Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Ichambue jalada ya tamthilia ya Kigogo

Ichambue jalada ya tamthilia ya Kigogo

Answers


ESTHER
Jalada ni ile sehemu ngumu ya kitabu. Kupitia jalada, tunaweza kudokeza ya kutarajiwa katika kazi ya fasihi.
Jalada la tamthilia hii lina anwani ya tamthilia: Kigogo. Kigogo ni mtu mwenye mamlaka au madaraka ya kiutawala au kiongozi. Mwandishi wake ni Pauline Kea
Anwani ya kitabu imeandikwa kwa rangi ya majano.
Kuna mchoro wa bara la Afrika lililoinama. Mchoro huu umekolezwa rangi nyeusi; ishara ya kiza.
Nyuma ya mchoro huu kuna picha ya jua linalochomoza.
Chini ya mchoro huu upande wa kushoto, kuna mzee mkongwe aliyebeba fimbo. Vile vile amekolezwa weusi. Anaonekana kuzama katika mawazo.
Rangi ya kijani kibichi imetamalaki katika jalada
Nyuma ya jalada kuna muhtasari wa tamthilia yenyewe.
Afrika kuwa katika kiza inaashiria madhila chungu nzima barani baada ya uhuru.
Mzee mkongwe anayeonekana mwenye mawazo anaashiria viongozi wa awali waliopigania uhuru na ambao tayari wameiaga dunia. Ila, hata katika pumziko lao, hawana amani kwani waliochukua hatamu baada yao kufariki wameiua ndoto ya uhuru kamili wa mwafrika
Rangi ya kijani kibichi inaashiria ardhi. Masuala ya ardhi barani Afrika ni masuala sugu yanayoleta migogoro mingi
Rangi ya majano na jua linalochomoza linaashiria mwamko mpya au mabadiliko. Kuna tumaini kama wasemavyo wahenga, siku njema huonekana asubuhi

ESTHER STEVE answered the question on April 28, 2018 at 15:20

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions