Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.
Got a question or eager to learn? Discover limitless learning on WhatsApp now - Start Now!

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata. Mhudumu: Mnakaribishwa. Menyu hii hapa. Mtakula nini?

      

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.
Mhudumu: Mnakaribishwa. Menyu hii hapa.
Mtakula nini?
Mteja 1: Naomba uniletee mix na ugali. Fanya haraka.
Mteja 2: Mhudumu,hebu leta madodo na chemsha mbili. Pia niletee maji ya machungwa.
Mhudumu: Sawa. Baada ya dakika moja utapata yote uliyoagiza.
Mteja 1: (Akila) Wewe-Please bring me drinking water. Yawe baridi tafadhali.
Mhudumu: Ndiyo haya hapa mezani. Glasi ndio hii pia,karibu.
Mteja 2: Nina haraka mzee. Wapi tooth pick?
Mhudumu: Hizo hapo ,mezani karibu na maji.
Mteja 1: (Akiita) Mhudumu,naomba uniletee ugali saucer tafadhali.
Mhudumu: Naam.
Mteja 2: (Akisimama) Nimeshiba. Hizi hapa pesa
Niletee change haraka niondoke.

MASWALI
a) Ni sajili gani inayohusishwa katika mazungumzo haya?
b) Taja sifa zozote tano za sajili hii
c) Dondoa msamiati unaotambulisha sajili hii

  

Answers


Kavungya
(a) Sajili ya hotelini

(b) -Matumizi ya lugha ya ucheshi na utani
-Matumizi ya lugha sio lazima yazingatie kanuni za lugha sanifu ama ile
isiyofuata kaida za lugha
-Matumizi ya msamiati maalumu
-Lugha ya hotelini inaweza kuchanganya ndimi
-Ni lugha shawishi na rahishi kueleweka
-Wakati mwingine kuna matumizi ya chuku
-Ni lugha ya kupumbaza na kufurahisha kwa kuwa inanuiwa kuvutia.

(c) -menyu
Mix na ugali
-Madodo na chemsha mbili
-Tooth pick
Kavungya answered the question on November 24, 2022 at 07:04


Next: Tumia herufi mwafaka kuainisha maneno katika sentensi hii. Ingawa anataka kucheza karata,ni mlevi
Previous: Soma shairi ifuatayo kisha ujibu maswali CHEMA HAKIDUMU Chema hakidumu, kingapendekeza, Saa ikitimu, kitakuteleza

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • Tumia herufi mwafaka kuainisha maneno katika sentensi hii. Ingawa anataka kucheza karata,ni mlevi (Solved)

    Tumia herufi mwafaka kuainisha maneno katika sentensi hii.
    Ingawa anataka kucheza karata,ni mlevi

    Date posted: November 24, 2022.  Answers (1)

  • Sahihisha: Kwenye nilisomea ni bali.(Solved)

    Sahihisha:
    Kwenye nilisomea ni bali.

    Date posted: November 24, 2022.  Answers (1)

  • Nyambua Filisisha (tenda) (Solved)

    Nyambua
    Filisisha (tenda)

    Date posted: November 24, 2022.  Answers (1)

  • Tumia kitenzi jina na kivumishi kutunga sentensi.(Solved)

    Tumia kitenzi jina na kivumishi kutunga sentensi.

    Date posted: November 24, 2022.  Answers (1)

  • Andika sentensi hii katika ukubwa. Huyo nyoka alikatwa mkia na mvulana yule.(Solved)

    Andika sentensi hii katika ukubwa.
    Huyo nyoka alikatwa mkia na mvulana yule.

    Date posted: November 24, 2022.  Answers (1)

  • Taja visawe vya maneno yafuatayo. (i) Damu (ii) Mjinga(Solved)

    Taja visawe vya maneno yafuatayo.
    (i) Damu
    (ii) Mjinga

    Date posted: November 24, 2022.  Answers (1)

  • Andika katika udogo na wingi Njusi aliyekuwa na jicho moja alianguka mtoni.(Solved)

    Andika katika udogo na wingi
    Njusi aliyekuwa na jicho moja alianguka mtoni.

    Date posted: November 24, 2022.  Answers (1)

  • Tumia kiwakifishi kifuatacho kubainisha matumizi yake katika sentensi ili kutoa maana mbili tofauti. Ritifaa(Solved)

    Tumia kiwakifishi kifuatacho kubainisha matumizi yake katika sentensi ili kutoa maana mbili tofauti.
    Ritifaa

    Date posted: November 24, 2022.  Answers (1)

  • Tunga sentensi ukitumia viwakilishi vifuatavyo. (i) Nafsi viambata (II) Visisitizi(Solved)

    Tunga sentensi ukitumia viwakilishi vifuatavyo.
    (i) Nafsi viambata
    (II) Visisitizi

    Date posted: November 24, 2022.  Answers (1)

  • Geuza neno lililopigwa mstari kuwa kiwakilishi Mtoto mbaya aliadhibiwa(Solved)

    Geuza neno lililopigwa mstari kuwa kiwakilishi
    Mtoto mbaya aliadhibiwa

    Date posted: November 24, 2022.  Answers (1)

  • Onyesha vivumishi vya sifa katika sentensi zifuatazo. (i) Anayetaka chakula kitamu ni nani? (ii) Kiatu kirefu kimeng’oka kikanyagio. (Solved)

    Onyesha vivumishi vya sifa katika sentensi zifuatazo.
    (i) Anayetaka chakula kitamu ni nani?
    (ii) Kiatu kirefu kimeng’oka kikanyagio.

    Date posted: November 24, 2022.  Answers (1)

  • Tunga sentensi mbili kuonyesha tofauti kati ya maneno haya. (i) shuka (ii) suka (Solved)

    Tunga sentensi mbili kuonyesha tofauti kati ya maneno haya.
    (i) shuka
    (ii) suka

    Date posted: November 24, 2022.  Answers (1)

  • Eleza maana ya misemo ifuatayo. (i) kupiga domo (ii) kupiga kijembe(Solved)

    Eleza maana ya misemo ifuatayo.
    (i) kupiga domo
    (ii) kupiga kijembe

    Date posted: November 24, 2022.  Answers (1)

  • Bainisha vitenzi halisi katika sentensi zifuatazo. (i) Nyanchama hakufika mkutanoni (ii) Horukut amerudi kutoka masoni(Solved)

    Bainisha vitenzi halisi katika sentensi zifuatazo.
    (i) Nyanchama hakufika mkutanoni
    (ii) Horukut amerudi kutoka masoni

    Date posted: November 24, 2022.  Answers (1)

  • Onyesha nomino za jamii katika sentensi zifuatazo (i) Chuki baina ya jamii lazima ikomeshwe barani Afrika. (ii) Wageni watatumbuizwa na bengi ya kayamba Afrika.(Solved)

    Onyesha nomino za jamii katika sentensi zifuatazo
    (i) Chuki baina ya jamii lazima ikomeshwe barani Afrika.
    (ii) Wageni watatumbuizwa na bengi ya kayamba Afrika.

    Date posted: November 24, 2022.  Answers (1)

  • Onyesha kundi nomino na kundi tenzi katika sentensi hii. Nyayo za wanyama hao zimeonekana hapa. (Solved)

    Onyesha kundi nomino na kundi tenzi katika sentensi hii.
    Nyayo za wanyama hao zimeonekana hapa.

    Date posted: November 24, 2022.  Answers (1)

  • Eleza tofauti kati ya: (i) Mofimu huru (ii) Mofimu tegemezi (Solved)

    Eleza tofauti kati ya:
    (i) Mofimu huru
    (ii) Mofimu tegemezi

    Date posted: November 24, 2022.  Answers (1)

  • Eleza tofauti kati ya sauti /z/ na /f/ (Solved)

    Eleza tofauti kati ya sauti /z/ na /f/

    Date posted: November 24, 2022.  Answers (1)

  • Soma taarifa hii kisha ujibu maswali Kuna wataalamu siku hizi wanaosema kuwa jela si pahala pa adhabu bali pa matibabu. Yaani madhumuni ya kumtia mhalifu jela isiwe...(Solved)

    Soma taarifa hii kisha ujibu maswali
    Kuna wataalamu siku hizi wanaosema kuwa jela si pahala pa adhabu bali pa matibabu. Yaani
    madhumuni ya kumtia mhalifu jela isiwe kumwadhibu kwa makosa aliyofanya bali iwe kumtibu na kujaribu
    kumrekebisha tabia yake ili awe raia mwema.
    Zamani wahalifu waliadhibiwa kwa mujibu wa makosa waliyoyafanya. Mhalifu aliyefanya makosa
    madogo madogo alifungwa lakini mtu aliyeua naye aliuawa. Sasa wataalamu wanatuambia kuwa mhalifu
    akiadhibiwa anapokuwa kifunguno,basi akitoka hurejea tena kufanya uhalifu. Madhumuni ya kumtia jela iwe si
    kumwadhibu bali kumfunza tabia njema. Wanatuambia kuwa makosa afanyayo mhalifu yanatokana na
    matatizo ya jamii kwa jumla,nayo ni matatizo kama ya umaskini, msongamano wa watu, kosa afanyalo mhalifu
    si kosa lake pekee bali ni kosa la jamii nzima.
    Jitu lilizoea kuua halioni kitu kumpiga mtarimbo au rungu la kichwa na kumyang’anya kila alicho
    nacho. Siku hizi,jitu kama hili baadhi ya wataalamu husema lisiuawe lifungwe maisha tu. Lakini ‘kifungo cha
    maisha’ ni kama tunavyokijua. Muuaji hufungwa pengine miaka kumi tu kisha husamehewa muda uliobaki.
    Hapo tena huwa huru ama kuifichua mali aliyoiiba na kuistarehea raha mustarehe au kurejea tena kufanya
    uhalifu.
    Haya ni kinyume kabisa na mambo yalivyokuwa zamani. Aliyeua aliuawa kwa hivyo watu waliogopa
    kuua. Raia na pia askari waliokuwa wakiwasaka wahalifu walinusurika vifo kwani wahalifu wengine
    walichukua silaha za hatari kama bastola na bunduki.
    Sasa wale wahalifu wabaya sana – mijizi, minyang’anyi na wauaji ndio wanaotukuzwa. Magazeti
    huwashawishi makatili hawa na kuwapa mapesa chungu nzima waeleze maisha yao ya kikatili. Magazeti haya
    sasa ndiyo yanayopata wasomaji wengi. Pia wachapishaji vitabu vya hadithi zinazohusikia na uhalifu, biashara
    zao zinazidi kustawi. Kadhalika sinema zinazoonyesha picha za ukatili; wizi na mauji hujaa watazamaji
    wanaoshangilia uhalifu ufanywao.
    Wahalifu kwa upande mmoja wanatukuzwa na masinema vitabu na magazeti na kwa upande mwingine
    “haki” zao zinapiganiwa na baadhi ya wataalamu. Watu wanaowalaani wahalifu ni wale waliohasirika tu na
    kuteswa na wahalifu . Baadhi yao hata kulaani hawawezi kwa sababu wameshauawa,hawana tena kauli.

    MASWALI
    (a) Fupisha aya ya kwanza hadi ya tatu kwa maneno 50.
    Matayarisho
    Nakala safi

    (b) Fupisha aya mbili za mwisho kwa maneno kati ya 45-50
    Matayarisho
    Nakala safi

    Date posted: November 23, 2022.  Answers (1)

  • Soma taarifa hii kisha ujibu maswali ifuatayo. UKANDAJI Je,unajua kuwa ukandaji wa mwili umetumika kama njia mojawapo ya matibabu toka jadi?(Solved)

    Soma taarifa hii kisha ujibu maswali ifuatayo.
    UKANDAJI
    Je,unajua kuwa ukandaji wa mwili umetumika kama njia mojawapo ya matibabu toka jadi? Watu
    wanaofahamika kutumia ukandaji kimatibabu toka jadi ni Wahindi,Wachina,Wagiriki,Warumi na Waafrika.
    Ukandaji unajulikana kuwa na manufaa makubwa kimatibabu. Mathalani,ukandaji hufungua vitundu
    vya ngozi. Ufunguzi huu huondoa sumu mwilini kupitia kwa utoaji jasho. Pili,ukandaji hupunguza mkazo wa
    misuli. Misuli ikiwa na mkazo zaidi kwa muda mrefu huleta urundikaji wa asidi. Ukandaji huondoa asidi
    hii,huufanya mwili kuwa mlegevu,humletea mtu uchangamfu na kuondoa uchovu.
    Halikadhalika,ukandaji huimarisha mzunguko wa damu mwilini kwa wepesi. Hali hii huhakikisha kuwa
    virutubishi vya mwili huweza kufikia viungo vyote vya mwili. Hili nalo huchangia kuzidisha uwezo wa mwili
    kujikinga na maradhi. Hewa safi ya oksijeni huweza pia kusambaa kote mwilini kupitia kwa uimarishaji wa
    mzunguko wa damu. Aidha,ukandaji wa taratibu na polepole hupunguza mkazo wa neva na kuziliwaza
    ukandaji wa kasi huchangamsha neva na kuimarisha utendaji kazi wake.
    Ukandaji unaweza kufanyiwa kiungo chochote mwili ni. Ukandaji huu huweza kuwa na matokeo
    mbalimbali mwilini.
    Mathalani,ukandaji wa njia ya chakula mwilini,hasa tumbo na utumbo,huimarisha usagaji wa chakula na
    kuchangia uondoaji wa uchafu na sumu mwilini. Nao ukandaji wa njia ya mkonjo hustawisha uondoaji wa
    chembechembe za sumu mwilini.
    Kwa kawaida,viganja vya mikono hutumika katika ukandaji. Viungo hivi vinapaswa kuwa na wororo.
    Wororo huu hupatikana kwa kutumia mafuta. Mafuta ambayo ni bora zaidi kwa shughuli za ukandaji ni ya
    ufuta au simsim. Matumizi ya kitu chochote kama ungaunga kinachoweza kuziba vitundu vya ngozi
    hayapendekezwi.
    Ukandaji wapaswa kutekelezwa kwa njia ifuatayo. Mtu aanzie mikono na miguu. Kisha aingie kukanda
    kifua,tumbo,mgongo na makalio. Hatimaye,akande uso na kichwa. Mtu anaweza kutumia kitambaa kukandia
    mgongo. Ni bora kutumia viganja vya mikono kukandia. Kwa njia hii,manufaa huwa maradufu.
    Kwanza,tutanufaika na ukandaji na wakati huo huo tutakuwa tukifanya mazoezi ya viungo. Wasioweza
    kujikanda,wanaweza kuomba msaada. Ni muhimu ukandaji ufuatiwe na kuoga kwa maji vuguvugu.
    Kwa walio na tatizo la shinikizo au mpumuko wa damu wanaweza kubadilisha utaratibu wa ukandaji.
    Waanzie kichwani,kisha waelekee usoni,kifuani,tumboni,mgongoni,makalioni,miguuni na kuhitimisha
    mikononi.
    Hata hivyo,ukandaji haupaswi kufanywa wakati mtu anaugua maradhi yoyote. Wanawake wajawazito
    nao wanatakiwa kuepuka ukandaji wa tumbo. Halikadhalika,ukandaji wa tumbo hauruhusiwi wakati mtu
    anaendesha,ana vidonda vya tumbo au uvimbe tumboni. Hatimaye,ukandaji haupendekezwi iwapo mtu ana
    maradhi ya ngozi.

    MASWALI
    (a) Ukandaji ni nini?
    (b) Eleza manufaa matatu ya ukandaji.
    (c) Ukandaji unatakiwa kutekelezwa kwa njia gani?
    (d) Ukandaji unatakiwa kutekelezwa na nani na kwa nini?
    (e) Onyesha ni lini ukandaji haupendekezwi.
    (f) Eleza maneno yafuatayo kama yalivyotumika:
    (i) ufunguzi
    (ii) auni
    (iii) maradufu
    (iv) maji vuguvugu
    (v) shinikizo la damu

    Date posted: November 23, 2022.  Answers (1)