Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Linganisha bahari za shairi A na B

SHAIRI A: HOFU YA BIN-ADAMU

Hofu za wanyonge, ni nguvu za matajiri,

Ambazo zinawaponda, wanapotaka usawa.


Hofu ya watawala, ni kupoteza uhuru,

Wa kutawala kwa mbavu, pamoja na utukutu.



Hofu za mwanamke ,mwanamke wa sasa,

Ni kutumiwa ja rungu, daima kuwekwa nyuma.


Hofu za mmcha-mungu, ni maisha ya baadaye,

Maana hana hakika, ndio aogopa kifo.


Hofu za wasomi, ni kwamba wako baidi,

Na wale wateteao, ambao ni sawa nao.




SHAIRI B: AMANI

Uhuru pia Amani
Usifikirie ni zawadi
Ambayo inapeanwa
Pasipo mikwaruzano



Kama wataka hakiyo
Shariti uwe tayari Kupokeza roho yako
Pamoja na ya mwingine



Uhuru ja ini la fani
Ambalo kulifikia
Sharti uwe jasiri
Jasiri aso kifani


Linganisha bahari za shairi A na B

Answers


Maurice
Shairi A

(i) Tathnia(uwili)

(ii)Kikwamba-neno ‘’hofu’’ huanza kila mshororo wa kwanza.

(iii) Masivina-vina vyote kutofautiana.

(iv) Mandhuma-ukwapi unatoa wazo,utao unatoa jibu.



SHAIRI B:

(i) Utenzi-kipande kimoja.

(ii)Tarbia-mishororo mine.
maurice.mutuku answered the question on August 3, 2019 at 11:37

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions