bikira wala Malaya mwanaume. Mvulana ambaye hajajuana kimwili na mwanamke kabla ya ndoa huchukuliwa kuwa zuzu; ilhali anayetembea ovyo na wanawake ndiye dume.
    Fauka ya hayo, inasikitisha kabisa kuwa mwanamke hana mahali pa kutua kikamilifu duniani. Kabla hajaolewa nyumbani, huchukuliwa kuwa mpita njia tu. Na anapoolewa ni poa kaolewa. Isitoshe mwanamke huolewa, haoi wala yeye na mume hawaoani. Mwanamke mahali pake ni jikoni pia anaonekana tu; ni hatia kwake kujaribu kusikika.
    Mkutano kuhusu mwongo wa wanawake uliofanyika miaka miwili iliyopita jijini Nairobi ilinuiwa kupalilia vizuri mwamko juu ya ukweli kuwa binadamu ni binadamu na hakuna haja ya wao kubaguana. Tofauti za kimaumbile haziwezi kuwa hoja. Tusiupigie makelele ubaguzi wa rangi huko Afrika kusini ilhali kwetu tuna ubaguzi wa kimaumbile. Tusipozingatia ushauri huu daima tutakuwa kwenye kile kinaya cha kuchekwa katika muktadha wa methali kuwa nyani haoni ngokoye.
    Ni kweli kosa lilifanyika tangu awali ambapo kufumba na kufumbua, mwanamke akapigwa jeki na kuachwa akilewalewa katika hali ambayo hangeweza kujitetea hivyo basi akachukuliwa kuwa kiumbe duni. Lakini haidhuru, yaliyopita si ndwele, tugange yajayo. Kinachohitajika ni wanawake kuwa na nia na msimamo imara. Ni lazima wajifunge kibwebwe na kujitoa mhanga na kupambana dhidi ya taasubi ya kiume.


    (a) Andika kichwa kinachofaa kutokana na taarifa uliyoisoma
    (b) Taasubi ya kiume ilianzaje?
    (c) Katika utamaduni wa mwafrika ni kasumba gani anayosombezewa mtoto wa kike anapokua?
    (d) “Wavulana walidekezwa na utamaduni”. Eleza
    (e) Taja kwa ufupi mambo muhimu yaliyoshughulikiwa katika mkutano wa mwongo wa wanawake mjini Nairobi
    (f) Eleza maana ya semi zifuatazo kama zilivyotumiwa katika taarifa uliyosoma:-
    (i) Nyani haoni ngokoye .
    (ii) Akatiwa midomoni
    (iii) Huonyeshwa mbovu
    (iv) Wajifunge kibwebwe
    (v) Yaliyopita si ndwele ganga yajayo

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)

  • Uundaji wa istilahi – hasa za lugha ya Kiswahili ni shughuli nyeti na nzito hivi kwamba, haipaswi kupapiwa na mtu yeyote. Hii...(Solved)

    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali:-

    Uundaji wa istilahi – hasa za lugha ya Kiswahili ni shughuli nyeti na nzito hivi
    kwamba, haipaswi kupapiwa na mtu yeyote. Hii ni shughuli inayohitaji umakinifu zaidi kwa wanaoshiriki katika mchakato wa uundaji istilahi za kutufaa katika mawasiliano na kukuza Kiswahili kwa jumla. Ufanisi wa watu binafsi, vyombo vya habari kama vile Shirika la Habari la Kenya (KBC), Taifa Leo na mashirika mengineyo katika ukuzaji wa lugha hutegemea mno sera na utayarishaji wa serikali katika kugharamia shughuli hii. Aidha, shughuli za kukuza lugha hukwama kwa sababu ya ukosefu wa fedha pamoja na sera maalum ya serikali kuhusu lugha.
    Hata hivyo, katika kuyakwepa matatizo haya, pamekuwepo na hatua za kimataifa za kujaribu kusawazisha shughuli ya uundaji wa maneno. Hatua hii ilichochea kubuniwa kwa shirikisho la kimataifa la vyama vya usanifishaji istilahi mnamo 1936. Lengo la kitengo hiki lilikuwa ni kufafanua msingi madhubuti ya uundaji wa istilahi duniani. Kwa hakika, shirikisho hilo limesaidia mno katika kuweka misingi ya shughuli za ukuzaji wa istilahi. Misingi hiyo ni ya jumla na haihusu taaluma yoyote mahususi. Katika makala hii, tunapiga darubini baadhi ya misingi hiyo pamoja na mapendekezo yake.
    Mosi, uundaji istilahi unafaa uanzie kwenye dhana na wala sio neno. Hii ina maana kwamba, kwanza pawepo na dhana au hali ambayo inahitaji itafutiwe neno au istilahi ya kuielezea. Inasikitisha sana kwamba pana wataalamu ambao wanaukaidi au kuukiuka msingi huu. Wanataaluma hawa hufanya mambo kinyume kwa kujibunia maneno yao na kuyahifadhi kwenye mikoba yao – halafu wakasubiri dhana izuke ndiposa waipachike istilahi yao. Pili, dhana zinabuniwa au kutolea istilahi au maneo ni muhimu zielezwe kwa ukamilifu na uwazi. Istilahi zinazoundwa zinafaa ziwe fupi iwezekanavyo na ziwe na uwezo wa kuelezea dhana kwa njia inayoeleweka bila utata. Tatu, maneno yanayoundwa sharti yawe na uhusiano wa aina fulani na dhana zinazowakilishwa na maneno hayo.
    Uhusiano huo unaweza kuwa ama ni wa kimaumbile au wa kiutendaji. kwa mfano, Mzee Sheikh Nanhany wa Mombasa alipobuni istilahi ‘uka’ kwa maana ya ‘ray’. Neno hili latokana na kupambauka au (kupambazuka kwa lafudhi ya kiamu. Neno ‘image’ ni jazanda kwa Kiswahili. ‘Mirage’ kwa Kiswahili ni ‘mangati’ (kutoka kwa mang’aanti) – yaani kung’aa kwa nchi. Mtaalamu mwingine aliyewazia uendajikazi wa kifaa na kubuni istilahi inayokubalika mpaka sasa ni Prof. Rocha Chimerah ambaye alibuni istilahi ‘tarakilishi’. Pengine Prof. Chimerah alifikiria kazi ni kifaa husika na kuunda neno la Kiswahili linaloakisi kazi hiyo. Tunajua kwamba kompyuta hufanya kazi inayohusu tarakimu kwa haraka kama umeme. Labda Chimerah ameegemea sifa hii kuibuka na istilahi hii.
    Maneno mengine ambayo yamebuniwa kufuatana na msingi huu ni ya Mzee Nabhany-mathalan ‘barua pepe’ (e-mail), na wavuti (website). Tukiegemea maumbile, neno ‘kifaru’ lina maana ya vita ilihali tuna zana ya vita iliyopewa jina hilo kwa sababu ya labda kuwa na maumbile sawa na kifarumnyama. Nne, istilahi zinaweza kukopwa kutoka lugha nyingine. Yamkini hakuna lugha hata moja ulimwenguni-zikiwemo lugha duniani kama vile kiingereza zinazoweza kujitosheleza. Takriban asilimia 80 ya maneno katika kiingereza ni ya kukopwa. Kwa hivyo, lugha ya Kiswahili inapokopa, hali hiyo haipaswi kuchukuliwa kuwa ni lugha dhaifu.
    Hata hivyo, istilahi zinazokopwa zi-nafaa zichukuliwe zilivyo katika umbo lao asili. Umbo hili linaweza kufanyiwa marekebisho machache tu, kulingana na sarufi na matumizi ya lugha kopaji. Mifano ya istilahi kama hizi ni ‘televisheni’ (television), kopmpyuta (computer), kioski (kutokana na jina ‘kiosk’ la Kijerumani) na redio (radio), Tano, pale istilahi haiwezi kukopwa, lugha husika ijaribu kubuni msamiati ufaao, kufanya hivyo ni kuhakikisha kwamba, lugha inastawi. Lakini tahadhari inapaswa kuchukuliwa hivi kwamba, Kiswahili kisikope maneno kiasi cha kupoteza upekee wake. Mwisho, uundaji wa istilahi uzingatie mofolojia ya kawaida ya lugha. Istilahi zinazoundwa kwa kuzingatia mofolojia huwa rahisi kuiua maneno yenye uhusiano wa istilahi asili kwa njia ya mnyambuliko.



    (i) Taja mambo ambayo huchangia ukuaji na ufanisi wa jumla wa lugha ya Kiswahili
    (ii) “Lugha ya Kiswahili ni dhaifu na isiyotosheleza” Je, mwandishi wa makala haya
    ana msimamo upi kuhusu kauli hii?
    (iii) Tahadhari zipi zinazofaa kuchukuliwa kabla ya kukopa istilahi kutoka lugha zingine?
    (iv) Yape makala haya anwani mwafaka
    (v) Eleza maana ya maneno yafuatayo:
    (a) Dhana-
    (b) Takribani –
    (c) Istilahi – .
    (d) Mofolojia –...

    Date posted: October 4, 2019.  Answers (1)