Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Kuna umuhimu gani kufunza fasihi simulizi katika chuo za upili?

Kuna umuhimu gani kufunza fasihi simulizi katika chuo za upili?

Answers


KELVIN
a)Kuburudisha-kustarehesha, kufurahisha, kuchangamsha, kutuliza, kusisimua na kupumbaza akili na kiwiliwili - nyimbo, hadithi, vitendawili
b)Kufunza maadili kwa wanajamii kwa kuwahimiza kuiga sifa chanya na kukataa sifa hasi za wahusika.
c)Kukuza uwezo wa kufikiri/kudadisi k.m vitendawili na chemshabongo.
d)Kufariji k.m mbolezi na methali k.m. ‘Baada ya dhiki faraja’.
e)Vipengele vya fasihi simulizi k.v mashairi, nyimbo, nahau, hutumiwa katika uandishi wa fasihi andishi.
f)Kuhifadhi historia ya jamii k.m. mighani, visaviini, mapisi, tarihi n.k.
g)Kukejeli tabia zinazokiuka matarajio ya jamii k.v soga, methali, n.k.
h)Kuendeleza tamaduni za jamii kwani husawiri imani na desturi za jamii. k.v kitendawili ‘Nyumbani mwetu mna papai lililoiva lakini siwezi kulichuma.’ - Mtu hawezi kumwoa dadake.
i)Kuunganisha watu pamoja kwa kuwajumuisha pamoja wakati wa ngoma, kuimba, utambaji, n.k.
j)Kukuza lugha k.v. misimu inapokita kimatumizi na kujumuishwa katika lugha sanifu.
k)Kukuza uwezo wa kutumia lugha kadiri mtu anapoendelea kuwasilisha k.v. hotuba, vitanza ndimi husaidia kuboresha matamshi na kutofautisha maana za maneno.

kalvinspartan answered the question on October 20, 2017 at 16:32

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions