Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Soma dondoo lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata. Mwatani: Rusha hiyo ball haraka tumechelewa five minutes. Twende daro. Omoshi: Harakisha mode anacome.

Soma dondoo lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata.
Mwatani: Rusha hiyo ball haraka tumechelewa five minutes. Twende daro.
Omoshi: Harakisha mode anacome.
Bwana Kipiti: Nendeni darasani haraka! Kisha kiranja awape vitabu vyenu vya insha
ili mwandike barua.
Mwatani: Sawa mwalimu. Samahani kwa kuchelewa uwanjani.
Omoshi: Je, tutaandika barua rasmi au barua ya kawaida?
Bwana Kipiti: Mwandike barua rasmi. Je, mnakumbuka muundo wake?
Omoshi na Mwatani: Ndio mwalimu. Ulitufundisha jana. Asante sana mwalimu.
Bwana Kipiti: Kumbukeni idadi ya maneno. Idadi ya maneno ni muhimu katika uandishi
wa insha.

(i) Eleza sajili katika dondoo.
(ii) Eleza sifa nane za sajili hii zinazopatikana katika dondoo.

Answers


Kavungya
(i) Eleza sajili katika dondoo.
Sajili ya shule – kuna msamiati wa shuleni kama vile mwalimu na vitabu.

(ii) Eleza sifa nane za sajili hii zinazopatikana katika dondoo.
a. Msamiati maalum – mwalimu, vitabu na kiranja
b.Kuchanganya ndimi – Rusha hiyo ball haraka.
c. Kuuliza maswali – Je, mnakumbuka muundo wake?
d.Lugha ya heshima – asante sana mwalimu
e. Lugha sanifu huzingatiwa na wanafunzi wanapozungumza na walimu
f. Lugha ya kuamrisha – Nendeni darasani haraka.
g.Wanafunzi hutumia majina ya kimsimu – mode
h.Urudiaji kwa lengo la kusisitiza – idadi ya maneno
Kavungya answered the question on November 25, 2022 at 07:01

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions