Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Ainisha viambishi katika sentensi ifuatayo: Alimtembelea

      

Ainisha viambishi katika sentensi ifuatayo:
Alimtembelea

  

Answers


Kavungya
A-li-m-tembe-le-a
a-nafsi
li-wakati
m-mtendwa
tembe-mzizi
le-kauli
a-kiishio
Kavungya answered the question on November 22, 2022 at 05:52


Next: Akifisha sentensi hii. sikukuu ya madaraka nilikwenda eldama ravine kumwona yohana naye akasema atakuja kuniona pamoja na mkewe mariamu siku ya jumapili.
Previous: Majina yafuatayo yamo katika ngeli gani: Nywele Maji Jibwa

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • Akifisha sentensi hii. sikukuu ya madaraka nilikwenda eldama ravine kumwona yohana naye akasema atakuja kuniona pamoja na mkewe mariamu siku ya jumapili.(Solved)

    Akifisha sentensi hii.
    sikukuu ya madaraka nilikwenda eldama ravine kumwona yohana naye akasema atakuja kuniona pamoja na mkewe mariamu siku ya jumapili.

    Date posted: November 22, 2022.  Answers (1)

  • Andika kwa umoja. Machaka ya waridi hayazai maua meusi Walituandikia nyaraka ndefu.(Solved)

    Andika kwa umoja.
    Machaka ya waridi hayazai maua meusi

    Walituandikia nyaraka ndefu.

    Date posted: November 22, 2022.  Answers (1)

  • Ainisha silabi katika maneno yafuatayo Lugha Muhtasari(Solved)

    Ainisha silabi katika maneno yafuatayo
    Lugha

    Muhtasari

    Date posted: November 22, 2022.  Answers (1)

  • Onyesha matumizi matatu ya kiimbo katika sentensi ifuatayo: Mtoto analia.(Solved)

    Onyesha matumizi matatu ya kiimbo katika sentensi ifuatayo:
    Mtoto analia

    Date posted: November 22, 2022.  Answers (1)

  • Weka shadda katika maneno haya. Maharagwe Tupa(Solved)

    Weka shadda katika maneno haya.
    Maharagwe

    Tupa

    Date posted: November 22, 2022.  Answers (1)

  • Taja konsonanti ambazo ni viyeyusho.(Solved)

    Taja konsonanti ambazo ni viyeyusho.

    Date posted: November 22, 2022.  Answers (1)

  • Eleza sifa za sauti zifuatazo: /o/ /Sh/(Solved)

    Eleza sifa za sauti zifuatazo:
    /o/
    /Sh/

    Date posted: November 22, 2022.  Answers (1)

  • Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata: Hapo zamaniza kale palikuwa na mfalme aliyesifika sana. Sifa zake zilienea karibu na mbali. Zilienea kama moto nyikani msimu wa...(Solved)

    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata:
    Hapo zamaniza kale palikuwa na mfalme aliyesifika sana. Sifa zake zilienea karibu na mbali. Zilienea
    kama moto nyikani msimu wa kiangazi.
    Mstahiki Salamwana Salamwene, maana hili ndilo lilikuwa jina lake, alikuwa mtu wa ajabu sana. Asili
    yake yenyewe ilikuwa kitendawili. Inasemekana mamake alibeba mimba iliyopita miezi tisa. Na kila
    aliposhangaa alisikia sauti tumboni ikisema. “Mama kuwa na subira, bado ninalainisha lugha yangu”
    Baada ya muda mama alipolalamika alisikia, “Mama ninakaribia, ninamalizia kunoa ubongo wangu.”
    Halafu siku moja ikanyesha mvua kubwa iliyoandamana na radi. Waliokuwepo wanasema waliona
    mmweso mkali ulioangaza hata kwenye milima mikubwa. Salamwene akazaliwa. Moja ya sifa zake
    kubwa ilikuwa hekima na maarifa ya ajabu. Hakuna tatizo la watu wake ambalo alishindwa kulitatua.
    Watu wakawa wanafunga safari za siku nyingi kutoka mbali kuja kwenye ikulu yake. Wengi walienda kwa
    shida za dhati lakini wengine walikuja kumjaribu.
    Siku moja akaja mfanyabiashara tapeli na maua ya aina akamwambia, “Mstahiki mfalme, mtu wako
    anataka kuniuzia maua haya kwa vipande vingi vya almasi name nina shaka kuwa moja ni la bandia
    waweza kuniamulia?” Mfalme hakujibu. Naye inasemekana alipenda zaraa na hivyo alikuwa na miti na
    mimea iliyozaa maua na kutoa harufu anuwai. Basi akaja nyulu na kutua kwenye ua moja. Mfalme
    Salamwana akamtambulisha ua halisi.
    Muda ukayoyoma huku wahitaji wakiingia ikulu na kutoka. Siku moja akaja Binti mfalme mmoja kutoka
    nchi ya mbali na msafara mkubwa. Alipokewa kwa taadhima. Alikaa mwezi mmoja. Kila siku alikaa
    kwenye baraza akishuhudia mfalme akiyatatua matatizo ya watu. Jioni walikaa na mfalme pamoja
    wapambe wao akijifunza kutoka kwenye hazina kubwa ya busara ya Mstahiki Salamwana.
    Usiku uliotangulia kuondoka kwa mgeni, Salamwana alitoa amri za ajabu. Kwanza, aliamuru magudulia
    yote ya maji kwenye chumba cha kulala mgeni yabadilishwe. Pili, alimwamuru mpishi kupika chakula
    kilichokolea viungo kutoka Bara Hindi. Tatu, aliwaamuru wapambe kuwa mgeni akiomba chochote
    wasimpe ila wamfahamishe. Usiku huo, mgeni alihisi kiu kikali lakini aliponyanyua gudulia kumimima
    maji kwenye bilauri ya dhahabu, halikuwa na maji. Akajaribu la pili, magudulia yote ya shaba yaliyokuwa
    chumbani hayakuwa na maji. Alijitahidi kuvumilia lakini wapi! Ilibidi atafute msaada kwa wapambe nao
    wakamweleza walivyoambiwa. Mwanzoni aliona ni kukosa fadhila kumsumbua mwenyeji mwenye
    staha kama mfalme. Kiu ilipozidi kumkeketa koo alisalimu amri. Mfalme alifahamishwa. Na kama
    aliyejua alichoitiwa akaja na kigudulia kidogo chenye nakshi ya dhahabu na kifuko cha hariri. Alikuwa
    radhi kumpa mgeni sharubati ya kukata kiu ila kwa masharti. Anapokunywa maji ameze na zawadi
    atakayompa ambayo angeitapika afikapo nyumbani.
    Keshowe mgeni aliagwa kwa mbwewe na taadhima. Akaanza safari iliyochukua takriban mwezi mmoja.
    Baada ya miezi kumi, Mstahiki Salamwana Salamwene alipata risala kuwa Binti wa Mfalme alikuwa
    ameitapika zawadi aliyopewa kama alivyokuwa amekula yamini. Hicho kikawa kitendawili kwa watu
    wengi. Wakabaki wakiulizana jibu la fumbo hilo.

    Maswali
    1. Ipe hadithi hii anwani mwafaka.
    2. Kwa nini ilisemekana asili ya Mfalme Salamwana ilikuwa kitendawili?
    3. Eleza sifa sita za mfalme zinazojitokeza kwenye kifungu.
    4. Ni watu gani walikuja kwa mfalme.
    5. Mfalme alitumia hekima gani kutambua ua la bandia.
    6. Ni zawadi gani aliyopewa Binti mfalme aliyoitapika alipofika nyumbani?
    7. Ni ujumbe upi unaopatikana kutoka na hadithi hii.
    8. Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika kifungu.
    i. Maguduli
    ii. Sharubati
    iii. Dhati
    iv. yamini

    Date posted: November 22, 2022.  Answers (1)

  • Andika visawe vya viwakifishi hivi. (i)Nukta- (ii)Koma – (iii)Mkwaju- (iv)Mtajo-(Solved)

    Andika visawe vya viwakifishi hivi.
    (i)Nukta-
    (ii)Koma –
    (iii)Mkwaju-
    (iv)Mtajo-

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Ainisha mofimu na viambishi katika neno Aliyesomewa.(Solved)

    Ainisha mofimu na viambishi katika neno Aliyesomewa.

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Bainisha aina za maneno katika sentensi hizi. (i) Mwalimu anaandika . (ii) Mwalimu anaandika ubaoni.(Solved)

    Bainisha aina za maneno katika sentensi hizi.
    (i) Mwalimu anaandika .
    (ii) Mwalimu anaandika ubaoni.

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Kamilisha methali. Mgagaa na upwa(Solved)

    Kamilisha methali.
    Mgagaa na upwa

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Eleza sifa tatu za Kamusi ya lugha ya Kiswahili.(Solved)

    Eleza sifa tatu za Kamusi ya lugha ya Kiswahili.

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Tofautisha sauti /r/ na /l/(Solved)

    Tofautisha sauti
    /r/ na /l/

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Sahihisha sentensi hizi (i)Mtoto amerara usingizi mnono. (ii)Papu yangu ni mzee kiazi.(Solved)

    Sahihisha sentensi hizi
    (i)Mtoto amerara usingizi mnono.
    (ii)Papu yangu ni mzee kiazi.

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Tenga silabi na uainishe katika neno Muhtasari (Solved)

    Tenga silabi na uainishe katika neno
    Muhtasari

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Weka shadda neno barabara kuonyesha maana ya shwari na baraste.(Solved)

    Weka shadda neno barabara kuonyesha maana ya shwari na baraste.

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Onyesha matamshi ya vokali ukitumia mchoro huu wa pembe tatu.(Solved)

    Onyesha matamshi ya vokali ukitumia mchoro huu wa pembe tatu.
    fig7.png

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • UFAHAMU Ajira ya watoto Kingi alizaliwa vuruni kijiji kilichosifika kwa ukarimu wa wanakijiji wake.Ingawa walikuwa karimu,Wavuruni wengi walikosa elimu.(Solved)

    UFAHAMU
    Ajira ya watoto
    Kingi alizaliwa vuruni kijiji kilichosifika kwa ukarimu wa wanakijiji wake.Ingawa walikuwa
    karimu,Wavuruni wengi walikosa elimu.Fauka ya hayo,walininginia katika umaskini
    uliokithiri.Hivyo,wengi waliselea katika kazi za kijungu jiko.Watot wa umri wa kwenda shule
    walikosa elimu na kuzurura mitaani.Udhaifu huu ulimpa faida Mwakisu,tajiri mmoja aliyemiliki
    shamba kubwa.Aliwaajiri watoto hao.
    Mwakisu alikuwa mkwasi alietononoka si haba.Kama ni senti ,alikuwa nazo.Kilichotia doa
    jina lake ni kiburi.Mbali na kiburi hicho,yeye hakujaliwa moyo wa huruma na utu.
    Hakubarikiwa kuwa mwema .Maadili hutuongoza kila mara kuwa ‘wema hauozi’.
    Kwa Mwakisu,wema ulioza na kuvunda .Utu uling’oka katika bawaba za moyo wake na
    ukawa msamiati aliouchukia.Aliwatumikisha watoto wa wenzake huku wake wakisoma shule.Tabia
    yake hiyo ndiyo iliyowafanya Wavuruni kumtoa katika orodhayao ya watu wema.
    Mwakisu alistaajabisha!Hakutaka kununua mashine zozote za kufanya kazi shambani ingawa
    alikuwa nao uwezo.Alistahabu kuajiri watoto wadogo na kuwadhulumu.Mkwasi huyu alifurahia
    kuona vitoto vikimenyana na kazi shambani kwake tangu mawio hadi machweo na hatimaye kuwapa
    ujira mdogo.
    Siku moja Kingi alimtaka radhi, “Bosi naomba uniongezee chochote ,kwani tuna shida
    nyumbani.” Mwasiku alimkodolea macho huku mdomo ukimcheza.Hapo alimchomolea mwajiriwa
    wake tusi kubwa kutoka kwenye hazina yake isiyopungua.Tusi ambalo lilimtaabisha Kingi
    kulisahau.Lilikaririwa akilini mwake kwa sonono.Tangu siku hiyo Kingi akaona kuwa kuajiriwa na
    Mwakisu ni kufadhiliwa u chini.
    Kiburi cha mwakisu kilidhihirika kila mara .Kila alipomwona motto akilia kwa uchovu au
    maumivu ,ungemsikia akimfokea ,”Chapa kazi!Unalilia nani hapa?Kama humudu kazi rudi kwa
    mamako ukanyonye.”
    Kazi nyingi zilikuwa ngumu na hazikuwastahili watoto wenye umri mdogo.Si kipupwe, si
    kaskazi,si vuli,si kiangazi ,si kusi:kazi ziliongezeka na kuwaumiza watoto.Kingi,kwa
    mfano,alitakikana akame ng’ombe kumi na abebe maziwa hadi kwenye tangi kubwa .Kisha
    angewakatia mg’ombe nyasi na kuwasafisha .Hatimaye angehitajika kuzoa samadi.
    Msimu wa kipupwe uliwadia.Baridi ikawatafuna watoto hao waliokosa mavazi bora.Kingin
    aliugua.Watoto wengi wakapatwa na maradhi.Wawili wakaaga dunia.Wazazi walipoona maisha ya
    watoto wao yamo hatarini,wakaandamana hadi kwa Mwakisu.tajiri huyo aliwajia kwa meno ya
    juu,’msiniitie kibuhuti.Mimi niliwaajiri watoto,sio watoto na wazazi wao”.Wazazi wakatanabahi
    kuwa , ‘Pa shoka hapaingii kisu’.Waliandamana hadi kwa chifu.Chifu alipoyaona yamempita
    kimo,akafululiza hadi kituo cha polisi.
    Mwakisu akakamatwa ,akashtakiwa na kuhukumiwa .Alipatikana na makosa ya kuwaajiri
    watoto wenye unri mdogo na kusababisha vifo vya wawili hao.
    Serikali ikatoa amri kwa wazazi kupeleka watoto wao shuleni.Ikatoa pia misaada ya
    kuendeleza elimu;elimu ya bure kwa shule za msingi.Kingi akasoma hadi kuhitimu chuo
    kikuu.Akawa daktari.
    Alfajiri moja mahabusu waliletwa hospitali kuu ya mkoa kwa matibabu.Kingi akampa huduma mzee
    aliyejawa mvi na kukoboka meno.Alipomtazama kwa makini akamkumbuka.
    Mwakisu akabahatisha,”sura yako….ni kama Kingi…”Kingi akamjibu,”Mimi ndiye
    Kingi.”Wakakondoleana macho, huku machozi yakimtiririka Mwakisu.

    Maswali
    1.Toa kichwa kingine kwa habari hii.
    2.Taja matatizo mawili yaliyowakabili wanakijiji cha Vuruni.
    3.Ni mambo gani yaliyowafanya wanakijiji kumtoa Mwasiku katika orodha yao?
    4.Taja kazi alizofanya Kingi.
    5. Mwasiku alishtakiwa kwa makosa gani?
    6.Eleza maana ya semi hizi.
    (a)Kazi ya kijungu jiko.
    (b)Tononoka si haba.
    (c)Kodolea macho.
    7.Toa maana ya methali hizi:
    (a)Wema hauozi.
    (b)Pa shoka hapaingii kisu.
    8.Toa maana ya msamiati huu kama ulivyoptumiwa katika makala:
    (a)Fauka ya
    (b)Alistahabu

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)

  • Taja mambo/dhana nne zinazozingatiwa katika matumizi ya lugha. (Solved)

    Taja mambo/dhana nne zinazozingatiwa katika matumizi ya lugha.

    Date posted: November 21, 2022.  Answers (1)