Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Taja sababu zinazochangia katika kubadilika kwa Fasihi Simulizi

Taja sababu zinazochangia katika kubadilika kwa Fasihi Simulizi

Answers


KELVIN
a)Kuwasilishwa vibaya.
b)Fanani kusahau na kubadilisha yaliyomo na mtiririko.
c)Kubadilisha ili kukidhi mahitaji ya hadhira k.m. umri na uelewa wao- kutumia lugha nyepesi kwa watoto na pevu kwa watu wazima.
d)Mabadiliko ya mandhari/mazingira-vitu vilivyo katika mazingira halisi kukosekana katika mazingira ya usimulizi na msimulizi kutumia vitu katika mazingira yake vinavyokaribiana navyo.
e)Kutoeleweka na hivyo kuhifadhiwa vibaya.
f)Mabadiliko ya wakati k.m kitendawili cha wakati wa mkoloni kutumia mzungu na cha wakati wa mwarabu kutumia mwarabu na maana ni ile ile-Mzungu/mwarabu amesimama kwa mguu mmoja-mwavuli.
g)Mabadiliko ya falsafa ya vizazi na maingiliano katika jamii kusababisha kurithisha tu yale ambayo ni muhimu na kuacha mengine.
h)Kila fanani huwa na mtindo wake wa kuwasilisha/kisanii.

kalvinspartan answered the question on October 20, 2017 at 16:33

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions