Trusted since 2008
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Soma shairi lifuatalo kisha uyajibu maswali.Mungu naomba subira, subira nayo imaniImani iliyo bora, bora hapa dunianiDuniani mwa kombora, kombora nayo hianiHiani pamwe ukora wenye kuhini.Kuhini...

Soma shairi lifuatalo kisha uyajibu maswali.

Mungu naomba subira, subira nayo imani
Imani iliyo bora, bora hapa duniani
Duniani mwa kombora, kombora nayo hiani
Hiani pamwe ukora wenye kuhini.

Kuhini kwenye kiburi, kiburi na ufidhulu
Ufidhuli wa kudhuri, kudhuri wangu muwili
Muwili hata kiclari, kidari kuwa thakili
Thakili kisinawiri, kisinawiri misuli.

Misuli kuwa hafith, hafifu kama muwele
Muwele wa hitilafu, hitilafi ya nduwele
Nduwele kutakilifu, kutakilifu milele
Milele kutoniafu, kutoniafu na vishale.

Vishale vinitomele, vitomele vikwato
Vikwato pia maole, maole kufanya mito
Mito ya matozi tele, tele mithili kitoto
Kitoto kilo vipele, vipele vyenye fiakuto.

Fukuto lanipa neno, neno hili kutamka
Kutamka wazi vino, vino subira kutaka
Kutaka imani mno, mno n’sipate wahaka
Wahaka wa matukano, matukano na mashaka.

Mashaka haya ya leo, leo yawe yamepita
Yaniepita na vilio, vilia vipishe nyota
Nyota njema ing’arao, ing’arao kunikita
Kunikita salamani, salamani nikadata.

a) Kwa nini nafsi neni inaomba subira na amani?
b) Shairi hili ni la aina gani kwa kuzingatia
(i) Mpangilio wa maneno
(ii) Mpangilio wa vina.
c) Kwa kutolea mifano eleza mbinu mbili za lugha zilizotumika katika shairi
d) Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari.
e) Kwa kutolea mifano, eleza jinsi uhuru wa kishairi ulivyotumiwa kutekeleza arudhi

Answers


Kavungya
(a) Ili asiwe na wasiwasi ya kutukanwa na huhiniwa aepuke kufanyiwa mabaya.
(b) (i) Pindu/mkufu/nyoka
Kwa sababu neno la mwisho katika mshororo wa mwisho wa ubeti linatumiwa kuanzia ubeti
unaofuata.
(ii) Ukaraguni
Vina vya kati na vya mwisho vinatofautiana kutoka ubeti mmoja hadi mwingine.
(c) (i) Tashbihi
- Hafifu kama muwele
- Tele mithili kitoto
(ii) Uradidi/Takriri
- Subira’
- Bora, kombora, ukora
- Kiburi, kudhuri n.k
(d) (i) Misuli kuwa dhaifu sana kama ya mgonjwa.
(ii) Hasa mgonjwa mwenye tatizo la
(iii) Ambao unasumbua sana daima na
(iv) usiopona kwa vishale.
(e) (i) Inkisari - kuleta urari wa mizani k.m kilo — kilicho.
(ii) Tabdila - kuleta urari wa vina k.m. kudhuri — kudhuru maole — maozi.
- Kuleta urari wa mizani k.m nduwele — ndwele
muwili — mwili
(iii) Mazida - kuleta urari wa vina pia mizani.
- Vinitomele - vinitome.
Kavungya answered the question on October 4, 2019 at 13:25

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions