Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.
Got a question or eager to learn? Discover limitless learning on WhatsApp now - Start Now!

Yakinisha: Usipolipa usiingie ndani.

      

Yakinisha:
Usipolipa usiingie ndani.

  

Answers


Kavungya
Ukilipa uingie ndani.
Kavungya answered the question on November 25, 2022 at 06:23


Next: Tunga sentensi moja moja kudhihirisha matumizi ya i. Posa ii. Poza
Previous: Andika sentensi ifuatayo katika ukubwa. Uteo alionunuliwa umezeeka sana.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • Tunga sentensi moja moja kudhihirisha matumizi ya i. Posa ii. Poza(Solved)

    Tunga sentensi moja moja kudhihirisha matumizi ya
    i. Posa
    ii. Poza

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Kanusha sentensi katika hali ya kuamrisha wingi. Kimbia haraka – Amka -(Solved)

    Kanusha sentensi katika hali ya kuamrisha wingi.
    Kimbia haraka –
    Amka -

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Tunga sentensi yenye kivumishi cha jina.(Solved)

    Tunga sentensi yenye kivumishi cha jina.

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Tambulisha na ufafanue viambishi vilivyotumika katika Anamfundisha.(Solved)

    Tambulisha na ufafanue viambishi vilivyotumika katika Anamfundisha.

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Kanusha sentensi ifuatayo kwa umoja. Nywele zenu hukatika mnapoachana.(Solved)

    Kanusha sentensi ifuatayo kwa umoja.
    Nywele zenu hukatika mnapoachana.

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Huku ukitoa mifano taja miundo ya silabi.(Solved)

    Huku ukitoa mifano taja miundo ya silabi.

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Sauti /p/ ni kipasuo, sauti hizi ni gani? i. / f / ii. / l /(Solved)

    Sauti /p/ ni kipasuo, sauti hizi ni gani?
    i. / f /
    ii. / l /

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Soma taarifa ifuatayo kasha ujibu maswali Ilikuwa Jumamosi. Nilifika nyumbani kwangu saa moja jioni. Tangu nistaafu miaka miwili awali sikupenda kuchelewa Taarifa ya Habari.(Solved)

    Soma taarifa ifuatayo kasha ujibu maswali
    Ilikuwa Jumamosi. Nilifika nyumbani kwangu saa moja jioni. Tangu nistaafu miaka miwili
    awali sikupenda kuchelewa Taarifa ya Habari.
    Mwezi mmoja ukawa umepita tangu nipewe pesa za kiinua mgongo. Mwezi mmoja mzima
    nilikuwa katika shughuli za kulipa deni hapa na kulipa karo huku. Kuwekeza kwenye mradi ule na
    kununua hili. Sasa shilingi laki mbili tu zilikuwa zimesalia katika benki.
    Watu wengi walinishawishi nijaribu kilimo cha mahindi. Bei ilikuwa imeanza kuimarika.
    Katika taarifa ya habari jioni hiyo, Waziri wa kilimo alitangazaa bei mpya , shilingi 1,500 kwa kila
    gunia. Nami nilikuwa naanza kuumakinikia mradi huu.
    Baada ya taarifa, nilioga nikala na nikaenda kulala. Kwa sababu ya uchovu, usingizi
    ulinichukuwa mara moja. Usingizini niliota. Katika ndoto niliutekeleza mradi wangu. Msimu huo wa
    kulima nilitenga hekari kumi za shamba langu. Wataalamu walinishauri kuwa wakati mzuri wa kulima
    ni wa kiangazi. Mwezi wa Januari ulipoanza tu nilitafuta trekta na kulima. Malipo yalikuwa shilingi
    1,200 kila ekari. Katikati ya mwezi wa Mechi, nilitafuta trekta la kutifua shamba tena kwa gharama ya
    shilingi 15,000 ekari zote kumi. Kufuatia ushauri wa manyakanga wa kilimo, nililipa shilingi elfu
    kumi na tatu kupiga shamba lote haro.
    Mwishoni mwa mwezi huo, nilienda mjini kutafuta pembejeo. Kwanza, nililipa shilingi 20,500
    kwa magunia 15 ya mbolea. Kisha nilinunua magunia manne ya mbegu ya mahindi yenye uzani wa
    kilo 25 kwa shilingi 3,300 kila gunia. Mwezi wa Aprili ulipotimia tu, niliamua kupanda ili nipate mazao
    bora, nilipanda kwa tandazi. Gharama ilikuwa shilingi 1,000 kila ekari. Mvua ilinyesha vizuri na baada
    ya siku saba, mahindi yalianza kuota. Ilifurahisha kuhesabu mistari ya kijani iliyonyooka. Hali hii
    iliwezekana tu baada ya kuajiri vijana wa kuwafukuza korongo na vidiri ili wasifukue mbegu
    mchangani.
    Baada ya mwezi mmoja, hatua ya kupalilia ilifika. Nilitafuta vibarua wa kupalilia. Malipo
    yalikuwa shilingi 700 kila ekari. Kumbe kupalilia kulichochea mtifuko wa mahindi. Punde yakawa
    yananifikia magotini. Hii ikawa ishara kuwa yanahitaji kumwagiwa mbolea ya kunawirisha iitwayo
    ‘amonia’. Gharama yake ikawa shilingi 1,300 kila gunia. Hivyo , nikalipa shilingi 19,500 kwa magunia
    kumi na matano.
    Mahindi yalibadilika kimiujiza. Ghafla tu yalirefuka na kunenepa mashina. Yalibadilika rangi
    yakapiga weusi. Shamba liligeuka likawa kama msitu wa rangi ya kijani iliyokolea. Wapita njia
    waliajabia mimea na juhudi zangu. Shamba langu sasa likawa kielelezo. Maafisa wa kilimo wakawa
    kila siku wanawaleta wakulima wengine kujifunza siri ya ufanisi wangu. Hapo nikaanza kuhesabu
    mavuno nitakayopata na kukadiri faida. Nilipuuza kabisa ushauri wa wahenga kuwa ‘Usikate majani,
    mnyama hajauawa.’
    Bila taarifa wala tahadhari mvua ilitoweka. Hayakupita majuma mawili mahindi yakaanza
    kubadilika. Juma moja baadaye mahindi yalinyauka. Badala ya mahindi, shamba likageuka la vitunguu
    vilivyochomwa na jua. Makisio yangu ya faida yaliyeyuka jinsi ufanyavyo moshi.
    Lakini ‘Muumba ndiye Muumbua.’Siku moja mawingu yalitanda na mvua ikanyesha , muda si
    muda mahindi yalianza kunawiri. Kumbe tukio lililowavunja moyo lilikuwa laja. Siku moja mvua
    kubwa ilinyesha. Asubuhi nilipotoka nje nilipigwa na butwa. Barafu ilitapakaa pote. Shamba lilikuwa
    limetapakaa barafu nafuu. Nilipotazama upande wa shamba niliona dalili za majani mapya ya mahindi
    yakianza kuchomoza. Maumbile ni kitu cha ajabu kweli.
    Muda si mrefu mahindi yalirudia hali yake tena, kasha yakakomaa. Harakati za kutafuta watu
    wa kuyakata na kuyakusanya zilianza. Gharama ya shughuli hii ikawa shilingi 5,000 kuvuna kusafirisha
    kutoka shamba na kukoboa kwa mashine magunia 200 yakachukua shilingi 20,500. Kufikia hapo
    nilikuwa nimetumia takribani shilingi 192,700. Gharama nyingine zilikuwa za usafiri, gharama ya
    dharura na usimamizi, usumbufu wangu binafsi, gharama ya magunia na kadhalika. Mahindi
    yalipokuwa tayari kwenye magunia nilifunga safari kwenda mjini kutafuta soko. Niliposhuka tu niliona
    gazeti. Habari motomoto siku hiyo ilikuwa ‘MAHINDI GUNIA 900/=’ Niligutuka usingizini.

    MASWALI
    a) Ni changamoto zipi zinazokumba kilimo.
    b) Msimulizi alikuwa na kiasi gani cha pesa katika benki baada ya mradi kukamilika?
    c) Eleza maana ya methali zifuatazo kwa mujibu wa makala.
    i. Usikate majani, mnyama hajauawa.
    ii. Muumba ndiye Muumba.
    d) Eleza mambo mawili yaliyosababisha msimulizi asipate faida alivyotarajia.
    e) Kwa nini msimulizi alisema maumbile ni kitu cha ajabu?
    f) Eleza maana ya:
    i. Kiinua mgongo
    ii. Manyakanga wa kilimo.

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Bainisha nomino katika utungo huu. Watoto wameenda kucheza.(Solved)

    Bainisha nomino katika utungo huu.
    Watoto wameenda kucheza.

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Taja nomino zozote mbili katika ngeli A-WA na uonyeshe miundo yake. (Solved)

    Taja nomino zozote mbili katika ngeli A-WA na uonyeshe miundo yake.

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Andika udogo wa: Anacheza ngoma.(Solved)

    Andika udogo wa:
    Anacheza ngoma.

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Tumia kiunganishi kifaacho kuunganisha sentensi hizi. Mwizi alishikwa. Mwizi alipigwa sana.(Solved)

    Tumia kiunganishi kifaacho kuunganisha sentensi hizi.
    Mwizi alishikwa. Mwizi alipigwa sana.

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Bainisha aina za vielezi katika sentensi hii. Mtoto alikimbia mara sita uwanjani kisha akatembea kitausi.(Solved)

    Bainisha aina za vielezi katika sentensi hii.
    Mtoto alikimbia mara sita uwanjani kisha akatembea kitausi.

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Tunga sentensi yenye kitenzi kishirikishi kipungufu. (Solved)

    Tunga sentensi yenye kitenzi kishirikishi kipungufu.

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Pigia mstari vivumishi kwenye sentensi hizi na ueleze ni vya aina gani. (i) Mtoto mwenyewe ataleta kalamu. (ii) Kitabu cha Musa hakipo(Solved)

    Pigia mstari vivumishi kwenye sentensi hizi na ueleze ni vya aina gani.
    (i) Mtoto mwenyewe ataleta kalamu.
    (ii) Kitabu cha Musa hakipo

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Tunga sentensi katika wakati uliopita hali timilifu. (Solved)

    Tunga sentensi katika wakati uliopita hali timilifu.

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Bainisha aina zifuatazo za mofimu. (i) Mtu – (ii) Samaki – (iii) Anasoma –(Solved)

    Bainisha aina zifuatazo za mofimu.
    (i) Mtu –
    (ii) Samaki –
    (iii) Anasoma –

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Andika sauti zenye sifa zifuatazo: (i) Nazali ya kaa laini (ii) Kikwamizo ghuna cha mdomo na meno (iii) Irabu ya nyuma wastani (iv) Kimadende(Solved)

    Andika sauti zenye sifa zifuatazo:
    (i) Nazali ya kaa laini
    (ii) Kikwamizo ghuna cha mdomo na meno
    (iii) Irabu ya nyuma wastani
    (iv) Kimadende

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Soma shairi ifuatayo kisha ujibu maswali CHEMA HAKIDUMU Chema hakidumu, kingapendekeza, Saa ikitimu, kitakuteleza(Solved)

    Soma shairi ifuatayo kisha ujibu maswali
    CHEMA HAKIDUMU
    Chema hakidumu, kingapendekeza,
    Saa ikitimu, kitakuteleza
    Ukawa na hamu, kukingojeleza,
    Huwa ni vigumu, kamwe hutaweza
    Chema sikiimbi, kwamba nakitweza
    Japo mara tumbi, kinshaniliza,
    Na japo siombi, kipate n’ongeza,
    Mtu haniambi, pa kujikimbiza
    Chema mara ngapi, kinniondoka,
    Mwanangu yu wapi? Hakukaa mwaka,
    Kwa muda mfupi aliwatilika,
    Ningefanya lipi, ela kumzika?
    Chema wangu babu, Kibwana Bashee,
    Alojipa tabu, kwamba anilee
    Na yakwe sababu, ni nitengenee,
    Ilahi Wahhabu, mara amtwee.
    Chema wangu Poni, kipenzi nyanyangu,
    Hadi siku hini, yu moyoni mwangu,
    Yu moyoni ndani, hadi kufa kwangu,
    Ningamtamani, hatarudi kwangu.
    (Abdalla, Abdilatif, Sauti ya Dhiki)

    MASWALI:
    (a) Hili ni shairi la aina gani?
    (b) Taja na ueleleze aina zozote mbili za bahari katika shairi hili.
    (c) Eleza umbo la shairi hili.

    Date posted: November 25, 2022.  Answers (1)

  • Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata. Mhudumu: Mnakaribishwa. Menyu hii hapa. Mtakula nini?(Solved)

    Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.
    Mhudumu: Mnakaribishwa. Menyu hii hapa.
    Mtakula nini?
    Mteja 1: Naomba uniletee mix na ugali. Fanya haraka.
    Mteja 2: Mhudumu,hebu leta madodo na chemsha mbili. Pia niletee maji ya machungwa.
    Mhudumu: Sawa. Baada ya dakika moja utapata yote uliyoagiza.
    Mteja 1: (Akila) Wewe-Please bring me drinking water. Yawe baridi tafadhali.
    Mhudumu: Ndiyo haya hapa mezani. Glasi ndio hii pia,karibu.
    Mteja 2: Nina haraka mzee. Wapi tooth pick?
    Mhudumu: Hizo hapo ,mezani karibu na maji.
    Mteja 1: (Akiita) Mhudumu,naomba uniletee ugali saucer tafadhali.
    Mhudumu: Naam.
    Mteja 2: (Akisimama) Nimeshiba. Hizi hapa pesa
    Niletee change haraka niondoke.

    MASWALI
    a) Ni sajili gani inayohusishwa katika mazungumzo haya?
    b) Taja sifa zozote tano za sajili hii
    c) Dondoa msamiati unaotambulisha sajili hii

    Date posted: November 24, 2022.  Answers (1)